Monday, March 30, 2009

Prof mbele. mkomavu wa mijadala

Nilikutana na prof mbele kwenye kibaraza cha ruhuwiko. Nilikuta makala iliyonichanganya nikashindwa kujua usomi ninini. Basi nilibishana na mbele kwa akishirikiana na yasinta kwa muda mrefu.’

Mjadala ulikuwa mrefu na mpana kiasi cha watu wengine kuanza kuchukia. Kama kawaida yangu huwa siifichi kweli. Kweli kwangu huwa inatoka ikiwa uchi wa mnyama. Nilichofurahia katiaka makala hiyo ni juu ya ukomavu wa kidemokrasia au utu wa prof Mbele. Prof. Alikubali kujifunza kile tulichotofautiana mpaka akakubali ukweli.

Mjadala ule ulirefuka kiasi cha baadhi ya wachangiaji kuja kwa hasira wakinishambulia. Baadhi akiwemo
bwaya walaianza kulaumu lugha niliyotumia. Hawa walitoka nje ya mada. Niongee kihaya au kichaga, muhimu ni ujumbe. Hawa walihofia kutokukamilika kwa kihisia kwamba nitazua zogo.

Sijui kama walikuwa wakimpa pole Mbele kwa kumonyesha walivyokuwa na maneno matumu huku wakamacha mada au walijaribu kuwa walezi wangu wazuri. Hata hivyo prof, alielewa somo, akijifunza kutoka kwangu na mimi nikajifunza pia kutoka kwake.

Kumbe duniani hakuna matusi bali kuna tafsiri na hivyo kwa kuyatafsiri vizuri maneno yangu, prof aliweza kupata somo zaidi na mimi na yeyeyote aliyeusoma mjadala huo kwa lengo la kujifunza, alifanikiwa na kupata somo pia.

Namshukuru sana mbele na wapenda mijadala, tuendelee kugongonisha mawazo bila kuamshi hisia wala kuhemkwa. Tunaweza kujifunza hata kutoka kinywani mwa kichaa endapo tutamtafisiri vizuri. Karibu kijiweni.

tembelea mjadala hiyo
hapa na hapa.

9 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Kamala inafurahisha kusikia ya kuwa wote tumejifunza kitu. Hicho ndicho kikubwa kujifunza.

Koero Mkundi said...

Hata mimi nilijifunza pia, kweli mjadala ule ulikuwa na lugha gongana ... hakika nimepata elimu ya bure kabisa

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Prof. Mbele ni mmoja kati ya wasomi waliobobea na wenye upeo mpana sana. Jaribu kusoma vitabu vyake pamoja na makala zake nyingi utaona. Mimi ningekuwa raisi ningetenga fungu kutoka katika mabilioni yanayorudishwa na mafisadi kwa ajili ya "kuwarubuni" baadhi ya wasomi kama akina Prof. Mbele kurudi nyumbani. Nikiwapa mashangingi ya bure na nyumba pamoja na mshahara wa "kibinadamu" sidhani kama wangekataa ukizingatia kwamba wengi wao wana "unyerere" mwingi tu katika damu zao.

Egidio Ndabagoye said...

Mijadala mitamu ni ile yenye kuleta migongano.

Bwana Masangu Raisi Kikwete namsoma kila mara akienda ughaibuni anawaambia watanzania warudi,lakini hasemi wakirudi wafanye nini.Yeye anasema kazi zipo na wakati nchi kauza kwa walowezi waliowabatiza jina wawekezaji.

Bwaya said...

Tunazo sababu za kujivunia ukwasi wa maarifa alionao Profesa Mbele. Ni bahati kuwa tunao watu wa aina yake katika blogu. Tunayo mengi mno ya kujifunza kutoka kwake.

Mzee wa Changamoto said...

Nilisema kuwa tukiangalia "tone" ya mwandishi hatutasonga mbele. Bali tubanane kwenye "point of view" na kujali migongano katika uhalisia na kuacha kumfikiria mtu kihisia.
Nani aliyesoma mijadala ile akashindwa kutambua kuwa Prof Mbele si msomi tu, bali muelewa.
Ni furaha kuwa na watu ambao wana uelewa mkubwa na wanautumia kuielimisha jamii ambayo ni kama "inatengwa" na wenye kudhani wana uelewa.
Heshima kwako Prof Mbele na Kaka Kamala kwa kurejesha shukrani kwa mafunzo tuliyopata na tunayopata

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

massangu, sio lazima wasomi warudi nyumbani ili kutuletea maendeleo. hatua ya akina wewe kama msomi, mbele na wengineo kufngua blog za kiswahili na tena kuwa tayari kubishani na vijana wadogo bila kujali lugha zetu, wanaishia kutufundisha mengi na kutuambukiza usomi wao.

siamini kabisa kwamba ili uwe msomi unahitaji vyeti na kuvuka madaraja, bali kuelimika, ukabadilika na kuisadia jamii.

sio lazima wasomi waajiriwe serikalini na sio lazima tutumie gharama lukuki kuelimisha 'wateule' wachache, bali kwenye mijadala ya wazi kama hii na mengineyo, tunaelimisha jamii pana.

badala ya kutumia usomi wetu kutumikia watu wachache, tunautumia kuelimisha jamii kubwa na pana zaidi.

koero ulijawa na woga sana juu ya hoja zangu ehe? mpaka ukanionea huruma. ukijisimamia na kujiamini, inapendeza sana na inasaidia kuwapa wengine ulicho nacho nawe kupata kikubwa zaidi na wengine kukiremba zaidi.

daima tunajifunza zaidi kwa misuguano. ni kwa kusuguana kwa njiti na mgongo wa kiberiti ndipo moto unawaka, ni kwa kusuguana kwa sehemu ziitwazo za siri mimba zinakuwepo na watu kuongezeka duniani. ni kwa misuguano mimngi maendeleo huja.

fred katawa said...

Kwenye ule mjadala ulisema kuwa hauna lugha tamu kwa kuwa umekulia kijiweni.Mbona hapa umeonyesha kuwa huenda ulikulia kanisani au msikitini?

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

fred, labda hilo ni moja kati ya mambo niliyojifunza kwamba lugha ya kanisani na mskitini inahitajika kidogo.