Wednesday, March 25, 2009

eti Tanzania ni Nini?

uliwahi kujiuliza tanzania nini? swali hili lilizuka pale nilipoanza elimu ya utambuzi na kuulizwa mimi ni nani / nini? nikawatwanga jina langu, kumbe sio langu bali nilipewa na wazazi, nikaamua niwape la kanisani, kumbe sio mimi.

nikasema mimi ni mwili, kumbe naumiliki, nikasema ni akili, kumbe nazimiliki pia.

sasa mimi nimilikiye hayo nini ni?????

ndivyo ilivyo kwa wewe unayejiita mtanzania, tanzania ninini?

walokole humshukuru Mungu kwa kuwapa nchi (tanzania) nzuri, lakini je, Tanzaninia ilitoka kwa MUNGU?

mungu aliumba ulimwengu na vitu vyake, aliumba Afrika, na mabara mengine, Tanzania ni matokea ya roho mbaya ya uchoyo wa wakristo a.ka wakoloni ya kuigawanya afirka ili waitawale

kwa hiyo wajivuniao tanzania nia lazima wawe wakoloni wanaojivunia himaya yao au watumwa wanaojivunia mabwana zao na labda ndio maana ilitoka kwa Mungu waliyekuja naye wakoloni

7 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Mimi ninavyoelewa na ninavyojua Tanzania ni nchi. Tena ni nchi yenye amani,hekima na umoja pia uhuru.

Koero Mkundi said...

Hivi yule mwarabu aliyejitokeza na jina lake kutawala vyombo vya habari kuwa ndiye aliyebuni jina la Tanzania, baada ya kushinda shindano la kutafuta jina la nchi hii baada ya kuungana na Zanzibar, yuko wapi?

Nilisoma habari zake kipindi fulani, halafu wanasiasa wakaanza kubishana, mara kimya, sijasikia tena.

Duh....Hivi kumbe hata hili jina la Tanzania wamelibuni hawa hawa wakoloni.......

Digna said...

Habari za hapa kaka Kamala.

Nimepita hapa kibarazani kwako kujitambulisha kuwa nimefungua kijibaraza changu kitakachokuwa kikijihusisha zaidi na masuala ya vijana.
Nimekuwa nimsomaji wa blog yako kwa muda mrefu, na sasa nimeamua na mimi nijitose uwanjani ili kuongeza mchango katika kuielimisha jamii.
Niko ntayari kuelimishwa na kukosolewa pale nitakapoonekana natoka nje ya mstari.
Natarajia ushirikiano wako.

Digna

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

yasinta usibweteke na kung'amg'ania uliyolishwa kama vile ni msahafu kwa kufikiri ni y kweli. tanzania ina amani wakati walimu wanapigwa na rais mstaafu anaamatwa makofi? hiyo ndiyo amani?

hekima na umoja viko wapi kama sio kwenye wimbo wa taifa pekee? mbona kuna wenye nacho na msio nacho, huo ndio umoja?

koero, ni kweli jina lilishindaniwa na yakapatikana kama vile, tangbar, tanzibar, tanbar lakini TanZania likashinda.

Digna, karibu katika bolgging. tunahitaji mabinti wa kutosha bloguni! njoo usaidiane na koero

SIMON KITURURU said...

Hivi Tanzania si ni neno?
Hivi kama sio porojo, Watanzania wangapi wakifika mpakani wanaweza kustuka kuwa wako Msumbijina si Kigoma?
DUH!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

kitururu, nimefika mipakani marakadhaa na sijawahi kugundua mpaka pale ninapoona kibao na kuulizwa passport. vinginevyo nika-ujinga fulani tunakokaendekeza. unakuta jamaa eti linajivunia tanzania yake, ipi hiyo?

Shabani Kaluse said...

Hata mimi nilihisi kuwa wako ambao hawakumuelewa Kamala, niliposoma maoni ya Kaka Mubelwa niliona kama anategua kitendawili kilichojificha katikati ya ule mjadala.
kama alivyosema Koero nakubaliana nae kuwa wengi tumejifunza kutokana na huu mjadala.

Kamala ahsante kwa kusherehesha huu mjadala kwani wengi walikuwa hawajakuelewa...