Friday, March 20, 2009

utumwa wa kiakili na kiroho vs ule wa kimwili!

utumwa wa kialakili na kiroho, ni utumwa mbaya sana na mchafu kuliko ule wa kimwili. walikuja wakoloni, wakatutawala kwa nguvu, mambo yakaonekana sio mabo kwao, basi wakabadilisha stairi yao ya kutawala, badala ya kutupeleka kwa mbinde, basi wakahamia kwenye akili na roho.
waliamua kutupeleka kanisani na misikitini kwa kutubatiza, huku wakitukana ibada zetu za asili kuwa ni za kishenzi, kipuuzi, uchawi, ushirikina na ushetani. wakati hayo yanafanika, walibatiza watu wetu majina yanayofahamika kwa Mungu na kuondoa ya kishenzi, yaliyofahamika zaidi kwa Mungu wa kiafrika.
wakaja na kuendelea kututawala, na picha za kuonesha yesu na Mungu wakiwa wazungu huku Shetani akiwa muafrika mwezetu yaani mweusi. kama vile haitoshi, waliendelea kujenga ngome zao za kivita au maandaki ya kujificha, huku wakiyahita makania. ukitembelea manikanisa yote yaliyojengwa na wkoloni au wakristo, kama akili yako ni nzuri, hutashindwa kuona kwamba ni handaki au pango la kujificha, japo sisi tunadhani ni nyumba ya Mungu!
ujinga huu uliendelea wakati wakiwapiga watu wetu na kuwalazimisha kubatizwa na kufuata imani za kikoloni ili wataawale vizri na ndio maana mpaka leo kuna watu wanaojiita wakrist au waisilamu hapa nchini bila kujiuliza kuwamba kwanza mababu zao walilazimishwa kujiunga na dini hizo, lakini pia wenyewe hawazieelwi dini hizi japo wanazifuata tu kimsukule. dini za ugomvi, za ubaguzi za shali wakati Mungu wetu ni wa upendo, hana ubaguzi wala upendeleo wa taifa au kabila lolote lile.
baada ya kutubatiza, wakajai na ujinga wa kutupumbaa kupitia elimu zao za kizungu. mpaka sasa hatujiulizi ni kwa nini dini hakuna dini hata moja yenye makao makuu hapa Afrika, zote ni ulaya na marekani na picha za mitume wao wanaonekana kuwa wakwao na sio wa afrika.
eti tumesoma, elimu inatulazimisha kukumbatia hata upumbavu wa wa zungu, kisa? wametusomesha na kutupangia jinsi ya uishi, pia sauti yao ni ya Mungu kwani ndio wachapishao vitabu vyote vya ibada na kuiviuza huku tkkilazimishwa kuvinunua na kuvisoma utadhani bila wao tusingeishi.
wanaojiita wasomi sasa nao wamekaa kumtukuza mzungu badala ya kutafuta njia zao na mawazo mapya. elimu inatufunga kiujinga tu kiasi kwamba mtu akisome udaktari, basi kila mtu anayemuona sio mtu bali ni mgonjwa. hivyohiyo kwa mfanyabiashara, yeye anaona wateja tu na wala sio watu wao. kilichobaki ni mtu asiyejua kiingereza, bai ni mjinga. ndo elimu hiyo ya kuona ulaya na kuleta kwetu. kila kitu tunaiga tu.
hata hivyo oelimu na dini hizi hatujaweza kuona kwamba hazitufai kwani miaka yote hakuna maendeleo na utu vya kueleweka, bali majigambo vurugu na unyama wa kutisha duniani. kwa mfano hakuna msomi aliyekwisha kugundua kwamb pamoja na elimu hizi na dini, bado jamii inakuwa ya kilevi, ngono, starehe na ulokole. mpaka sasa papa wa kikataoliki anaelekeza watu jinsi ya kufanya ngono wakati inasemekena yeye hafanyi na hajui utamu na uchungu wake badala ya kuangalia matatizo ya binadamu.
tumelagahihiwa kuwa kuna watu wa ulaya ndio wanaomiliki funguo za kuingilia mbinguni. bila kufunguka macho tuakakaa kug'ang'ania ujinga wa kikoloni kisa ni wawazungu, basi hali ni hatari. tunashindwa kuona jinsi elimu na dini za kizungu zinavyotupoteza lakibado tunaiga tu kisa ni za wazungu bila kuhoji. tunasahau utu wa mwafika alioishi nao vyema kabla ya kuja kwa wakristo au wakoloni.
naishia hapa kwa leo, endeleeni kutawaliwa kiakili na kiroho. sijui upi ukolono mzuri kati ya ule wa kimwili na wa kiroho!

