ukisema au ukisikia wanasema jamaa anapenda sana wanawake, waelewa kuwa anapenda zaidi labda ''kusini mwa Afrika'' mimi nafagilia kila kiumbe cha kike, wanasema wanawake ni wadhaifu, kumbe sio, bali ni walaini. kwa sababu yao, ndiyo maana ulimwengu unazidi kuwepo. kwa sababu ya uwepo wa viumbe wengine wa kike ndio maana ulimwengu unazidi kuwa na viumbe hivyo. uanaume wangu, unajidhihirisha ndani ya mwanamke. ni kwa kumpataia mbegu, ndipo anazaliwa mtoto wa kuniita baba. ni mwanamke. upendo wa mama sio wa kawaida kwa wanae, atafanya kila awezalo kumlinda mwanae. Mwanamke anatumbo la ajabu, ni tumbo linalotunza na kuzaa viumbe vingine. tunamla mwanamke kwa kunyonya maziwa yake na kwa hiyo mwili wake ndio chakula chetu. mwanamke sauti yake ni nzuri, sauti yake ni njema sio ya kibesi wala nini. NAMPENDA mwanamke. lakini unaweza kuamini kuwa tangu nizaliwe sijawahi kuunja upendo wa mama wala wa Mwanamke yeyote?? nakosa mengi ndugu, sikuwahi kuuonja upendo wa kweli japo natambuaumuhimu wa mwanamke. aaaamina
Friday, July 17, 2009
nawapenda sana wanawake na ma Jike pia
ukisema au ukisikia wanasema jamaa anapenda sana wanawake, waelewa kuwa anapenda zaidi labda ''kusini mwa Afrika'' mimi nafagilia kila kiumbe cha kike, wanasema wanawake ni wadhaifu, kumbe sio, bali ni walaini. kwa sababu yao, ndiyo maana ulimwengu unazidi kuwepo. kwa sababu ya uwepo wa viumbe wengine wa kike ndio maana ulimwengu unazidi kuwa na viumbe hivyo. uanaume wangu, unajidhihirisha ndani ya mwanamke. ni kwa kumpataia mbegu, ndipo anazaliwa mtoto wa kuniita baba. ni mwanamke. upendo wa mama sio wa kawaida kwa wanae, atafanya kila awezalo kumlinda mwanae. Mwanamke anatumbo la ajabu, ni tumbo linalotunza na kuzaa viumbe vingine. tunamla mwanamke kwa kunyonya maziwa yake na kwa hiyo mwili wake ndio chakula chetu. mwanamke sauti yake ni nzuri, sauti yake ni njema sio ya kibesi wala nini. NAMPENDA mwanamke. lakini unaweza kuamini kuwa tangu nizaliwe sijawahi kuunja upendo wa mama wala wa Mwanamke yeyote?? nakosa mengi ndugu, sikuwahi kuuonja upendo wa kweli japo natambuaumuhimu wa mwanamke. aaaamina
huwa mnafikiria nini?

wengi wenu mkiingiaga kwenye mijengo kama hii huwa mnakuwa wanafiki wa kujifanya wanyenyekevu na wenye upendo, wapole, wasiopenda kuzini nk.
kumbe waongo mnaogopa ule mkwala mkuu upigwao wa siku za mwisho takutana na limoto la milele likuunguze mpaka kinyesi kilicomo tumbona mwako.
nawakemea. Mkasali bwana
Thursday, July 16, 2009
mmmmhhhhh nnnooooooot! unaona nini?
labda hata sungura wanazunguka,tafadhali blogu hii irudi kwenye maadili sio vitu vya gizani please, ombi!
Wednesday, July 15, 2009
Kila kitu kinazunguka.!
Wanasayansi wanatwambia kuwa ulimwengu / dunia tuishimo ni duara na kwamba inazunguka jua. Mzee mmoja kule kwetu anabishi kwamba dunia imetulia ila jua ndo lenye kiherehere linazunguka dunia. Kwake dunia ni kubwa kukliko jua.
Basi nyota nazo zinazunguka, mwezi nao mala kipande, mala mzima. Wengine wanasema macho yetu ndiyo yaonayo mviringo.
Basi bwana, maji tunayokunywa yanazunguka. Yanatoka mitoni, baharini au kwenye madimbwi kwa kuakisiwa au kuchavushwa na baadaye kunyesha kama mvua. Hata mikojo, vinyesi na mate, yanaakisiwa na kunyesha kama mvua harafu wewe unakunywa. Yawezekana maji unywayo sasa ni mkoja au mimate ya lijamaa usilolipenda!!
Chakula nacho ndo hivyo. Ukijisaidia shambani yanaota mazao mazuri yenye mbolea na matamu kula, yanazunguka. Binadamu naye anazunguka, tuachane na reincarnation, unatoka hapa na pale huku na huku kule na kule. Damu inazunguka mwilini na ikisimama hamna uhai!!
Akili zetu nazo ziko bize, mara hiki, mara kile, mara sijui nini. Mchana mawazo, usiku ndoto, zikisimama wafa. Kila kitu ni mzunguko tu. Basi kama kuna herufi nzuri, ni O au 0 kwani zinaonyesha uhalisi. Ni mzunguko tu ndg.
Nini kingine kizugukacho? Si hata gari lazima lizunguke ili kukufikisha uelekeako?
ZUNGUKA TU
Monday, July 13, 2009
unamtafuta Mungu? acha hizo!
Hatuwezi kumjua Mungu na hivyo tunachokijua ni kama punje ya mchanga baharini. Mungu hayuko mbali nasi. Hatuwezi kumtafuta huku au kule, tunaweza kumpata kwa njia ya uamsho pekee, uamsho (awakening) wa roho zetu. Roho pekee ndiyo inayoweza kumwona Mungu. Ndio maana wanasayansi hukataa juu ya uwepo wa Mungu hata kama ukubali juu ya uwepo wa nguvu wasiyoielewa inayomiliki na kutawala kila kitu..
Uamsho wa roho zetu huanza kwa kujitambua. Ukijitambua utamtambua Mungu. Uamsho wa roho ni sawa na sayansi ya roho, sayansi iwezeshayo kumuona Mungu. Kwa uamsho wa roho zetu, tutamhishi na kumfurahia Mungu. Roho ina kazi maarumu ambayo ni kumhisi, kumjua na kufurahia baraka za Mungu.
Vitabu vya dini (misaafu) husisitiza kuwa sisi ni roho na kama ni roho sisi hatuna mwanzo wala mwisho na sisi na Mungu ni sawa na maji. Mungu ni mkubwa kama bahari na sisi ni wadogo kama tone la mvua na hivyo basi tone la nvua lidondokapo baharini huwezi tena kuyatenganisha. Bahari hupokea maji ya kutoka kila upande kama ishara ya umoja wa binadamu wote wenye rangi, kabila na mataifa tofauti. Bahari hupokea maji kutoka bara ulaya, Amerika, Afrika na kwingineko lakini maji yale yaingiapo baharini huwa kitu kimoja. Rangi moja, radha moja na sifa zilezile. Huwezi kuyatenganisha tena kwa kuangalia yalipotoka. Hivyo ndivyo ilivyo kwetu sisi kama roho tukifika mbele ya Mungu huwa kitu kimoja
Vitabu vya dini pia huongelea juu ya nuru na sauti (neno). Mungu yumo ndani mwetu na nilazima tumjue huyo wa ndani kabla ya kumtafuta wa nje yetu kwani tukimhishi ndani mwetu tutapata Muunganisho naye (kwanjia ya roho) na hivyo sisi na yeye kuwa wamoja kama ulivyo ukweli mkuu. (kumbuka sisi ni sehemu ya ukweli mkuu au ukweli mkuu umo ndani mwetu)
Thursday, July 9, 2009
Njia ya kuelekea kwa Mungu
Kutoa huduma kwa wengine bila kujigamba na kuheshimu kila kiumbe chake kuazia kwa binadamu, wanyama miti nk.
Kukumbuka na kulinuiza jina lake na upendo wake wakati wote (tahajudi ya nuru / inner-light meditation).
Kusikiliza maneno yake na sauti yake kupitia kwa viumbe vyake (tahajudi ya sauti / inner-sound meditation)
Na kuishi kwa uwepo (kuishi sasa / consiousness)
Haya yote yatatuelekeza kuishi kwa upendo, amani, mafanikio vitakavyo zaa heshima, umoja, kuvumiliana, heshima na kutupelekea kwenye uhalisia wetu (ukweli mkuu) ambao inasemwa kuwa mkiijua kweli itawaweka huru na hakuna uhuru bila kujitambua (self realization) ili kumtambua Mungu (God realization)
Kristo (yesu) anatwambia kuwa kama mnanipenda, basi ziiishi amri zangu
Tuesday, July 7, 2009
njoo darasani tujitambue wewe!
Familia ya Jitambue (FAJI) ni Umoja wa Wananchi wa Tanzania wanaojishughulisha na maarifa ya utambuzi. FAJI ni Taasisi iliyosajiliwa Mwaka 2007 yenye namba ya Usajili 15579 chini ya Msajili wa Jumuiya, Wizara ya Mambo ya Ndani.
Utambuzi ni maarifa yanayolenga kumuwezesha mtu kubaini kuhusu yeye na yanayomzunguka ili aweze kukua, Kimwili, Kiakili, Kihisia na Kiroho. Kwa kuyapata maarifa hayo yanamuwezesha kuachana na mazoea yanayomuumiza na kuumiza wengine; kukabiliana na vikwazo, vurugu na changamoto mbalimbali za kimaisha; kufikiri vizuri, kujiamini, kuwa mbunifu, kufikia malengo yake na hivyo kujiletea mabadiliko katika maisha yake na maendeleo ya jamii kwa ujumla. Pia humfanya mtu awe na ufahamu yakinifu wa ubinadamu wake na hivyo kuweza kuishi maisha yenye Furaha, Amani, Utulivu na Upendo wa kweli. Kujifunza maarifa hayo huhitaji kuwa na sifa yoyote maalumu kama cheti cha shule, umri, jinsia, dini, imani nk. Kitu kikubwa ni uwezo wako wa kuyatekeleza unayojifunza kwa vitendo.
Kwa sasa FAJI inajishughulisha kusambaza maarifa hayo kupitia vyombo mbalimbali vya habari pamoja na Madarasa yaliyopo kwenye Kituo cha FAJI Kimara Rombo Dar es Salaam.
Maarifa haya pia yanatolewa kwa njia ya Semina kwenye Shule, Vyuo, Taasisi na Mashirika mbalimbali.
Baadhi ya mada zinazofundishwa ni:-
Namna ya kupata utajiri pamoja na mafanikio katika biashara, kiuchumi, kazini na shuleni; namna ya kujenga mahusiano mema kazini na upendo wa kweli katika ndoa, suluhu ya tendo la ndoa; namna ya kujiamini; kuondoa msongo wa mawazo, chuki, kijicho na hasira za ziada; kinga ya uchawi; namna ya kupata chochote utakacho maishani; kuondoa tabia sugu kama ulevi, uvutaji sigara n.k., kuondoa hofu na aibu, kupata afya nzuri kimwili kwa njia ya tiba mbadala, kufikiri vizuri, n.k.
Tunafundisha mada nyingi zaidi ya zilizotajwa hapo juu.
Kwa maelezo zaidi tafadhali wasiliana nasi kupitia:
Sanduku la barua namba 22040 Dar es Salaam. Simu namba 0652 626996, 0715 627003 au 0784771301 na 0713 250701, Email – faji.jopo@gmail.com au fika katika kituo cha FAJI kilichopo barabara ya Morogoro Kimara Rombo na utaliaona Jengo la Taasisi ya FAJI kulia kwako ukiwa unatokea Ubungo.
wakazi wa Mwanza darasalitakuwepo kabla mwaka huu haujamalizika, jiandikishe kwangu kupitia 0754 771 601
Monday, July 6, 2009
wajasiliamali wa bongo wanaigana!
ubunifu ni mdogo sana. yaani mtu anashindwa hata kuogeza vikolombweizo na kuwa na tofauti na mwenzie, kila bidhaa ni zile zile. kwa maneno mengine ukitembelea banda moja la wajasiliamali wa bongo huhitaji wenda kwingine kwani unakuwa umeona kila kitu ambacho labda ungekiona kwingine! duh
mimi ni mpenzi wa nguo za kiafrika, hakuna jipya! nguo zote zinafanana. nilipowatembelea wakenye, kidogo nikaona utafouti na mvuto. sikupiga picha labda ningekushirikisha kwa picha ukaona. ni lini wajasiliamali watakuwa wabunifu na kushindana vyema? mimi sijui na labda sitaki kujua saana.
ndo hayo
Thursday, July 2, 2009
Tumesahau na kuacha kazi iliyotuleta duniani.
makala haya niliwahi kuyaandika katika jarida la rai.......
Binadamu kama viumbe vingine kaletwa duniani kwa sababu maalum ili kukamilisha kazi maalumu ambayo maumbile (Mungu?) yalimtuma kuja kuifanya hapa duniani. Ndio maana kuna watu wenye vipawa na uwezo tofauti tofauti katika mazingira yetu tunayoyaishi. Kila mtu katumwa kuja kuitenda kazi fulani na akiimaliza, arudi au aondoke.
Wengi tumepotea na kupotoka na kuingia kwenye vitu vingine. Tumevamia kazi za wengine na kuishi kwa kuongozwa na tamaa kwa kuvutiwa zaidi na anasa za dunia hii. Mwili wetu wa hisia kwa kushirikiana na akili zilizojazwa mawazo hasi kuliko yale ya chanya, ndio umekuwa kiongozi wetu. Tunapenda kujionyesha, kujisifu, kujisikia na hivyo tunatawaliwa na matatizo ya kihaiba (ego) zaidi kuliko uhalisia wetu.
Mtoto akishinda mtihani au akipelekwa shuleni, haruhusiwi kusomea kile anachokipenda bali hulazimishwa na wazazi kusomea kile kilichowashinda wao au chenye sifa ili waje kujisifu jinsi walivyokuwa na kijana msomi wa fani fulani nzuri hata kama yeye haipendi na hivyo kumpotezea lengo lake la kutimiza kile kilichomleta duniani kufanya.
Maisha yetu yanazidi kuwa ya hovyo yasiyo na msimamo wala mwelekeo, ni bora liende tu kama vile tulikuja duniani kwa bahati mbaya vile!
Wanasiasa na viongozi mbali mbali wapo kwenye nafasi walizonazo ili wapate wao mradi au kwa sababu kunalipa japo yawezekana hawapendi kufanya kazi wanazozifanya. Hata wewe unayesoma hapa yawezekana hupendi kazi yako, unaifanya basi tu kwa sababu ulilazimika kuisomea au upate pesa. Hakuna binadamu aliyekuja duniani kutafuta pesa bali pesa ni matokeo ya kufanya vyema kazi zetu na hasa zilizotuleta.
Ndio maana tunaishi na jamii yenye uchungu, visasi na hasira kwa sababu kila mtu anachukia kila hali na mazingira ya kazi yake kwa sababu hakupaswa kufanya kazi hizo.
Ukichukia kazi yako kwa kujua au kwa kutokujua, basi ujue unajichukia wewe mwenyewe na huwezi kujipenda. Ndio maana wanasiasa wanajiongezea pesa na wengine kukumbwa na kashifa kibao za rushwa, ni kwa sababu waliingia kwenye kazi hizo kwa tamaa ya fedha na sio kwa upendo wao au kazi zilizowaleta duniani.
Wazee wetu wakizeeka tunawatafutia vijikazi ili wazeekee pale, je unategemea ufanisi hapa ua kuboronga kama tunavyoona? Sasa tunakaa penmbeni hata majukumu yetu tunawalaumu wengine kwa kutokuyatimiliza. Tunategemea misaada kutoka kwa wahisani na tunailalamikia serikali na kuitukana utadhani sio serikali yetu kumbe suruhuisho la matatizo yetu yamo ndani mwetu!
Hatuna budi kujikagua na kutafuta ni wapi tulipoteleza na kurekebisha mara moja. Yatubidi kudadisi na kujua kazi zilizotuleta duniani ili tuishi vyema kwa furaha na kwa faida ya jamii pana. Ndio maana wasanii wa miziki ya kizazi kipya wanaimba nyimbo za kimapenzi tu. Kwa sababu wao hawajazaliwa kuimba hata kama wanasauti nzuri na hivyo wanaimba tu kwa sababu wamepata nafasi ya kuimba. Waigizaji wa filamu nao hawana jipya. Ukiangalia filamu zao hazifanani na mazingira ya ‘Bongo’ na hivyo kuigiza sio kazi yao, ni kwa sababu wamejikuta huko au mazingira yamewalazimisha kuingia huko au hawana jinsi.
Tafuta kazi yako na uifanye vyema. Kazi yako ya kwanza iliyokuleta duniani ni malengo. Wanasema maisha ni malengo na kwa hiyo lazima ujiwekee malengo ya msingi na kuyafuata. Nasema malengo ya msingi kwani malengo mengine hayana maana. Kama lengo lako ni kujilimbikizia pesa au kupata utajiri mwingi basi iwe ni kwa kufanya mambo ya msingi na sio kupitia njia za panya kama kuingia madarakani kwa kununua kura nk kwani kufanya hivyo kutakusababishia matatizo ya shutuma, tuhuma, malalamiko na laana.
Basi lengo letu kubwa liwe ni kujua vipawa vyetu na kazi zilizotuleta duniani ili tuishi vyema na kwa furaha. Kumbuka kuwa lengo ni jambo lolote lile ambalo katika kulitimiza kwako unakuwa na furaha na kwa hiyo kama unataka pesa lakini unafanya kazi usiyoipenda, ni bora kuachana nayo na kufanya ile uipendayo ili uwe na ufanisi na ubunifu katika kazi yako.
Utajua kazi iliyokuleta kwa kuifanya, kuifikiria au kuona wengine wanaifanya. Ni kazi itakayokupatia furaha na ridhiko la kweli kila uifanyapo au uonapo wengine wanaifanya. Tusiogope sana vitisho vya dini zetu kwani dini zetu nyingi nazo zimevamiwa na watu ambao hawakupaswa kuziongoza na ndiyo maana vitisho vya kuingia motoni vinaongelewa zaidi kuliko uhakika, usalama na amani ya kuingia mbinguni (kiimani zaidi)
Niwakati wa kuitafuta na kuitumikia kazi iliyotuleta duniani. Sisi kama binadamu ni lazima tuwe na utu, upendo na amani ili tuweze kuheshimiana na kusaidiana vyema na kuishi maisha ya ukweli na uhalisia kuliko ya kufoji yenye mateso na lawama tele.
Ebu kila uamkapo asubuhi jipangie ni kazi gani utafanya na ni ipi unayoipenda na jioni kabla ya kulala angalia ni kwa kiasi gani umeitenda kazi hiyo na kujipongeza hata kama ujaimalizia kwa kujihaidi kuimaliza tena. Furaha ya kweliitaanzia hapo na malengo ya kweli na ya msingi utayatengeneza na hiyo itakuwa ni hatua nzuri ya kuwa na malengo nakubwa zaidi yatakayofanya kipato chako kuongezaka.
Tutafute sababu ya kuumbwa ketu na kuikamilisha. Tujenge moyo wa kujiamini kwani tukijidharau tutadharariwa ila tukijiamini, tutaaminika na kuishi vyema. Eti wewe ungependa ukishakufa (kwani ipo siku uataondoka tu) au ukiacha kazi yako au uwanasiasa wako, ukumbukwe kwa lipi? Tuhuma, uzembe, majungu unafiki au kusaidiana, heshima, umoja malengo nk? Kwa nini usikumbukwe kwa jambo zuri la kusaidia jamii? Unadhani akina Nyerere walifanya nini zaidi ya kuitumikia jamii kwa moyo, uadilifu, umoja na malengo?
Rudi kwenye kazi iliyokuleta duniani bwana.
Wednesday, July 1, 2009
umeoa / olewa?
|
Monday, June 29, 2009
unapolazimika kuficha kicwa, unaacha nguo......

Ukimfumania Nyani au ngedere shambani mwako badala ya kukimbia huwa anachukua vidole na kujificha uso akidhani humwoni kumba unaweza kumtungua utumbo ukumwagika woote nje! Duh
Kuna yule ndege maarufu akikuona anaficha kichwa mchangani na kuacha kiwiliwili nje akidhani kwa kuwa hukuoni basi na wewe humwoni na kwa hiyo utaendele kumbe anaogopa kufa anaona!
Sasa angalia huu ubunifu. Jamaa anaacha miguo yake michafu, anakimbia kuingia nyuma ya pazia kumbe kuna kijibwa chenye kiherehere. Imajini jamaa kaacha kila chake, harafu yuko mbele ya luteni Kanala ambaye kwa vyovyote ana mguu wa kuku! Duh sijui anafikiria nini hapa.
Walianza labda kwa kutaniana na kujikuwa sehemu za kusini kwa miili yao zinachekelea kwa misuguano na migogoro ya kelele zisizosemekana na kusahau kufunga mlango. Hapa wanatamani wasingejuana aka wanajuuuuuuta kujuana.
Je ungekuwa wewe mmoja wa hawa na hasa huyu nyuma ya pazia, ungefanyaji? Au iliwahi kukutokea? Unadhani ungekuwa hili lijamaa la manyota ungepata fundisho gani? Au ungepige mtu tu ili akukome?
Unataka kujua ningekuwa mimi ningefanyaje? Je huyo nyuma ya pazia akijulikana kuwa ni ndugu wa hili lenye manyota, au bosi wake au mwajiriwa wake, house boy je? Nini kiliendelea?
Mimi simo!
Friday, June 26, 2009
Michael Jackson alipata maumivu ya kihisia na kiakili akajikana

Nimesoma kwenye mtandao mmoja kwamba baba yake Jackson alipendendelea kumuita bignNose a.k.a puaKubwa. Bila shaka Jackson alibeba kichwani mwake kuwa pua lake ni libaya na labda ngozi yake ni mbaya na labda jinsia yake ni mbaya, nk nk. Hapo ndipo lilipotatizo la kutukana watoto wetu na kwa hiyo mike Jackson kujibadili rangi na kila kitu ilianzia kwa babake.
Mwalimu wangu wa maarifa ya utambuzi hayati Munga tehenan aliwahi kutembelewa na mtu mmoja akitaka ushauri kuwa afanya nini kwani alijiona mbaya na mwenye masikio mabaya saana. Munga akamwita mwanae aliyesoma darasa la saba wakati huo. Akamwambia amwangalie jamaa Yule kwa dakika kama mbili, na baadaye akamwambia unamwonaje? Motto akajibu ni mzuuri sana. Akamwuliza tena, na masikio yake Je? Mtoto akayaangalia masikio na kujibu ‘mbona mazuri sana kuliko hata ya kwako baba?’
Jamaa hakuamini, alipoulizwa kwanini alijiona vibaya, akajibu kuwa tangu azaliwe mamaye alikuwa akimtusi kuwa yeye ni mbaya, mjinga na hana akili. Mimasikio yake imekaa kama ya popo na matundu ya pua yake ni mabaaaya sana
Hivyo hivyo namdada mmoja alikuwa akitukanwa usukumani kwao kuwa ni mbaya. Akakutana na shangaziye jijini Dar, shangaziye akamsifia, kuwa ni mzuri, hakuamini na alipojalibu kuingia katika mashindano ya urembo na kupata nafasi ya juu. Yeye alijiona mbaya na kuambiwa kuwa wewe ni jinga na baya ni hatua ya kuizarau sipoweza kuziepuka.
Hata mimi ndugu msomaji, udogoni nilikuwa nikiambiwa kuwa mimi ni jeusi na baya kule shuleni. Jinga nyumbani na nina bichwa kubwa. Duh, kumbe sifai. Nilipoenda kusoma mjini moshi, nikashangaa na kujisikia vibaya kwani wacchaga (na hasa mabinti) walikuwa wakiniangalia kwa mshangao na kwa mud mrefu. Kwa hiyo kila niliposalimiana na mchaga kwa kusikana mikono, niliangalia rangi. Kono langu lilionekana jeusi kama mkaa mbele ya ule wa mchagga!
Duh nikaja kugundua baadaye kwamba kumbe wachaga walinipenda na walishangaa sana kuona rangi ya ngozi yangu. Kumbe hata kama ni mweusi, bado ninangozi nzuuri ya kuvutia nay a ajabu *(si unajua weusi wa kihaya) kumbe wachaga walinifuraia na kunipenda wakati nikijikana na kujiogopa. Ningekuwa Michael Jackson, ningejichubua kumbe najiharibu.
Hata wewe jikague, linganisha maneno uliyoambiwa udogoni na jinsi yanavyokuathiri saana maishani mwako, lakini pia kuwa makini na maneno unayowaambia watu na hasa watoto na wale walioko chini ya mamlaka yetu, yanaweza kuwaathiri maisha yao yoote na kujikuta tunawapoteza. Penda kuwa chanya a.k.a positive katika maneno na matendo uwatendeayo wengine, ni muhimusana. Mike aliharibiwa na baba yake bila baba kujua, kwa kumwita pua kubwa!
Thursday, June 25, 2009
Monday, June 22, 2009
Maisha yetu bongo na jamii yetu…
Bongo kuna shirika la TGNP, linapambana na matatizo ya kijinsia, kweli? Si mradi ule? Unadhani wanapenda kupunguza matatizo ya wanawake? Yakiisha watakula wapi? Angalia machapisho yao, mengi yameandikwa kwa kiingereza! Na picha zake zinaonyesha wale wanaopigwa na kunyanyaswa, hazionyeshi wale wanaoishi vyema na siri ya wema huo ili kiwe chanzo cha mabadiliko!
Kwenye mikutano yao wanawajaza hasira wamama! Hivi mtu ambaye hajajitambua anaweza kweli kushinda matatizo ya kijisinsia? Shirika la kupigania wamama wa Tanzania linatoa machapisho kwa kizungu. Lipo mtandaoni, linajulikana kwa wato wa nje (watoa pesa aka donors kuliko walengwa). Machapisho ndo hivyo ya kizungu kwani si donor anajua kizungu?
Wanaonesha matatizo na sababu ya kuendelea kupewa pesa badala ya kumaliza tatizo. Liishe ili? Kila mtu ni mradi. Wajanja wanatumia matatizo yawengine kuwa miradi kuna mashirika kibao ya vijana, wafungwa, wazee, wagonjwa nk.
Yanajulikana zaidi kwa wenye fedha kuliko walengwa. DUH inatisha, wajanja wameshatufanya miradi yao, wanafanikiwa pia. Ni maisha ya Bongo. Kila kitu kina milikiwa na kina wenye nacho.
Tamaa zatuongoza. Kila mtu anatamani mke, wake waume nyumba, magari nk. Bongo ni kulewa na kukimbizana. Sisi ni masikini, hatuna kitu. Tunalia tunajiendea tu
Vijana wanatafuta nafasi za kwenda nje kusoma, na kufanya utumwa, wanaita green pastures! Ni maisha ya bongo, watoto wa mitaani wanaongezeka, wanajilea, wanapigwa tu. Hupigwa na jua, mvua, baridi, joto, mawe, wapiti njia na hata miti. Hawajawahi kupendwa, hawajui kupendwa, wakiwa wakubwa itakuwaje? Ni bora ufe wapate sh 500 kuliko kuishi wakaikosa.
Ni maisha ya bongo, ni utanda wazi, ni diri za miradi! Kila mtu sasa diri. Kuna mradi unaokufanana unaendelea. Vijana wanaamini kutika imani za ajabu kupata utajiri. Dini zipo na vitisho zinavyojua kupeleka watu mbinguni wakati duh? Tungekuwa na dini matatizo yangeongezeka hivi?
Bongo, bOngo, boNgo, bonGo, bongO ni maisha ya BONGO ndani ya ugiligili na ubeuzi
Sunday, June 21, 2009
maisha ya Bongo.... --4
sasa tuangalia juu ya kinachoitwa vita ya kijinsia. eti mwanamke ananyanyaswa na kuna watu wanapigania kinachoitwa haki sawa, eti kumtetea mwanamke asinyanyaswem wanataka mwanamke awe kama mwanamume, naye afanye kazi kama afanyazo mwanamume.
unaweza kujiuliza bila jibu kuwa; haki za mwanamke ni kuwa kama mwanamume au zimeshikiliwa na huyo mwanamume? sasa mambo yamebadilika, mwanamke anafanya kazi kufukuzia ela ili aheshimiwe na mwanaume hivyo hivyo, watoto wanajilea kupitia house girl kwa kusaidiana na TV, ndo hilo taifa la hovyo linajengwa
vita ya kijinsia inapamba moto, mitandao kama TGNP inaangahika kutetea haki za wanawake, inawashauri waachane na mijianaume ya hovyo, mama anatii, unakuwa mwanzo wa watoto wasio na baba wala wazazi,. baada ya kutoka kwenye ndoa, mwanamke anagundua sio suruhu ya matatizo, anatamani kurudi, Mume alishaoa tena, ni matatizo juu ya matatizo kumbe yawezekana tatizo sio mwanaume.
tunaishi tu, tumeoana bila elimu yoyote juu ya ndoa wala tendo la ngono. mambo ni hovyo, haielewiki hatuelewani. maisha ya bongo yamejaa simanzi na majuto ya hapa na pale. tunajiendea hovyo. fumanizi ni nyingi. watu wanajaribu kuonja radha tofuti, kumbe si suruhu pia. ni ndoa Bongo ni maisha ya vijana wa bongo; yamepoteza maana, yamepoteza uhalisia, ni hovyo, ni vurugu kwa kwenda mbele!
