Wednesday, April 1, 2009

kifo na maluweluwe yake.

mida kama hiyo sara huwa muhimu kwa ujinga wa kujipendekeza kwa umwobaye

pepe hii imetoka kwa ndugu yetu Chacha wa Musoma....


Mdau, jumapili tarehe 29 March nilisafiri kutoka Mwanza kwenda KIA Kilimanjaro kwa ndege aina ya ATR 72 mali ya kampuni ya PrecisionAir. Tuliondoka katika muda ulopangwa yaaani saa 7.40 mchana tulitarajiwa kuwa KIA baada ya muda wa saa 1 dk 10 hivi. Tulianza safari vizuri kwa mujibu wangu kutokana na uzoefu wangu lakini kwa wenzangu walidai kulikuwa na matatizo wakati tunaondoka. Tulisafiri kwa muda takribani dk 30 hivi na ghafla tukasikia ile kengele ya kumuita muhudumu ikilia mara tatu mfululizo. Mhudumu wa kike alkwenda katika chumba cha marubani na kwa haraka tulimuona akirudi haraka huku kwetu tokea chumba cha marubani. Kisha kengele ikagongwa tena mara tatu tukamwona mhudumu wa kiume aitwae S Mukama akienda kwa haraka huko kwenye chumba cha marubani na hatukumwona tena akitoka. Kilichofuata ni ndege ikipanda na kushuka hewani kama vile gari aina ya Corolla ikipita katika matuta ya viazi kwa kasi ya ajabu. Wakati hali ya mtikisiko ilipoanza ndipo nilipoanza kusikia na kuona vituko humo ndegeni. Vituko hivo ni pamoja na watu kukemea mapepo kwa jina bwana…; kupiga kelele na mayowe kibao. Nilikaa na rafiki yangu mfanyabiashara mmoja mwanye asili ya india na alionekana kupata shida sana na aikuwa mmojawapo wa wale walokuwa wakipiga kelele sana wakati ndege ilipokuwa ikishuka na kupanda. Bila shaka mnakumbukwa wale Vijana wanavosema katika vichekesho vyao vya ‘presha inapanda presha inashuka!’
Ndege ikageuka na kurudi Mwanza kwani tuliona ziwa na baadhi yetu tukadhani tumekaribia ziwa Manyara ndipo tulipoangalia na kung’amua kuwa tulikuwa tunarejea Mwanza. Mhudumu wa kike akasema kuwa ‘ abiria fungeni mikanda tayari kutua mwanza’. Tulitua kwa kasi ya ajabu na breki zilikuwa zikikanyagwa utadhani fisi mwoga akimbiaye mtu mwenye kijiti kiwakacho moto. Ile kusimama tu kila mtu alinyakuwa mzigo wake toka kwenye kebini ya mizigo kana kwamba ndege ingewaka moto. Mhudumu wa kiume alitoka katika kebini ya rubani akiwa anatokwa machozi na mwenzake alimkumbatia huku naye akilia! Muhudumu aliwaomba watu warudi vitini ili ndege iende kupaki. Walitii amri hiyo na kurejea vitini mwao na ndege ikaenda kuegeshwa.

Tulishuka na ndipo tukaambiwa kuwa rubani Mosha alokuwa anaiendesha alipata dharura kama vile ya mshituko wa moyo ama tumbo kali likamfanya awe ‘incapacitated’ kwa mujibu wa watu wa precisionair. Na hivo yule mhudumu wa kiume ndo alisaidiana na rubani msaidizi ambaye pia ni mwanafunzi kutufikisha ardhini! Walituleleza kuwa wataleta rubani mwingine toka KIA kwa ndege charter hivo Tulipelekwa ‘lunch’ hotel LaKairo iliyoko kirumba tukapata chakula (na pakawa sehemu yenye kujaa watu walokuja kuwapa pole wapendwa wao kwa kukoswakoswa na kifo!) mpaka saa 12.30 tuliporejea uwanja wa ndege tayari kwa kuruka kuelekea KIA. Tulipoanza kuondoka tulielezwa kuwa rubani Mosha alikuwemo ndani ya ndege akiwa abiri lakini alikuwa katika kebini ya marubani!!!! Na wakasema kuwa rubani ‘msangi was in control of that aircraft!’ pengine psychologically, walitudanganya ili watu wasipate wasiwasi kutokana na hali tulokuwa nayo.

Kwa kifupi, kwa wengi (asilimia 99.99 ) walikuwa wakisimulia ama kuzungumzia tukio hilo kila baada ya dk 5. Sikujihusisha sana na mazungumzo yaona wala wasiwasi haukuwepo hata tulipokuwa angani tunasukwasukwa bali nilikuwa nikiuliza maswali mengi. Pengine kauchawi ka akina Kaluse na Kamala kalipataga wakati huo nkawa kama asosikia kitu.