8 comments:

SIMON KITURURU said...

DUH!

Ngojea niende kukojoa kwanza:-(

Masangu Matondo Nzuzullima said...

"The most potent weapon of the oppressor is the mind of the oppressed" Steve Biko.

Ni kosa letu wenyewe. Tusilaumu mtu!

Chacha Wambura said...

Tangu leo naacha kusoma 'The New Earth!!!'

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

kitururu, unakojoa mara ngapi mpaka urudi?

matondo, lengo sio kumlaum mtu ila ni kuonyesha udhaifu uliopo pale tunapodhani pana msaada kwetu na hivyo kutuwezesha kutafuta njia mpya za maisha.

Luangisa aliwahi kuonya juu ya kumtuma mtu mwenye njaa akawaanglie maenbe, akipanda juu atakula kwanza na kushiba kisha kukaa hukohuko mpaka asikie njaa tena. hao ndio wasome wetu na tatizo letu kama hujuligundua na linakuhusu pia

chacha, ukiacha kukisoma, basi ntakichambua na kukiweka hapa ili ukisoma hapa bloguni. kumbuka baniani mbaya.........

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Kamala, Luangisa ni nani? Wakati ule nikiwa Kahororo jamaa mmoja mcheshi aitwaye Luangisa alikuwa anagombea ubunge na alishinda. Sijui sasa yuko wapi.

Je, huyo aliyetumwa maembe akiyaleta yataliwa na nani? Pengine yataliwa (au kuhifadhiwa) na watu wachache tu - tena ambao hawana njaa na hawayahitaji. Akiwa na ugunduzi huu - mimi nadhani ni sawa tu hata abakie huko huko mtini, hasa ukizingatia kwamba hana njia ya kuyafikisha hayo maembe kwa wanaoyahitaji hasa bila kukwaruzwa na waliomtuma. Na kazi yake mara nyingi haina shukrani- Anaweza kujitolea na kuyaleta maembe lakini shukrani watapewa waliomtuma na siyo yeye. Hata akibakia huko huko mtini mimi kabisa simlaumu!!!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

matondo, ndo huyo huyo aliyekuwa akiongea vithembe kila wakati na sasa ni meya wa mji wa bk.

tutendapowqema tusingoje shkrani twende mbele ili tufut\rahie wengine waafanikiwapo kupitia kwetu kama walivyofanya akina kristo

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Enzi zile Luangisa alikuwa akijinadi "mimi nawathindaga ivi ivi na huyu nitamthinda!" Na kweli akashinda ubunge.

Halafu leo umenifurahisha. Kwa mara ya kwanza umemtaja Kristo katika mtazamo chanya! Katika komenti zako nyingine kwingineko nilikuwa nimepata picha kwamba wewe na "Mungu wa Waisiraeli" kamwe mlikuwa hampikiki chungu kimoja. Isije ikawa umeokoka bwana. Tuseme Aleluya au tusubiri???

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

aisee
kuna tofauti kubwa sana kati ya kristo na Mungu wa israel kama hujui.

mimi simchukii kristo, napenda sana maneno na mafundisho yake yalikuwa ni matumu kwa kiasi chake na kwa kweli alikuwa mtu mwema mwenye mfano wa kuigwa.

mimi ninatatizo na dini zetu za leo ukiwemo ukristo ambao hakuuanzisha kristo mwenyewe na unaofuata maagizo ya mwanadamu yasiyo kuwa ya kristo wala nini.

kuokoka kwanga haitakaa itokee mpaka mwisho wa dunia au labda sielewi ulokole ninini!

luangisaa aliwasindaga mpaka akaamua kuwa mpole tu