Friday, June 19, 2009
maisha ya Bongo, vijana wa bongo maisha yetu duh-3

Wednesday, June 17, 2009
maisha ya Bongo, vijana wa Bongo - 2

naendelea kuyaangazia maisha ya wabongo na ya vijana wa Bongo
maisha ya vijana wa bongo walioko mashuleni na vyuoni ndo mawee? ukimuuliza kijana anayesoma kuwa anapenda kusomea nini atakwambia kozi yoyote au kozi fulani kama vilie uhasibu. ukimuuliza kwa nini uhasibu atakwambia kuwa una ajira nyingi> duh ikiwa na maana kuwa yeye alikuja duniani kufuanya chochote au kutafuta pesa ili ale anywe ashibe na afanye ngono!
kacha! akimaliza shule ajira ndo hivyo, anakaa kijiweni, maisha ya shule ndo hivyo, hayakuwa na muelekeo. alifukuzwa, alikula mlo mmoja nk. akiingia kazini sasa basi, ni pesa, ni rushwa ni lawama. atatembelea viwanja vyote as if duh, aliishi ili vimkome. ukimpa uongozi ndo rushwa tu si alisomea msosi?
kijana anatanga tanga mitaani, akikutana na wanaofanya kazi wanamtishia na kumpiga mkwara kuwa hakuna kazi au akushinda vizuri. kijana msomi wa bongo sio mbunifu, anatafuta ajira! kah! inauma!!!! yupo yupo. anatamani gari, ndoa na maisha yoyote. ni mlevi, mulokole na ni mbahatishaji.!
kanicosha kijana wa bongo, mawazo yake duh
Tuesday, June 16, 2009
maisha ya Bongo, vijana wa bongo maisha yetu duh-1

Monday, June 15, 2009
mipira yetu, ngumi na haira badala ya raha


ndg,
angalia hizo picha mbili, majamaa wanasaidiana kuruka ukuta ili wakaangalie mpira, harafu wakiisha kuwa ndani basi ni ubabe kwa kwenda mbele. sasa angalia hiyo picha ya chini mijamaa inapimana nguvu.
udogoni nilishabikia saana mpira. mpaka nakuwa kijana niliitwa Jonas Lunyamila (jina la mchezaji wa yanga) na baadaye nikaitwa davd becham kwa sababu nilicheza namba saba. nashangaa kwanini nilioewa majina wa wachezaji wakubwa namna hiyo wakati mpira ulikuwa haupandi! nilikuwa nikiingia uwanjani dakika za mwisho au kujaza tu pengo!
ningeweza kujifunga au kuacha mpira nikakimbia mbiyoooo kama vile nina mpira! duh, asikwambie mtu.
basi ukubwani nilipunguza hiyo hamu ya mpira. miaka yoote niliyokaa Dar sijawahi kuingia uwanja wa Taifa zaidi ya kupita kwa nje nielekeapo mbagara rangi tatu. kilichonikatisha tamaa ni baada ya kusikia story za kutisha kuhusu utazamaji.
eti ukikaa upande wa simba, yanga ikafunga ukashangilia, unatwangwa mkanda! mara majamaa wanakujoa kwenye chupa ya maji na kukurushia! duh mara nini. sasa angalia hao wanavyokamatana mashati
Saturday, June 13, 2009
Thursday, June 11, 2009
Turudi kwa wakristo na msalaba.
Unajua toka nikiwa mdogo ilipenda sana utafiti. Na ndio maana ninablog kwani inanisaidia kujua mengi na kuwajulisha mengi wengine. Udogoni nilipouliza maswali ya kutaka kujua zaidi hasa juu ya dini nilikwidwa. Kwa mfano kuna siku tulienda kanisani kumwomba mungu atulinde dhidi ya wezi wa usiku, kesho yake kanisa tuliliosalia likavyunjwa na kuibwa viyoo na milango, nilipouliza juu ya huyu mungu asiyelinda kanisa atatulindaje sisi? Nikajibiwa eh? Unasemaje
Nikadhani sikueleweka nikauliza tena, mbona kanisa tusaliamo limeibiwa sasa tutakuwaje na usalama?
We!! Nilisikia kofi nikadhani ni muujiza na lundo la fimbo, kisa? Nimekufuru na nisipotubu nitaenda motoni. Ningekuwa nimepata kipaimara basi ningezuiwa kushiriki mpaka chini ya marudi, we?
Tuyaache hayo. Swali langu la wakristo kuutukuza msala na kuufanyia biashara limepanuka na labda kujibiwa. Gazeti moja linaonyesha ushahidi kuwa hapo kale warumi walinyanyasa watu na kuwatundika kwenye mti imara ulionyooka na sio msalaba. Linasema msalaba ni ishara ya kumtukuza Mungu wa uzazi wa enzi za mababiloni na sio kweli kuwa alitundikwa Yesu bali yesu alitundikwa kwenye mti mmoja ulioonyooka kwani wanasema biblia ya kigiriki inasema tauros likinaanisha mti mmoja na sio msalaba kama tudanganywavyo
Linauliza swali juu ya kuutukuza msalaba kuwa kama nduguyo kapigwa na rungu kichwani na kufa, utapenda kuchukua rungu hiyo kama ukumbusho? Je utaiigiriza na kutoa nyingine kama hizo na kuwsambazia nduguzo wote ili muutuze kama ukumbusho wa hasira na kifo au mtautupilia mbali kupunguza hisia kali?
Ukiangalia siku hizi misalaba ni dili namingine ni ya dhahabu na bei juu. Mingine inauzwa bei kali na inaabudiwa kuliko hata Yesu mwenyewe namafundisho yake, je wewe unafikiri vipi juu ya Mungu wa kibabiloni na alama zake? sijiui
Wednesday, June 10, 2009
nyimbo hii nazo
Sikiri mimi masikini uvivu wangu nyumbaani,
ukiwa huunjiana nakufa hapa kwa nini
sadiki sasa ashiiba chakula kingi kwa baba
nirudi tena kwa baba nakufa hapa kwa nini
naombaradhi nimekoosa ntakuwa mtoto mwema sasa
nitakuwa kama sadiki
na nyumbani tena sitooki baba na mamanisameeni
twapenda mambo yoote ya shule kabisa
kujua kusooomatwaona furaha
hhhA hhhE hhhI hhhO hhhU
twaimbavyema leo..
ongeza nyinine basi na wewe. hii inaitwa short break
Monday, June 8, 2009
furaha nini na iko wapi?
katika ulimwengu huu tunaoishi, mwanadamu amehangahika na anaendelea kuhangahika akaiitafuta furaha, amani na upendo wa kweli. katika hilo, kwa kutumia akili zake, binadamu ameishia kutengeneza matatiizo lukuki yasiyoongeleka.
je wewe unajua furaha ni nini na inapatikana wapi? amani ya kweli na upendo je?
tunafananisha furaha na vitu vya duniani kama vile fedha, utajiri, majumba magari nk, lakini wenyenavyo nao hawana furaha wala amani. wanajifungia jera kwa kulinda mali zao hizo. je furaha ya kweli iko wapi sasa? na mamani je?
hata kwenye nyumba za ibada ni vita. mitaani mamamaa, baa duh. elimu ndo maweee, utawala wakisiasa nk. wengine wamekuwa wachawi, ulevi nao ndo hhuo lakini mwisho wa yote nimateso.
waafrika tunatafuta utajiri japo nchi tajiri watu wanaongoza kwa kujiua kisa? hawaoni maana ya maishi hata kwa kuzunguwa na utajiri. je waafrika tunaishi maisha yenye maana zaidi? furaha inakaa wapi lakini?
Obama anatafuta amani ya dunia huku akiwa na siraha kali na jeshi kubwa, kamwe hawezi kuipata. tumeshindwa kujua kuwa furaha na amani ya kweli vimo ndani mwetu. tunasahau msemo wa bible kuwa amani ya Mungu ipitayo uelewa woote......
vijana wanapiga miziki yamapenzi na kutogozana, wanaishia kuchanganyikiwa na kuuwana kama sio kubadili wachumba na kupata ukimwi
Je Unafurahi kwa kusoma hap?
ukijani huuu
Thursday, June 4, 2009
sara na maombi, je wewe unaombaga?

Sijui cha kupost nini maana nimebanwa na shughuli za kidunia vya kutosha sana. Japo tunasubilia majibu ya yasinta juu ya incarnation. Tuna kiporo cha meditation lakini duh, mambo magumu.\
Labda tuongelee juu ya sala. Eti sala au maombi ninini? Kwa nini watu huomba? Tofauti kati ya prayer / praying ndo ipi? Je unaamini juu ya nguvu ya maombi kwamba yaweza kuamisha milima? Kama ndio, wewe uliwahi kuombea nini kisicho cha kawaida na kikawa? Je ni kwanini sala au maombi ya wengi huwa hayafiki au hayajibiwi? Lakini ni kweli kuwa hayajibiwi?
Kwani wewe huwa unasali au kuomba? Je inabidi tusalie na kuombea wapi na wakati gani kwa kuelekea wapi? Kwanini kuna wanaoomba vijisanamu kama wakatoliki vile?
Jibu kadri ya majibu uliyonayo
Monday, June 1, 2009
Tuangalie juu ya re-incarnation
Maumbile (Mungu?) yaliumba mara moja. Ni siku ya uumbaji pekee ndipo kila kitu kilipoumbwa. Hakuna kazi nyingine ya kuumba iliyofanyika baadaye kama unaamini katika uumbaji kwani hata vitabu vitakatifu vinatwambia hilo.
Basi bwana, mimi nimekuwa nikiamini juu ya hilo na ninaamini kuwa niliwahi kuishi sehemu fulani kabla ya kuzaliwa tena leo nikiwa mhaya wa bukoba. Nimekuwa nikihoji watu wengi juu ya hili, wengi ukiri kuwa walipokuwa wadogo waliwahi kufikiria juu ya watu kuzaliwa pahala na kuzaliwa tena. Yanakumbukwa udogoni labda kutokana na kuwa na kumbukumbu ya tulipotoka.
Semina ya utambuzi pale FAJI, mwanafunzi mmoja alifundishwa meditation na hypnosis, kesho yake alitwambia kuwa alifanya hivyo akarudi nyuma na kuwaona wazazi wake wakifanya ile ngono iliyomleta yeye duniani! Hii inadhihirisha kuwa sisi ni zaidi ya miili na hatuna mahala pamoja.
Ilitokea nchini India, mtoto wa miaka kama 15 akafariki kwa ajali ya baiskieli na baadaye akazaliwa mtoto katika familia ya jirani, ajabu mtoto huyo alianza kuongelea juu ya ajali hiyo na alivyokufa! Mtoto huyo alianza kudai hata nguo zake za zamani kwani walizivaa wale waliokuwa wadogo zake kabla hajafa. Alisema jina lake alilotumia nk, nk.
Sasa katika TV show moja ya Oprah mmalekani, alionyesha dakatri mmoja nchini humo akiwa-hypnotize watu na kuwafanyia regression mmoja aliongea kichina, alipoletwa mkalimani, akasema huyu jamaa anajiona akiwa china sijui na watu gani hivi. Mwingine ni mwanamama naye ni mmarekani, alianza kuonge lugha ya majamaa wa Nepal, akaletwa makalimani.
Mama yule alijiona akiwa nchini Nepal kijiji fulani akiuza gengeni kwenye soko moja. Ili kujua kama ni kweli, wakasafiri kwenda Nepal. Wakauwauliza wenyeji wa mji ule juu ya uwezekano wa kuwepo soko na kila kitu. Wakapelekwa kwa mbabu mmoja. Mbabu yule alikubali kuwa enzi zili lilikuwepo soko na mambo kadhaa aliyoyasema yule mama.
Na Mzungu mwingine alienda nchini Mali, alipofika eneo fualani akahisi kama anapafahamu vile kama ndo kwao vile NK. Je wewe unaamini katika re-incarnation? Kumbuka sisi ni zaidi ya mwili na hivyo ni kweli kuwa tulikuwepo, tupo na tutakuwepo. Sio swala la imani bali la kisayansi. Kama unataka kujua uliishi vipi na wapi kabla ya kuishi kwenye mwili wako wa sasa, nendo kwa ma-hypnotist au tuwasiliane na kupeana tekiniki za hypnosisi. Sio imani bali ni ukweli na ni uhalisia.
Hiyo ndiyo proof kwamba binadamu wote ni kitu kimoja na sisi sote ni wa moja. Hata mitume kama Kristo ukisoma utagundua kuwa aliwahi kuishi kama watu fulani na baada ya kufa, nguvu yake ikaingia kwa petro na baadaye kwa Paul au Sauli. Mpaka sasa yupo ila hatumwoni kwa sababu tunamtafuta kwa macho, kiburi na ujuaji, ukitulia utamwona.
Je wewe utakufa au unataka kufa au kuishi milele?
Thursday, May 28, 2009
mbibi akisubilia mambo


mnamuona alivyompole, kuna jamaa kavaa 'vyeupe' anataka kumkabidhi kachakula fulani ka baada ya kipaimara. sasa nami naingia msituni ili nikue kiroho usiponiona hapa siku mbili tatu ujue sijakususa niko msituni, hija, polini natafuta kukua zaidi na zaidi au sio?
nakumbuka enzi hizo wanakuja kwetu kumlisha bibi kamkate hako, duh nilidhani kanatokea mbinguni
Tuesday, May 26, 2009
Nyegerage waitu! Amana vijana senta, byalimana
Utaratibu wa kunyoa nimeutelekeza kwa Muda. Kila nikienda saluni mashine zinawasha na muda unabana lakini pia nimeachana na mashindano ya kunyoa leo kesho zinaota. Kwa hiyo Markus aliona kama naelekeana na picha kwenye blog lakini akakaa kimya. Nilipomwambia kuwa ndiye Mimi mwenyewe, basi alishutuka, alifurahi na kunikumbatia. Tuliongea kwa Muda mfupi na akahaidi kukwambia na wewe kuwa tumeonana.
Mpangala aliniuliza, lilli neno Nyegerage linamaana gani? Nikajua ameshawaza sauzi Africa ya nguoni!. Basi nikafikiri na wewe una hofu na neno hili si unajua linafanana na yale ya kuamsha waliolala? Basi leo mambo yanabwagwa hadharani.
Neno Nyegerage linatokana na neno la Kihaya a.k.a kikwetu, Nyegera, Lenye maana ya karibu na nyegerage ni karibuni sana, huwa wanasema nyegerage mugile akanyeto wakimaanisha njoo kwa kwa madaha mmeshafika, karibuni. Hiyo ndiyo maana yenyewe.
Basi bwana, ukiwa maeneo ya Ilala to Buguruni, kuna kituo kinaitwa AMANA. Duh! Ili neno amana kule kwetu ukilitamka wanakushangaa kwani halitamkwigi hadharani. Kwetu ukisema amana ni kuongelea pale njiani ulipopitia kuingilia duniani a.k.a kuzaliwa. Basi usimwambie mhaya ashuke amana, atakuchapa makofi na kukushitaki, atakuuliza; wangambila nshuke amana? Olifakubi iwe kyana!
Basi bwana neno amana halitamkwi bukoba (buhaya) kwani ni tusi a.k.a siri wakati Rwanda wana neno Imana, neno hila hufanana lile la kihaya la kituo cha basi Amana japo kwao ndo jina la Mungu. Wanyaranda huita majina ya Byalimana wakimaanisha yote kwa Mungu lakini jina hili likitamkwa, wahaya huinama na kucheka kinoma eti kwao linamaanisha vimekula ile njia ielekeayo duniani kutoka mimbani! Duh basi kama wewe unaitwa byalimana, ukitambulishwa kule Bukoba, utaona majamaa yanakukaribisha kwa furaha na vicheko, usidhana yanakufurahia, yanakucheka ile mbaaaya kwa chakula hicho.
Hiyo ndiyo maana ya neno Nyegerage, karibuni sana. Kikwenu inamaana gani?
Monday, May 25, 2009
Tahajudi na wengine huita taamuli basi sisi tuiite meditation.
mdada kama huyu waweza dhanimkosawa kumbe labda ashapasua hanga yuko kama mbingu ya nane hivi kwa mjuao spiritual planesSwali hili lina maana kuwa amani ya kweli imo ndani mwako na hakuna awezaye kukupa wala kukunyanganya amani hiyo japo wengi hatuna na tunaitafuta kwa wenzetu na kamwe hatutaipata Utulivu wa akili kwa kiingereza wanasema ni peace of mind ndio utuletea amani ya roho na nyinginezo.
Kwa njia ya tahajudi na meditation utapata amani. Inasemekana nusu ya wakazi wa Dar ni nusu-vichaa kwa sababu ya kutokutulia wala kupata muda wa kulala vya kutosha. Wengi hushinda barbarani, kwenye daladala na ukiwa nyumbani kamwe huna utulivu. Usiposikia kelele za majirani basi utasikia mtoto akilia au gari likipiga honi au kelele za mwizi angalau jirani yako kafungulia redio hiyoooooo.
Ukifuatailia kwa miaka kadhaa wewe mkazi wa Bongo hujawahi kuwa Kimya bali unashinda kwenye kelele na hivyo huwezi kuisikia asili ikikuliwaza. (nature au Mungu)
Ni lazima tuwe na utaratibu wa kukaa mahali patulivu na kujiambia maneno yenye furaha naya kututia amani. Kwa mfano waweza kuandaa neno au kikundi cha maneno wengine huita mantra na kukirudia rudia. Kwa mfano; Amani, upendo mafanikio. Kaa mahali penye ukimya peke yako pasipo kuongea na mtu, fumba macho au angalia upande mmoja tu kama vile pembe, picha, kiti, nk.
Kaa zaidi ya muda wa nusu saa na ukiweza masaa ukirudia maneno hayo bila kusikiliza kelele za nje au kufikiria kitu kingine. Baada ya muda ukimaliza utajisikia amani, furaha na upendo wa kutosha. Ni vyema kufanya hivi kabla ya kulala na baada ya kuamuka kabla ya kuondoka kitandani.
Kaa jiambie unataka siku yako ienende vipi au kaa kumbuka yoote uliyoyafanya siku nzima kabla ya kulala na kujisifia kuwa umeweza kuyafanya yale uliyoyafanya kisha lala. Utapata amani ya kutosha nakwambia. Ni vyema kufanya meditation kwa masaa zaidi ya mawili lakini kwa kuanza, anza na nusu saa tu.
ONYO!!! Usiinuke haraka baada ya meditation. Kaa kidogo kama dakika tano kwani kuinuka ghafra sio vyema sana.
Kama wewe ni mtu wa dini basi waweza kuunda maneno au mantra inayoendana na dini yako lakini chunga kujiambia yale usiyoyapenda au mabaya. Kwa mfano usijiambie au kumwambia Mungu wako ulivyokuwa mtenda dhambi,no! kwani utazitenda kweli. Jiambie meneno kama, Yesu nakupenda, au nataka nimwone Yesu au Yesu kimbilio
langu au Mungu ni mkubwa.
Kwa waisilamu tumia kama ile ya ALLAH AKBAR nk.
Rudia rudi maneno haya kwa Muda mrefu na kwa utulivu. Huu sio muujiza kwani utaoona matokeo yake kila umalizapo kuyasema, utaondoa kelele kichwani mwako na kuwa na amani. Kichwa chako kina kelele ndio maana hata ukiwa peke yako utulii. Utasoma gazeti, utafugulia redio, utaenda kijiweni kuongea na washikaji au utamkaribisha mgeni lakini ukiwa na utulivu yote sawa.
Meditation ijaribu sio imani wala kusubili kufurahi baada ya kifo, ni uhalisia
Ifuatayo tutaona juu ya kuvuta vitu vizuri kwa njia ya meditation.
.
Sunday, May 24, 2009
kchimba dawa nako
ujumbe wa jumapili tundugumpendwa
Thursday, May 21, 2009
kwa nini wakristo hujiita wana wa ISRAEL?
kwa maana hiyo kumbe na wewe unaweza kuwa mu-Israel na usichangaye kutembea katika sheria ya Mungu na hofu juu ya Mungu kwani kumbuka Mungu ni upendo na sio vitisho vya kuogopwa. basi ndiyo maana wakristo huongela mbingu mpya na nchi mpya (yerusalemu mpya) sio mashariki ya kati plz. mbingu mpya ni pale utakapo mgundua Mungu wa ndani yako esp. kwa njia ya tahajudi (meditation) na kupata 'connection' na kuishi ukiwa connected na ile mbingu mpya (ndani mwako) ikitoka nje yako basi hiyo ndiyo nchi mpya (yerusalemu mpya) mwisho wa dunia ni pale tutakapo pata na kuishi katika uwepo wa Mungu (devine connectio) ambapo mwili wa akili (mind) utashindwa na kutawaliwa na mwili wa roho.
hapo hakutakuwepo na jambo baya wala zuri. kila jambo litakuwa ni jema kama biblia inavyosema kuwa alipomaliza kuumba, Mungu alsema yoooote ni mema japo mwanadamu akataka kujua mabaya kwa kula mti wa uelewa, akayajua mabaya mpaka leo yanampeleka puta. zambi tano za kifo ndo zinatawala; tamaa, hasira/visasi, ujuaji/ubinafsi, attachment, uchoyo na matatizo ya kiaiba (ego) mwisho wa dunia undugu, utaifa, ubaguzi wa rangi, mataba nk vitaisha kwani binadamu ataona ukweli kuwa woote tu wamoja tukiunganishwa na Mungu na Mungu ni mmoja na sote ni ndugu.
ndipo tutakapothamini viumbe na kuwa kitu kimoja, tutaishi kwa kumtukuza Mungu, tutaimba, tutasifu, tutawapenda wenzetu. ujinga wa kutengeneza siraha utaisha tutaingia kwenye ukweli halisi nayo hiyo kweli itatuweka huru. waubiri wenye kuombea watu wapate wake/waume, utajiri, vyeo nk watapukutika na tutakuwa na lengo la kumtukuza Mungu. upendo utaongezeka, amani ndo basi nk. hiyo ndiyo Yerusalemu mpya, mwili wako utakapotumika kama hekalu la Mungu badala ya kuwa karakana la kutoa mawazo, maneno na matendo mabaya.
yerusalemu mpya sio ile wanayopigwa wapalestina ili ijengwa, bali ni ile utakapofika mbingu mpya moyoni mwako na mbingu hiyo ikijidhiirisha kwa nje, basi hiyo ndiyo nchi mpya, itakuwa raha mustarehe, raha kuliko zile uziitazo raha. sihubiri wandugu, najaribu tu kuelezea maaana ya jina Israel na kuwa taifa teule la MUNGU aka NGUVU KUU aka SUPREME BEING aka UNMOVABLE MOVER aka THE ONE nk nk nk.
je unatamani kwenda yerusalemu wewe?
Wednesday, May 20, 2009
Fascinating Rwanda
Rwanda is a beautiful country. Infrastructure has been improved significantly for the past 15 years. You cannot imagine that it was in massive massacres before. Love is a predominant feature you will find among Rwandans.
Among ”fascinating” things I have discovered in some Rwandans, probably peculiar in the world are:
People can request a lift on commercial public transport and accepted, like city buses. When you hire a taxi, don’t be surprised people to come to your taxi driver and ask a lift while you are ignored, and of course a driver will offer them a lift without your permission despite that you will be the one paying (it happened to me more than once).
Some bank clerk can spend more than 30 minutes attending one client with simple transactions which at home hardly takes 5 minutes, and yet other clients don’t complain, but I was told that according to Rwandan traditional values “it is bad to complain”!!!
If you meet somebody whether you know him/her or you don’t, the greetings has to be by handshake, if you don’t, it signify hatred, and if someone you know him/her very well, then you must hague and gives each other three kisses on cheeks. Don’t be surprised if your way is blocked by friends when they meet along the road and greet each other, just pray they will not be more than 5, as all have to be treated the same way. Aye, greetings can take even 5 minutes or more if the group is big, even in the middle of supermarket, just find your way outer there otherwise......
Now, there are several workshop conducted to different firms especially those dealing with customers to improve hospitality and customer care.
Monday, May 18, 2009
wakazi wa Dar wanaisha kwenye magari na vituoni!
nikiongea na jaamaa yangu aishiye mbezi bich na kufanya kazi posta, aliniambia
kuwa kila siku huamka saa kumi asubuhi na kupanda basi saa kumi namoja na nusu asubuhi. hufika posta saa mbili kasoro. basi jamaa huyo hutoka kazini na kupanda gari saa kumi na moja na kufika saambili na nusu au tatu nyumbani!! ukipiga hesabu jumla, jamaa huyu anakaa kwenye dala dala zaidi ya masaa sita kila siku!!
duh, unashangaa! ama wewe ni mwanafunzi ndo maweeeeeee. saa kumi namoja upo kituoni daladala zinakuepuka kama mafua ya nguruwe. unakaa masaa lukuki na ukipanda ndo foleni kurudi hivyo hivyo! DUH
basi bwana, stori sio nyingi, kwa foleni za dar, watanzaniawaishio dar tunaishi kwenye dala dala na wengine kulala kwenye magari binafsi, kuna haja ya kujenga, kupanda na kununu nyumba nzuri wakati wanaishi ma-hausi gelo tu?
ndio maana washikaji wanaotamani kuhamia dar huwa nawashangaa na nashidwa kuwashauri, japo mimi naonekana bonge la chiiiizi kupanga kuhama dar! mh, niishi kwenye dala dala tena kwa kushika bomba au kwenye gari binafsi? duh.
Saturday, May 16, 2009
vijana wana umhuhimu gani katika mabadiliko ya kiuchumi na kisiasa?
basi nipatieni japo yako maoni juu ya nafasi/umhuhimu wa vijan katika mabadiliko ya kijamii-kisiasa na kiuchumi "the role of the youth in socio-political and economic transformation".
nataka iwe pepa itakayobadilisha watu, vijana na sera za mataifa ya africa na kwa hiyo ni kazi kubwa naomba maoni yako. nitaiwasilisha pale IFM kwa njia ya video conference mwezi ujao na wewe nitakualika rasmi tuwe wote. ni mkutano utakaounganisha matifa zaidi ya saba ya kiafrika ikiwemo Tanzania, Uganda, Ghana, Ethiopian, Kenya, Madagascar, Zimbabwe, na afrika ya kusini
naomba maoni yako bwana si unajua tenaaaaaaa
Thursday, May 14, 2009
Wednesday, May 13, 2009
Tuesday, May 12, 2009
kuchapa viboko, moja na moja ni moja,
Kamala, nilichapwa hizo fimbo nikingali mdogo (nyumbani) na zilizidi nilipoingia shule hadi darasa la sita!
Leo hii nakubaliana nawe kuwa hiyo tandikwa tandikwa sio njia ya kufundisha watoto wetu. Na hata kwa wafungwa nayo haisaidii!
Nimevutwa na hilo la mantiki ya hesabu (moja ongeza moja ni moja).
Mantiki hii nimeitumia katika makala moja, niliyokwisha andika...lakini bado kuchapishwa... kuhusu demokrasia yetu nchini.
Hususan, nimeitumia katika mkitadha wa kujaribu kusuluhisha au kutafuta muafaka miongoni mwa sehemu za Muungano (Tanzania Bara na Tanzania Visiwa)...Napenda kuiita Tanzania Visiwa na wala si Visiwani, kama vile tunavyoiita Tanzania Bara na wala si Tanzania Barani!
Kwahiyo, niruhusu niiendeleze hesabu hiyo, ki-siasa:
Akingali hai, Mwenyekiti wa CCM Mwalimu Julius Nyerere alilikemea kwa ukali pendekezo la kuunda federesheni na serikali zake tatu, yaani, Serikali ya Tanzania Bara, Serikali ya Tanzania Visiwa na Serikali ya Muungano.
Mwalimu Nyerere alidhihirisha kwa mantiki yake kwa hesabu za vitu-guswa (au vitu-onekana).
Ni hesabu ya mwanzo kabisa: moja ongeza moja ni mbili. Nyerere alikataa kata ya kukubali: moja ongeza moja ni tatu!
Mpaka sasa tunaamini kuwa jumla hiyo ya moja ongeza moja ni mbili ni kweli kila mara bila kujali mikitadha! Ndio maana hata Mwalimu Nyerere alikazania kuwepo kwa serikali mbili tu.
Mimi binafsi si mtaalamu wa hesabu – somo lililokuwa likinipa ushindi wa chini shuleni.
Naafiki na Mwalimu Nyerere kwa dhati kwamba katika mikitadha ya hesabu/nambari za vitu-guswa au vitu-onekana viwili: moja ongeza moja ni mbili.
