Wednesday, April 8, 2009

Binadamu wote ni sawa!

Hii ni kauli uliyosikika sana hapa nchini Tanzania ‘enzi za mwalimu’. Ni kauli nzito ambayo mpaka leo inaonekana kama ni ya kigeni. Kuna binadamu wanaojidharau kwa sababu za kukosa fedha, kuwa na maumbile tofauti, na hivyo hivyo kuna wanaojikweza kwa kuwa na utajiri au kuwa na maunbo yanayoaminika kuwa mazuri zaidi.

Kuna mataifa yanayojiona bora kuliko Mengine, na makabila pia. Kuna wanaothamini watu wa makabila yao tu na kuwadharau wengine lakini wanasahau tu kwamba makabila yao pia sio yao bali walizaliwa tu mahali pale na hivyo sisi sote kama binadamu bado ni sawatu. Dini je! Mwisilamu na mkristo hawapatani, mkatoliki na mprotestanti nao wanazarauliana. Hata ndani ya dini hizo kuna ubaguzi kati ya wale waliokaribu na kiongoza wa dini, wanaohudhuria sana na wale wanaotoa sadaka kubwa za kutosha.

Ndnivyo ilivyo, tunadharauliana. Kazini kwako salamu unayompatia bosi ni tofauti na ya wafanyakazi wengine, bosi akikooa unajipanga vyema! Na bosi naye anakuchukulia hivyo hivyo. Unawadharau watu wa fulani na kuwatukuza wengine. Ubaguzi mapaka dunia imegawanyika. Nchini Tanzania kuna wenye nazo na watu wa kawaida.

Vitabu vya dini vinatuasa kuwapenda wote mpaka maadui zetu, lakini kwa ubaguzi huo huo tunavitumia vitabu vya dini kubaguana na kuuana. Wana wa Israel wanawauwa wapalestina ili wapate ardhi, na wapelestina wakipata nafasi wanawaua WaIsrael kwa sabubu tu ya ardhi nyuma ya pazia la imani, imani zinazotuambia kuwa sisi sote ni sawa mbele za huyo tunayemwamini.

Yaani tumejisahau na kupotoka, tumekumbatia mali za dunia hii na kuwabagua wenzetu. Sasa kuna watoto wanaoitwa wa mitaani kumbe ni watoto kama wengine tu. Tunafanya manyanga na upuuzi bila kujua, huku tukibaguana sisi ambao ni wamoja na wanaopaswa kupendana.

Unataka ushahidi kuwa mimi wewe na yule ni sawa bila kujali fedha, cheo, kabila au taifa lako? Ukipata ajali na gari lako likakulalia, au moto ukishambulia nyumba ulimolala humwiti mkeo ndugu au mtoto, unalia ukiita msaada, msaada msaada. Kwani msaada ni jina la mtu? Hapana ila ni huduma ambayo anaweza kuitoa mtu yeyote na utaupokea tu. Sasa kwa nini tusilitambue hili kwamba wenzetu ni muhimu kuliko sisi ndio maana hutuwezi kujipatia msaada mpaka wao waje?

Bado sisi ni wamoja tu. Sisi wote tunapumua hewa moja ile ile. Tunakula chakula kilekile tunaishi maisha yanayofanana. Sasa itakuwaje wengine wanajiona wazuri kuliko wengine? Mbona sote ni wazuri mbele ya muumbaji?

Unamwani Mungu ehe? Wakati mwingine nivigumu ku -mwamini Mungu anayesemekana kuwapenda watu fulani pekee wakati Mungu huyo huyo huduma zake zinafanana kwa wote na huwagawia wote sawa. Hewa tunayopumua, mvua, jua, upepo nk. Uliwahi kukona huduma hizi haziwafikii baadhi ya watu unaofikiri Mungu hawapendi?

Bila kunipenda mimi au huyo jirani yako huwezi kumjua Mungu na kumpenda kwani yeye ni pendo na anajulikana kwa kupenda tu kama wewe ulivyokuwa na Moyo wa kupenda ila unaufunikia kwa pazia la ubaguzi. Uliwahi kuona daktari asiyeweza kuwatibu watu wenye rangi tofauti? Si mtu akisomea udaktari anatibu watu wote? Sasa iweje leo umbagua Albino eti kwa sababu mna rangi tofauti?

Labda ndio maana taifa fulani linapigania masuala ya Kimungu dhidi ya taifa lingine lakini mataifa yote hayo kati ya mpigaji na mpigwaji yanaendelea kupata baraka za Mungu huyo huyo mmoja kuanzia hewa, maji, chakula, mvua, jua, joto baridi nk. Kama kuna linalopendwa zaidi na Mungu ni kwa nini Mungu asilinyime hewa lililisilopendwa ili lifutike na life kabisa? Anayapenda yote, ni ubaguzi wetu tu

Kumbuka sisi wote ni wa moja na tutarudi kwa huyo huyo Mungu (Muumbaji) kwani sote tu wa Moja! Muumbaji na maumbile yaliumba watu wa rangi tofauti ilikupendezesha ulimwengu. Kamwe huwezi kukuta mpaka rangi akiwa na aina moja tu ya rangi, lazima ziwe nyingi ili ukuta uonekane mzuri na ndivyo hivyo tulivyoumbwa weusi, weupe nk ili ulimwengu uonekana vizuri na lugha mbali mbali.

Wote tutarudi kwa Mungu. Uliwahi kuona bahari yenye maji tofauti? Hapana. Bahari hupokea maji kutoka pande zote za dunia lakini maji yote yakifka baharini ugeuka na kuwa sawa, kuwa kitu kimoja, rangi moja na chumvi ile ile, basi ndivyo ilivyo kwako wewe, na yule jamaa wa dini nyingine, au kabila umchukiaye. Si umeona nyote unapumua hewa moja? Kama ilivyomaji ya bahari, mtakuwa wamoja na kurudi kwa Mungu mmoja mkuu

Mimi,wewe na yule ni sawa na ni kitu kimoja na tutaendelea kuwa wamoja tu.

1 comment:

Mzee wa Changamoto said...

Mmhhhh!! Nadhani nimejifunza kuliko ninavyoweza kuchangia. Asante kwa maarifa