Friday, April 3, 2009

Kutana na mwinilisti paul mwangosi na uchumi wa dunia.

Nimekutana na mwinjilist wa kanisa la KKKT jijini Dsm, naomba usiniulize nilienda kufanya nini kanisani japo yawezekana labda nilienda kufunga ndoa (cheka). Basi Mwinjilist Paul ameonyesha kufikiri chanya juu ya vitisho vya kuporomoka kwa uchumi wa dunia.

Mhubiri huyo wa linaloaminika kuwa ni neno la Mungu japo sio lazima Mungu anayemuamini wewe, amekemea ’ktk jina la yesu’ ujinga wa kutegemea wahisani kutoka ulaya eti tutakufa njaa kwa sababu ya kuporomoka kwa uchumi wa wazungu.

Paul anaesema, chakula hutoka ardhini na ardhi yenyewe haitoki ulaya bali tunayo hapa hapa nchini. Kwanini tusilime hapa hapa kwa kutumia mvua tulizo nazo?

Anasema alikatiza dodoma kwenye kijiji kikame, na kushangaa watu wanakufa njaa, anasema, kwa nini watu wasichimbe mabwawa makubwa na kuhifandhi maji ya mvua zinnyeshazo?
Anasisitiza kwamba kuna miti inayotunza maji, unyevunyevu na kuhifadhi mazingira na kuwa ikipandwa kando kado ya bwawa, italisaidia lisikauke muda mrefu huku watu wakilima na kupata maji kwa mahitaji yaoa ya kila siku.

Anasema katika uchimbaji huo, sehemu zenye mchanga zipigwe udongo wa mfinyanizi ili zisivujishe maji hayo haraka. Linaweza kuonekana ni wazo la kitoto kwako wewe unayejiita msomi lakini wazo kama hili liliwasaidia sana watu wa Buganda enzi za kabaka Mutesa aliyetengeneza ziwa kwa kuamrisha wakazi wote wa utawala wake kusomba maji na kujaza bwawa hilo lililosaidia kuleteleza mapinduzi ya kilimo.

Mwinjiliist paul yeye siyo msomi. Ni mnyakyusa aliyewahi kula bangi na kuwa jambazi kabla ya ’kutembelewa ya Yesu’ nakuzaliwa mara ya pili na sasa anamtukuza yesu. Paul alifika Dar bila makazi, alilala kanisani na elimu yake ni ya shule ya msingi tu. Lakini sasa anamiliki studio ndogo ya muziki wa injili inayomsaidia kufyatua na kuuza CD za muziki.
Ameoa anaishi sinza kapanga nyumba nzima eneo la sinza na analea yatima kibao kwa fedha zake mwenyewe.
Ile imani yangu ya elimu sio lazima shule inazidi kupata mshiko. Labdatufanye utafiti juu ya mawazo ya watu wasio soma tunaweza kupata suruhu kwani hawa hawajaathiriwa na mifumo hovyo ya kufikiri na wanaona uhalisia.

Nakuomba tena usiniulize nilienda kufanya nini eneo la kanisa. Labda nataka kufunga ndoa? Kristo kanitembelea? Sikuwa na kazi ya kufanya? Namfukuzia mtoto? Au nilenda kumhoji mwinjilist paul? Unafikiri nilienda kukingama mvua? Si kanisa liko wazi kwa wote na zaidi sisi watenda yasiyotendwa hadharani na waumini?
Turudi kwa mwinjilist paul

4 comments:

Masangu Matondo Nzuzullima said...

"Ile imani yangu ya elimu sio lazima shule inazidi kupata mshiko. Labda tufanye utafiti juu ya mawazo ya watu wasio soma tunaweza kupata suruhu kwani hawa hawajaathiriwa na mifumo hovyo ya kufikiri na wanaona uhalisia..."