Lakini si kweli hata kidogo katika mikitadha mingine!
Kwahiyo, ninahitilafiana na Mwalimu Nyerere kwa kufikiria kuwa Tanganyika na Zanzibar ni vitu-guswa au vitu-onekana!
Tanganyika na Zanzibar sio chungwa au embe, ambayo chungwa moja ongeza chungwa moja ni machungwa mawili ua embe moja ongeza embe moja ni maembe mawili!
Tanganyika na Zanzibar ni ideas. Na mantiki yake ni ya moja ongeza moja ni moja!
Na hii iko sawa pia kwa vitu-onekana vyenye uwezekano wa kuunganishwa, kwa mfano, majumba. Majumba mawili yakiunganishwa, linakuwa ni jumba moja tu kubwa).
Nitatoa mifano miwili kudhihirisha mantiki hii ya moja ongeza moja ni moja kutoka katika Biblia. Mifano hii ni kati ya vitovu vya imani ya wa-Kristu:
Mfano 1: Mwanzo 2:24 na Marko 10:7 tunaambiwa kuwa mwanaume na mwanamke wakioana wanatekeleza idea ya ndoa inayovuka mikitadha ya vitu-guswa au vitu-onekana viwili (mwanaume na mwanamke)!
Cha maana kinakuwa ni ndoa; ni mkataba. Na mkataba wa ndoa, kama ilivyo mkataba wowote, hauvunjwi hovyo hovyo! Wawili hao wanafikiriwa kuwa kitu kimoja.
Kwahiyo, tunaweza kutamati kuwa ndoa ya ki-Biblia inauminisha kuwa moja ongeza moja ni moja!
Kwa waliooana, kama kila mmoja atajiona kwamba moja ongeza moja ni mbili, basi mtafaruki utaanza na kuleteleza kutengana, kuachana na kuvunjika kabisa kwa ndoa yenyewe, hatimaye.
Matokeo yake yatakuwa kwa hao wawili kubakia ya moja ongeza moja ni mbili!
Mfano 2: Kwa kifupi, imani ya ki-Biblia inawaasa waumini kuwa kuna Mungu mmoja tu ingawa kuna Mungu Baba, Mungu Mwana na Roho Mtakatifu (Utatu Mtakatifu).
Kwahiyo, mfano huu ni sawa na kusema moja ongeza moja, ongeza moja na ongeza moja ni moja na wala si tatu!
Tuingie ya kwetu hapa - ya ki-dunia - kwa kutoa mifano minne:
Mfano 1: Bila kujali ukubwa, eneo, uzito, ujazo, na kadhalika, tuangalie ya vimiminiko au dabwadabwa, kwa mifano, matone ya kahawa, lubisi, kangara, ulanzi, maji, maziwa, chai, asali au damu (hakuna cha ushirikina hapa), na kadhalika.
Ukidondosha tone moja la kahawa juu ya karatasi au chombo kingine, halafu uongeze tone la pili juu ya la kwanza, huwezi kuona matone mawili; utaona tone moja tu kubwa kwa vipimo vyake.
Na unaweza kuongeza tone la tatu au la nne huwezi kuona matone matatu au manne ya kahawa! Utaona tone moja tu kubwa kwa vipimo vyake!
Kwahiyo, kulingana na mkitadha huu, moja ongeza moja ni moja!
Mfano 2: Tuangalie mkitadha mwingine, u-rafiki.
Kama ilivyo ndoa niliyoitaja hapo juu, u-rafiki wa watu wawili (au zaidi) ni sawa na moja ongeza moja (hadi kufikia hiyo jumla ya nambari ya ma-rafiki) ni moja!
Kwahiyo, kiini cha u-rafiki ni moja!
Mfano 3: Tuangalie tena ya mikoa ya nchi yetu. Kama mikoa miwili ya Lindi na Mtwara ikiungana, itakuwa ni moja ongeza moja ni moja (mkoa mmoja mkubwa kwa vipimo vyake)!
Mfano 4: Tuangalie ya timu ya mpira wa futiboli (soka) au kandanda. Upande mmoja huchezwa na watu 11. Lakini hatusemi tumeingiza uwanjani wachezaji wetu 11; tunasema tumeingiza uwanjani timu moja.
Kwa mantiki hii hii, ili kuendeleza Muungano wetu wa nchi mbili huru za Tanganyika na Zanzibar zilizoamua kuungana (wa-Uingereza wanaita, to exercise a political marriage of convenience), tuuchukulie Muungano wetu kwa mifano ya ndoa, Utatu Mtakatifu, urafiki, jumba, mikoa, timu au matone mawili ya kahawa, lubisi, kangara, ulanzi, damu, maji, asali au soda bila kujali ukubwa au udogo wa kila tone!
Tukizingatia saizi, kwa mantiki hii hii, tone moja kubwa (Tanganyika) ongeza tone moja dogo (Zanzibar) ni tone moja kubwa zaidi (Tanzania)!
Mantiki hii inaweza kabisa kutusaidia kunasua a political marriage of inconvenience inayojining’iniza machoni petu, kuhusu Muungano wetu!
BAP
Sunday, May 10, 2009
nina machungwa matanosio manne; moja + moja ni ni moja
watoto kama hawa unyeshewa mvua ya viboko kwa sababu ya busara zao wazitoazo mbele ya ajinga (wazazi, walimu,walezi na wewe)aisee wengi mumelelewa katika mazingira ya kuchapwa viboko na waliojuu yenu. siku zote napinga kuwachapa wanetu na wadogo zetu kwani sipendi wajisikie kama mimi nilivyojisikia nilipochapwa. naamini katika ukaribu, kubebeana, kusameheana na kujadiliana.
basi inasemekana Kim JongHill aliulizwa moja kujumlisha moja ni ngapi? akajibu ni moja. ungekuwa wewe shule za kjijini kwenu basi ungemwagiwa mvua ya fimbo na matusi jinsi ulivyokuwa zoba, japo yawzekana akwambiaye hivyo ni zoba zaidi yako.
basi bwana Kim aliambiwa adhibitishe jibu lake, akasema; nikiwa namwagia maji bustani, viudongo viwili huruka na kutua juu ya jani, viundongo hivyo utengeneza kiudongo kimoja kikubwa zaidi na kwa hiyo moja kujumlisha moja ni moja na sio mbili! kuna mantiki hapo ungekuwa wewe mamaaaaaaaaa pwaaaaaaa mpaka ngozi ibanduke!
basi mwalimu mwingine alimpatia mwanafunzi machungwa manne, akamuuliza una machungwa mangaipi? dogo akasema matano. basi mwalimu akamnyanganya na kumpatia mawili, kisha mawili na kumuulza una machungwa mangapi? dogo akasema matano! duh!
yule ticha akapagawa,akamtukana kidogo kisha akamnyanganya machungwa yote na kumuuliza tena, sasa una machungwa mangapi? dogo akajibu moja! duh, ticha akaona dogo lilivyokuwa zoba, akaagiza fimbo, wakati fimbo inafuatwa, ticha akauliza liko wapi hilo? dogo akasema liko nyumbani alipewa na baba asubuhi!!!!!!
kumbe ticha ndo zoba. kwa hiyo huwa tunatumia viboko kuingiza ujinga vichwani mwa tuwachapao badala ya kujifuza busara zao!!!
wewe je!? usipigane namtu wala mtoto. yawezekana ana akili kuliko za kwakowewe.
eti we ni zoba mbele za mwanao ehe??
Friday, May 8, 2009
We mtoto utalaaniwa, maweeeeeee
Nilikataa kumtembelea na kumjulia khali kiongozi mmoja wa dini, nikakumbushwa kua yeye ndiye mtoa laana na baraka na hivyo anaweza kunifanya zoba na kuniamria kwenda kwa kaka shetani \9kama kweli yupo)
Nikajulishwa juu ya stairi ya maisha yangu kuwa nisipokuwa makini na kufuata ninayoambiwa na wazee, basi nitaalaaniwa na kufia mbali au kuwa zoba!
Duh! Nilienda kumtembelea mchungaji Fulani, nikambishia na kukataa mikwara yake, akanishitaki nikaonywa juu ya laana!
Kila ubishi wangu au mtizamo wangu, ni wa kudai laana tu. Yaani mimi siwezi kuwa na maoni au mitizamo kwani kufanya hivyo nitalaaniwa!
Aisee yaani kila maongezi ni lazima nipigwe mkwara wa laana. Ila niligundua wazee wanatumia msemo huu ili kulinda hatma yao kwani uzee umeingia na hivyo wanahitaji ukaribu na vijana kwa hiyo wanajilinda kwa kukumbusha juu ya uwepo wa laana bila kukumbuka kuwa dua la kuku halimpatagi mwewe siku zote kwani anapaa na kuruka dua hilo
Siamini juu ya uwepo wa laana hata kidogo. Lakini nilijiuliz swali ,je kwani mimi sina laana? Nikimaanisha; mimi siwezi kuwawahi na kuwalaani wale woote wajifanyao wana uwezo wa kunilaani?
Mtu akinipiga mkwara wa kunilaaani, namtangulia na kumwahi kwani na mimi laana ninayo na haina umri na labda yangu nikali kuliko yake!
Thursday, May 7, 2009
kinyawawa, ekinyawawa au ebinyawawa

fu shambani mwako au karibu na kwenu ndo maweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee ukimkuta kafa njiani wewe geuza njia urudi kwako. ukimsikia analia usigeuka asije akakutwanga mkosi wa kifo! duh naishia hapa
Tuesday, May 5, 2009
Munga tehenan; kifo chake sasa ni mwaka M1
nilikwenda kumjulia hali, nikamkuta anapumua kwa mashine, kwa ugumu wa kuongea, akaniangalia na kusema, 'kamala, karibu, hali yangu inaendelea vizuri, kama nisingeletwa hapa (hosp) jana, sasa hivi mngekuwa mnajiuliza huu mwili muutupe wapi, kama ni Moshi, Morogoro au Dar'
alipojaribu kunielekeza kitu, wakaingia madaktari na kuniamuru niwapishe kidogo, na walipoondoka alikuwa amezuiwa kuongea tena na kucheka kwani vilimaliza nguvu. aliongea kwa ishara tu kila nilipomtembelea. ilikuwa ni siku ya jumapili tarehe nne, nikiwa naishi eneo la posta, nilifika Hindu mandal kumjulia khali, nilizuiwa kuingia kwani muda ulienda sana. jumatatu ya terehe tano, nikiwa naelekea hospitalini hapo, ilingia SMS kwenye kiselula changu kuwa, Munga amefariki asubuhi hii!
nikastuka, lakini nikakumbuka jinsi Munga mwenyewe alivyonifiundisha kutokuogopa wala kutishiwa na kifo kwani nikizuri. nilifika hospitalini mida ya saambili asubuhi na kumkuta mwanafuzi mwenzangu Aisha, akiwa amesimama machozi yanamlengalenga. nilichungulia dirishani, mwili wake ulilazwa na kufungwa kama gunia la viazi, basi nikasaidia kuupeleka mochwari, keshoyake tukauzika mwili ule kwenye makaburi ya kisutu hapa jijini.
kifo cha jamaa huyu alikijua mapema kwani alikuwa akituaga darasani nasi tusijue anamaanisha nini. changamoto ikabakia kwetu kueneza alichotufundisha na sisi kuendelea kuwa imara. mpaka sasa tunaendelea kujifunza utambuzi, kujitambua na kuwaelimisha wengine kwa njia ya ana kwaana na mtandaoni. bado tunachangamoto ya kurudisha gazeti la jitambue sokoni.
namshukuru Munga kwani alinibadilisha haswa, maisha yangu yakawa yamaana na kuondoa vurugu, maumivu na matatizo ya kihaiba (ego). japokuwa hakuwa muumini wa dini yoyote, mwili wake ulizikwa kwa taratibu na 'heshima' zote za dini ya kiisilamu aliyokuwa amezaliwa na kulazimishwa kuifuata kama wengi mfuatavyo dini mlizochaguliwa na kulazimishwa kuzifuata.
aliacha mke, watoto wa 3; Kilonzo, Nuru tatu na mwingine. kituo chetu alichokianzisha kinaendelea vizuri pale kimara-Rombo.
sasa anafurahia maisha nje ya mwili kwani alionekana kuchoshwa sana namaisha ya mwili na kabla ya kufa aliandika makala tatu za kutuaga ikiwemo ile ya tutaogopa kufa mpaka lini, maiti hii ni ya nani nk.
je wewe ukifa utaacha nini cha kubadilisha jamii?
Monday, May 4, 2009
Hii ndiyo dini yangu -- hitimisho

Katika post ya kwanza juu ya dini yangu ndg fred katawa alitamka dini kadhaa kuwa ndiyo zangu. Nilishangaa na kujaribu kukubaliana naye. Misahafu karibia yoote huongelea kitu kimoja na kitu hicho pia hukiongea kwa lugha na tamaduni tofauti japo ukifuatilia kiini basi huwa kimoja.
Kinachowachanganya binadamu wa sasa wenye kutaka ugomvi huwa ni lugha tu na mazingira kitu hicho kilivyosemwa.
Dini zote huamini katika utu, umoja, ushirikiano na mshikamano. Zote huamini katika Nuru (mwanga), sauti (neno) na upendo. Huwezi kumtofautisha Mungu na upendo na huwezi kumtofautisha mwanadamu na upendo. Kwa hiyio Mungu na mwanadamu na mwanadamu na mwanadamu huunganishwa na upendo na hivyo upendo ndio msingi wa misahafu yote.
Dini nyingi huamini wasichoelekezwa na waasisi wake na hivyo hufuta maagizo ya wanadamu. Wakatoliki hupenda kujigamba walivyo kuwa kanisa kubwa duniani lenye waumini wengi japo waumini hao na ukubwa wa kwanisa hilo havinamaana sana kwani bado yale maasi yanayopingwa na dini hiyo yanazidi kuongezeka kama waumini waongezekavyo.
Mengine huwakumba mpaka viongozi wa dini zenyewe.
Kwahiyo sio vyema kujivunia ufuasi wako badala yake muhimu ni kufuata maelekezo ya dini yako na kukua kiroho zaidi. Tunaenda mbinguni tukiwa hapahapa kwanzana lengo letu liwe na kuifanya dunia kuwa paradizo na sio vinginevyo.
Basi huwa napenda kusalia katika kila dini. Msikitini huwa siendi ila nasikilizaga tu mihadhara yao kwani mike zake ni pana (vipaza sauti). Nikiwa Dar, mara moja kwa mwezi, huwa naenda KKKT-azania, au DPC kinaondoni kubadilishana mawazo na kuonana na washikaji na kufurahi kidogo juu ya vitisho vya kuingia motoni usipotoa sadaka ya kutosha!
Katikati ya wiki nikiwa na muda basi huwa naingia kwenye kijikanisa kidogo cha mtakatifu Yosefu ili kupata meditation moment. Binfasi naamini katika Nuru, sauti, Upendo. (Love and respect to every God’s creation)
Imani yangu inanifanya kutokuwala wenzangu na hivyo kuwa vegetarian! Siamini hata kidogo bali natenda. Wabadha wanaita ‘ihi passika’ njoo uone na sio uamini tu! Kwa hiyo najua na nikishajua natenda na nikishatenda naona na kuzidi kujua—ndiyo sara yangu.
Siombi kimyakimya na kusubili majibu kesho au kwenda mbinguni baada ya kufa. Natenda na kupata majibu pale pale kama ni mbinguni kufika sio ishu yaani, nikukaa na kutulia na kujiendea nakurudi!
Basi naamini katika kutokuwatendea wale ambaya mimi sipendi kutendewa. Kufanya kazi kwa bidii, kuwasaidia wengine nk. Fred alipatia kwani nasoma misahafu karibia yote niliyonayo na niikutayo maktaba na internet. Sisi tu wamoja bwana.
Kwa kifupi hiyo ndiyio imani yangu, iliyonifanya kuijua mbingu na nchi mpya, wakristo waiitayo Yerusalemu Mpya.
Niulize ni ipi hiyo?
Thursday, April 30, 2009
picha za home bwana


Wednesday, April 29, 2009
milipuko ya mabomu na ugomvi wa binadamu!
ukiwa na kijiti namimi ninakijiti, basi tutachokonoana macho ili tuanze kupigana. kama unakijiti peke yako, basi utajiumiza mwenyewe na kuanza kulia lia.
ndilo lililotokea mbagala leo hii. mimi nilidhani ni radi kwani kulikuwepo na mawingu ya mvua.
jiulize ni kwanini mwl Nyerere alitumia pesa nyingi kumpinga Amini asichukue kale kaeneno ka Kyaka? kwani mpaka wa Tz na Ug uliwekwa na Nyerere, au amini? si wakoloni waroho? ina maana nyerere aliheshimu mipaka ya kikoloni na hivyo kutotaka kuona mswahili akitengua mipaka hiyo? kwani amini au uganda wangechukua eneo hilo, Nyerere au Tz tungepoteza nini?
sasa nchi inayoamini katika amani, leo siraha zimeuwa raia wema wasio jua hata kuwasonya wanajeshi, kwa nini? hivi ni uelewa gani wa mtu wa leo kukaa na kubuni siraha hatari za kuua? anataka kumuua nani?
sasa zimekosa wa kumuua, zimeuwa wenzetu wema tu kuliko hata waliozitengeneza. badala ya kununua madawa na mahitaji muhimu, tunanunua siraha za kivita eti kulinda mipaka iliyowekwa na wakoloni, ili iweje? kwani mtu akitanua mpaka tutakosa nini?
yaani vitu vingine bwana,binadamu wa leo na mawzo ya kumiliki nchi wakati nchi inammiliki yeye. very interesting ehe?
Tuesday, April 28, 2009
mimi ni dini gani?-2
Kamala asiwe na dini ndiyo maana anauliza ajue.
Wengi tunaamini
binadamu + Dini = Imani juu ya Mungu
Binadamu - Dini = Mungu hajupo
Jamani ukiwa katika dini utajikuta unakosa mabo mengi sana juu ya kumjua mungu,lakini ukitoka nje ya dini utamjua mungu na utakuwa na imani nzuri.
April 16, 2009 10:33 AM
Chacha Wambura said...
Kamala, Tweleze kwanza dini yako kwani hatutojua ya kwako mpaka utwambie. Labda kwa kuwa muwazi zaidi twambie unachokiamini; kama ni yesu, mohamadi ama mti uliyoko kanyigo kagera!!!! Lakini pia itatusaidia saaana kama ukitwambia dini ni nini ili tuweze kujua kama tunaamini katika dini ama ushabiki kama wa yanga na simba tu!!
April 14, 2009 12:51 PM
fredkatawa said...
Wewe ni Mkriislabuyahi,yaani mkristo,islam,budha yahudi,hindu.
April 14, 2009 9:15 PM
Monday, April 27, 2009
nimefika jiji ni tena
basi lilipaswa kulala lakini wapi! tulipenyeza mpaka jijini. nilishangaa basi nililopnda halikuonekana kuingia sheli kujaza mafuta na kumbuka lilitoke kampala. sijui linatumia upepo?
tulisimama kahama kupata msosi wa jini, kuna vijana walioonenaka kama wanafunzi tuliwaacha pale kwani mpaka gari linaondoka walikuwa hawajaonekana, siuji waliendawapi mpata tuwaache! niijaa vumbi kutokana na kukaa siti ya mwisho kabisa. basi lilipakia bata, kuku, na bidhaa lukuki.
sasa niko jijini, nayakosa mazuri yote ya BK na zaidi hali ya hewa nzuri kwa meditation.
basi tuendeleze maisha. si mnakumbuka tulisitisha mada yetu juu ya Dini yangu mimi?
twende kazi
Sunday, April 26, 2009
bye kagera, narudi bongo, natamiss mengi
Mkoa wa kagera ni mzuri na una mambo yake mazuri nay a kufurahisha. Kwanza n ilipofika hapa simu yangu ilinikaribisha Uganda eti vodakom wananitakoa makazi mazuri Uganda! Redio ni za nchini Uganda nyingi ila kuna za humu humu kama vile redio kasibante fm iliyoko bukoba mjini, redio karagwe na redio fadeko.
Zote ni za hapa na wakati mwingine hutangaza kwa kihaya, kinyambo, kiganda, kinyankole, Kinyarwanda na Kirundi! Yaani maisha ya hapa ni mazuri na very interesting kwa kweli. Vyakula ni nachulo na halisi, hali ya hewa maweeeeeeeeee
Watu wa mkoa huu wamepambana na kubadilika kwa tabuia nchi a.k.a kuongezeka kwa joto duniani. Kama tungewaiga wenyeji wa hapa kwa kukpanda miti na kutunza misitu na vichaka vya asili, basi kusingekwepo na tishio la gulubo warming na ziwa Victoria lingejaa maji kama nini sijui.
Mvua zinavyesha mpaka ardhi tu inatabipa maji. Maji ni bidhaa ya kawaida nay a kuchezea hapa sio kama Dar na kwingineko. Najiuliza ni kwanini niendelee kuishi mijini wakati hapa kuna kila kitu? Nafikiria vizuri juu ya kuhamia huku bwana. Mijini ni ubishoo tu.
Basi nisiongee mengi, naelekea kituoni kupanda basi aina ya falconi litokala kampala nchini UG ili nirudi kwenye joto letu na misongamano ya watu, mgari, majunmba na uchafu ili maisha yaendelee,.
Nakushukuruni kwa ushirikiano woote wa safari hii, amina
Friday, April 24, 2009
niko wilaya ya karagwe

mini katika usema ule wa ' japo kuwa mtu hawezi kuishi bila mkate, lakini hataishi kwa mkate tu......'
Wednesday, April 22, 2009
makala ya siku ya kuwasili bk, iligoma mtandaoni......
Safari ilianza asubuhi saana. Tulipofika Dodoma basi likasimama kupakia abiria, basi wewe unashuka kuchimba dawa, bado umechuchumaa, unasikia honi za gari mara pipipiiiiiiiiip. Derava anakanyaga mafuta anaashiria kuondoka, wewe nawe bado unashusha zigo huku wengine wanasuburia kuingia, unajiuliza lipi jema kati ya kumaliza ufanyayo na kuwahi basi, ahaa
Unanyofoka mbiooo sijui kama ulitoka ukiwa salama huko utokako.
Kuna sehemu kubwa barabara ni ya enzi za mwalimu, wewe? Unakata kiuno bila kupenda. Basi mnakumbushana barabara ilivyokuwa enzi zile, kwamba mlisafiri basi moja likiwa na abaria waliosiamama wengi kuliko mliokaa.
Wagogo na wasukuma walipanda na kuku wao na mizigo vichwani, ilikuwa tabu, safari ya dar bk ilichukua siku nne hivi. Haya yamepita sasa. Nafika bk, kitu cha kwanza mimi na vumbi langu ni kutafuta ilipo netcafee ili nikupe habari hizi. Nakupenda sana msomaji wangu au sio.
Basi mji wa bukoba ni mzuri na unavutia. Ni wakijani kama vile nini sijui. Maji yamkoa huu ni ya baridi yasiyo na madini wala nini. Hata hivyo huduma za basi hili nazo ni poa.
Naelekea kwetu kashura vilimani, ni kwa usafiri wa pikipiki. Familia nzima yanisubiri, kwani wanajua mimi ni vegetarian? Hawajui, sijala bado. Kwenye basi kuna watu waliokuwa wanalia, wanaenda msibani, kwa kumlilia marehemu, wengine harusini, na mimi kwenye mishe zangu. Mji huu ni mdogo hauna foleni wala nini, ni msafi kiasi.
Basi niko hapa ‘nazimikiwa’ nimetoka mjini.
Naishia hapa ngoja nile na kupumzika. Nimefika vyema, sasa ni kula ndizi kwa kwenda mbele
Monday, April 20, 2009
net inazingua ngoja niende bush labda
Mtu unaweza kusoma makala nzima kwenye gazeti na kuimaliza kabla page haiafunguka. Kwa mfano hiyo post hapo chini, niliweka stori nzima ya safari yangu sasa nashangaa kiliingi kichwa cha habari tu. Nilikuwa nimetundika stori na picha juu ya safari.
Yaani neti iko slow harafu bei juu. Ukiwa na hasira unaweza kulima screen makofi harafu na kumfuata cafee operata na kumpatia matusi yoote unayoyajua. Yaani? We acha tuu.
Basi wandugu, nilikuja kupost hii mara moja kabla ya kuelekea kijijini ketu. Kwa ukimya wangu nimekula ugali na chai kwani majamaa walipika zile mboga. Ngoja nikaone bush kukoje na labda kesho ntawapeni habari kwa kina kizuri japo sijui kama net ya hapa itaruhusu.
Inaonekana bwaya ana uzoefu na net zetu hizi huku. Yaaaa.
Vinginevyo huku ni kihya kwa kwenda mbele vitu kama maweeeeeeeeeeeeeeee ndo lugha ya kawaida sana hapa
Vinginevyo nafurahia maisha, hali ya hewa ni bariidiiiii mazingira ni yakijaniii ukiwa na mke au mume basi njoo hanimuni uku maana du! Joto ni muhimu kupeana hapa
Ngoja nikimbilie bush bwana, habari zaja msiwe na hofu
Saturday, April 18, 2009
Thursday, April 16, 2009
naelekea Bukoba kwanza, byeee
ukisikia basi hilo limepinduka na kuuwa basi ujue naacha mwili, japo muda bado na hilo halipo, kwa hiyo ni safari ya kurudi kule ninaokuita kwetu japo mwili huu nyumba yake ni udongo na nyumbani kwetu ni kule mbaali kufia kwa mwili lakini karibu sana kwa roho
najiuliza itakuwaje viwanja vya kwetu. mimi nafika nymbani, kuna washikaji wangu wa BK town tuliozoea kunywa na kulewa katika baa za garden, west point, contena, softrok, bunena beach nk.
nikienda kijijini basi tunaingia kwenye vilabu vya pombe na kunywa konyagi, nguuli, kalinya, na lubisi lukusharila na olwikunulila. sasa naenda home nikiwa sionji hata punje ya pombe, sasas je, washikaji watanipokeaje? je utamaduni wetu wa pombe?
ndo nimekuwa wa mjini kwa kupuuzia kinywaji muhimu cha utamaduni wangu? je wanaojiandaa kuikaribisha nitawaambiaje? si ni ishara yaupendo kwao kuniandalia Lubisi?
sili tena nyama wala samaki, nimekuwa vegeterian, je, familia nayo itanipokeaje? nitawaambia ni sababu gani sili nyama wala samaki? dokta kanizuia au nimeutelekeza ukristo na kubadili dini wakati lengo ni niwe mkristo?
maswali lukuki ndugu japo kwenda ni lazima.
nimelazimika kusimamisha mjadala wa dini kwani safari ya mamba na kenge wamo kumbuka mikoani net nd hivyo lakin i tutakuwa pamoja na nikirudi, nitaendeleza na labda kumalizia mada juu ya dini yangu.
all the best. byeee siwezi kumisi blug zenu ni lazima nijikomit. nitakaa kijijini bila net, sijui nitakuta post ngapi na email ngapi kwenye inbox.
mwenda kwao si mtoro.
Tuesday, April 14, 2009
mimi ni dini gani?
kumbuka kuna tofauti kubwa kati ya dini, imani na kukua kiroho. natafuta sana kukua kiroho bila kujali sana dini. je wewe uko dini gani na unadhani mimi ni dini gani? dini iipi niliyoichagua na labda kwa nini watu wengi wana dini japo wanashindwa kuziishi bado wanazig'ang'ania na kuonekana kuzimiliki hadi kizihodhi?
je, wewe waweza kufia dini gani au kuhangaika kusambaza dini ipi ikizingatiwa unataka wengine wanufaike na habari nzuri na maisha mema kama ya kwako?
mimi ni dini gani na wewe ni dini gani unaifuata na kwa nini? je umewahi kujuliza maswali juu ya dini yako au unaogopa kukufuru zaidi ya kupenda kukua kiroho?
Wednesday, April 8, 2009
Binadamu wote ni sawa!
Kuna mataifa yanayojiona bora kuliko Mengine, na makabila pia. Kuna wanaothamini watu wa makabila yao tu na kuwadharau wengine lakini wanasahau tu kwamba makabila yao pia sio yao bali walizaliwa tu mahali pale na hivyo sisi sote kama binadamu bado ni sawatu. Dini je! Mwisilamu na mkristo hawapatani, mkatoliki na mprotestanti nao wanazarauliana. Hata ndani ya dini hizo kuna ubaguzi kati ya wale waliokaribu na kiongoza wa dini, wanaohudhuria sana na wale wanaotoa sadaka kubwa za kutosha.
Ndnivyo ilivyo, tunadharauliana. Kazini kwako salamu unayompatia bosi ni tofauti na ya wafanyakazi wengine, bosi akikooa unajipanga vyema! Na bosi naye anakuchukulia hivyo hivyo. Unawadharau watu wa fulani na kuwatukuza wengine. Ubaguzi mapaka dunia imegawanyika. Nchini Tanzania kuna wenye nazo na watu wa kawaida.
