Monday, April 6, 2009

Hivi kwa nini wakristo wanajiofa wako sawa kuliko wengine?

imani kwa matendo ni kujitafuta ndani na kuona ukweli badala ya kuambiwa habari za kutia moyo juu ya kesho (maisha baada ya kifo)

Najiuliza swali hili kutokana na mikusanyiko na majadiliano kadhaa ya kimaisha na karibia katika blogu zetu hizi. Kila ukikutana na mkristo ukamweleza juu ya dini yako, anakwambia kuwa wewe hauko sahihi, yaye ndiye anayeabudu Mungu katika roho na kweli.

Sasa najiuliza ni kwanini mtu anapinga imani asiyoijua? Siku zote mkristo anapenda umuige na kumfuata yeye kuwa ndiye anayefanya imani za kweli na zinazokubalika. Za kwako ni za kishenzi tu. Yaani inakera wakati mwinginine. Watu wanapenda ufuate wanachokifuanya wao bila kuhoji.

Ukristo ni imani ambayo hupaswi kuuliza maswali na ukiuliza inabidi uulize maswali Fulani pekee na ukiuliza mengine, basi umekufuru inabidi utengwe na waaminia mahiri juu ya imani hiiyo. Hata hivyo wakristo hawajaona kuwa imani yao ina mapungufu kadhaa kwani bado wafuasi wake hawatendi yale waagizwayo na wengi hutenda maagizo ya wanadamu na wala sio ya yesu mwenyewe.

Hata hivyo ukristo inabidi uishi tu harafu utaingia mbinguni ukisha kufa na wanaamimini katika ufufuo wa mwili wakati roho haina mwanzo wala mwisho.
Mimi naamini katika imani ambayo nadhalia au maneno ni kidogo lakini matendo ni mengi na ndiyo yanayotawala. Unatenda na kuona ukweli mwenyewe sio mpaka aje sijui nani na hotuba zake za kuandika ili akwambie ufanye nini.

Hivi usahihi uko wapi kati ya kutenda na kuyaishi unayoyaamini na kufuata mkumbo kwa kuamini usiyoyatenda na kuishi kama msukule?


uisilamu nao unaamini kuwa ndiyo dini sahihi pekee ya Mungu zilizobaki ni bomu! yaani vitu vingine bwana. sijui ni llini sisi tutatafuta kweli na kuifuta. ni lini tutajitafuta sisi wenyewe na kukgundua kuwa Mungu wetu yuko ndani mwetu na tunaweza kumpata kwa kujitafuta wenyewe ndani yetu? si yesu mwenyewe aliwaambia kuwa ufalme wa Mungu uko ndani mwenu? mtume mohammad je na vita ya nafsa?


9 comments:

Yasinta Ngonyani said...

"ni lini tutajitafuta sisi wenyewe na kukgundua kuwa Mungu wetu yuko ndani mwetu" Kwa hiyo Kamala kila huna sababu ya kuyumbayumba. Ni imani yako tu.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

yasinta Mungu kuwa ndani mwetu sio imani na sio hadith, ni uhalisia, ni reality, halina ubishi ni kwa kujua tu jinsi ya kulitafuta. hii sio imani hata kidogo plz. jifunze uone na sio usubiri kufa

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Daima mwamba ngoma huvutia kwake. Hata ndani ya Ukristo wenyewe kuna madhehebu mbalimbali na kila moja linaamini kwamba ndiyo liko sahihi na wengine ni wababaishaji tu. Wasabato, Wakatoliki, Wapentekoste, Walutheri n.k, n.k...Hata ndani ya Uislamu wenyewe pia kuna makundi. Ni nature yetu kuamini tukiaminicho, kukipigania na kuwafanya wengine pia wafanye vivyo hivyo. Ndiyo maana watu wako tayari kufa wakipigania imani zao.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

labda matondo umejibu swali la wakristo na imani zao lakikni ni too much. ni lazima waache wengine waamini waam inivyo na hata kama hatuko upande wao, tuna kila sababu ya kuhakikisha angalau tunajua imani zao juu ya wanachokiamini na sababu badala ya kuwainga na kutaka kuwabdilisha.

imani ya kujitafuta na kujenga 'inner strength' sio ya mtu bali ya kila mmoja. ni kitendo cha kuamka tu na kujigundua na wala sio hadith na siokuamini asecho fulani, bali ni kufanya ukaona matokeo wewew mwnyewe. dininyinginezo husubilia siku ya mwisho ili mkipate cha moto wa petroli

SIMON KITURURU said...