Kamala, umesoma hadithi ya marafiki watatu na Simba katika blogu yangu? Niliiweka makusudi kuchangia suala hili la msomi ni nani. Kosa kubwa tunalofanya ni kudhani kwamba watu ambao hawakwenda shule hizi za kisasa tulizoletewa na wazungu na hawana madigrii ya uzamili na uzamifu hawajui cho chote. Kwamba eti wanatakiwa kuelekezwa na kufundishwa kila kitu. Sera nyingi zingeweza kufanikiwa kama tungeuliza maoni yao na kuona masuluhisho waliyo nayo. Nitakupa mfano. Wakati fulani nilikutana na jamaa wanagawa maboksi ya kondomu katika mbina (michezo ya jadi ya Kisukuma) kule Bariadi. Vijana walikuwa wanagombania hayo maboksi na wagawaji walikuwa wanafurahia
sana. Baadaye nilipata bahati ya kuongea na hao vijana. Niliwauliza kama walikuwa wanakwenda kweli kuzitumia hizo kondomu. Wengi walisema hapana kwani kwanza walikuwa hawajui jinsi ya kuzitumia, pili walikuwa wamesikia tetesi kwamba kondomu hizo zina wadudu wa UKIMWI tayari na tatu walidai kwamba ukizitumia hupati utamu. Na kweli kesho yake kulikuwa na maboksi ya kondomu yamemwagwa kila mahali. Waliokuwa wanagawa hizi kondomu wangewauliza maoni yao wangesikia na pengine wangechukua mkabala mwingine...

Endelea kutembelea makanisa na si ajabu siku moja roho wa Yesu atakushukia kama alivyofanya kwa Mwinjilisti Paul Mwangosi. Yesu Hashindwi kitu ati! AMEN!

Yasinta Ngonyani said...

Kamala, hakuna anayekataza kutembelea makanisa kwa hiyo endelea tu. Nadhani mwisho wake utaona. Nakutakia mafanikio mema.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

Masangu Matondo Nzuzullima,

nitaanza kufanya utafiti wa hawa jamaa wasio soma ili tuone mwisho wa siku tnaweza kupata matokeo makubwa na suruhu kwa matatizo ya jamii zetu za leo.

sasa mnaponishauri kuendelea kutembelea kanisani siwaelewi, kwa nini mnishauri kwenda huko harafu hamniulizi juu ya imani yangu kama huo sio ubinafsi na kujipenda kwa kufikiri kuwa nyie mko kwenye njia sahahihi? kwa nini msifikiri kuwa nyie mmepotea na mimi niko kwenye njia sahihi?

labda tuweke mada ya kukua kiroho.

kwani kanisa na kazi ya kanisa ninini? ili si ni socio-economic institutions? si zipo kuidhibiti tu serikali na kutawala roho za watu?

najua hazuiwi mtu kwenda kanisani, na sio lazima nizuiliwe, bali najizuia mimi mwenyewe.

pplz. kabla ya kunikaribisha kanisani, ebu tafakarini nanyi imani yangu kwanza ambayo sio uisilamu wala ukristo na sio ubudha. fuatilia mienendo ya maisha yangu muone kama ni ya shetani nk.

karibuni

Kissima said...

Luta Kamala,mwinjilist alitoa mawazo mazuri sana kuhusu suluhisho la njaa huko dodoma, je mawazo hayo yaliwafikia wahusika? Yani wananchi wenyewe? Au mawazo hayo mazuri ya huyo mtumishi yaliishia kwako tu?

Imani kwa mtizamo wangu ni kadiri ya nafsi yako inavyojisikia/guswa/msukumo na jambo fulani. "mtu anaweza kuambiwa kuwa asipite ktk msitu fulani kwa sababu kuna simba wakali na ni wiki tu imepita na watu wawili waliliwa na simba,jamaa anaweza kuamua kupita na asidhurike" sasa ni kitu gani kilichomwambia/ishawishi nafsi yake mpaka akapita? Mwingine anaweza kunywa hata sumu huku akijua wazi kuwa anayokunywa ni sumu(either asife au anaweza kufa,lakini yeye swala la kutokufa kaliweka pembeni) kitu gani kimempa msukumo ilihali anajua kabisa kwa kunywa sumu mauti yapo karibu?wote hawa wameondoa kifo kabisa akilini mwao,sababu hasa ni nini? Mimi nadhani kitawalacho hapa ni imani, ndio maana mimi si mdharau mtu na imani yake awe anaamini jiwe,mbuzi,ng'ombe ilimradi tu imani hiyo isiutoe uhai wa mtu.