Vitabu vya dini vinatuasa kuwapenda wote mpaka maadui zetu, lakini kwa ubaguzi huo huo tunavitumia vitabu vya dini kubaguana na kuuana. Wana wa Israel wanawauwa wapalestina ili wapate ardhi, na wapelestina wakipata nafasi wanawaua WaIsrael kwa sabubu tu ya ardhi nyuma ya pazia la imani, imani zinazotuambia kuwa sisi sote ni sawa mbele za huyo tunayemwamini.
Yaani tumejisahau na kupotoka, tumekumbatia mali za dunia hii na kuwabagua wenzetu. Sasa kuna watoto wanaoitwa wa mitaani kumbe ni watoto kama wengine tu. Tunafanya manyanga na upuuzi bila kujua, huku tukibaguana sisi ambao ni wamoja na wanaopaswa kupendana.
Unataka ushahidi kuwa mimi wewe na yule ni sawa bila kujali fedha, cheo, kabila au taifa lako? Ukipata ajali na gari lako likakulalia, au moto ukishambulia nyumba ulimolala humwiti mkeo ndugu au mtoto, unalia ukiita msaada, msaada msaada. Kwani msaada ni jina la mtu? Hapana ila ni huduma ambayo anaweza kuitoa mtu yeyote na utaupokea tu. Sasa kwa nini tusilitambue hili kwamba wenzetu ni muhimu kuliko sisi ndio maana hutuwezi kujipatia msaada mpaka wao waje?
Bado sisi ni wamoja tu. Sisi wote tunapumua hewa moja ile ile. Tunakula chakula kilekile tunaishi maisha yanayofanana. Sasa itakuwaje wengine wanajiona wazuri kuliko wengine? Mbona sote ni wazuri mbele ya muumbaji?
Unamwani Mungu ehe? Wakati mwingine nivigumu ku -mwamini Mungu anayesemekana kuwapenda watu fulani pekee wakati Mungu huyo huyo huduma zake zinafanana kwa wote na huwagawia wote sawa. Hewa tunayopumua, mvua, jua, upepo nk. Uliwahi kukona huduma hizi haziwafikii baadhi ya watu unaofikiri Mungu hawapendi?
Bila kunipenda mimi au huyo jirani yako huwezi kumjua Mungu na kumpenda kwani yeye ni pendo na anajulikana kwa kupenda tu kama wewe ulivyokuwa na Moyo wa kupenda ila unaufunikia kwa pazia la ubaguzi. Uliwahi kuona daktari asiyeweza kuwatibu watu wenye rangi tofauti? Si mtu akisomea udaktari anatibu watu wote? Sasa iweje leo umbagua Albino eti kwa sababu mna rangi tofauti?
Labda ndio maana taifa fulani linapigania masuala ya Kimungu dhidi ya taifa lingine lakini mataifa yote hayo kati ya mpigaji na mpigwaji yanaendelea kupata baraka za Mungu huyo huyo mmoja kuanzia hewa, maji, chakula, mvua, jua, joto baridi nk. Kama kuna linalopendwa zaidi na Mungu ni kwa nini Mungu asilinyime hewa lililisilopendwa ili lifutike na life kabisa? Anayapenda yote, ni ubaguzi wetu tu
Kumbuka sisi wote ni wa moja na tutarudi kwa huyo huyo Mungu (Muumbaji) kwani sote tu wa Moja! Muumbaji na maumbile yaliumba watu wa rangi tofauti ilikupendezesha ulimwengu. Kamwe huwezi kukuta mpaka rangi akiwa na aina moja tu ya rangi, lazima ziwe nyingi ili ukuta uonekane mzuri na ndivyo hivyo tulivyoumbwa weusi, weupe nk ili ulimwengu uonekana vizuri na lugha mbali mbali.
Wote tutarudi kwa Mungu. Uliwahi kuona bahari yenye maji tofauti? Hapana. Bahari hupokea maji kutoka pande zote za dunia lakini maji yote yakifka baharini ugeuka na kuwa sawa, kuwa kitu kimoja, rangi moja na chumvi ile ile, basi ndivyo ilivyo kwako wewe, na yule jamaa wa dini nyingine, au kabila umchukiaye. Si umeona nyote unapumua hewa moja? Kama ilivyomaji ya bahari, mtakuwa wamoja na kurudi kwa Mungu mmoja mkuu
Mimi,wewe na yule ni sawa na ni kitu kimoja na tutaendelea kuwa wamoja tu.
Monday, April 6, 2009
Hivi kwa nini wakristo wanajiofa wako sawa kuliko wengine?
imani kwa matendo ni kujitafuta ndani na kuona ukweli badala ya kuambiwa habari za kutia moyo juu ya kesho (maisha baada ya kifo)Sasa najiuliza ni kwanini mtu anapinga imani asiyoijua? Siku zote mkristo anapenda umuige na kumfuata yeye kuwa ndiye anayefanya imani za kweli na zinazokubalika. Za kwako ni za kishenzi tu. Yaani inakera wakati mwinginine. Watu wanapenda ufuate wanachokifuanya wao bila kuhoji.
Ukristo ni imani ambayo hupaswi kuuliza maswali na ukiuliza inabidi uulize maswali Fulani pekee na ukiuliza mengine, basi umekufuru inabidi utengwe na waaminia mahiri juu ya imani hiiyo. Hata hivyo wakristo hawajaona kuwa imani yao ina mapungufu kadhaa kwani bado wafuasi wake hawatendi yale waagizwayo na wengi hutenda maagizo ya wanadamu na wala sio ya yesu mwenyewe.
Hata hivyo ukristo inabidi uishi tu harafu utaingia mbinguni ukisha kufa na wanaamimini katika ufufuo wa mwili wakati roho haina mwanzo wala mwisho.
Mimi naamini katika imani ambayo nadhalia au maneno ni kidogo lakini matendo ni mengi na ndiyo yanayotawala. Unatenda na kuona ukweli mwenyewe sio mpaka aje sijui nani na hotuba zake za kuandika ili akwambie ufanye nini.
Hivi usahihi uko wapi kati ya kutenda na kuyaishi unayoyaamini na kufuata mkumbo kwa kuamini usiyoyatenda na kuishi kama msukule?
Friday, April 3, 2009
Kutana na mwinilisti paul mwangosi na uchumi wa dunia.
Mhubiri huyo wa linaloaminika kuwa ni neno la Mungu japo sio lazima Mungu anayemuamini wewe, amekemea ’ktk jina la yesu’ ujinga wa kutegemea wahisani kutoka ulaya eti tutakufa njaa kwa sababu ya kuporomoka kwa uchumi wa wazungu.
Paul anaesema, chakula hutoka ardhini na ardhi yenyewe haitoki ulaya bali tunayo hapa hapa nchini. Kwanini tusilime hapa hapa kwa kutumia mvua tulizo nazo?
Anasema alikatiza dodoma kwenye kijiji kikame, na kushangaa watu wanakufa njaa, anasema, kwa nini watu wasichimbe mabwawa makubwa na kuhifandhi maji ya mvua zinnyeshazo?
Anasisitiza kwamba kuna miti inayotunza maji, unyevunyevu na kuhifadhi mazingira na kuwa ikipandwa kando kado ya bwawa, italisaidia lisikauke muda mrefu huku watu wakilima na kupata maji kwa mahitaji yaoa ya kila siku.
Anasema katika uchimbaji huo, sehemu zenye mchanga zipigwe udongo wa mfinyanizi ili zisivujishe maji hayo haraka. Linaweza kuonekana ni wazo la kitoto kwako wewe unayejiita msomi lakini wazo kama hili liliwasaidia sana watu wa Buganda enzi za kabaka Mutesa aliyetengeneza ziwa kwa kuamrisha wakazi wote wa utawala wake kusomba maji na kujaza bwawa hilo lililosaidia kuleteleza mapinduzi ya kilimo.
Mwinjiliist paul yeye siyo msomi. Ni mnyakyusa aliyewahi kula bangi na kuwa jambazi kabla ya ’kutembelewa ya Yesu’ nakuzaliwa mara ya pili na sasa anamtukuza yesu. Paul alifika Dar bila makazi, alilala kanisani na elimu yake ni ya shule ya msingi tu. Lakini sasa anamiliki studio ndogo ya muziki wa injili inayomsaidia kufyatua na kuuza CD za muziki.
Ameoa anaishi sinza kapanga nyumba nzima eneo la sinza na analea yatima kibao kwa fedha zake mwenyewe.
Ile imani yangu ya elimu sio lazima shule inazidi kupata mshiko. Labdatufanye utafiti juu ya mawazo ya watu wasio soma tunaweza kupata suruhu kwani hawa hawajaathiriwa na mifumo hovyo ya kufikiri na wanaona uhalisia.
Nakuomba tena usiniulize nilienda kufanya nini eneo la kanisa. Labda nataka kufunga ndoa? Kristo kanitembelea? Sikuwa na kazi ya kufanya? Namfukuzia mtoto? Au nilenda kumhoji mwinjilist paul? Unafikiri nilienda kukingama mvua? Si kanisa liko wazi kwa wote na zaidi sisi watenda yasiyotendwa hadharani na waumini?
Turudi kwa mwinjilist paul
Wednesday, April 1, 2009
kifo na maluweluwe yake.
mida kama hiyo sara huwa muhimu kwa ujinga wa kujipendekeza kwa umwobayeMdau, jumapili tarehe 29 March nilisafiri kutoka Mwanza kwenda KIA Kilimanjaro kwa ndege aina ya ATR 72 mali ya kampuni ya PrecisionAir. Tuliondoka katika muda ulopangwa yaaani saa 7.40 mchana tulitarajiwa kuwa KIA baada ya muda wa saa 1 dk 10 hivi. Tulianza safari vizuri kwa mujibu wangu kutokana na uzoefu wangu lakini kwa wenzangu walidai kulikuwa na matatizo wakati tunaondoka. Tulisafiri kwa muda takribani dk 30 hivi na ghafla tukasikia ile kengele ya kumuita muhudumu ikilia mara tatu mfululizo. Mhudumu wa kike alkwenda katika chumba cha marubani na kwa haraka tulimuona akirudi haraka huku kwetu tokea chumba cha marubani. Kisha kengele ikagongwa tena mara tatu tukamwona mhudumu wa kiume aitwae S Mukama akienda kwa haraka huko kwenye chumba cha marubani na hatukumwona tena akitoka. Kilichofuata ni ndege ikipanda na kushuka hewani kama vile gari aina ya Corolla ikipita katika matuta ya viazi kwa kasi ya ajabu. Wakati hali ya mtikisiko ilipoanza ndipo nilipoanza kusikia na kuona vituko humo ndegeni. Vituko hivo ni pamoja na watu kukemea mapepo kwa jina bwana…; kupiga kelele na mayowe kibao. Nilikaa na rafiki yangu mfanyabiashara mmoja mwanye asili ya india na alionekana kupata shida sana na aikuwa mmojawapo wa wale walokuwa wakipiga kelele sana wakati ndege ilipokuwa ikishuka na kupanda. Bila shaka mnakumbukwa wale Vijana wanavosema katika vichekesho vyao vya ‘presha inapanda presha inashuka!’
Ndege ikageuka na kurudi Mwanza kwani tuliona ziwa na baadhi yetu tukadhani tumekaribia ziwa Manyara ndipo tulipoangalia na kung’amua kuwa tulikuwa tunarejea Mwanza. Mhudumu wa kike akasema kuwa ‘ abiria fungeni mikanda tayari kutua mwanza’. Tulitua kwa kasi ya ajabu na breki zilikuwa zikikanyagwa utadhani fisi mwoga akimbiaye mtu mwenye kijiti kiwakacho moto. Ile kusimama tu kila mtu alinyakuwa mzigo wake toka kwenye kebini ya mizigo kana kwamba ndege ingewaka moto. Mhudumu wa kiume alitoka katika kebini ya rubani akiwa anatokwa machozi na mwenzake alimkumbatia huku naye akilia! Muhudumu aliwaomba watu warudi vitini ili ndege iende kupaki. Walitii amri hiyo na kurejea vitini mwao na ndege ikaenda kuegeshwa.
Tulishuka na ndipo tukaambiwa kuwa rubani Mosha alokuwa anaiendesha alipata dharura kama vile ya mshituko wa moyo ama tumbo kali likamfanya awe ‘incapacitated’ kwa mujibu wa watu wa precisionair. Na hivo yule mhudumu wa kiume ndo alisaidiana na rubani msaidizi ambaye pia ni mwanafunzi kutufikisha ardhini! Walituleleza kuwa wataleta rubani mwingine toka KIA kwa ndege charter hivo Tulipelekwa ‘lunch’ hotel LaKairo iliyoko kirumba tukapata chakula (na pakawa sehemu yenye kujaa watu walokuja kuwapa pole wapendwa wao kwa kukoswakoswa na kifo!) mpaka saa 12.30 tuliporejea uwanja wa ndege tayari kwa kuruka kuelekea KIA. Tulipoanza kuondoka tulielezwa kuwa rubani Mosha alikuwemo ndani ya ndege akiwa abiri lakini alikuwa katika kebini ya marubani!!!! Na wakasema kuwa rubani ‘msangi was in control of that aircraft!’ pengine psychologically, walitudanganya ili watu wasipate wasiwasi kutokana na hali tulokuwa nayo.
Kwa kifupi, kwa wengi (asilimia 99.99 ) walikuwa wakisimulia ama kuzungumzia tukio hilo kila baada ya dk 5. Sikujihusisha sana na mazungumzo yaona wala wasiwasi haukuwepo hata tulipokuwa angani tunasukwasukwa bali nilikuwa nikiuliza maswali mengi. Pengine kauchawi ka akina Kaluse na Kamala kalipataga wakati huo nkawa kama asosikia kitu.
Ukweli ni kuwa watu wanaogopa kifo sana. Mmoja alisema kuwa alipoona hali hiyo alianza kukumbuka ndugu zake wote walo hai na walokufa. Mwingine alisema kuwa alipoona ziwa alifurahi sana kwani alijua hata likidondoka majini hatapasuka sana!! Uwanjani penyewe kuna mdada wa musoma alinambia kuwa walipoambiwa kuwa ndege hiyo inarejea kwa ajili ya kutua in emergency alikuwa akijiuliza namna atakavyopata shida ya kupanda viungo vyangu vilivyotawanyika ktk jeneza!!!
Kaluse na Kamala washaandika sana kuhusu hilo suala lakini kwa kweli Kifo, mh! Kinakanganya sana watu wengi.
gazeti la kwana jamii na malakala zake
Monday, March 30, 2009
Prof mbele. mkomavu wa mijadala
Mjadala ulikuwa mrefu na mpana kiasi cha watu wengine kuanza kuchukia. Kama kawaida yangu huwa siifichi kweli. Kweli kwangu huwa inatoka ikiwa uchi wa mnyama. Nilichofurahia katiaka makala hiyo ni juu ya ukomavu wa kidemokrasia au utu wa prof Mbele. Prof. Alikubali kujifunza kile tulichotofautiana mpaka akakubali ukweli.
Mjadala ule ulirefuka kiasi cha baadhi ya wachangiaji kuja kwa hasira wakinishambulia. Baadhi akiwemo bwaya walaianza kulaumu lugha niliyotumia. Hawa walitoka nje ya mada. Niongee kihaya au kichaga, muhimu ni ujumbe. Hawa walihofia kutokukamilika kwa kihisia kwamba nitazua zogo.
Sijui kama walikuwa wakimpa pole Mbele kwa kumonyesha walivyokuwa na maneno matumu huku wakamacha mada au walijaribu kuwa walezi wangu wazuri. Hata hivyo prof, alielewa somo, akijifunza kutoka kwangu na mimi nikajifunza pia kutoka kwake.
Kumbe duniani hakuna matusi bali kuna tafsiri na hivyo kwa kuyatafsiri vizuri maneno yangu, prof aliweza kupata somo zaidi na mimi na yeyeyote aliyeusoma mjadala huo kwa lengo la kujifunza, alifanikiwa na kupata somo pia.
Namshukuru sana mbele na wapenda mijadala, tuendelee kugongonisha mawazo bila kuamshi hisia wala kuhemkwa. Tunaweza kujifunza hata kutoka kinywani mwa kichaa endapo tutamtafisiri vizuri. Karibu kijiweni.
Wednesday, March 25, 2009
eti Tanzania ni Nini?
nikasema mimi ni mwili, kumbe naumiliki, nikasema ni akili, kumbe nazimiliki pia.
sasa mimi nimilikiye hayo nini ni?????
ndivyo ilivyo kwa wewe unayejiita mtanzania, tanzania ninini?
walokole humshukuru Mungu kwa kuwapa nchi (tanzania) nzuri, lakini je, Tanzaninia ilitoka kwa MUNGU?
mungu aliumba ulimwengu na vitu vyake, aliumba Afrika, na mabara mengine, Tanzania ni matokea ya roho mbaya ya uchoyo wa wakristo a.ka wakoloni ya kuigawanya afirka ili waitawale
kwa hiyo wajivuniao tanzania nia lazima wawe wakoloni wanaojivunia himaya yao au watumwa wanaojivunia mabwana zao na labda ndio maana ilitoka kwa Mungu waliyekuja naye wakoloni
Monday, March 23, 2009
Dini usomi na kupotea kwa binadamu wa leo.
Angalia matatizo tuliyo nayo katika maisha ya Ulimwengu huu enzi zetu zimegeuka kuwa enzi za chuma wakati mwanzo palikuwa enzi za zahabu (iron and gold age).
Tuanzie katika uchafu wa mazingira kiasi kwamba badiliko la tabia nchi linatutishia na linatishia kila kiumbe hai, mimea, wanyama nakadhalika.
Tuje kwenye magonjwa hatari yasabibishwayo na dawa za kutibu magonjwa mengine, magonjwa yatokanayo na ’maendeleo’ ya binadamu wa leo kama vile salatani, ukimwi nk
Bila kusahau ukosefu wa chakula halisi na cha asili kilichotolewa na Nguvu kuu (MUNGU?) na sasa ni kula makemikali yanaonekana kuwa matamu mdomoni kumbe ni sumu mwilini.
Amani, umoja na mshikamano hakuna tena. Binadamu wa sasa amewekeza katika kupenda na kuthamini vitu vya duniani hata vile asivyovihitaji na sasa utu umeisha ni mali kwa kwenda mbele. Ni bora ufe ili jamaa apate pesa zake hata kama ni ndogo utadhani tunaweza kuishi peke yetu duniani kwa kukumbatia vitu au utajiri hata ule tusiouhitaji huku tukiwanyanyasa wenzetu.
Ukitembea sehemu zozote, hutakosa askari wenye siraha kali na hatari eti wanalinda usalama! Watu wananunua bastola ili kujilinda sijui dhidi ya nani, na mwisho wa yote zinawalipukia na kuwaua wao au jamaa zao mbao hata sio majambazi wala nini na wakati mwingine kuwapeleka kifungoni.
Viwanja vya michezo, ndege, kumbi za starehe nk, zimekuwa sasa ni za kuingia kwa kukaguliwa na mitambo maalumu ili kuzuia uharifu lakini wapi, bado kila kitu sasa kimekuwa ni saraha ya kujeruhi na kuuwa kama vile viti, meza, chupa za maji, bia na hata soda. Ikishindikana basi jamaa wanakojoa kwenye chupa za maji na kukurushia ili tu udhibitishiwe kuwa dunia si mahala salama pa kuishi
Vijana wamejiingiza katika uvutaji bangi, ulevi na madawa ya kulevya. Sigara na pombe ni halali kwa kila mtu. Eti serikali zinazuia uvutaji sigara, lakini unaruhusu matangazo ya kuvutia vijana wavute sigara yakiwa na kijisehemu kidogo kisichoonekana vizuri, kinachoonya juu ya hatari ya uvutaji sigara.
Pombe nayo ni kilevi hatari kinachouzwa hadharani. Serikali zinafurahia ulipaji kodi kwani zenyewe zinafurahia pesa na kutajirika fasta fasta bila kujali madhara. Ninauhakika kama wauzaji wa ’unga’ wangejiandalia njia nzuri za kulipa kodi, basi serikali za dunia hii zingeruhusu yauzwe yakiwa na nembo ya kuonya kuwa ni hatari.
Eti sasa tuna dini zenye lengo la kutuwezesha kukua kiroho na kutupeleka kwa Mungu, wakati ndo zinaleta ugigiri kati kati yetu. Kwanza kazi yake ni kusambaza woga juu ya uwezekano wa Mungu kutuchapa, kutuua na kututelekeza motoni, utadhani wesemayo hayo wanamfahamu Mungu au wanaukaribu naye wa kutosha.
Viongozi wa dini wametumia nafasi zao kwa kuweka maagizo yao ili watafutao kukua kiroho wayafuate, kumbe hamna lolote. Mungu mwenye upendo, sasa amekuwa Mungu mwenye kutisha. Anamiliki moto, siraha kali na funguo za kuzimu, tayari kutudumbukiza humo! Kumbe yeye amejaa upedo tu anapenda kila kiumbe.
Baada ya dini kuwa zimekuja na ubaguzi wa kila moja kusema kwamba Mungu wake ni bora kuliko wa mwingine, sasa dini hizo zimechagua mataifa (yale zilikoanzia au yalikokuwa makao yake makuu) na kuyaita eti ni mataifa teule ya Mungu.
Kwa mfano upande wa wakristo, wao wanataifa la Israel eti ndo taifa teule la Mungu pekee duniani. Wanadhibitisha hilo eti kwa kuangalia mapigano ya kijinga na ya kinyama duniani kati ya israel na palestina eti waisrael wanashinda kwa sababu Mungu yupo nao.
Swali gumu na linaloonyesha upotofu hapa ni eti taifa teule la Mungu kazi yake ni kupigana, kuuwa na kushinda vita kwa kugombania tu ardhi? Je ni kuendelea kiteknolojia kwa kutengeneza siraha za kuulia watu wa Mungu? Eti ni kukua kiviwanda na kuharibu hali ya hewa ili binadamu na viumbe vingine viteketee bila makosa? Ni Mungu gani huyo? Huu ndio upendo wa Mungu kupitia taifa lake teule?
Hapa ndipo wanakuja wale wanaojiita wasomi na hoja zao za usomi wa kukubali kila akifanyacho mzungu kuwa ni sawa na sahihi wakati tukipeleka ulimwengu mahali pabaya na hatari. Hatuna watu wa kuangalia kwa makini na kufikiri kabla ya kutenda ila usomi wetu ni kuiga kila ujinga wa Mzungu.
Tuna wanasiasa wanaopenda sana na watu wao lakini kila mahali wanakuwa na ulinzi mkali, sasa wanapendwa na nani? Mlinzi anayewafuata futa na bunduki kila mahali au jamaa wanaotamani kuwachapa makofi na mateke? Eti wanabaraka za Mungu kuongozwa, japo wanalindwa vikali wakati Mungu na siraha hawafanani hata kidogo!
Kama nilivyomnukuu msemaji hapo mwanzo, alimalizia kwa kuonya kwamba, kamwe huwezi kumaliza matatizo kwa kutumia fikra zile zile ulizotumia kuyatengeneza. Na sasa ni lazima tubadilike, tuitafute kweli ili ituweke huru. Ni lazima turudi nyuma. Tuige maisha kama zilivyoishi jamii za kiafrika za enzi zile ili tuweze kuanza upya na kuishi kwa kuthaminiana na kupendana.
Naishia hapa lakini kumbuka akili zetu ni tunazojisifia nazo, zinatuongoza kufikiri upumbavu kuubariki na kuuishi. N i lazima tuishi kiroho zaidi badala ya kimwili, kiakili na kuongozwa na hisia
Friday, March 20, 2009
utumwa wa kiakili na kiroho vs ule wa kimwili!
Monday, March 16, 2009
Nchi yetu ni ubabe kwa kwenda mbele.
Sasa ona visasi vinaenda mbele zaidi. Ni hivi juzi juzi tu walimu wa kule Bukoba walipochapwa viboko na mkuu wa wilaya eti kwa sababu tu wamekosa kufundisha vizuri. Yaani mkuu wa wilaya, anatibu dalili tu badala ya mizizi ya ugonjwa.
Kama kushindwa mitihani ilikuwa ni lazima, basi mkuu wa wilaya ilibidi ajue kabisa kutokea mwanzo mwa mwaka kwamba maendeleo ya elimu sio mazuri na hivyo kufanya mikakati yake vyema na hata kama suruhisho lingekuwa viboko, basi angepiga wakati wa maandalizi na sio mwisho wa kutibu matokeo.
Sasa shule zisizokuwa na tija, mtu na busara yake anakuja kuwatandika walimu ambao malipo yao ni madogo na hawayapati kabisa wala hawana miundombinu mizuri ya kuishi wala nini kama yeye mkuu wa wilaya anayeishi mjini, malipo lukuki na vikoromboizo kibao.
Sasa mzee mwenyewe naye kacharazwa makofi. Hii nichimbuko la hasira kutokana na propaganda za kijinga pamoja na kuchanganyikiwa kwa kizazi cha sasa kilicholelewa na serikali ya mwinyi mwenyewe.
Kijana alliyempachika kofi mwinyi alikuwa na umri wa mwaka mmoja wakati mwinyi anaanza kutawala na hivyo sasa vijana wamechoshwa na propaganda za kinafiki na za kipuuzi za danganya toto kutoka kwa wanasiasa eti nchi yetu ni masikini huku wao wenyewe wakiishi maisha kama ya peponi bila kulazimika kufa
Anayekwambia nchi yetu ni masikini ni tajiri wa kutosha. Sasa tunatishiwa na ukimwi eti tutakufa! Vijana wamechoshwa na upuuzi huu ndio maana wengine wamekuwa walevi, wazinzi na wabwia unga kwani maisha yanakatisha tamaa. Kila siku wanashuhudia ahadi na propaganda za kijinga.
Hii ni ishara ya hatari katika jamii yenye kupaswa kujenga misingi bora ya utu, umoja na ushirikiano. Katika kipigo cha mzee mwinyi, walitokea majamaa wengine wenye hasira za kupiga utadhani walimtegeshea jamaa ampige mzee mwinyi ili nao waje kumpiga jamaa.
Eti wanaitwa wanausalama, wapo na masuti yao kwenye joto kali la bongo, harafu jamaa mmoja anatoka huko na kuchapa mtu wanayemlinda kofi zuri la mwaka. Baadaye wanamshughulikia. Badala ya wanausalama hawa kupigana wao kwa wao sasa wanamshambulia huyu mshindi mmoja na kumpiga kipigo cha nyoka.
Namwita mshindi kwa sababu wewe ona majamaa kibao eti wanamlinda mtu mmoja, harafu bw. Mdogo anapenyeza na kumfyatua kofi wamlindaye, harafu na wao eti wanakuja kumlipiza kwa makofi na mateke.
Kumbe wao ilibidi wajiuzulu kazi mahali pale kwani walishashindwa kazi muda mrefu. Lakini hayo wanayaona? Si wanahasira na wanapaswa kumchapa makofi mtu? Hizo ni hasira. Kijana kelelewa mazingira ya kuchapwa, na wanausalamu hiivyo hivyo na mpaka shuleni kwao walifundishwa njia bora za kuchapa.
Hii ndiyo jamii yetu. Mukandara anafanya yake chuoni na wewe unayesoma hapa ikitokea jamaa kwenye daladala akakukanya, wewe! Unalalamika na kumtusi utadhani kakunyea. Ndo hivyo unalalamika na kugombana.
Ebu jikague uone ni mara ngapi unatenda mema au kuongea vizuri, ni matusi na malalamiko badala ya shukurani. Ukienda kwenye jumba la ibada basi unaambiwa ulivyotenda dhambi na utaenda motoni. Maisha yanakuwa magumu, yanatisha na kuogofya na hivyo tunaishi kupigana.
Tumekuwa wakali kuliko hata simba. Sasa hasira zetu zote wanakoma watoto. Kwenye daladala tunawasimamisha eti kwa sababu wanalipa ela ndogo, wababa wanatongoza vibinti na wamama wanatongozi vivulana.
Tunawaonyesha picha za ngono na kuwaathiri kisaikolojia na kuwaalibia masomo. Walimu wanawachapa ila wakichapwa walimu ni kinyume cha haki za binadamu. Akichapwa mwinyi ni kuffungo cha mwaka na mateke ila wakichapwa walimu DC anaonywa na kubadilishwa kazi au kufukuzwa ila wakichapwa watoto bwana yesu asifiwe! Wanawajengea nidhamu! Asifiwe kwa lipi?
Toka lini yesu akawanyanyasa watoto zaidi ya kuwatetea na kuwaokoa dhidi ya mijianafunzi yake nyenye kiherehere? Soma matayo19:5
Yaani ni hasira kwa hasira visasi hakuna kusamehe wala kuchukuliani. Wazazi wanawapiga watoto, walimu wanawapiga wanafunzi, viongozi wa dini wanawatishia waumini, waume wanawapiga wake zao na wake wenyenguvu wanapiga waume zao.