Ukweli ni kuwa watu wanaogopa kifo sana. Mmoja alisema kuwa alipoona hali hiyo alianza kukumbuka ndugu zake wote walo hai na walokufa. Mwingine alisema kuwa alipoona ziwa alifurahi sana kwani alijua hata likidondoka majini hatapasuka sana!! Uwanjani penyewe kuna mdada wa musoma alinambia kuwa walipoambiwa kuwa ndege hiyo inarejea kwa ajili ya kutua in emergency alikuwa akijiuliza namna atakavyopata shida ya kupanda viungo vyangu vilivyotawanyika ktk jeneza!!!

Kaluse na Kamala washaandika sana kuhusu hilo suala lakini kwa kweli Kifo, mh! Kinakanganya sana watu wengi.

8 comments:

SIMON KITURURU said...

Tatizo kwa waogopao ni ka ukweli MANUKATO ya kifo hayaachi kunukia na sekunde usomazo sentensi hii makali ya manukato yanakolea kwa sekunde ulizotumia!:-(

Nuru Shabani said...

Duh!
Inafurahisha sana.

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Watu wangekuwa wanajua kwa uhakika nini hutokea baada ya kifo pengine ingesaidia. Tulizonazo ni nadharia kanganyifu tu kuhusu jambo hili na imani kadhaa mchafukoge. Watu wakifikiria miili yao waipendayo na kuihangaikia kuoza na kuliwa na mafunza dah! Wanakinaika! Kama watu wanaodai kwamba walishakufa wakafufuka wangetuambia waliona nini huko walikoenda ingesaidia. Ajabu ni kwamba hata Yesu hakusema lolote kuhusu alichokiona huko (najua Kamala hapa ataunguruma!). Mwaka jana kulikuwa na jamaa mmoja hapa kutoka Ghana alikuwa kwenye vipindi vya hawa matelevangelist karibu wote. Yeye alikuwa anadai kwamba alikufa na ushahidi anao kutoka kwa madaktari lakini alifufuka. Alisema kwamba alikokwenda alisikia sauti kubwa za watu wakiomboleza na kusaga meno katika moto wa milele na alitishika sana. Yeye alionyeshwa vitu hivi vya kutisha na alienda kuonana na Yesu laivu. Sikumwamini huyu kwani nadhani lengo lake kuu lilikuwa ni kujaribu kuwaaminisha watu kwamba Jehanamu ipo, na moto wa milele upo na kwa hivyo WAOKOKE. Kifo kitaendelea kusumbua watu mpaka tutambue hasa ni nini hasa kinachokufa, na hicho kinachokufa (kama kipo) kinakwenda wapi? Na huko kinakokwenda kinaishije - ni raha mustarehe (mf. kutanua na mabikra 70, kuishi milele na milele huku kikiimba na kumsifu Mungu). By the way, mimi ni muoga sana wa kupanda ndege na kama ningeweza kupiga mguu kutoka hapa Marekani kwenda Bariadi ningeweza. Huwa napanda tu kwa vile sina jinsi. Watu wa utambuzi msinicheke!

Yasinta Ngonyani said...

Aise, kazi kwelikweli mi nasema tu neno IMANI

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

masanguuuuuuu.

mimi sina la kusema kuhusu Yesu na kifo chake pale mtini ambapo waliomuua ndio wanasambaza neno lake wakitumia taratibu na tamaduni zisiizo zake au hata zile ambazo alizipiga na au walizomuua ili asizipinge.

ajabu ya Yesu; alikufa, 'roho' yake ikaenda mbinguni, harafu siku ya tatu akafufuka na kupaa kwenda mbinguni, sasa je, kufufuka kwake kuna maana ya kurudi kuuchukua mwili au? labda ndio maana wakristo mpaka leo wanaamini katka ufufuo wa mwili uliokwisha liwa na wadudu!

yawezekana huogopi ndege bali vitu fulani uvifananishavyo na ndege

Chacha Wambura said...

Nimerejea Musoma, pamoja na habari kutoka katika gazeti la Ze African Weekender, nilipofika Mwanza niliwauliza maswahiba wangu kilichotokea hasa na nkaambiwa kuwa rubani wangu huyo alikutwa na malaria +15!!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

maweeeeeeeeeee alipenda sanahela kuliko uhai wake. lazima ni mwenyeji wa kilimanjaro huyo

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

maweeeeeeeeeee alipenda sanahela kuliko uhai wake. lazima ni mwenyeji wa kilimanjaro huyo