Kamala jaribu kutembelea tena Wayahudi ambao wamefikia kujiamini hata ktotaka kukushawishi wewe uwe Myahudi kwa kuwa wewe usiye Myahudi sio safi. Wapitie tena Waislamu ambao wapo watakao kushauri ujiunge na ukikataa unaweza kuuawa kwa kuwa wewe ni InIFIDELI. Cheki wahindi wa kihindu uangalie wanafikiria nini kuhusu waislamu wa kihindi au hata wawaitao UNtouchables.

Sijaona hata dini moja iitwayo dini isiyona kasoro uziongeleazo kwenye yako atiko.

Carlos said...

Iwe mashaija nogambaki? Siyo kwamba sipendi na wala napinga mijadala ya dini la hasha. Lakini ulivyoaandika inaonyesha wewe unamsimamo mkali kuliko hata hao unao washutumu. Majumuisho kwamba 'wakristo' kwa kiingereza kuna neno linaitwa "fallacy" kiswahili chake nadhani ni kukengeuka(nitafuta). Ndio kusema huwezi tu, mathalani, kusema "kila mtu anafahamu hivyo." Nikiuliza hapa barazani kama kuna mtu anafahamu Maskati fisi iko mkoa gani sidhani kama wote wanaweza kunijibu. Nikifuata ujumuishaji wako nitasema, "mbona kila mtu anafahamu." Kwa hiyo kusema wakristo nikukengeuka kwani wako mabillioni sasa wote hawa utawawekaje katika kundi moja kwa sababu tu unafahamu, mmoja, kumi, alfu au hata laki? Mimi hapa ni mkristo(siandiki haya kwa sababu hiyo) lakini sina mawazo hayo ulioyasema na mke wang ni Muislam sasa kama ningekuwa kama unavyodai wewe ningeo muislam?
Halafu maada umeweka wakristo aya ya mwisho ukawageukia waislamu ni watu gani hasa uliowalenga hapa? Dada Yasinta kakupa ushauri mzuri sana kwenye sentensi ya mwisho, labda kama hao wanaokubugudhi wanakutishia maisha lakini kama suala ni kupinga unachoamini wewe fuata hayo maneno ya sentensi ya mwisho. Matondo naye kakupa maneno mazito tu lakini naona unamwekea maneno mdomoni kuwa kawajibia wakristo wakati kakupa hulka ya binadamu ambayo ama kwa hakika wewe ndiyo unainyesha waziwazi maana kama watu watabaki wakristo kwako wewe watakuwa wanakupinga na hawataki uamini unachoamini. Tatizo lako hapa ninalo una ni neno UKRISTO na wala si matendo ya hao wakkristo.

Carlos said...

Oooops!
hapo kwenye mabano nilikusudia kuandika 'nitatafuta' na siyo 'nitafuta' nikimaanisha nitatafuta tafsri ya neno fallacy.
Kunradhi.

Mzee wa Changamoto said...

Dah!! Dini ni issue nyingine kabisa. Maana japo twaamini sote tutaenda mbinguni (na wakati mwingine twaamini kuwa ni mbingu moja tutakayoenda), lakini bado tunaamini njia za kutufikisha huko ndio zitushindazo.
Lakini sina jibu la swali la KWANINI ila naamini kuna haja ya kujiangalia vema kujua kilichomo ndani mwetu kwa ajili yetu na mbingu zetu kwa maisha yetu yajayo.
AMANI

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

kitururu,tatizo unaloliongelea ni sawa na nililoliongelea kwa njia tofauti sasa kwamba kuna upande mwingine wa kujiona tuko sawa kuliko wengine.

carlos nenio fallacy mimi nalifananisha na fyongo. ni kweli mpo kama wewe wenye wake waisiliamu, lakini viongozi wako wa dini wanakwambiaje na kukufananishaje? je wanakupa zile mnaita haki za mkristo? ukristo si una msemaji wake ambaye kwa vyovyote hawezi kufungisha ndoa kama ya kwako? si unaambiwa pia hutaingia mbinguni pia?.

mzee wa c/moto, mbingu na maisha ya mbingu unayo hapa hapa na nilazima uanze kwa kuyaishi hapa ndipo uende mbinguni vinginevyo unajipa moyo na kusubilia re-incarnation nyingine na nyingine