Polisi inawapiga wanafunzi na mgambo inawapiga vijana wanaojitafutia ajira a.k.a machinga, na sasa vijana wameanza kuwapiga wakuu wa nchi na tuone nani mjanja sasa!
watoto wetu jamani cjui ni nani wa kuwasemea watoto kwani kila mahali wao wanatuhumiwa, wanauwawa, wanapigwa, wanabakwa, sijui twende wapi, sijui tumwombe Mungu yupi wa kukomboa watotoo wetu. inauma sana.kuna akina sisi tuliokua bila wazazi wakati wako hai, lakini sasa mambo ni magumu sana.nilipambana na wakristo fulani kisa niliandika makala ya kuwatetea watoto wasipigwe, wanarejea andiko la mithari 22;15, nikatamani hata watoto wangeshirikishwa katika kunadika hiyo biblia. inaummasasa dini hizo ndizo chanzo cha migogoro yoote ya mauaji. ukiangalia nyma ya ubaguzi wa rangi, kuna dini fulani.watanzania waliandamana kupinga kuuwawa na kuonewa kwa waisilamu wenzao wa palestina, lakini kawme siio wa Darful, kwa nini?tunafanya maasi wizi na ujinga kwa jina la dini. marekani akimpiga iraq, tunajidanganya eti imeandikwa. israel ndo baaasi, taifa teule la Mungu. sijui ni mungu yyupi huyo anayemilikiwa na waislaeel na anayewawezesha kuuwa na kutengeneza siraha hatari duniani badara ya kueneza amani, uipendo, mshikamano na umoja! huyo mimi namwita Mungu kichaa kama kweli yupo.tunachafua uliwmengu eti kwa jina la Mungu. marekani wameandika kwenye pesa zao kwamba, in god they trust, sijui ni mungu yupi wanayemwamini huyu.ukoloni, utumwa na uuaji, yalifanyika kwa jina la Mungu wa watu fulani. leo Dafur ni kwajina la Mungu fulani japodini moja lakini Mungu anapendelea ngozi fulani zaidi, wapalestina wafwa, kisa? taifa teule la Mungu linataka kurithi mali za duniani. ni mungu yupii anapenda mali za duni kulikoo kuwapenda watu wake? kwa nini Mungu analiwezesha taifa lake teule kuuwa na sio kuokoa na kukomboa watu wake.ni lazima tumtafute Mungu wa kweli na kueneza ulio ukweli badala ya propaganda za kibanadamu eti mungu anapendlea wajinga fulani wa tifa linalojiona ni lake zaidi.lazima turudi kwenye msingi wa imani halisi na sio bangi hizi kwa jina la mungu etina walilia watotoo, japo ipo siku Mungu wa kweli na mungu wa watu wote na viumbe, atawasikia. ni mungu asiye na taifa wala kabila ni mungu apendaye na kusamehe na kuwakaribisha wote kwake, sio mungu wa kubagua kama tuliye naye sasa
PARADOX OF OUR TIME
Saturday, March 14, 2009
email kutoka kwa Fredi katawa
Subject: UTAPELI
To: mwafrikahalisijlkamala@yahoo.com
Date: Saturday, March 14, 2009, 4:37 AM
JE HII NI AINA MPYA YA UTAPELI?
Ni asubuhi ya alhamisi mojawapo ya mwezi huu wa tatu,nimeamka mapema naitizama siku naona kuwa ni njema kama zilivyo siku zingine.Nachukua kitabu changu kidogo na kuandika mambo nitakayoyafanya kwa siku hiyo
Kati ya mambo mengi ninayopanga kufanya siku hiyo,mojawapo ni kunyoa nywele na ndevu kwenye salon za hapa Bongo.
Saa tisa alasiri inanikuta nikiwa maeneo ya Biafra Kinondoni kandokando ya barabara ya Kawawa.Nikiwa natembea kwa miguu ghafla macho yangu yanaona neno ........SALON.Nakumbuka kuwa mojawapo ya mambo inayotakiwa nifanye kwa siku hiyo ni kunyoa nywele.
Naingia kwenye hiyo Salon.na kupokewa na hali ya ubaridi wa kiyoyozi.Kama ilivyo ada yangu naangalia bei ya huduma imeandikwa hivi,kunyoa nywele tsh 1000,nywele na ndevu tsh 2000.Nashtuka kidogo kwa kuwa nimezoea salon nyingi hapa Dar kunyoa nywele na ndevu ni tsh 1000.
Baada ya kuangalia mandhari ya salon hiyo inanivutia na ninaridhika kunyolewa kwa tsh 2000nikizingatia kuwa mfukoni nina tsh 10,000 naona haitaniathiri sana katika bajeti yangu ya siku hiyo.
Ninapoendelea kunyolewa naanza kuchunguza zaidi mandhari ya salon hiyo,naona kuna screen ikionyesha " Super sports" na kandokando kuna vikorombwezo kibao vya gharama kubwa.Kinachonishangaza zaidi ni simu walizonazo hawa vinyozi wasiopungua watano.Simu moja inagharimu kati ya tsh 400,000 na laki 600,000 ninajiuliza moyoni kwa kazi hii tu ya kunyoa nywele ndo inawafanya wamiliki vitu hivi?
Sauti ya kinyozi inanishtua "bro una mba wengi kichwani"ni kweli ninamjibu"kuna mafuta nitakupaka yatakusaidia sana"ananieleza,ninamshukuru ."naona usoni una chunusi "ninakubali,ananiambia anayo mafuta mazuri kwa chunusi kwa hiyo atanipaka pia,namshukuru tena kwa mara nyingine.
Baada ya kumaliza kuninyoa na kunipaka mafuta nampa noti ya tsh 10,000 anakwenda nje kutafuta chenji,anarudi na kunikabidhi tsh 2,000,ninamkumbusha kuwa nimempa tsh 10,000.Ananiambia kuwa gharama ya kunyoa ni tsh 2000 na kupaka mafuta ni tsh 6,000 ninapigwa na butwaa ninamuuliza kwanini hakunieleza mapema na ubaoni hazijaandikwa gharama za kupaka mafuta?Ananiambia kuwa alidhani ninajua kwa kuwa wote wanaoingia kwenye hiyo salon wanajua hilo.
Napanda daladala kuelekea kwangu,bajeti yangu imetibuliwa na mambo yameenda ndivyo sivyo.Ndani ya daladala ninajiuliza,JE HII NI AINA MPYA YA UTAPELI?
MR KAMALA TUNDIKA KWENYE GLOBU YAKO UKIPENDA,ILI WADAU WATUSAIDIE MAJIBU,KATAWA
Thursday, March 12, 2009
Kukuojoa usiku sometimes ni noma.
Mkojo siku zote huonekana kama ni noma kwani kuna mpaka ’tusi’ la kiswahili kwamba ’una kiherehere kama mkoja wa asubuhi’ ikiwa na tafsiri kibao kwamba mkoja wa asubuhi unatesa na unanyanyasa sio siri kwani wewe unavuta shuka, wenyewe unakutaka ukachungulie toilet aka choo.
Basi bwana udogoni kule kijijini kwetu Igurugati kata ya Bugandika wilaya ya misenyi, tulikuwa na utaratibu wa kulala na Besseni moja kwa ajili ya kuikojolea ubanwapo na mkojo usingizini ili usije jikojolea.
Ilikuwa ni besseni moja kwa ajili ya nyumba nzima na hivyo mzee, ni lazima utoke chumbani, uingie kwenye varanda, mpaka mahali ilipo beseni na besseni yenyewe ilikuwa ikiwekwa karibu na mlango wa kutokea wa nyuma, na karibu kabisa na master-bedroom.
Basi nndugu zangu, Dingi yangu alibahatika kapata pesa toka enzi, nikiwa na maana kwamba tuliishi kwenye nyumba nzuri kubwa yenye vyumba vitano, yatofari iliyopakwa rangi, imewezekwa kwa bati, na chini imepigwa sakafu!
Pamoja na uzuri wote wa nyumba yetu, lakini haikuwa na ceiling board, kwa hiyo kwa maneno mengine, sauti zilipaa kila mahali. Mara ulisikia aina kadha za mirindimo; wa suti kali kidogo ukianza chorororoorororororroro ikimaanisha ni mwanaume aliyesimama, anatoo vitu vyake au shoroshoroshoroshoroshoro, ikkimaanisha ni mwana mama sasa kachuchumaa juu ya besseni kubwa. Nani atoke nje usiku mnene?
Ngoma nzito ilikuwa pale unafikia beseni, kama mwanaume unaanza kulipapasa kwa miguu, si ni giza na hamna umeme? Harafu kibatari mlizima mapema na watoto hamruhusiwi kuwa na kiberiti msije unguza nyumba?
Basi nikwambie, unalipapasa besine kwa mguu mmoja ukichoka unaweka wa pili, gafura unagonga mlango na mkuu wa kaya anastuka ’nani wewe’ aha, nimimi natafuta ka-karahi (besini) kakukujoamo, ’ahahaha, si ufanye taratibu’
Basi unajua ulivyopotea na unatafuta direction nyingine. Sasa ulivyobanwa na mkojo na usingizi, unatafuta kwa kasi nakwa hasira kidogo, ghafra ”pwaaaaaa” umekipiga teke kibeseni, eheee ahasante yesu. Basi unafungua suruali yako ili uanze kushusha vitu.
Unashikiria kidude chako kwa kubahatisha, sasa unatoa mkojo, aha! Kumbe ulipopiga teke beseni lilisogea mbali na wewe. Unakojoa badala ya kusikia kororororororor, unasikia tiririririririr kiwa na maana kuwa unaliwaga chini. Unanza kuzungusa kidude chako aka uume sasa kutafuta beseni, hujui iliko. Unazungushia kushoto na kulia, mbele na nyuma, gafhra unasikia kororo, ikiwa na maana mkojo umeonja beseni
Lakini kumbuka spidi ya kuzungusha ni kubwa na hivyo unapitiliza na ukija kuipata beseni vizuri, asilimia 80 uliimwaga chini. Basi unarudi kulala. Asubuhi nyumba nzima inanuka mkojo. Akitafutwa ninani kalimwaga chini, unaufyata si mulikuwemo wengi usiku ule? Kwani mkoja unasura?
Ndo hayo kwa leo lakini usiombe ije ile wanaita haja kubwa, utakoma na hapa sikupi mchapo huo usijeshindwa kula buree.
UKIPATA NAFASI YA KUKOJOA WEWE KOJOA BWANA KUNA WANAOJARIBU KUUBANA JAPO HAUBANIKI VYEMA. AMINA
Monday, March 9, 2009
Sala la kusali kabla ya kula.
Labda sina jibu la moja kwa moja la swali hili. Lakini tuangalie sala hizi. Wapo watu wanaoombea vyakula hatari kama vile pombe nk, na wanakula. Wapo wanaoombea chakula kizuri kumbe kimetiwa sumu, pamoja na sala zao, bado wanakula sumu na zinawazuru na kuwauwa wakati walimwomba Mungu na akawaambia wale tu. Wengine hapatwa magonjwa kama vile ya kuhara kwa sababu ya kula chakula kichafu japo Mungu alimruhusu kula kwa njia ya sala!
Swali na sala na zielekezwapo, kwa kweli ni gumu kulielewa sana. Ninamiaka zaidi ya kumi sijaombea chakula nikilacho hata kama hakinizuru isipokuwa niwapo mbele za watu kwamba ni lazima kama kikundi muombe (basi huwa nakunja uso)
Nilipokuwa sekondari kuna kiana mmoja alifunga macho kuombea chakula, alipofungua tu macho yake, akakuta majamaa yamesha sogeza chakula chote na alilala njaa! Yaani Mungu aliyekuwa akimwomba, alikaribiwa na jamaa yakaiba msosi wake bila mungu kumstua. Yawezekana hata muibaji alikuwa akimwomba Mungu asikamatwe na kamwe hakukamatwa.
Wanaoishi kwenye miji kama ya dar es salaam, waweza kufunga macho yako kuomba, kumbe kunguru kajisaidia kwenye msosi au kachukua kipande cha mboga. Labda kama kuna umuhimu wa sala basi tusali tukiwa macho vinginevyo tunajitafutia hatari kubwa tusiojua.
Wakati mnasali, wapo wakumbukao vitu vya kijinga, vya ajabu na vya kutisha na hivyo mawazo yao huwa mbali sana na sehemu ya chakula na chakula kiombewacho!
Ni kweli kuna umuhimu wa kusali a.k.a Kuomba kabla ya kula ili kuvutia na kuandaa mmeng’enyo wa chakula kupokea chakula na kukimeng’enya itakiwavyo.
Kwa mfano. Ulikuwa na mahasira yako ya kutosha, ni wazi ukikaa mezani utatafuna msosi kama huna akili nzuri vile, harafu utashangaa kimeishaje fasta vile.
Kwa hiyo unapotulia na kusali au kuomba kabla ya chakula, basi ujue unaandaa afya bora na spidi nzuri ya kula ili mambo yaende murua kabisa. Kumbuka tunashauriwa kula taratibu na kwa muda mrefu. Waweza kufanya ka-meditation kadogo kabla ya kula kama wewe unaungana na mimi katika kutokuamini sala za utunzi wa maneno kufuatana na mtunzi atakavyo
Mwisho; niendapo kijijini kwetu ni lazima tuombe na kusali kabla ya kula. Bibi yangu huongoza sala kama ilivyokuwa tangu nikiwa mdogo. Kwa hiyo huwa miminshajua yoote atakayoyaomba na tunaambiwa Mungu anajua hata mawazo yetu kwa hiyo huwa nimeshaomba zamani, kuna haja gani ya kuomba tena? Sara hazipitwi na wakati? Labda japo zamani kulikuwepo sala za watu fulani na siku hizi sijui vp
ZE ENDI
Saturday, March 7, 2009
Hitimisho juu wa misosi, vyakula na afya zetu.
Kama tulivyoona katika makala hizi ndefu juu ya vyakula kwamba binadamu wa leo hajui haswa ni ichakula gain anapaswa ale kwa afya yake. Tunajua mengi yaliyoko nje yetu, lakini ya ndani mwetu hatuyajui ikiwemo chakula kizuri na muhimu kwa maisha yetu na kwa afya zetu.
Sasa kuna wale wanaoishi na virusi vya ukimwi, wengi wao huishia kutumia ARV wakati chakula mwilini mwao ni kidogo. Ni bora kutokutumia ARV lakini ukapata mlo kamili kuliko kula sumu hizo bila mlo kamili. Tafiti zilizofanya na mmarekani mmoja zilionesha uimara wa afya kwa wagonjwa wa ukimwi na uwezekano mdogo wa kuambukizwa ukimwi kama unakula mlo kamili wa kujenga afya.
Siku hizi kuna dawa kibao za kuongeza nguvu za kiume, nyingine ni za uwongo na nyingine za ukweli, wengi hatujui kuwa nguvu za kiume zinapungua pamoja na mambo mengine ni ukosefu wa mlo kamili. Wewe mtu unakula chips, kitimoto na bia, kweli nguvu zitakuwepo? Kwanza uume utashindwa kusimama na ukisimama kichwa chake kitashindwa kupenya na ukipenya basi huwezi kukata mauno kwani nguvu huna, huli mlo kamili!
Maisha yetu ya viwandani, moshi na kemikali kibao, ni mlo kamili tu unaohitajika. Angalia makabila yanayoonekana kuwa na wasomi wengi, ni yaleyalimayo mazao kibao na hivyo kubalansi msosi au VP
Kumbuka kula ukazidisha kitu kimoja ni noma, ni sumu japo maji ni muhimu. Tunashauriwa kunywa maji kuanzia lita tano kwenda juu kwa siku moja.
Nahitimisha kwa kuwakumbusha kutafuta taarifa kuhusu sisi na kujua vyakula vilivyovuzuri kwetu.
Nice timez
Hitimisho juu wa misosi, vyakula na afya zetu.
Kama tulivyoona katika makala hizi ndefu juu ya vyakula kwamba binadamu wa leo hajui haswa ni ichakula gain anapaswa ale kwa afya yake. Tunajua mengi yaliyoko nje yetu, lakini ya ndani mwetu hatuyajui ikiwemo chakula kizuri na muhimu kwa maisha yetu na kwa afya zetu.
Sasa kuna wale wanaoishi na virusi vya ukimwi, wengi wao huishia kutumia ARV wakati chakula mwilini mwao ni kidogo. Ni bora kutokutumia ARV lakini ukapata mlo kamili kuliko kula sumu hizo bila mlo kamili. Tafiti zilizofanya na mmarekani mmoja zilionesha uimara wa afya kwa wagonjwa wa ukimwi na uwezekano mdogo wa kuambukizwa ukimwi kama unakula mlo kamili wa kujenga afya.
Siku hizi kuna dawa kibao za kuongeza nguvu za kiume, nyingine ni za uwongo na nyingine za ukweli, wengi hatujui kuwa nguvu za kiume zinapungua pamoja na mambo mengine ni ukosefu wa mlo kamili. Wewe mtu unakula chips, kitimoto na bia, kweli nguvu zitakuwepo? Kwanza uume utashindwa kusimama na ukisimama kichwa chake kitashindwa kupenya na ukipenya basi huwezi kukata mauno kwani nguvu huna, huli mlo kamili!
Maisha yetu ya viwandani, moshi na kemikali kibao, ni mlo kamili tu unaohitajika. Angalia makabila yanayoonekana kuwa na wasomi wengi, ni yaleyalimayo mazao kibao na hivyo kubalansi msosi au VP
Kumbuka kula ukazidisha kitu kimoja ni noma, ni sumu japo maji ni muhimu. Tunashauriwa kunywa maji kuanzia lita tano kwenda juu kwa siku moja.
Nahitimisha kwa kuwakumbusha kutafuta taarifa kuhusu sisi na kujua vyakula vilivyovuzuri kwetu.
Nice timez
Hitimisho juu wa misosi, vyakula na afya zetu.
Kama tulivyoona katika makala hizi ndefu juu ya vyakula kwamba binadamu wa leo hajui haswa ni ichakula gain anapaswa ale kwa afya yake. Tunajua mengi yaliyoko nje yetu, lakini ya ndani mwetu hatuyajui ikiwemo chakula kizuri na muhimu kwa maisha yetu na kwa afya zetu.
Sasa kuna wale wanaoishi na virusi vya ukimwi, wengi wao huishia kutumia ARV wakati chakula mwilini mwao ni kidogo. Ni bora kutokutumia ARV lakini ukapata mlo kamili kuliko kula sumu hizo bila mlo kamili. Tafiti zilizofanya na mmarekani mmoja zilionesha uimara wa afya kwa wagonjwa wa ukimwi na uwezekano mdogo wa kuambukizwa ukimwi kama unakula mlo kamili wa kujenga afya.
Siku hizi kuna dawa kibao za kuongeza nguvu za kiume, nyingine ni za uwongo na nyingine za ukweli, wengi hatujui kuwa nguvu za kiume zinapungua pamoja na mambo mengine ni ukosefu wa mlo kamili. Wewe mtu unakula chips, kitimoto na bia, kweli nguvu zitakuwepo? Kwanza uume utashindwa kusimama na ukisimama kichwa chake kitashindwa kupenya na ukipenya basi huwezi kukata mauno kwani nguvu huna, huli mlo kamili!
Maisha yetu ya viwandani, moshi na kemikali kibao, ni mlo kamili tu unaohitajika. Angalia makabila yanayoonekana kuwa na wasomi wengi, ni yaleyalimayo mazao kibao na hivyo kubalansi msosi au VP
Kumbuka kula ukazidisha kitu kimoja ni noma, ni sumu japo maji ni muhimu. Tunashauriwa kunywa maji kuanzia lita tano kwenda juu kwa siku moja.
Nahitimisha kwa kuwakumbusha kutafuta taarifa kuhusu sisi na kujua vyakula vilivyovuzuri kwetu.
Nice timez
Thursday, March 5, 2009
hii ni aina ya misosi ya kweli.
lakini kwa ujinga wa binadamu chini ya kiburi cha uelevu, akaanza kula vya kula vya ajabu, vya viwandani, wanyama na hata binadamu mwenzake. sasa mambo yamemgeuka, magonjwa kibao. tumefika pabaya mpaka tunaharibu ardhi, hewa na mwangu wa jua eti kwa sababu tumeendelea, tuna akili nyingi na wakristo wanasema eti Mungu alitupatia tuvitawale vyote. sasa sijui kama kutawala ni kuharib au la!
zamzni vita ilipiganwa kati ya jeshi na jeshi. siku hizi eti ikwa akili na kwa nguvu za kutawala alizottupatia "mwenyezi Mungu" tunapiga na kuwaumiza watu wasiohusika na ugonvi wetu, na sio hao tu, bali tunaangamiza kila kiumbe kwa kuharibu ardhi, miti, nyasi, maji na kila kiumbe cha Mungu, eti kwa sababu tuna akili nyingi.
tumeacha dawa za asili kwa njia ya chakula, tunakula kemikali eti ni maendeleo! kumbe twafwa! wako wanywap gongo, sigara nk. toka lini mwili wa binadamu ukapitishiwa moto au moshi? si ni hewa tu ukiwemo ushuzi? ushuzi si ni alama ya kula hewa ya kutosha? sasa moshi na moto vya nini?
tuwe makini na ujinga wa binadamu wa leo uliojificha chini ya kiburi na kivuri cha maarifa na akili nyingi eti!
Tuesday, March 3, 2009
Tatizo la kula nyama
Wengi wetu wanapenda sana kula nyama na kula bila kujali nini wanakula. Lakini kuna matatizo lukuki juu ya nyama. Nyama inamatatizo ya kiafya na kiroho!
Matatizo ya ki
afya ni pamoja na ugumu wa kumeng’enywa na hivyo hatushauriwi kula chakula kigumu kumeng’enywa. Nyama inaongeza mafuta mengi mwilini ambayo huleta matatizo ya kutosha,
Nyama pia huanza kuoza, na hivyo hata tukiila,huendelea kuoza mwilini mwetu. Ndio maana mla nyama akienda chooni, choo chake hutoa harufu isiyokuwa ya kawaida na choo kizima, hubakia kunuka kwa muda mrefu na hata jamaa akitoka chooni, yeye na nguo zake heuendelea kutoa harufu kali ya #%#%
Wanyama walao nyama kama vile simba na chui, hawawezi kamwe kula nyama ya wanyama wanaokula nyama, bali hula nyama ya wanyama wanaokula majani. Yaani simba kamwe hamli chui, bali swala, punda milia nk
Protini na virutubisho vingi vipatikanavyo kwenye nyama, huweza kupatikana kwenye nafaka nyingine kama vle maharagwe, kunde, mbaazi, njugu nk, kwa nini tusile hizi nafaka tukimbilie nyama?
Kabla lya kuachana na kula nyama, niliwasahili madktari kibao, walionishauri kwamba kama ninaweza, ni bora nisile kabisa nyama, japo wao wanakula eti kwa sababu ni tamu!
Matatizo ya kula nyama kiroho ni kwamba, tunaua viumbe na kuzuai uwepo wake, tunavitesa, tunachinja na kuvifanya kitoweo. Pili tukila kiumbe fulani, tunarithi itabia zake zote na labda ndio maana binadamu wa leo anatabia nyingi za kinyama.
Ukila mnyama mwoga unakuwa mwoga, ukila mkali unukuwa mkali, muuaji na kadhalika. Hatahivyo mnyama tunayemla natuachia laana yake ya kutosha na ni kweli inatutafuna mpaka kufa.
Kudhibisha tabia, hebu angalia makabila yanayokulal nyama, tena mbichi kama vile wamasai, wakurya nawajaluo. Haaishiwi na ugomvi usio kuwa wa maana na kiwango chao cha hasira kiko juu kiasi cha kuweza kujirusha kutoka juu ya mti au gari liendalo kwa kasi. Pamoja na kwamba TZ ni nchi ya amani, bado wao wana vita zao ndogo ndogo!
Tabia nyingine zitokazo kwa wanyama ni pamoja na kuongez spidi kama mnyama. Angalia makabila yanaoongoza kwa kukimbia sana afrika, ni pamoja na wamasai na majamaa ya ethiopia. Majamaa haya kwa sababu ya kula nyama na kunywa damu mbichi yanakuwa na spidi kama simba au chui na hasira ya kutosha.
Kutokula nyama husaidia sana majamaa yanayofanya tahajudi / taamuli au meditation. Hutuliza mawimbi, na kukufanya kuzama ndani zaidi na kufurahia nguvu za maumbile vyema.
Je wewe unakula nyama? Wengine walizaliwa vegeterian na sasa wanajilazimisha kula viumbe wenzao. Wapo wanaokula mpaka binadamu wenzao. Kumbuka hata biblia inatuasa kutokula nyama kwa wale waiaminio. Kama unabisha, soma mwanzo 1;27-31. hii ni kabla ya kufanyiwa ammedment za kuingiza maagizo ya wanadamu. WEWE!
Thursday, February 26, 2009
Ni chakula gani unachokula?
Magonjwa mengi na maradhi ya mara kwa mara, yanasababishwa na upungufu / ukosefu wa chakula mwilini. Tukienda kwa madakatari huwa hawatwambii mizizi ya ugonjwa tulio nao ni ipi. Wao hutukandamiza dawa.
Kwa mfano wengi wetu hatujui hata umuhimu wa kunywa maji. Niliwahi kuisha na dada fulani hapa jijini dar, wadada hao walikuwa wakichukua maji ya moto na kuweka kwenye mashine ili kulemba nyuso zao zilizo kaukiwa. Wadada hao walisahau kwamba uzuri uanzia ndani kwamba ilibidi pamoja na kula chakula bora, matunda nk, wanahitaji kunywa maji mengi ili ngozi yao yote iteleze bila kusahau mzunguko mzima wa chakula mwilini.
Wengi wetu hupata shida hasa wakienda chooni. Vyoo vyetu visivyona siri, utasikia jamaa akisumumiza utadhani anazaa mtoto, yaani ni mhhhh, mhhhhuuuuhh. Wote ukiwaambia kunywa manji, hawana muda mchafu.
Tunapenda saana kula kitimoto na bia. Jamaa yanakula kitimoto, mbuzi, ngombe nk. Yanasahau vyakula muhimu sana na vya kurutubisha mwili. Unakutana na jamaa anakitambi kama vile ana mimba ya mapacha, ukimuuliza anakwambia eti ni afya. Vifo vingi vinasababishwa na kula chakula hafifu.
Ni bora kutokusoma shule ukajua chakula kikupasacho kula, kuliko kusoma ukaishia kula vyakula unavyoamini vinastarehesha kumbe vinaua na kuumiza zadi. Dada Vai alinisimulia jinsi mamaake aliyeishia darasa la nne, alivyojua kabisa ni chakula gani kiliwafaa wanae, kwamba ni lazima wale mchicha mbichi kidogo na matunda na maharage nk.
Lishe katika miili yetu huwa ni tiba kuliko tiba za hospitalini. Lishe kwa watoto wadogo hujenga afya na zaidi afya ya akili. Siku hizi unakutana na katoto kanene kama nini, kisa? Kanakula kuku. Nilienda kumtembelea mama yangu wakati wa krismass, nikakuta nyama za kufa mtu; kitimoto, mbuzi, ngombe na kuku. Kisa? Sikukuu. Nikamuuliza kama kuna maharagwe, alinikemea kwa kuniambia sio vyakula vya sikukuu, ilinibidi niwe mpole. Ilibidi nilie mboga za majani tu.
Hata hivyo wengi wetu sio kwamba tunapenda kula sumu. Nilipoachana na kunywa pombe, nilipongezwa na wajomba zangu wawili, mama na washikaji. Nilikutana nao eneo la kunywa pombe, mara ya kwanza sikuwambia kama niliamua kuachana na pombe. Siku nyingine wakaona mara sinywi, tena. Basi kaka yangu akaingilia na kuwaambia uamuzi wangu wa kuachana na pombe. Wote waliinuka na kunipongeza kwa uamzi huo na wengine kunikumbatia huku wakiwa na bia mikononi. Kumbe wengi hawapendi kunywa pombe japo wanakunywa!
Vyakula kama pombe, sigara, cocain nk, tunapaswa kuviepuka sana na hata nyama! Soda pia sio nzuri kwa afya zetu. Chukua jino lililong’oka, litumbukize ndani ya kokakola, nakwambia asubuhi yake hulikuti. Au kama una nati (nut) ya gari, geti nk iliyona kutu, imwagie koka au pepsi, kutu itapungua na nati italegea utaifungua vyema, je hiyo nayo yafaa kunywa?
Inasemana kokakola moja, inavijiko 18 vya sukari nyeupe ili iweze kuwa tamu. Kunywa maji baridi ya jokofu (fridge) mara baada ya msosi ni hatari. Inasemekana maji hayo yaingiapo tumboni, hugandisha mafuta yote ya chakula ulichokula na hivyo kuweza kuleteleza kansa!
Vyakula vya viwandani ni vya kuangalia kwamakini sana mjue! Vegetarian na fruitarian diet are highly recommended. Angalia unachokula kisiwe kitamu mdomoni wakati ni sumu mwilini. Take care my dear. Kula kikupacho afya na afya njema hutokana na chakula bora kinachoweza kuwa sio kitamu au hata kichungu mdomoni lakini muhimu mwilini.
