Monday, March 16, 2009

Nchi yetu ni ubabe kwa kwenda mbele.

mzee kama huyu ukimwendea vibaya shauri yako. sijui ni DC mnali

Katika maandalizi yangu ya kuandaa na kuandika kitabu cha kuwasemea watoto na kuelekeza njia mpya za malezi, nazidi kukutana na changamoto za ajabu sana. Siku zote naamini kwamba kuwapiga watoto sio ukweli kwamba wanastahiri kupigwa, ila tunawapiga na kuwaone kutokana na visasi tulivyonavyo ndani mwetu.

Sasa ona visasi vinaenda mbele zaidi. Ni hivi juzi juzi tu walimu wa kule Bukoba walipochapwa viboko na mkuu wa wilaya eti kwa sababu tu wamekosa kufundisha vizuri. Yaani mkuu wa wilaya, anatibu dalili tu badala ya mizizi ya ugonjwa.

Kama kushindwa mitihani ilikuwa ni lazima, basi mkuu wa wilaya ilibidi ajue kabisa kutokea mwanzo mwa mwaka kwamba maendeleo ya elimu sio mazuri na hivyo kufanya mikakati yake vyema na hata kama suruhisho lingekuwa viboko, basi angepiga wakati wa maandalizi na sio mwisho wa kutibu matokeo.

Sasa shule zisizokuwa na tija, mtu na busara yake anakuja kuwatandika walimu ambao malipo yao ni madogo na hawayapati kabisa wala hawana miundombinu mizuri ya kuishi wala nini kama yeye mkuu wa wilaya anayeishi mjini, malipo lukuki na vikoromboizo kibao.

Sasa mzee mwenyewe naye kacharazwa makofi. Hii nichimbuko la hasira kutokana na propaganda za kijinga pamoja na kuchanganyikiwa kwa kizazi cha sasa kilicholelewa na serikali ya mwinyi mwenyewe.

Kijana alliyempachika kofi mwinyi alikuwa na umri wa mwaka mmoja wakati mwinyi anaanza kutawala na hivyo sasa vijana wamechoshwa na propaganda za kinafiki na za kipuuzi za danganya toto kutoka kwa wanasiasa eti nchi yetu ni masikini huku wao wenyewe wakiishi maisha kama ya peponi bila kulazimika kufa

Anayekwambia nchi yetu ni masikini ni tajiri wa kutosha. Sasa tunatishiwa na ukimwi eti tutakufa! Vijana wamechoshwa na upuuzi huu ndio maana wengine wamekuwa walevi, wazinzi na wabwia unga kwani maisha yanakatisha tamaa. Kila siku wanashuhudia ahadi na propaganda za kijinga.

Hii ni ishara ya hatari katika jamii yenye kupaswa kujenga misingi bora ya utu, umoja na ushirikiano. Katika kipigo cha mzee mwinyi, walitokea majamaa wengine wenye hasira za kupiga utadhani walimtegeshea jamaa ampige mzee mwinyi ili nao waje kumpiga jamaa.

Eti wanaitwa wanausalama, wapo na masuti yao kwenye joto kali la bongo, harafu jamaa mmoja anatoka huko na kuchapa mtu wanayemlinda kofi zuri la mwaka. Baadaye wanamshughulikia. Badala ya wanausalama hawa kupigana wao kwa wao sasa wanamshambulia huyu mshindi mmoja na kumpiga kipigo cha nyoka.

Namwita mshindi kwa sababu wewe ona majamaa kibao eti wanamlinda mtu mmoja, harafu bw. Mdogo anapenyeza na kumfyatua kofi wamlindaye, harafu na wao eti wanakuja kumlipiza kwa makofi na mateke.

Kumbe wao ilibidi wajiuzulu kazi mahali pale kwani walishashindwa kazi muda mrefu. Lakini hayo wanayaona? Si wanahasira na wanapaswa kumchapa makofi mtu? Hizo ni hasira. Kijana kelelewa mazingira ya kuchapwa, na wanausalamu hiivyo hivyo na mpaka shuleni kwao walifundishwa njia bora za kuchapa.

Hii ndiyo jamii yetu. Mukandara anafanya yake chuoni na wewe unayesoma hapa ikitokea jamaa kwenye daladala akakukanya, wewe! Unalalamika na kumtusi utadhani kakunyea. Ndo hivyo unalalamika na kugombana.

Ebu jikague uone ni mara ngapi unatenda mema au kuongea vizuri, ni matusi na malalamiko badala ya shukurani. Ukienda kwenye jumba la ibada basi unaambiwa ulivyotenda dhambi na utaenda motoni. Maisha yanakuwa magumu, yanatisha na kuogofya na hivyo tunaishi kupigana.

Tumekuwa wakali kuliko hata simba. Sasa hasira zetu zote wanakoma watoto. Kwenye daladala tunawasimamisha eti kwa sababu wanalipa ela ndogo, wababa wanatongoza vibinti na wamama wanatongozi vivulana.

Tunawaonyesha picha za ngono na kuwaathiri kisaikolojia na kuwaalibia masomo. Walimu wanawachapa ila wakichapwa walimu ni kinyume cha haki za binadamu. Akichapwa mwinyi ni kuffungo cha mwaka na mateke ila wakichapwa walimu DC anaonywa na kubadilishwa kazi au kufukuzwa ila wakichapwa watoto bwana yesu asifiwe! Wanawajengea nidhamu! Asifiwe kwa lipi?

Toka lini yesu akawanyanyasa watoto zaidi ya kuwatetea na kuwaokoa dhidi ya mijianafunzi yake nyenye kiherehere? Soma matayo19:5

Yaani ni hasira kwa hasira visasi hakuna kusamehe wala kuchukuliani. Wazazi wanawapiga watoto, walimu wanawapiga wanafunzi, viongozi wa dini wanawatishia waumini, waume wanawapiga wake zao na wake wenyenguvu wanapiga waume zao.

Polisi inawapiga wanafunzi na mgambo inawapiga vijana wanaojitafutia ajira a.k.a machinga, na sasa vijana wameanza kuwapiga wakuu wa nchi na tuone nani mjanja sasa!

4 comments:

Koero Mkundi said...

Wale wazee wa BUKOBA, walidai kuwa yule DC ni shujaa, kwani amewakumbusha enzi za jeremani!
Ni Viboko tu.....

SIMON KITURURU said...

Ama kweli Tanzania tuna Amani!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

koero,maana ya katerero ni mahali pa kupigia viboko na labda ndio maana walifurahia.

Mzee wa Changamoto said...

Maoni yangu yako kwenye aya mbili za mwisho. Nadhani ume-conclude hapo. Yaani kila mtu amsake mnyonge wake kisha "amtandike".
Tutafika?