I LOVE YOU
Next issue, tutaona juu ya ubaya wa kula nyama.
Tuesday, February 24, 2009
Leo ni kutoka katika SMS
Basi ndugu yangu, leo nimeonelea nitundike baadhi ya SMS nizipokeazo kwenye ka-selula kangu.
1. kwa nini unaomba hivyo?
Binti mmoja wa kikatoliki, alidondoka katika Mapenzi na jamaa wa kiisilamu. Akawaabia wazazi wake ili wamwombee ili mshakaji abadili dini na kuwa mkiristo ili waoane. Siku moja akarudi nyumbani akiwa na machozi makali. Wazazi wake walipomuuliza kulikoni? Akasema walizidisha sala kwani sasa mshikaji alitamani kusomea upadre!!
Somo; ubaguzi wa kidini ni noma, utakufanya umpoteze umpendaye kwani jamaa akiwa padre si itabidi akae mbali na wanawake?
2. wewe ni shujaa?
Shujaa ni yule jamaa anayeweza kukuzishinda tamaa na matamanio yake, kuliko yule anayeza kumteka adui yake, maana ushindi mgumu kabisa ni mtu kujishinda mwenyewe na tamaa zake.
Swali; Je! Wewe ni shujaa? Kama ndio mbona hujazishinda tamaa zako za kutaka kusoma mahali hapa?
3.maisha yako yanafurahisha/
Mabadiliko na changamoto ni sehemu muhimu sana ya maisha yetu ya kila siku. Jiinsi navyopokea changamoto hizo na kuzikubali ndivyo unavyozidi kupata furaha zaidi ya maisha.
Swali: kwani maisha yako yana furaha? Mbona lile lijamaa lililokukanyaga kwenye dala dala umelisuta? Kwani ukimfumania mwenza wako utampokea na kumkubali?
4.Kanuni hizi.
Kusamehe fasta, kupenda kiukweli ukweli, chenka bila kujidhibiti mpaka jino la mwisho lionekane, na usijutie jambo hata majo kati ya yale yaliyokuzuia kutabasamu
Swali; mbona mpaka wenye dini wanahasira na wanawaua watu wa Mungu kwa kisingizio kuwa sio wateule wa Mungu na wakati waliumbwa na Mungu huyohuyo? Kana kwamba unafiki wao hautoshi, wote wanapumua hewa moja, wanakunywa maji yale yele, wanategemea chakula cha ardhi ileile n.k.
5. nini kinamshangaza Muumbaji a.k.a Mung/Golove?
Siku kuu mojawapo, jamaa alimuuliza Mungu kwamba nini kinamshangaza katika maisha ya binadamu?
Naye akajibu; wanaharibu hafya zao kutengeneza pesa harafu wanapoteza pesa ili kutengeneza afya zao. Kwa hofu na wasi wasi mkubwa wanafikiria ya kesho na kuyasahau ya sasa na kwa hiyo hawaishi maisha ya sasa wala ya kesho. Wanaishi utadhani hawatakuja kufa na wanakufa
Swali: wewe mbona unakumbuka jinsi nilivyokutukana tu badala ya kunisifu nikuandikiapo ujumbe huu? Mbona hujiambiii umependeza mpaka jamaa likwambie na lisipokwambia unalimaindi? Kwani wewe ukijiambia kwamba li mimi limependeza huwezi kufurahia?
Yatosha kwa leo, na wewe tupe SMS uzipokeazo hasa yale mambo ya Xyz
Friday, February 20, 2009
ndoa, tendo la ngono-hitimisho
Mtaenda kanisani, msikitini, bomani na kwingineko mkujuakwa kwa kujidanganya eti mnafunga ndoa na mnaweka mambo hadharani, lakini kuna tendo ambalo hata siku moja hamtaliweka hadharani wala nini. Tungekuwa wawazi wa kutosha, basi tungeanza kwa kuvua nguo zetu na kufanya mambo madhabahuni ili waonaji waone, lakini hapana, tunaenda nyumbani, tunajifungua na tunanon’gona ili hata mijusi wanaopita wasituone, hivyo ni suala la binafsi ndio maana tunajificha gizani kufanya hivyo.
Tukumbuke baadhi ya mambo ili kulinda ndoa zetu, mawasiliano ni muhimu saana, kwa walioko mbali, basi simu, email, sms za mara kwa mara ni muhim sana ili kudumisha ndoa lakini hata walioko karibu na wanaoishi pamoja, mawasiliano mazuri ni muhimu pia. Nikisema mazuri namaanishi kusikiliza vyeema kabla ya kuamua lolote lile.
Mwenzio haweza kukusema vibaya, wewe jifanye hujasikia na kwmwomba arudie tena, kamwe, hatarudia bali atasema mengine mazuri au kuomba radhi. Ni lazima tuwasishe wenza wetu katika furaha zetu na huzuni zetu zote.
Tupende kuwaambia siku ya leo imeendaje huko ofisini, shuleni au shambani kwamba, mambo yalikuwa mazuri au hivi na hivyo! Tusitafute vitu vya kutuchanganye vichwa kwa makusudi, kwa mfano wivu wa kusoma sms za mwenzio, utatafuta ubaya ni ukiutafuta utaupata na kuishia kuwa wakorofi na wakufokeana.
Tupende kubebeana mizigo na kusaidiana. Tusilinganishe sana wenza wetu na wengine. Tuwapokee tukijua kabisa kwamba ni binadamu na wanaweza kukuosea, hivyo tuwe wepesi wa kusamehe na kutazama pazuri badala ya bapaya. Kama mwenzio alikukosea, msammehe harafu maisha yaendelee kwa maana kwambawewe kumbukia mazuri aliyokutendea badala ya kutafutana ubaya utakaoishia kuwagombanisha.
Tusiendekeze tabia za watu wengine kuingilia ndoa zetu na hasa ndugu wa kike wa upande wa mwanaume. Hawa hudhani wanammiliki kaka yao na hivyo kuona mabaya ya mkewake tu na kumlingia wasivyokuwa na undugu wa damu naye, husahau kabisa kwamba kaka yao hawezi kulala nao kitanda kimoja wala nini!
Mkiwa na mgogoro wowote, ni vyema kutowahisisha ndugu. Kama kuna haja ya kuwahusisha ndugu, basi wawe ndugu wa pande zote mbili na sio upande mmoja, vinginevyo nenda kwa mshauri atakayekuwa tayari kuwasikiliza na kuwashauri vyema.
Kumbuka tumekamilika, tuwe na upendo, tuwapende weza wetu, tuwetunapeana vizawadi na kufurahi pamoja. Maisha ni matamu, ni mazuri na tuyapende. Kuna haja ya kuhakikisha tunapata muda wa kutosha wa kuwa karibu na familia zetu na wenza wetu.
Mwisho wa masuala ya ndoa. Nakaribisha maoni, vinginevyo tutahamia kwennye misosi kwanza. byyyyyyyyeeeeee
KUMBUKA, MAPENZI NI MATENDO KULIKO MANENO. WAWEZA USIMWAMBIE UNAMPENDA. LAKINI UKAMTENDEA MATENDO YA KUMPENDA.
Monday, February 16, 2009
Katerero, mwalimu wa katerero kuchwapwa hadharani.
Ni hivi karibuni tu nilipoanza mada juu ya tendo la ngono na mambo ya ndoa, japo wapo wengi walalamikao kwamba ndoa za siku hizi hazidumu, nami nikiwa sijui inabidi zidumu mpaka wapi kwani kila chenye mwanzo lazima kiwe na ncha.
Basi kama utukizi vile, wakati nakuhaidi kuongelea kiutu uzima juu ya kagera style au kagera teknology, basi limetokea zali kama lilivyoripotiwa na vyombo vya habari kwamba mkuu wa wilaya ya bukoba ameagiza kuchapwa viboko hadharani kwa walimu wa shule ya msingi katerero, kanazi na kasenene.
Hili limenipa amani kuweza kutamka neno ”katerero” baada ya wengi kujihakikishia kuwa sasa hili ni jina la shule na wala sio matusi. Sio shule tu bali kuna kata, iitwayo katerero au katelelo kufuatana na matamshi ya mtamkaji.
Basi kwaza kabisa, walimu wale walistahiri kuchapwa kwani, jina katerero linatokana na neno ”kutera” limaanishalo kupiga, kuchapa nk. Enzi za ukoloni, wakosefu walipelekwa pale na kuchapwa na hivyo kupaita katerero.
Sasa ni kwa nini na yale mambo mengine mfanyayo wawili mkiwa mmefunga mlango yaitwa jina kama la kata au shule ya katerero?
Ni kwa sababu wakoloni wa kijermani na wafanya biashara wa kiarabu, waliwachapa waafrika viboko vya ki-hamsa ishirini. viboko vya hamsa ishirini ni vile ambavyo ukipiga mtu, basi kiboko kinaenda harafu kinarudi na kupiga tena, yaani kama mpinde wa mvua namaanishwa rain-bow.
Basi ukipiga unarudisha kwa kupiga tena na tena.
Ukishika shule ya msingi kanazi (kanazi ni kiji-mnazi kidogo/kakiboko), basi sogeza kwa mpigaji, piga taratibu juu na chini huku mpigaji na mpigwaji wote wamekaa chini kitako kwa kuangaliana na mpigwaji kainua makanyagio juu ya mpigaji. Basi piga kwa stairi juu na chini, vumilia usijeumizwa na utamu wa mapi go yenyewe, mwangalie mpigwaji, atalia vilio vya ajabu, ghafura ukija rusha kanazi (kakiboko) ndani, kanakuta machozi yakiwa yamejaa, machozi sio ya kawaida, urushaji wa kiboko ni mzuri sana kwa mrushaji na mrushiwa ohhh mungu wako, hutatamani urushaji huishe, eeeeeehh Mungu wako wee aliyemuumba wa Yakobo na Lutatinisibwa, ohhhh, eeeehh, ni noma.
Natumaini mmeelewa somo, kwa watakaolitenda vyema, mtaongeza tija ya ndoa zenu, mtaonekana wamaana sana wa kila siku mtatamani kuwa pamoja. Lazima zawadi ya kasenene (senene) itatolewa tu kama ishara ya upendo.
Udumu mkuu wa wilaya kwa kipigo hicho. Ushindwaye kikipiga, uliza swali, tupo pamoja?????
Eeeeeeeeeeeeeeeehhhhhh ohhhhhhhh, mungu wako weeeeeeeeeee. Senene ni tamu, kushinda nyama
Thursday, February 12, 2009
ndoa huvijika kwa sababu ya tendo
tendo la ngono linahitaji ubunifu mkubwa kutoka kwa mwanaume ili aweze kumridhisha mwanamke. unajua kabla ya tendo ni lazima waote wawili muwe tayari kwamba dume liwe limesimamisha vya kutosha kama ukuni mkavu na jike liwa llina maji maji yakutosha ili kukaribisha uterezi wa kikweli tayari kwa kazi. kuna njia kadhaa ikiwemo ya kufanya romance ya kutosha.
lakini mkiisha kaa muda mrefu wakati mwingine romance huwa haipandi japa mashine zataka kutwangana. basi mumu hupaswi kutwanga kwa hasira kama vile unatwanga mahidi makavu kwa anjili ya kuppika makande, unapaswa utwange kwa utaratibu mara spidi kunwa, mara kati, mara ndogo, mara unaacha na kupiga stori kidogo au busu nk. kwa kweli ni sanaa nba inabidi uwe msanii kidogo ili mwanamke naye aweza kuionja tamu yake.
sio kwenda kasi kama vile unamkomoa mtu, inabidi uwe mpole kiasi kwamba goli likija unalizuia kidogo ili umkae muda wa kutosha na mwanamama ajisikie freshe.
basi kuna ile inayoitwa kagera style, kagera teknoloji au gulioni katerero, hiyo husaidia kufanya kinu kiwe kama barafu iliyomwagiwa mafuta ya mgando na sabuni isyoisha, utelezi wake ninomoooma ndugu zangu, hii hufanya watu wa kabila langu zaidi.
mwisho basi, mechi sio kutuafuta magori mengi, bali kwenda kwa sataili kadahaa na kuhakikisha mamanaye anaona umuhimu wa wewe kuingiza joka lako litemalo hovyo mahali pale. AMEN
Monday, February 9, 2009
ndoa na tendo la ngono
lakini suala lenyewe ni je, kwa nini hutana mifumo mizuri ya kufundisha vijana wetu mambo mbali mbali yahusuyo ndoa, tendo la ngono na kadhalika? tunaishia kuwafundisha ukimwi na kuwaonya juu ya hilo lakini hatujiulizi kwamba hatujawahi kuwafundisha tendo lenyewe.
na ndio maana siku hizi ndoa zinavunjika kama daraja lisilo imara na kuhatarisha mahusiano na kuzalisha watoto wanaoitwa mitaani, kwa nini vijana hatufundishwa wala kufundishana mambo ya ndoa wakati tunapewa wa kuoana nao?
Saturday, February 7, 2009
kutembelewa na marehemu na miili
hawa mara nyingi wanaorudi na kutembelea watu ni wale majamaa ambao kifo kiliwaijia lakini hawakuwa tayari kufa. kwa mfano kuna watu wafao kwa njia ya ajabu, uko naye mara huyoo kafa. lakini kuna wengine hata kama alilazwa miezi kadhaa, wakati wa kufu ukifika, huwa na nguvu za ajabu, hupigana na kukibishia kifo mpaka mmshike mikono na miguu ili afe vema. basi wafao hivyo huweza kurudi kwa njia mbali mbali.
wahaya huita "enchweke" na marehemu hurudi kama kuagiza kitu fulani kifanyike kama kufuata ela yake sehemu, kulea watoto nk. hata hivyo marehemu hawa hawawezi kupitia kwa mtu aliyeko imara, bali wenye matatizo ya kihisia, kimwili au hata wenye nguvu za ziada. sio kila mtu anaweza kutembelewa na marehemu bila ridhaa yake.
hata hivyo marehemu hupaswa kupingwa na kufukuzwa kwani muda wake wa kuishi umeisha kweisha. marehemu pia hawezi kuja na mwili wake wa zamani kwani umeshazikwa na kuoza hivyo mtembelewaji anaweza kumuona kwa mwili hii ni kutokana na labda upungufu wake wa kihisia
mwisho huo wa masuala ya vifo
Thursday, February 5, 2009
mwili huu ni wa nani?
Hivi karibuni nimesoma kuhusu mtu anayedaiwa kuwa mzee kuliko wote duniani kwa sasa. Mtu huyu mwenye umri wa miaka 111, ambaye ni Mjapani, alipoulizwa maoni yake, alisema, hataki kufa. Nilianza kujiuliza, hivi ni lini kifo kitakuwa ni jambo la hiari na lenye kupendeza? Lakini, hata hivyo, mbona maisha ni mafupi sana, hata kama mtu atapewa miaka 200 ya kuishi! Binafsi, napenda kufurahia maisha yangu, lakini najua kwamba maisha ni mafupi sana. Watu wengine wanakiona kifo kama tatizo kubwa linalowazonga. Watu wengi ambao walishaaga dunia kama vile mababu wa mababu zetu mimi nahisi kama wanaishi vizuri tu huko walikoenda. Ni kujisumbua kukikataa, kukiogopa au kukiona kifo kama ni tatizo kubwa ajabu. Wengi wa waliokufa wanakiona kifo sawa na mtu aliyemaliza shule na kufuzu. Inabidi hivi sasa tubadilike na tukione kifo kama mtu aliyepitiwa na usingizi wenye jinamizi na kuamkia kwenye ulimwengu wenye amani na usalama. Lazima wote tufe! Lazima tuishi maisha haya tuliyoyazoea na baadaye tuondoke twende tukaishi maisha mapya ambayo hatukuyazoea. Tujue kwamba maisha tuliyoyazoea ni ya muda tu, na maisha ambayo hatukuyazoea ni ya muda mrefu. Kama umetafakari kwa makini nafikiri umeshaona kwamba hakuna binadamu anayeishi milele. Mamilioni ya watu wanaoishi duniani ni wafu watarajiwa.Wengine wanajitahidi kusogeza maisha yao mbele lakini iko siku itawadia na wataondoka, watake wasitake. Nahisi kwamba watu hung’ang’ania maisha ya dunia kwa sababu hawajui maisha baada ya kufa yakoje.Wazo langu ni kwamba kifo si chanzo cha mateso. Chanzo cha mateso ni raha za muda ulizonazo duniani. Unaona kwamba kifo kitakuondolea raha hizo. Hivi mtu ambaye yuko kwenye maumivu makali ya kupigwa risasi na damu inamwagika kwa kasi bado atatamani aishi? Atataka afe ili aondokane na maumivu makali anayoyapata. Kifo ni rafiki yetu wa kweli. Kifo kinatutahadharisha kwamba tusiyategemee sana maisha tunayoishi. Kifo kinatukumbusha kwamba kila dakika tuliyonayo inapaswa itumike ipasavyo. Somo kubwa tulipatalo kutokana na kifo, inabidi liwe kwamba maisha baada ya kifo ni ya furaha na watu tukubali kifo, tuwe tayari wakati wowote kufa. Hebu jiulize swali lifuatalo: ‘Hivi niko tayari kufa sasa hivi?’ Kama jibu lako ni hapana, ni kitu gani kinachokufanya utake kuendelea kuishi? Unaogopa kufa au unaogopa kupoteza mali zako ulizochuma kwa jasho? Ukweli ni kwamba kama kifo kipo na haijulikani kitakufika lini, haina haja wewe kuogopa kwa sababu una umri mdogo au una mali nyingi. Uoga huu ni kwa sababu hatujajiandaa kufa. Kama unataka suluhu na kifo basi jiandae kufa. Siyo lazima uwe tajiri sana, na baada ya kufikia lengo hilo ndiyo uwe muda muafaka wa kufa. Hivi sivyo. Sijatimiza yote niliyopanga, lakini niko tayari kufa sasa hivi. Ndiyo maana siogopi kifo na wala sikioni kifo kama janga. Kifo ni sehemu muhimu kwenye maisha yangu!Kweli kuna mambo mengi sijayafanikisha, lakini juhudi nilizofanya zilikuwa sahihi. Sasa tatizo liko wapi hadi nidhani nastahili kufa baada ya mafanikio tu! Malengo yangu yalikuwa mazuri sana lakini sikuyatimiza kama nilivyopanga. Hapa cha msingi ni malengo kuwa mazuri lakini kama binadamu nina kikomo cha uwezo wangu. Maumbile hayakutaka kila nililotakla liwe kukamilika.Hii inatosha kukufariji na kujua kwamba umetenda uliyopaswa kufanya, na hii inatosha kukikaribisha kifo kikuchukue bila woga, kwamba kuna kitu hukukitimiza. Ukishajua hivi hutakiogopa kifo na utaishi maisha yenye furaha uwe na umri mdogo, maskini au tajiri. Kuogopa yanayohusu kifo hilo ndilo janga la kweli, lakini kifo kamwe si janga. Kwani, aliyekwambia kwamba, kifo kina ubaya ni nani? Ni dini yako, ambayo inakutishia kuhusu moto, majoka na hasira za Mungu! Dini ingekwambia, baada ya kifo ni amani na furaha tupu isiyo na mwisho, usingethamini maisha haya ya shida ya kidunia.Maisha baada ya kifo ni ya milele. Kama ni ya milele yataweza vipi kuwa ni maisha ya shida na mashaka? Maisha ya shida na mashaka ni ya yale yenye muda maalumu, tena mfupi. Kila mmoja anataka kutimiza jambo fulani na anafukuzana na muda katika kutaka kufanya hivyo. Ndiyo maana kifo kinatazamwa kama adui.Kama nilivyosema awali, kila mtu amefundishwa kuwa kifo hatima yake ni shida na mateso, ni hofu na vitisho. Mimi siamini kwamba, kwa Mungu mwenye upendo na huruma na usamehevu kunaweza kuwa katika mazingira ya aina hiyo. Jela za binadamu ndiyo ziko hivyo kwa sababu wana visasi, siyo kwa Mungu!
Monday, February 2, 2009
wanaotembelewa na maiti!
Wow!! Hapa sasa tutakuja kwa namna watu watakavyotafsiri. Na hapo ndipo panapikuwa na tatizo. Nadhani tafsiri ta nilichokisoma itanisaidia na nawaombea watakaosoma nao wajitambue.
Hivi Kamala, kuna kitu "kutembelewa na mfu"? Na kama kipo basi wale "wanaowaona wafu" wakiwatembelea huwa wanakuja na miili gani? Ile iliyozikwa ama kuchomwa ama tuna mwili zaidi ya mmoja ama ndio tuseme huwa hakuna ukweli katika hilo? Sijawahi hakikishiwa na mtu yeyote kutokea kwa hilo, lakini najiuliza tu kama kuna ukweli na kama upo basi tujue tunaweza ku-renew umiliki wa miili yetu mara ngapi?
Thursday, January 29, 2009
HII NI MAITI YA NANI!!!!!
Nilipokuwa mwanafunzi wa sekondari, niliwahi kushuhudia mwili wa mwanafunzi mwenzetu ukigombewa na wazazi wake. Huyu mwanafunzi mwenzetu alifariki ghafla shuleni na ikabidi wazazi wake wafahamishwe ili waseme maiti isafirishwe kwenda wapi.Mama alisema, maiti ya mwanaye ibaki hapo alipofia, kwani atakuja kuichukua na kuisafirisha kuipeleka kwao (mama) kwa mazishi. Baba naye alisema hivyo hivyo.
Walimu wakaamini kwamba, baba na mama wanazungumza jambo lilelile. Lakini walipowasili pale shuleni, ndipo walipogundua kwamba, hawakuwa wanawasiliana na watu walio pamoja.Baba alikuwa na dini nyingine na mama alikuwa wa dini nyingine na walishaachana kitambo. Tangu walipoachana wazazi hawa, kila mmoja akawa anamvutia mtoto aingie au afuate dini yake. Kwa jinsi tulivyokuwa tunamfahamu marehemu, hakuwa hasa mtu wa dini fulani. Wakati wa vipindi vya dini, huyu mwenzetu alikuwa anaingia mara kwenye madarasa ya waislamu, mara wakristo na alikuwa anaingia kwenye madhehebu mbalimbali.Basi, wazazi hawa walikuwa kila mmoja akitaka kuchukua mwili wa marehemu.
Kila mmoja alikuwa akitoa maelezo ni kwa nini yeye ndiye anayestahili kumzika mtoto kwa dini yake. Malumbano haya yalikuwa makubwa mpaka vyombo vya dola vikahusishwa. Nakumbuka alikuja afisa mmoja wa upelelezi kwenye malumbano hayo. Katika kujaribu kutafuta muafaka, afisa huyu alizungumza kama vile kwa kuhutubia akisema: Inasikitisha kwamba, kijana wetu mpendwa, anaingizwa kwemye choyo na ubabe wa kuoneshana nani zaidi, katika hali hii ambapo hawezi kujitetea. Naamini, huyu marehemu kwa sasa anawachukia wazazi wake wote, kwani anajua wazi hakuna anayempenda hata mmoja, bali wanatumia kifo chake kama uwanja tu wa mapambano ya kujitosha kwao.
Naamini, hivi sasa marehemu angeombwa kuchagua rafiki na ndugu wa kweli, angechagua wanafunzi wenzake na walimu wa dini. Hii inatokana na ukweli kwamba, hawa hawakutaka kumpangia aabudu au kuifuata imani gani ya dini. Tunaambiwa aliingia kwa waislamu, na aliingia kwa wakristo pia, hakuzuiwa au kusemewa, alikuwa huru. Kuwa na dini ni kuwa na uhuru. Kuwa na dini ni kuwapa wengine uhuru wa kuwa wao. Kuwa na dini siyo kutumia tatizo la mwingine kujifaharisha, kuonesha ubabe na urijali ulionao.
Hiyo ni kibri ambayo kwa mtu aliyepoteza mwili kama huyu kijana wetu anaiona na kuijua vizuri, haipendi hali hii..Hotuba hiyo ilisaidia sana, kwani hatimaye ndugu wa upande wa mama na wale wa upade wa baba walikaa chini wakiwa na adabu mpya na kujadili. Hatimaye walikubaliana kijana azikwe kwa dini ya mama yake.Miaka 30 baadaye, nakutana tena na watu wanaogombea maiti, watu wanaoamini kwamba mzoga wa binadamu una maana yoyote.
Sijawahi kuona mtu akitoa shati au gauni kwenye mfuko wa nailoni na kuvaa mfuko huo badala ya kuvaa shati au gauni, nimesema sijawahi kuona, huko ni kujidanganya. Nimekuwa nikiona sana jambo hilo, ambapo ni pale watu wanapogombea mwili.Inaonesha wazi kwamba, binadamu. bado ni mjinga sana juu ya maisha yake. Mwili, mwili ni nini, na hadi wapi? Kama mwili ungekuwa na maana sana, baada ya mtu kufariki usingekimbizwa mochuari, usingepakwa asali au usingechomwa sindano ili usiharibike na kuleta usumbufu wa harufu na maradhi. Mwili siyo mimi wala wewe.
Mwili haujawahi kuwa mwenye mwili na hautakuja kuwa. Mwili ni kama tochi tu, ambayo umeiazima ili iweze kukusaidia kufika kijiji cha pili, kutokana na giza na njia ya uchochoro ambayo unatakiwa kuipita ili kufika kijiji hicho cha pili. Mwili ni kifaa na siyo wewe, bali wewe unakitumia kifaa hicho Binadamu anajibainisha kwenye maisha haya ya hapa duniani kupitia mwili wake, lakini yeye siyo mwili. Mwili ni ubainisho, ni chombo cha kutumika kwa kusudi la kidunia tu. Baada ya muda mwili hukoma kuwepo, hujimaliza wenyewe au kumalizwa, ili binadamu amudu kuingia hatua nyingine ya maisha ambayo haitumii au haihitaji mwili.
Tangu ulipozaliwa umeoneshwa na kufundishwa kwamba, wewe ni mwili kwa njia zote. Akili yako imeshika kutu kwa kuamini kwamba, mwili ni wewe na wewe ni mwili. Huna uwezo tena wa kuuona ukweli, kwa sababu vipimo vyako vyote kuhusu maisha vinaishia kwenye akili, ambayo nayo pia haikuhusu, siyo yako, umepachikwa tu. Kwa ujinga huu wa kutojua mwili ni nini na sisi ni nani, ndipo ambapo tunaingia kwenye ujinga wa kuendeshwa na miili yetu, hisia zetu na akili.
Kila mmoja anaamini kwamba, mwili wake ukipotea, ukishindwa kutumika, yaani akifa, basi huo ndiyo mwisho wake. Kama hiyo ni kweli, ina maana binadamu hana maana kabisa, ni upuuzi usiofaa kuelezewa!Yaani binadamu amekuwepo ili awepo kwa mwezi mmoja, miaka kumi, hamsini, sabini, tisini, au mia tu. Halafu baada ya hapo basi. Huu ni uongo mkubwa sana, unaoweza kukubaliwa na akili makapi ya kulishwa tu! Anayetafakari zaidi kidogo, atabaini kwamba, mwili ni mwili tu, ni kasha tu.Ni kasha ambalo muda wake wa kutumika ukiisha mtumiaji au [wewe] analiacha kwa sababu haliwezi kukidhi kile anachokihitaji hapa duniani. Mtumiaji anachukua kingine ambacho kinakidhi wakati huo [baada ya kifo] .
Kwa hiyo, binadamu hafi bali mwili ndiyo unaofikia ukomo wa muda wake wa matumizi kwa sababu mbalimbali.Anapokufa John au Hamisi, haina tofauti. Anapokufa mkulima hohehahe au tajiri kuliko wote duniani, pia haina tofauti. Wote wanapita kwenye hatua muhimu ya mabadiliko, ambapo wanaacha matumizi ya kifaa kilicho kuwa ndicho pekee kinachoweza kuwabainisha na wengine hapa duniani na kuchukua kingine ambacho hakiwezi kuwabainisha tena na wale wenye miili bado.
Anapokufa John au Hamisi, haijalishi kama amezikwa kwa jeneza la dhahabu na mizinga 100 au kwa masululu butu na kaniki. Kuzikwa ni utaratibu wa kimazoea wa kuhifadhi mwili ambao sasa ni mzoga tu, ili usisumbue watu wengine kwa harufu na maradhi. Kuzika haina maana kwamba, kunambadili aliyekuwa akitumia mwili huo [marehemu], la hasha. Kama unadhani kwamba Mungu anahesabu umezikwa na dini gani, umezikwa na shehe au padri gani, ndiyo afanye uamuzi wa kukupokea mbinguni au hapana, ujue unahitaji msaada wa haraka, kama siyo kupelekwa milembe.
Ujue hujui chochote ingawa umekuwa ukujidanganya kwamba unajua.Mungu wa kweli hahangaiki na mzoga, bali sisi kwa ufinyu wetu ndiyo tunaodhani kwamba, mizoga au[maiti] hii ina maana. Mara nyingi nimekuwa nikiwaambia jamaa zangu, ‘nikifa, mtaangalia ni mazingira gani ni rahisi kwenu kuutupa au kuuhifadhi mwili wangu. Kwa nini? Kwa sababu, kama sikuwa karibu na Mungu wakati nikiwa na mwili, huo, ukaribu utaletwa leo wakati nimeupoteza mwili huo kwa sababu tu, mwili wangu umezikwa kwa dini ya babu yangu?
Ukosefu wa ufahamu wa kiwango kikubwa sana. Kama nilikuwa karibu na Mungu wakati wa uhai wangu, basi hata nikitupwa chooni baada ya kufa, ukaribu huo hautakufa. Mungu hayatazami mambo kama Abdallah Juma au John Maiko! Kwani kuzika hasa ni kitu gani. Hatuziki watu ili waende mbinguni. Kama ni hivyo, wanaoliwa na wanyama, kuungua na kuteketea kabisa, wao Mbinguni hawatafika? Kama hawatafika, watahukumiwa vipi siku ya mwisho? Mwili hautakiwi Mbinguni, hauna kazi huko, kwani huko siyo makazi ya miili. Mwili unafaa tu duniani Kuna zile jamii ambapo mtu akifa mwili wake huchomwa moto na kuteketezwa kabisa Unadhani hizi jamii hazimjui Mungu kama wewe unavyomjua? Zinamjua, tena pengine vizuri zaidi yako.
Lakini, zimeng’amua kwamba, mwili ni kasha tu, likishindwa kufanya kazi, ni sawa na taka nyingine, hutupwa dampo na kuteketezwa kwa moto. Mtu akishauacha mwili wake [kufa] hana tena uhusiano na mwili huo. Mtu huyo anakuwa ameingia kwenye awamu nyingine ya maisha ambayo haihitaji mwili na ambayo haihitaji kujua huo mwili umezikwa na nani na wapi. Ni akili isiosogea ndiyo ambayo inashindwa kufanya mikokotoo midogo kama hii.
Ukiona watu wanagombea maiti, jua kwamba, hata kama wamevaa masuti na kubandika digrii zao kwenye kila ukuta, ni watoto wadogo kiufahamu. Ukiona mtu pia anaacha wosia mrefu wa namna anavyotaka akifa azikwe, naye huyo ni mpujufu tu wa ufahamu. Kwa nini? Unagombea kuuzika mwili wa fulani ili upate kitu gani, ili huyo marehemu naye apate nini? Hata usipouzika, kumbuka kwamba, ameshakufa na ukiuzika, ameshakufa pia. Haifanyi tofauti yoyote kwa kweli.
Kama nilivyosema awali, huuziki mwili ili uende Mbinguni kwa sababu mbingu haiko ardhini. Unaufukia ili usisumbue kwa harufu.Ukienda kwenye nchi zenye vita hasa vya wenyewe kwa wenyewe, utagundua kirahisi kwamba, maiti hana maana, maiti ni msumbufu kwa kunuka na kusambaza magonjwa. Tunazika kwa sababu tuna nafasi ya kuhifadhi mwili kwa heshima na taratibu ambazo zinaonesha kujali mwili wa mwenzetu ambao ulitumika kufanya mema au maovu.
Kwenye kizuizi na misukosuko au vita, hakuna anayeweza kukumbuka, siyo kuzika bali hata kufukia maiti. Kila mmoja anafikiria kuendelea kubaki na mwili wake kwanza. Aliyepoteza wake, basi hakuna anayemjali, kwani haina maana kabisa kumjali. Hata aina nyingine za mazishi zinaonesha tu ujinga na utoto wa binadamu. Mazishi ya kifahari yenye kuhusisha majeneza ya dhahabu na vyakula na vinywaji vya bei mbaya. Ni ujinga uliopindukia kwa sababu, inawezekana kabisa marehemu au wanaotoa fedha hizo hawajawahi kumsaidia aliye hai hata kwa chupi ya mguu. Sasa kusaidia huo mzoga kwa mapambo inaongeza kitu gani? Nimesema unapoona mtu anaacha wosia ili azikwe vipi, wosia ambao wakati mwingine ni kero tupu, ujue huyo naye ni mtoto wa miaka sita, bila kujali anamiliki au amesoma hadi kiwago gani.
Ni utoto kwa sababu, unapoacha mwili, siyo kazi yako kusema huo mwili ufanyiwe kitu gani. Waliobaki, wanaweza kuamua kuuchoma mishikaki [kama wanakula watu], wanaweza kuukausha na kuuweka kwa maonesho, wanaweza kuufukia kwenye kijishimo cha futi tano na ukafukuliwa na fisi usiku, na wanaweza kuuzika kwa matarumbeta na sanduku la dhahamu. Ni hiari yao. Ukishauacha mwili huna mamlaka nao tena. Ni wale waliobaki ndiyo wanaolimbuka nao tu. Nimekuwa nikitazama hii tabia ya kugombea maiti kwa jicho lenye mashaka na ufahamu wa binadamu, hofu zake na ufisadi wa nafsi alionao. Mtu amekufa, wewe unasema nataka nimzike mimi, sawa. Kwani mbona huendi hospitalini ukaulizia maiti ambazo hazina ndugu na kuzichukua ili ukazizike? Wewe si unapenda kuzika na unaamini kumzika mtu kwa dini yako ni jambo kubwa na la maana sana? Pia hospitalini, utapewa maiti nyingi zisizo na ndugu.
Ukishazipata zibadili majina na kuziingiza kwenye dini yako kwa mujibu wa utaratibu wa dini yako. Halafu zika! Hiyo huitaki kwa sababu haina maslahi, haina kuonesha ubabe ambao umefundishwa na wazazi, na jamii na pengine hata na dini yako hiyohiyo. Kugombea maiti ni kujiogopa. Kugombea maiti ni kujitafuta kimakosa. Kugombea maiti ni kutojua dini. Kugombea maiti ni kudhani mtu anaweza kuwa na uhuru wa kuwa mtu mwingine. Kugombea maiti ni kufikiri wewe ni mwili, Kugombea maiti ni njaa ya mali au haja ya kupanda kithamani. Kwa ujumla ni ubabe wa kimtaa zaidi. Mara nyingi imeshatokea, anapookotwa maiti na watu wakaanza kuulizana, jamani maiti hii ni ya nani? Ujue maiti hiyo itazikwa na serikali. Hakuna mtu au kundi la kidini la eneo hilo ambalo litajitokeza kuichukua na kuizika maiti hiyo kwa imani yake. Hilo haliwezekani kwa sababu halina utamu. Halina kubishana, halina kulumbana, halina ujuaji na ubabe. Anasubiriwa mtoto mwenye mzazi walioachana na walio na dini tofauti. Huyu akifa, hasira na visasi vyote vya nyuma vinaishia kwenye mwili wake. Atasubiliwa yule ambaye alishakuwa kwenye dini yetu akatoka, huyo akifatuna sababu ya kugombea maiti. Kama nilivyosema, hapo kuna malumbano na ujuaji na kuoneshana. Halafu bado mnajiita mnatumikia dini, zipi? Ni ujinga tu.
Tuesday, January 27, 2009
Na kuhusu kifo.
Ndio maana tawala wa enzi zile, walileteleza salamu za “uishi milele kuhani mkuu” nk. Waliogopa kufa, hawajui juu ya kifo. Kumwambia mtawala kwamba ipo siku atakufa, ni utovu wa nidhamu, ni sawa na uchawi na mtu kama wewe adhabu yako ni kifo au manyanyaso kwa kumkumbusha mkuu kwamba ipo siku atakufa.
Kutokueleweka kwa kifo, ndio mwanzo karibia wa dini zote. Binadamu alianza kujiuliza mambo mengi na magumu juu ya kifo, na mwisho wa yote kifo kikaonekana kama adhabu kwa wakosaji wa nguvu kuu (mungu) na hivyo ikabidi watu waanze kufanya vituko ilimradi tu waibembeleze hiyo nguvu ili iwasamee.
ndio maana kwenye majanga ya asili, watu hukusanyika na kuomba pamoja ili wasamehewe. Hata hivyo, maombi mengi, yako kibinadamu zaidi ya kimungu. Ndio maana nguvu kuu au mungu hupewa majina ya juu ya kibinadamu lakini binadamu wale wenye vyeo kama vile mfalme, samba wa Yuda nk.
Ndio maana wewe unafanyaga sherehe ya kukumbuka kuzaliwa kwako a.k.a bethdei, ukikumbuka na kuogopa kufa kwamba hujafa mpaka leo. Baada ya kugunndulika kwamba kifo hakikwepeki, majamaa wakaleta heri juu ya maisha ya baada ya kufa kwamba ukifuata masharti yao, basi ukifa huendi tena motoni, bali peponi. Yaani yakaweka moto na pepo!
Wagonjwa hukimbia kuombewa makanisani, lakini mwisho wa yote hata wale wawaombeao, hufika wakati wakaugua na kufa pia, lakini hili bado halijawa somo kwa waombewao kwamba kumbe hata waombeao hufa na hivyo sio suruhisho la magonjwa na kifo chao hata kama baadhi huendelea kuamini hivyo.
Basi tuachane na propaganda, hakuna kitu kinachoitwa kifo kwa mwanadamu. Ukikumbukia makala ya sisi ni nini, utagundua kwamba binadamu huwa hafi wala nini. Unaokufa labda ni mwili wake lakini sio yeye kama binadamu. Miili yetu ina mwanzo na mwisho. Miili ilanza kutengenezeka baada wa wazazi kuwa na nyege na hivyo kufanya tendo liliokufanya wewe na mimi tuendelee na safari ya kutoka kwenye manii na yai na kujengeka.
Basi hapo ndipo tukaendelea kuivaa miili na ipo siku ya kuivua. Kwa hiyo kufa ni kuuvua mwili wa nyama. Ni kutoka kwenye mwili na kuendelea na maisha mengine. Ndio maana utasikia wakikwambia hii ni maiti ya KOERO au BWAYA au KAMALA. Kwa sababu yeye hayupo tena kweye huu mwili japo sisi tunao mwili huo.
Basi nisikuchoshe, sisi huwa hatufi, bali tunaachana na miili wakati ukifika na kuenda kuishi maisha mengine. Kufa ni raha na kuzuri kuliko kuishi. Ukishaachana na huu mwili, unaachana na kero mbali mbali za huu mwili. Huhitaji kula, kunya, kukojoa wala kuuosha mwili nakuuvalisha.
Huhitaji tena maswali ya kutia/kutiwa wala kukereka. Ebu angalieni hii miili yetu. Ukiwa na njaa ni matatizo, ukishiba ni matatizo pia. Ukiongeleshwa na matatiozo na usipoongeleshwa ni matatizo pia. Ukiwa masikini hupendi na ukitajirika unaishi kwa wasi wasi na hofu. Sasa je kwa nini tusifurahie kuvua miili (kufa) na kuishi nje ya miili hii inayotuletea kero za kutosha? Akina Kristo waliyaona haya mapema.
Ndio maan bibilia inasisitizo juu ya kutotawaliwa na miili na hata korani inafanya hivyo pia.
Kuogopa kifo, ni kuogopa kivuli chako, ni kuogopa haki yako ya msingi kabisa. Nikuogopa kuendelea na safari yako ya kuwepo na kuendelea kuwepo na kubadilika.
Mwisho basi, hakuna kufa, bali kuna kuachana na miili hii yenye usumbufu na kero vya kutosha.
Saturday, January 24, 2009
ubishi, ujuaji na kupayuka.
hacha hizo. hakuna ajuaye kuliko mwingine, bali kuna mitizamo. wewe eleza mtizamo wako, kaa kimya. ukibishi maanake hujui kwani huwezi lazimisha mtu akukubalie. kumbuka sote hatujui, ila tuna mitizamo tuu
au vp wananchi?
Wednesday, January 21, 2009
hasira, hasara, majuto. sameheni tu
Hasira uendana na chuki, woga, visasi, kuwekeana miiko, nk. Katika maisha yetu ni lazima tuwe na hasira kwani bila hasira maanake hatupo, hatuishi kwa hiyo hakuna awezaye kujigamba kwamba yeye hanaga hasira au hachukiagi. Wote tuna hasira na kukasirika/shwa, ni sehemu ya maisha yetu ya kila siku.
Taizo ni pale tunapotafuta vitu vya kutuboa, ili tukasirike. Hata hivyo hatupaswi hatakidogo kudhibitiwa na kuongozwa ha hasira. Wewe muda wote unatafuta ni nani wa kukukasirisha, au ukikutana na jamaa zako, jambo la kwanza kukumbukia ni jinsi alivyo kukasirisha.
Umewahi kuona na kutenda yafuatayo. Jitu limekukasirisha na wewe unaamua kuondoka kwa hasira, unatembea bila kufikiri, mwishowe unajikwaa na kudondoka chini na kuumia. Au unaendesha gari kwa hasira na mwishowe ni ajali ya kuumiza, kuuwa na kuharibu.
Mpenzio anakukasirisha unatangaza talaka, na mengineyo mengi. Tumesikia mengi juu ya watu wanaolipiza visasi, huishia kujiumiza wao wenyewe na wengine kuuwa na kubakia na majuto ya ningejua nisingefanya hivi na hofu za matokeo ya matendo ya hasira yawapatiayo majuto!
Lazima tuwe sisi, tutangulize kuwachukulia wengine kama walivyo na kuwasamehe na kutenda yaliyoyetu. Kwa wakazi wa Bongo-DSM, bila shaka umeishawahi kugongwa na lijamaa litembealo kwa hasira. Yaani mtu anatembea kwenda kupanda dala dala huku akikumbukia jamaa aliyemkasirisha jana au aliyemdharumu. Mwisho wa siku anahishia kuwagonga wengine na kujiumiza zaidi.
Tujifunze kuzidhibiti hasira zetu na kutokuziachia nafasi ya kututawala. Tunaweza kuzidhibiti kwa kufanya mambo kama haya; kuhesabu moja mpaka kumi, kwamba jamaa linakutukana na kukusema vibaya ili mpigane, au limekukanyaga bila hata kukuomba samahani au umemfumania mwenzio live akinanahiliiiiiiwa, basi kabla ya kufanya uamzi wowote, chukua muda kidogo. Fumba macho au weak uzingativu wako sehemu, harafu hesabu moja mpaka kumi au zaidi, hili upate nafasi ya kufikiri na kuamua vyema bila kuongozwa na hasira kufanya lolote.
Mchukulie kama alivyo; jamaa kakukuta baa unakunywa soda, kaanza kuongea maneno ya fedheha kwamba soda ni kinywaji cha masikini. Wewe jiambie kwamba hanitukani, ila huo ndio ujuaji wake na hivyo mchukulie kama alivyo na usilazimike kumfundisha, bali mwache na uelewa wake huo.
Kwa vyovyote tusikubali kuachia mihemko kama ya hasiri kututawala, fanya lolote ili uzitawale hasira. Kunywa maji, jifungie chumbani na kuvuta hisia zenye kukufurahisha, msikilize anayekusema vibaya na kusapot, fanya lolote zuri ilimradi usichokozeke na kufanya yale yatakayokuumiza wewe.
Sijui wewe unasemaje.
Tuesday, January 20, 2009
mgogoro wa UD, mtizamo wangu
huwa najiuliza maswali mengi juu ya fikra za wasomi wetu wenye madigirii, PhDs profs na wewe unayesoma hapa. huwa nashangazwa na maamuzi ya wasomi. yaani vitu kama hivi vya kuwafukuza wanafunzi mimi sielewi. kwa mtizamo wangu tatizo hili linatokana na watu kutokujiamini, kutokufanya walipendalo maishani (kufanya chochote mradi kinallipa), na kuishi tu kwa kuwa tupo bila kujali tunaishi kama nani na kwa nini tupo.
wengi wetu tunaishi kama miili ndio maana tunafanya maamuzi ya kimwili zaidi badala ya kiroho na kifkra halisi.
sasa hapa kinachonifurahisha ni jinsi maprof. kama Mukandara, kuwafukuza wanafunzi ambao kimsingi ndio waajiri wao kwani hamna mwalimu au mkuu wa chuo bila wanachuo. wao wanajiona juu kwa sababu wamechaguliwa na rais badala ya kuangalia hali halisi juu ya kwa nini wako pale.
tatizo ni kulelewa katika mazingira ya mpishe mwenye nguvu yale ya kupigwa viboko yanayoamini kwamba mkuu anajua matitizo yako kuliko wewe mwenyewe. kumkosoa mkuu ni dhambi inayositahiri kufukuzwa chuo na hata kuuwawa kama lilivyofanya kanisa katoliki enzi zile kwa watu kama Galileo, Wyclif nk. kwamba mkuu (mukandara) ndiye mwisho wa ujuaji na kauli.
sasa majamaa yamefunga barabara ili wategemezi wa njia hizo wasipate huduma muhimu za kibinadamu kama kuawahi job, hosp, nk.
tunalaumu ufisadi wa EPA richmond, nk lakini kumbe kuna viufisadi vya kutisha, majumbani mwetu, vyuoni, na hasa ndani ya vichwa vyetu sisi wenyewe! ndio maana msomi wa leo anailalamikia serikali harafu akipata nafasi humo humo serikalini anawashangaa wanaoilalamikia na kuikosoa serikali kama alivyofanya yeye mwenyewe enzi zake za kulalamika.
ndio maana wizara zinajitahidi kila mwaka konyesha mafanikio na kujisifia badala ya kutanguliza changamoto na mapungufu ili zijipange vizuri namna ya kukabiliana nazo. tunaishi ishi tu kwa sababu tupo (existing) na hatuishi kama chochote, mwisho wa siku tunaogopa na kukimbia kifo.
"sauti ya watu wengi ni sauti ya Mungu" sasa watu wanaotumia muda wao kunyanyasa viumbe vya Mungu ndo hivyo saa yao ya kuacha mwili (kufa) ikifika wanaangahika na kulia lia kwani waliisha mtesa Mungu wao hapa duniani (watu wengi/wanachuo) na hivyo maisha yao baada ya kifo yanatisha kwani wanastahiri kukutana matendo yao (karma).
Ebu jaribu kufikiri chuo kama UD bila mabishano wala kutofautiana, kitakuwa chuo kweli au genge la kufyatua wajinga kwani wahenga husema, akili tupu ni karakana la shetani! (an empty mind is devil's workshop) sasa hilo ndo akina mukandara wanatafuta!
Lakini sio akina mukandara tu hata sisi tukijikagua tutagundua mambo ya kijinga na kishetani ndani mwentu na katika maisha yetu ya kila siku. Jitu kama wewe na mimi linabishana na mjinga au asiyeelewa badala ya kumwacho na kumchukulia kama alivyo. Somi kama wewe linaongea kiswakinge mbele ya hadhira isyojua hata goodmorning ili lionekane lilivyosoma badala ya kuongea kiswazi na kufikisha ujumbe (lengo husika)
Basi ndo maisha, twende mbele, lyf goes on, akina mwenye Rungu anamfyatua asiyena Rungu naye akipata Rungu basi mtamkoma.
Lakini maajabu yapo mengi duniani kama vile padri na papa kuvaa gauni wakati ni wanaume, papa john paul II kuongelea kondomu wakati hafanyi ngono, ndivyo ilivyo kwa Mukandara na wenzake kuwatendea unyama waaajiri wake utadahani kuna chuo bila wanachuo.
mwisho wa siku wanafunzi ndio tatizo kubwa na la kimataifa labda, nakumbuka majamaa hawa wakipokea kadi za CCM pale diamond jubilee, na kupiga kampeni, kura NK, harafu mshindi ndo anachagua uongozi wao na kuamua wapewe shilingi gapi za kusomea na kuishi. Sasa wanamlaumu mukandara ambaye lazima atii mawazo ya bwana mkubwa aliyempatia huo ulaji. (natamani ningeweza kusikiliza maongezi ya siri ya simu kati ya mukandara na JK kabla ya kuchukua uamuzi wa kufukuza wanachuo)2010 yaja mambo yale yale, hata hivyo wamchague nani wakati kuna wanaohaidi ahadi zisizo eleweka hata masikioni mwa chizi?
Naishia hapa na hoja zangu hizi zisizokuwa za kisomi kama zenu, nimechoka kutaipu na sipendi siasa wala elimu hizi, napenda elimu ya utambuzi na kujitambua kujikagua mwenyewe badala ya kulalamikia wengine kwani yawezekana mimi ndio tatizo labda!.
nimechoka kutaipu bye nitembelee bloguni;
http://kamalaluta.blogspot.com
hii niliitoa kwenye mjadala fulani na wasomi kadhaa
Saturday, January 17, 2009
sms za mwaka mpya na mambo yake
Hata hivyo SMS niliyoipenda iliandikwa hivi;
“ON A GREAT DAY, A PERSON ASKED GOD: WHAT SURPRISES YOU ABOUT MANKIND? GOD REPLIED: THEY LOSE THEIR HEALTH TO MAKE MONEY AND USE MONEY TO RESTORE THEIR HEALTH. BY THINKING ANXISIOUSILY ABOUT THE FUTURE THE FORGET THE PRESENT, SUCH THAT THEY NEITHER LIVE FOR THE PRESENT NO FOR THE FUTURE. THEY LIVE AS IF THEY WILL NEVER DIE AND DIE AS IF THEY NEVER LIVED. IT IS NO TO LATE TO MAKE A DIFFERENCE IN 2009”
sijui mnasemaje wananchi.
Wednesday, January 14, 2009
kuwachapa watoto, vp na sisi tukichapwa
Kuchapa watoto viboko kunatujengea jamii sugu.Naandika baada ya kusoma barua ya msomaji wa raia mwema na.050 katika ukurasa wa saba anayesema kwamba migomo mashuleni; tunavuna tulichopanda.
Mwandishi wa barua hiyo bwana Paul Mtebwa wa Muleba, anaumizwa na hatua ya serikali ya kuamuru mtoto kupigwa viboko vitatu tu kwa kosa kubwa tena kwa idhini ya mwalimu mkuu. Kwa mtizamo wake viboko vingezidi na kuwa vingi zaidi hata kwa kosa dogo tu.
Anasema migomo iliyoko mashuleni kwa sasa inasababishwa na ukosefu wa adhabu ya viboko vya kutosha. Na mwisho wa yote anapendekeza adhabu mbadala kama viboko vikisitishwa.
Nimeshindwa kumwelewa ndugu huyu kwamba, kama yeye alichapwa basi kila mtoto wa leo anastahili kuchapwa! Hii si sawa na si haki kwa watoto kwamba wao ni watu wa kuchapwa hata kama makosa yao ni ya kawaida sana .
Yatupaswa tuelewe kwamba tunalea watoto ili wakikosa tuwakosoe na kuwaweka katika njia sahihi kwa kuwafundisha na kuwaelekeza na wala sio kuwacharaza viboko kama vile sisi huwa hatukosea, tunajiona Miungu watu ambao tunajua kuyaangalia makosa ya watoto na kuwacharaza tu.
Je! Wangapi kati yetu walifurahia hali ya kuchapwa walipokuwa wadogo au wangapi wangependa kuchwapwa leo? Kama ndugu Mtebwa angekamatwa na kosa leo na kuambiwa achague adhabu kati ya kuchapwa na kulipa faini, angechagua ipi kama sio kulipa faini hata kama hana fedha si angechukua mkopo na kuepuka ubaya wa viboko?
Kwa nini sasa tuwachape watoto wetu wakati sisi hatupendi hiyo hali ya kuchapwa?
Ndio maana leo tunaishi na jamii sugu, jamii iliyolelewa kwa kucharazwa haiwezi kuwa na ubinadamu wa kutosha, si ilishajengewa imani ya kwamba yenyewe ni yakucharazwa tu? Kwamba ikosee kidogo (kukosea ni sehemu kubwa ya maisha yetu, kuna msemo kwamba tunajifuza kupitia makosa) nikuchapwatu sasaunategemea jamii hii iwe na amani?
Bara la Afrika linaongozwa na viongozi wababe na wenye kulipiza visasi pamoja na sababu nyingine, kubwa zaidi ni kulelewa katika jamii yenye kulipiza visasi. Unaposikia leo hii kiongozi wa serikali anasimama na kusema “mimi ndiye mwenye mamlaka yote, naweza kuamurisha fulani akamatwe na akakamatwa” bila kujali sheria na haki za msingi na bila kujiuliza katiba yetu inasemaje, unafikiri sababu nini kama sio matokeo ya kulelewa kibabe kwa kulipiza kosa na viboko?
Wanawake au akina mama ndio wachapaji wakuu wa watoto. Kumbuka mtoto wa Kiafrika analelewa na mama kwa muda mrefu zaidi. Ukipita katika mitaa yetu, utasikia wamama wakiwatukana watoto matusi ya ajabu na kuwafananisha na wanyama wakali, wachafu nk. Na hata kuwachapa makofi na viboko. Wakati huo huo wamama hao wameunda mitandao ya kupigania haki zao kwa kukataa kunyanyaswa kijinsia ikiwemo kutukanwa na kuchapwa na Waume zao, je hii ni sawa kwamba watu wazima wanaoweza kusema wakasikika wasichapwe kwani sio haki huku wao wakiwachapa na kuwatukana watoto wao?
Kwa nini tuendelee kujenga kizazi sugu chenye visasi na chuki? Kwa nini tusijifunze njia mpya ya kulea watoto wetu kwa kuwafundisha, kuelimisha na kuwaongoza?
Nilipokuwa mwanafunzi wa shule ya msingi na sekondari, nilishindwa kuelewa somo la Hisabati lakini nikaja kuliweza nilipofika chuoni. Sababu kubwa ni kwamba walimu wote walionifundisha somo hilo , waliingia darasani na kiboko mkononi siku zote na akiuliza swali kabla ya kutoa muda wa kufikiri na kujaribu na kuangalia jinsi ulivyojaribu kujibu swali, aliishainua kiboko na kukuchapa.
Viboko vinatujengea jamii sugu, jamii yenye hasira, kiburi na malipizo. Tunahitaji jamii yenye kupendana na kusameheana na sio yenye hasira na visasi.
Kama viboko vinawafaa watoto kama anavyoshauri bwana Mtebwa, basi tumchape kila mkosaji na sio watoto pekee. Tuwachape maaskari wanaokula rushwa, tuwachape viongozi wanaoshundwa kuwapatia wananchi huduma sahihi. Tuwachape na walimu wanaoshindwa kufika shuleni kufundisha, tuwachape wanaume wanaowatukana na kuwapiga wake zao. Tuwachape madereva wazembe, tuwachape viongozi wa dini wanaoshindwa kutenda yale wanayowambia wafuasi wao wayatende.
Tuwachape waandishi wanaoandika habari za uongo, tuwachape viongozi wasio waadilifu na wanaotoa ahadi hewa. Tuwachape madaktari wasiootibu wagonjwa vyema, tuwachape wanasiasa wanaofoji vyeti, tuwachape wazembe wote, tuwachape wazazi wanaoshiindwa kuwapatia haki za msingi watoto wao kama vile chakula n.k., tuwachape tuwachape………. Harafu ndipo tuone kama kuchapa ni vyema.
Sisi tunawachapa watoto wasio kuwa na uwezo wa kujitetea wala nguvu. Wanaozuia kuwachapa watoto wanaonekana kama wanaiga Uzungu. Tukianza kumchapa kila mmoja, basi tutaona jinsi viboko vilivyokuwa vibaya kwa kila mtu.
Je wewe unayemchapa mtoto akikua na kukugeuka na kutaka kukuchapa pale unapokosea utafurahi? Nani anapenda kulipizwa? Mbona tunaenda kwenye nyumba za ibada kumwomba Mungu asituchape wakati sisi tunawachapa watoto?
Ndugu Mtebwa anashindwa kutambua ya kwamba nyakati zimebadirika. Huu ni ulimwengu wa uwazi na ukweli, ulimwengu wa maoni na wa kusema kile utakacho na kukosoa bila kujali unamkosoa nani. Nimjulishe tu kwamba migomo ya wanafunzi mashuleni ni hatua kubwa muhimu ya kuonyesha jinsi watoto wanavyodai mabadiliko kwa kueleza yaliyo mioyoni mwao.
Tunaishi katika enzi za kutumia nguvu ya hoja na sio kunyamazishana kwa viboko na vitisho. Ni enzi za kuwasikiliza hata watoto. Lazima tuwapende watoto na kujua kwamba nao wana yao moyoni ya kueleza badala ya kuwachapa. Ni lazima tuwaelimishe walimu wetu na walezi juu ya umuhimu wa kuwapa uhuru watoto, kuwasikiliza, kuwapenda na kuwaelimisha kwa kuwambia jambo mara kadhaa mpaka waelewe na kujenga jamii imara.
Watoto wanahaki ya kusikilizwa, kukosea ili wakosolewe, haki ya kufanya wapendalo hata kama wakikosea wakijua kabisa kwamba kuna mtu wa kuwaongoza. Hapo ndipo tutakapokuwa tumefanikiwa kujenga jamii inayopendana na kusikilizana badala ya Usugu na Ubabe wa kulipizana visasi
maoni yakoyatasaidia kwenye muhtasari wa kitabu changu ninachokiandika cha kutetea haki za watoto.
Friday, January 9, 2009
Mungu na upendo ni kupendana
laikini kumpenda mtu ni kumkubali na kumpokea kama alivyo. ili tumjue Mungu, tunalazimika kuwa na upendo. sio upendo kwa Mungu pekee bali kwa kazi zake zote. "upendo na heshima kwa kila kiumbe cha Mungu" ndiyo njia kuu ya kupenda. nilazima nijipende, nikupende naunipende ili kukamilisha amri hii ya maumbile.
ukinipenda basi hutayajali sana mapungufu yoyote ntakayokuwa nayo kwani unanipenda. ukinipenda, utanithamini utaniheshimu na utaniamini na upendo yatupasa kumkubali kila mtu na kila kitu kama kilivyo.
penye upendo kuna kuamniniana na penye kuaminiana kuna amani na penye amani kuna urafiki, umoja na maelewano.
sio kupendana sisi tu bali na vitu vyote vilivyokaribu yetu. hatupaswi kuwa watu wa kulalamika. kwa mfano mvua ikinyesha, unalalamikia matope, kulowa nk. na jua likiwaka, unalalamikia kuungua, kuumia macho nk. na yatandapo mawingu, basi wewe unalalamika kwamba siku haieleweki, sio mvua sio jua yaani unaboreka. huu sio upendo na sio heshima kwa Maumbile na pia twazijaza fikra zetu mambo mabaya na sisi twawa wabaya pia.
ndio maana ukikuta wanampiga mwizi nawe unajiunga kumpiga bila kujiuliza maswali na hivyo tayari unahasira zako za kumallizia kwa mwizi badala ya kuwa na upendo wa kujua kwamba naye ni binadamu kama wewe, labda kasingiziwa na labda ........
Maumbile au Mungu ndiye mfano mkuu wa upendo. angalia jua liwakavyo kwa watu wote, mvua inyeshavyo, maji yatirirkavyo na kadhalika.
tukipenda tutazaa matunda mema na tusipopenda basi sisi tutakuwa wasio na maana.
hebu jaribu kupenda harafu uone furaha utakayokuwa nayo. chukulia kiurahisi kila kitu. umekosa chakula, wewe jiambie kwamba labda ilibidi leo nifunge. umekosa usafiri jiambie kwamba labda ilibidi leo nifanye zoezi kidogo la kuutembea, utaona amani itakayokujia.
duniani tumekuja kutoa upendo kuliko kupokea. ni lazima tutoe upendo bila malipo wala kudai malipo kwani tupo ili kutoa upendo huo. angalia miti itoavyo matunda bila kujali inamtolea nani, yenyewe ni kutoa tu. ardhi itoavya mimiea lukuki, miti inatoa kivuli, hewa safi upepo nakadhalika bila kujali inamtolea nani. yenyewe imekuja kuotoa.
tusipopenda nakutoa upendo au tukipenda kwa masharti, basi tutakuwa kama mti usio zaa matunda wakati wa njaa na wala usiotoa kivuli. tutakuwa kama mto utaoya maji machungu yasiyofaa kunywewa na hivyo yatupidi kulaaniwa. upendo ni muhimu sana kwetu kuutuo na kumuka hatuwezi kupendwa kama hatupendi
mwenzako akikukanynaga kwenye gari, basi jiambie kwamba ni bahati mbaya badala ya kumrukia. nakumbuka siku moja nilijikwaa na kudondoka, nilicheka na kushangaa kwa kujiuliza mara ya mwisho nilidondoka lini, sikuweza kukumbuka na hivyo nikasema 'siku nyingi sijaanguka ehe' nikainuka kwa amani na kwenda kuwasimulia wenge kwamba leo nimejikwaa na kuanguka tena.
sijui niseme nini lakini huu ndio mtizamo wangu juu ya kitu kinachoitwa upendo. jipenda, jikubali na jipokee kama ulivyo kwani ni wewe na ulivyo umekamilika!
kama dini zetu au angalau moja ingeweza kuapenda waumini wake bila kuwatenga, basi tusingekuwa na dini kibao kwani upendo ungetuvutia kwani upendo kawaida yake ni kuvutia vinavyo/wanaotafuta kupendwa.
MIMI NAKUPENDA. UNIPENDE USINIPENDE HAINIHUSU, KAZI YANGU NI KUKUPENDA TU. i LoVE u
Wednesday, January 7, 2009
Kuhusu Mungu na upendo.
Upendo ni kitu gani na nitajuaje jinsi ya kupenda? Nani ananipenda na nani nimpende? Kwanini tupendane? Kila mtu anatamani kupendwa na mtu akijua anapendwa hufurahia japo wengine huzoea kupendwa na kuishia kuchukiwa. Lakini je tunapendaje?
Wanasema Mungu ni pendo, ina maana tukipenda tutamjua Mungu? Mbona watu wanadai wanapendana lakini hawamjui mungu? Kama kristo anavyosemekana kiulipenda kanisa, ndivyo Nyerere na Mandela wanavyosemekana kuipenda afrika na waafrika kuliko wale jamaa waliokufa vitani wakidai kuipigania Afrika kama akina mkwawa mirambo nk, sasa je upendo ni nini?
Inasemekana viongozi wa dini huwapenda waumini wao kwa kuwachunga kama kondoo, japo waumini hawa wakifanya kinyume na maagizo ya viongozi wa dini hizo, hunyimwa baadhi ya huduma, je upendo upo kweli hapo? Au ndo ishara zenyewe za upendo?
Kwani wewe unanipenda mimi? Je mimi nakupenda? Unanipenda kwa sababu nayanndika haya kwenye blog, na ninakupenda kwa sababu unayasoma maandishi haya, je hi indo ishara nzuri ya upendo? Twapendana hivi?
Biblia inadai Mungu aliupenda ulimwengu na kusadaka mwanae wa pekee, wakati sote ni wana wa Mungu, kwa nini iseme mwanae wa pekee wakati sote ni wanae? Au ndo upendo wenyewe?
Tuesday, January 6, 2009
Kuhusu Mungu na dini zetu hizi.
Ebu angalia karibia kila dini hujiganmba ilivyokuwa sahihi. Mungu wa kila dini ni mzuri kuliko Mungu wa dini nyingine. Tamaduni na matendo ya kila dini ni bora kuliko ya mwingine. Mwisilamu anamchukulia mkristo kama mtu aliye potea na mkristo hivyo hivyo kwa mwisilamu na hivyo Mungu wetu sio mmoja tena bali kila mtu ana Ka-mungu kake.
Hata kwenye dini moja bado kuna Mungu bora kuliko kwenye dini nyngine. Kwa mfano ndani ya uiisilamu pekee kuna wa suni, wa shia nk. Ukiristo kuna protestants na katoliki. Ndani ya katoliki kuna karismatiki na isiyo karismatiki nk. Katika u-protestant kuna dini lukuki na mitizamo lukuki.
Kwa mfano kwenye uluteri kuna waliozaliwa mara ya pili na waliozaliwa mara moja. Kuna watakaoenda mbinguni na watakaoungua moto wa milele. Kila dini na ka-utaratibu kake na ka-jimungu kake. Viongozi wa dini karibia zote husujudiwa na kupigiwa magoti.
Mwisho wa yote dini hizi huwa ni za kusaidia watawala kuwatawala watu katika mienendo yao ya kila siku. Ndio maana vitu kama ndoa hufungwa kwenye nyumba za ibada. Eti mnaenda kwenye nyumba ya ibada, mnavalishwa chuma cha mviringo (pete) eti mmeunganishwa na Mungu. Harafu mnatia sahihi kwenye makaratasi na kuondoka kwenda kufanya kadri ya uwezo wenu.
Sasa kuna tofauti gain kati ya kuamua kukaa pamoja bila kwenda kwenye nyumba za ibada? Migogoro mingi ya mauaji ina mikono ya dini nyuma yake. Wakristo wengi hutamani kuwa sehemu ya waisrael, taifa gomvi kuliko yote.
Kwa hiyo basi, kwa kutengeneza viji-mungu vyetu na kuvisujudia, hatuwezi kusema kwamba tumekua kiroho (sipiritualy) au tumemjua Muumbaji kamwe dini zetu hazitatuwezesha kujua chanzo chetu kwamba sisi ni wamoja kwani mungu wetu ni mmoja, bali zitatufanya kukalia mnalumbano ya Mungu wa kila upande ni bora kuliko Mungu wa upande mwingine.
Yatubidi kukua kiroho sio kukuza haiba za kidini
Monday, January 5, 2009
Je Mungu wetu ni jua (mwanga)
Katika kujaribu kujua kuhusu Mungu na utendaje kazi wake, hapa kuna maswali juu ya mwanga.
Angalia ulimwengu ulivyo. Jua ndilo lisaidialo viumbe vyote kukua. Tunategemea jua kupata mwanga, joto, nk. Mwezi hutumia jua kuakisi mwanga, nyota hivyo hivyo.
Mimea hutegemea jua kwa kiasi kiubwa. Na kumbuka bila mimea, binadamu na wanyama hatuna chakula. Hivyo tunalitukuza jua kwa kutupatia chakula kwa kukuza mimea.
Wakristo kwenye biblia kuna kitu kinachoitwa nuru ya rohoni. Walokole hujiita nuru iangazayo njia sahihi. Buddha wanakitu kinaitwa enlightenment katika nirvana, ambay ndiyo buddhaland au God land. Santmat meditation wtuna kitu kinaitwa, inner light and sound.
Kwa wanaofanya meditation ya kina, wanaweza kuelezea uzuri wa mwanga wauonao kwenye meditation zao ambao huwaonyesha makuu na kuwafikisha kwa Mungu mkuu au nguvu kuu.
Sasa je, Mungu nijua/Mwanga au hufanya kazi kwa kupitia jua au mwanga?
Saturday, January 3, 2009
Tuzijize fikra zetu na mambo mazuri ya kwetu
Mwili mwingine wa nne ambao sitajihusisha nao sana hapa ni mwili wa roho. Mwili huu wa roho ukiingilia kati na kutuongoza, basi tutaenenda vizuri kuliko kuongozwa na miili hii mingine ya nyama, akili na hisia. Kwa kuanzia basi leo tuungalie kwa kina mwili unaotutawala na kutongoza ambao ni mwili wa akili.
Mwili wa akili au akili ni chanzo kikuu cha fikra zetu kwani hubeba mawazo ambayo hubeba fikra na kumbuka jinsi unavyofikiri ndivyo unavyokuwa na hii inadhihirisha ni jinsi gani kwa kiasi kikubwa mwili wa akili unatupangia na kutuamulia mambo mengi na tukiweza kuudhibiti, basi tutakuwa watu wazuri wenye amani, ridhiko, furaha na mafanikio
Mtoto anapozaliwa, akili yake huwa ni kama karatasi nyeupe isiyokuwa na maandishi yoyote kwani yeye huja duniani kwa mara ya kwanza na husubilia kufundishwa na kuelekezwa kila kitu kutokak kwa wazazi au walezi wake na mazingira kwa ujumla.
Kadri anavyoendelea kukaa duniani, akili yake hiyo mithili ya karatasi, huanza kuandikwa au kuchorwa vitu mbali mbali. Kwa bahati mbaya, akili za wengi hujazwa na vitu hasi zaidi badala ya chanya. Mtoto huanza kuona tofauti ya watu na vitu. Humwona mama, baba, maziwa, godoro, hujua jina lake na vitu vingine.
Sitaonogelea kwa undani jinsi akili inavyoendelea kukua, kwani lengo ni kuyaangalia na kuyakagua mawazo yetu na labda kuyarekebisha pale yanapojaribu kutupotosha. Kisayansi wanasema binadamu ana aina kadhaa za bongo, lakini hii pia sitaiongelea katika makala ya leo.
Basi mtoto anavyozidi kukua au sisi tulivyozidi kukua, ndivyo mazingira yetu yalivyozidi kutupangia na kutwambia sisi ni watu wa namna gani na tuenende vipi au tuwe vipi kutokana na yale yanayojazwa vichwani wetu au maandishi/michoro inayochorwa kwenye karatasi zetu (akili zetu)
Tunaonyeshwa ndugu zetu, wazazi wetu, majirani zetu na hata maadui zetu. Tunaambiwa sisi ni nani kwa njia tofauti. Tunapewa majina, tunachaguliwa dini zetu, kabila, taifa, vyakula, vinywaji nguo za kuvaa wapi na zisizo za kuvaa, vipawa vyetu, uwezo wetu, majanga na kadhalika.
Wakati hayo yote yanachorwa kwenye karatasi zetu au kujazwa kwenye bongo zetu, wengi wetu huwa hatujui kama tunajazwa vitu hivyo na hata walezi wa watoto wakati mwingine, huwa hawajui kama wanawajaza vitu fulani ambavyo mwisho wa siku huja kuviamini na kugeuka kuwa kama walivyojazwa akilini mwao.
Mazingira nayo kwa kiasi kikubwa hutupangia na kutuamulia mambo kwa ujumla. Jaribu kujikagua leo, matendo yako, tembeaji yako, jinsi unavyoongea, kucheka na hata kukasirika, utajikuta kwamba kuna mtu au watu unaowaigiza na hasa wale uliokuwa karibu nao enzi za utotoni.
Kuna baadhi ya watu ambao wanafuata dini au dhehebu walilopelekwa na wazazi au familia zao, lakini wanavutiwa na dini au dhehebu nyingine kutokana na kuzungukwa na watu wengi wa dhehebu au dini hiyo. Kwa kiasi kikubwa akili zetu au sisi wenyewe huathiriwa na mazingira zaidi ya yale tuliyoanzia maisha.
Swali ni je, mbona sisi tunazidi kuonekana wabaya, tusiofaa, tusioweza, wa kubahatisha na wenye kutarajia maanguko? Mbona sisi ni wajinga, wagomvi, wenye visasi na wenye wasi wasi? Maswali haya na mengineyo mengi yatajibiwa kadiri tunavyoendelea kuusoma na kuukagua mwili wetu wa akili na ukweli ni kwamba mambo yote mabaya sio yetu kwani sisi ni wazuri sana na tumekamilika.
Malezi tuliyolelewa sisi na tunayowalea wadogo zetu au hata watoto wetu ni malezi ya vitisho, kukatisha tamaa na kutarajia maanguko. Ni malezi ya matusi na kupigana. Ebu jaribu kukagua maaisha yako mpaka leo uone ni mara ngapi katika maisha yako uliwahi kupongezwa, kuambiwa unaweza, kuheshimiwa maoni yako hata kama ni yakitoto, kusamehewa, nk?
Mara nyingi tukiwa watoto tunaitwa wakorofi, wasumbufu, vikojozi, mitoto mibaya nk. Ni watu wakuchapwa viboko, makofi na hata kufananishwa na wanyama kama simba, paka, mbwa, mbuzi, kunguru, bata n.k sisi ni wajinga tusioweza lolote, wezi, mateja, majambazi nakadhalika.
Turejee mfano wa hapo juu wa kufananisha akili zetu tulipozaliwa na karatasi nyeupe isiyokuwa na andishi au doa lolote, tutagundua kwamba mpaka hapa tulipo, karatasi yetu hiyo imechafuka na haitamaniki kwa kiasi kikubwa. Imejaa wino mchafu, vinyesi vya ndege na wanyama. Haitamaniki karatasi hii isipokuwa kijisehemu kidogo tu cha ambacho iliwahi kupewa matumaini ya angalau ukifa utakwenda mbinguni kwenye raha zisizoelezeka kiurahisi.
Hao ndio sisi wenyewe, sisi halisi, wenye akili zilizojazwa mambo ya ajabu, kulipiza visasi na kutafuta ubaya katika kila jambo. Ni akili zetu zinazotufanya tatarajie na kuangalia yale tusiyoyapenda au tusiyoyahitaji. Sio sisi tunaofanya hivyo, bali ni akili zetu. Akili zetu zilikwisha kuambiwa sisi tuwe watu wa namna gani na tuenende vipi
Tujikague upya na kujiuliza vitu kadhaa, tujiulize ni kweli lazima tufanye mambo fulani. Hivi ni lazima tulewe ili kudhihirisha uanaume wetu? Ni kweli tusipolewa hatutakuwa wanaume? Lazima tujihusishe na masuala ya ngono kwa kujidanganya kwamba hatuwezi kujizuia? Kwani hatuwezi kuishi bila ngono holela?
Kuanzia leo tuanze kufikiri vizuri kwa makusudi, tunakila haja ya kufuta mawazo mengi tuliyolishwa na kuingiza mawazo mapya tunayoyahitaji. Tutazame na kutafuta pazuri. Tusijihusishe na mambo yanayoweza kutuharibia amani kwa kutuletea hasira na ugomvi. Tujifunze kusamehe na kusahau badala ya kujiandaa kulipiza visasi kwani tunapolipiza visasi na kubeba hasira tunaumia sisi wenyewe na sio walengwa.
Kwa wale wenye dini zao nanyi jipeni moyo mnapokwenda kwenye nyumba za ibada au mnapotafakari juu ya Mungu au maisha yenu baada ya kifo. Ni kweli kwenye nyumba za ibada tunaambiwa na kuonywa zaidi juu ya uwezekano wa kwendo motoni, kukutana na majoka makali na maumivu tele endapo hatutatenda yale tunayoambiwa na viongozi wetu wa dini au misahafu.
Unachohitaji hapa ni wewe kujiambia kwamba, mimi nitaenda peponi, mbinguni au mahali pazuri kufuatana na imani yako. Ukijiambia juu ya kwenda pazuri, basi kwa vyovyote matendo yako yatakuwa mazuri kama unavyoelekezwa. Kumbuka hapa sio kujitapa na kuwatambia wengine juu ya Mungu, bali ni wewe kuzijaza fikra zako kile unacho kitaka ili uanze kukifanyia kazi kwani kumbuka tunafikiri kwanza na fikra ndizo zinazotuongoza kufanya tunayoyafanya.
Tukiwa na fikra nzuri za amani, upendo, umoja, kusamehe, kujiamini, kuweza nk, na sisi tutakuwa wazuri na kutenda yaliyo mazuri. Usimwogope sana shetani, bali mpenda sana Mungu kwa kumfikiria na kumshangaa alivyokuwa mkuu muda wote.
Wednesday, December 31, 2008
Madarasa ya utambuzi yanaanza karibuni
Kuna wenye visingizio vya tunapenda kuhudhulia lakini muda wakazini, ohh mara umbali wa kimara, msiwe na hofu, nyie njoo jumamosi hii na utaratibu utafanyika wa kuhakikisha mnapata elimu hii endapo tu mtaonyesha kuihitaji.
Wenzangu mlioko mikoani nanyie msiwe na hofu. Tuwasiliane kwa simu namba 0754 771 601 au kwa email na kutafuta jinsi ya kufanya kazi hii adhimu.
Tupo kimara Rombo kati kati ya kituo cha Rombo na Kona katika jengo lenye langi nyeupe na bluu
Yua mositi welkamu.
Tuesday, December 30, 2008
Tulishawahi kujiuliza sisi ni nani / nini?
hiki ni kisehemu cha makala iliyoandikwa katika gazeti moja la kila wiki.....;l
Ulishawahi kukaa chini na kujiuliza juu ya wewe ni kitu gani au ni nini? Unatoka wapi na unakwenda wapi na kwa nini hii leo huko hapa au unasoma jarida hili? Ulishawahi kuwaona watu wanakufa ( kama kweli wanakufa!) na wengine wanazaliwa na bila shaka unajua ipo siku na wewe utakufa. Na bila shaka unaogopa kufa kama wengine.
Tunajitahidi kula vizuri, kuvaa vizuri kuendesha magari mazuri na kujitafutia umaarufu, tukidhani kuwa sisi ni hii miili yetu inayoonekana. Tunajaribu kuipa raha miili yetu lakini bado haturidhiki. Haturidhiki kwa sababu sisi sio hii miili, bali ni kitu kingine na labda kikubwa zaidi ya miili.
Sisi ni binadamu. Sawa. Lakini huyu binadamu ni nani/nini haswa? Ukiitwa mbuzi, paka au boga, unahisi mapungufu. Unaamini kwamba una thamani zaidi ya mbuzi, paka au boga. Kwa hiyo basi, sifa yetu na ukamilifu wetu sio kuishi tu, bali kuishi kama nani.
Tofauti kati yetu na mbuzi sio kutembea kwa miguu miwili, sio mkia na wala sio manyoya bali ni jinsi tunavyofikiri na hivyo basi, kwa kiasi fulani tunaweza kusema; sisi ni jinsi tunavyofikiri. Kwa kufikiri kwetu, tunakuwa kama tulivyo ambao ndio sisi wenyewe.
Japo kuwa twaweza kusema kuwa sisi ni uwepo na kwamba sisi kama binadamu hatuna mwanzo na mwisho lakini mawazo yetu, huathiri sana na kutufanya tuwe kama tulivyo. Wengi wetu hudhani kwamba, walianza kuwepo pale tu walipozaliwa na watatoweka pale watakapo kufa.
Hii yaweza kuwa si sahihi sana kwani kuzaliwa kwa maneno mengine ni kuuvaa mwili na kufa ni kuuvua mwili. Bila shaka ulishawahi kusikia kwamba fulani amekufa na hivyo maiti yake iko mochwari au tunaenda kuiaga maiti ya fulani. Hiyo ni maiti yake lakini siyo yeye. Utasikia mtu akiwambia kwamba, mwili wangu hauna shukrani, unanenepa hovyo nk.
Sasa sisi ni roho? Kama ni kweli mbona tunawaambia watu kwamba wana roho mbaya japo wao sio wabaya? Sasa sisi tunaomiliki hii miili, roho, akili na kila kitu, tuko wapi? Sisi ni vitu gani kama sio uwepo? Tukifa hatuendi kaburini kwani ushahidi unaonyesha kwamba inazikwa miili yetu au maiti zetu lakini sio sisi.
Mawazo yetu na fikra zetu mara nyingi vinatufanya kuwa sisi tulivyo. Tatizo ni kwamba wengi tunakuwa kama hatujui jinsi ya kufikiri hata kama kufikiri hakufundishwi mahali popote. Tunafikiri muda wote wa maisha yetu na hivyo mawazo yetu yanafanya kazi kwa muda wa masaa 24, siku zote saba za wiki na siku 365 za mwaka.
Wengi tunadhani tukilala mawazo yanasimama, hii yaweza kuwa sio kweli kwani usiku ni wakati wa ndoto mbali mbali tunazoweza kukumbuka tukiamka na tusizoweza kukumbuka. Kwa hiyo mawazo yetu hufanya kazi hata wakati tumelala.
Inasemekana binadamu anapata mawazo kati ya elfu hamsini na sitini kwa siku na hivyo mawazo yetu ni mengi na mengine huwa hatuwezi kujua kama tunafikiri. Kwa mfano, ukiwa unaongea na mtu, ghafura inzi akakurukia jichoni, huwa unainua mkono na kumfukuza bila kufikiri kwani hii imeshakuwa moja kwa moja kwako. Na hata gari likipiga honi, jambo la kwanza unakimbia kutoka barabarani bila kufikiri na bila kugeuka nyuma. Huu ni mfano wa mawazo tunayowaza bila kujua kama tunawaza.
Kila binadamu ni kamili na hamna binadamu mwenye thamani kubwa au ndogo kuliko mwingine. Kufanya au kuwa vyovyote, ni lazima tufikiri kwanza na kuamua kuwa hivyo. Huwezi kuwa mlevi mpaka hufikiri kunywa pombe, na huwezi kuwa mkulima bora mpaka hufikiri kulima au huwezi kuwa mzinzi kama hujaamua kujaza mawazo yako na vitendo vya ngono
Kufikiri kwetu kwa kiasi kikubwa kunaathiriwa na mazingira tulimokulia, tulimozaliwa, tunamoishi, na hivyo, kufikiri kwetu ni kwa tofauti.
Kwa bahati mbaya, wengi tunafikiri vibaya. Tunafikiri vibaya juu yetu, juu ya wenzetu, juu ya wazazi wetu, juu ya walimu wetu, juu ya watoto wetu na juu ya kila mtu na mazingira yetu na hivyo kutufanya kuwa sisi wabaya!
Mwalimu anafikiri juu ya kumchapa mwanafunzi hata kama mwanafunzi hajakosea na hivyo kumfanya awe mwalimu wa kuchapa-mbaya. Mwanafunzi anajiandaa kumkwepa mwalimu hata kama mwalimu hapangi kumpiga na kwa vyovyote kuwa mwanafunzi mbaya.
Katika michezo, wachezaji wa timu A wanawaona wachezaji wa timu B kuwa ni wabaya na wa timu B hivyo hivyo kwa timu A na hivyo kila timu kuonekana/kuwa mbaya na hivyo kuanza michezo ya chuki badala ya kutafuta ushindi na burudani hivyo hufanya timu zote kuonekana kuwa ni mbaya hata kwa watazamaji wengine. Wanakuwa wabaya kwa sababu ya kufikiri kwao vibaya na sio kweli kwamba ni wabaya. Jinsi unavyofikiri ndivyo unavyokuwa!
Ukifanya vizuri darasani, wazazi wanakupenda na kukupongeza, lakini ukishindwa, unakoromewa na kutwikwa kila aina ya matusi na wakati mwingine baba anamuuliza mama alikutoa wapi toto baya kama wewe bila kujua kwamba katika maumbile hakunaga kushindwa bali kuna changamoto tu.
Timu yako ikishinda, unamsifia kila mchezaji na kumwona wa maana, lakini ikitoka sare au kufungwa, basi unalalamikia kila mtu, kuanzia kipa, wachezaji, kocha washangiliaji na wakati mwingine mpaka wadhamini badala ya kukubali matokeo na kujua kwamba mmoja alipaswa kushindwa ili awepo mshindi na kwamba hayo ni matokeo na nilazima uyapokee na kuyakubali ili ujiandae kufanya vizuri zaidi mbeleni.
Tumejawa na fikra zenye kutupa hasira, kukatisha tamaa, kutaka kulipiza visasi, kuhofia ya kesho, kujutia yaliyopita, kuwahukumu wengine kwa ubaya, kinyongo, chuki na fitina! Tunafikiri vibaya pia kwa kujikosoa wenyewe, kutilia mashaka uwezo wetu na vipaji vyetu, kutarajia maanguko na kujishusha sana !
Tunafanya hayo tukidhani tutapata furaha lakini kamwe, hatuwezi kupata furaha kwa kufikiri vibaya. Furaha, amani, na utulivu haviwezi kumea mahali ambapo fikra ni mbaya. Fikra za kujilaumu na kudhani tuna mkosi wa kutosha au kuna mkono wa mtu au hatusitahili kuishi au kuwa mahali tulipo.
Huko ndiko kufikiri kwetu kubaya, kunakotufanya kuwa sisi wabaya na wakati kimaumbile sisi ni wazuri na wenye uwezo wa kuwa wazuri na tumeumbwa ili tuendelee kuwa wazuri. Ni lazima tujifunze kufikiri vizuri ili tuweze kuwa sisi wazuri na wenye nia nzuri pia na mwishowe kuwa wenye furaha, amani na utulivu wa kweli.
Tumeona jinsi fikra za waliowengi zinatufanya kuwa sisi wabaya wasio na uzuri wowote. Ukitafakari vizuri juu ya swali la sisi ni nani, basi unaweza kushangaa ukigundua kwamba sisi ni watu wanaofikiria mabaya na hivyo ni sisi wabaya. Sisi ni wagomvi, wenye wivu, walevi, wazinzi, wabaguzi, masikini nk.
Ni lazima tujifunze kufikiri vizuri ili tuwe sisi wazuri, wenye malengo na wenye mafanikio. Ebu angalia maisha yako ya kila siku, ni watu wangapi unaokutana nao wakakusifia na kukwambia mambo mazuri? Je ni mangapi mazuri uinayojiambmia wewe?
Mzazi akikuamsha asubuhi ili uwahi shule, anakufokea kwa kukuita wewe “ritoto” amka huende shule. Kwa wale wa Dar es salaam , ukifika kituo cha daladala, makonda na wapiga debe wanakufokea na kukutimua kwamba wewe ni nuksi kwakuwa unalipa kidogo. Hata wale wa vijijini hali huwa kama hii na mfikapo shule, kila mwalimu anakofokea na kukuambia jinsi utakavyoshindwa mtihani wake.
Hata kwenye ndoa, mume aanamtishia Mke jinsi awezavyo kumpa talaka asipofika vizuri na kumfokea kwa kumuuliza “ni mewanake gani wewe” nk. Mifano iko mingi ya kutuonyesha jinsi mazingira yanavyotupangia na kutufanya kuwa sisi wabaya na hivyo kuishi bila malengo na kubakia kuwa watu waliokata tamaa na wa kulipiza visasi
Tujitahidi kufikiri vizuri ili tuwe sisi wazuri, wenye fikra nzuri, malengo mazuri na wenye hisia nzuri au watu wazuri. Kimsingi kufikiri vizuri ni ile hali ya kuzijaza fikra zetu na yale mambo yanayotupa furaha na matumaini. Hii uhusisha pia maneno yetu, matendo yetu na hata matarajio yetu.

