Wednesday, April 22, 2009

makala ya siku ya kuwasili bk, iligoma mtandaoni......

Nimefika bukoba kwetu kesho yake saanne kamili asubuhi. Safari ilikuwa nzuri yenye visa na mikasa ya kutosha, japo barabara ni njema na uendeshaji wa magari ni mzuri kwa kiasi chake.

Safari ilianza asubuhi saana. Tulipofika Dodoma basi likasimama kupakia abiria, basi wewe unashuka kuchimba dawa, bado umechuchumaa, unasikia honi za gari mara pipipiiiiiiiiip. Derava anakanyaga mafuta anaashiria kuondoka, wewe nawe bado unashusha zigo huku wengine wanasuburia kuingia, unajiuliza lipi jema kati ya kumaliza ufanyayo na kuwahi basi, ahaa

Unanyofoka mbiooo sijui kama ulitoka ukiwa salama huko utokako.
Kuna sehemu kubwa barabara ni ya enzi za mwalimu, wewe? Unakata kiuno bila kupenda. Basi mnakumbushana barabara ilivyokuwa enzi zile, kwamba mlisafiri basi moja likiwa na abaria waliosiamama wengi kuliko mliokaa.

Wagogo na wasukuma walipanda na kuku wao na mizigo vichwani, ilikuwa tabu, safari ya dar bk ilichukua siku nne hivi. Haya yamepita sasa. Nafika bk, kitu cha kwanza mimi na vumbi langu ni kutafuta ilipo netcafee ili nikupe habari hizi. Nakupenda sana msomaji wangu au sio.

Basi mji wa bukoba ni mzuri na unavutia. Ni wakijani kama vile nini sijui. Maji yamkoa huu ni ya baridi yasiyo na madini wala nini. Hata hivyo huduma za basi hili nazo ni poa.

Naelekea kwetu kashura vilimani, ni kwa usafiri wa pikipiki. Familia nzima yanisubiri, kwani wanajua mimi ni vegetarian? Hawajui, sijala bado. Kwenye basi kuna watu waliokuwa wanalia, wanaenda msibani, kwa kumlilia marehemu, wengine harusini, na mimi kwenye mishe zangu. Mji huu ni mdogo hauna foleni wala nini, ni msafi kiasi.

Basi niko hapa ‘nazimikiwa’ nimetoka mjini.

Naishia hapa ngoja nile na kupumzika. Nimefika vyema, sasa ni kula ndizi kwa kwenda mbele

3 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Ha hahahaha haaa Kamala umenichekesha kweli mpaka mbavu zimevunjika. Mmh jamani kusafiri huku kazi kweli kweli. Sasa unakumbuka kwa nini nilipoenda TZ niliandika lile tangazo la kukodi gari. Kwa sababu nilijua maswala haya mtu huwi huru haraka haraha na kubanana sana: Haya bwana usininyima hizo ndizi maana mie mgonjwa kweli wa ndizi. Nakutakia muda mzuri. Kazi kwelikweli.

Mwanasosholojia said...

Hongera mkuu Kamala kwa kufika salama! Vuta siku mbili tatu, shika kifaa cha kulimia ingia shambani...eee si wanasema kilimo ndio uti wa mngongo wa Taifa, lakini pia ndio hao hao wanaonoa meno yao vyema ili kula katika mikataba. Tutafika tu siku moja! Haya mkuu, kila la kheri, wasalimie sana rafiki zangu hapo, akina Mushumbusi, Mutakyamirwa, Rweyemamu, Rwezaula, Kamugisha na mke wake mama Kokubanza, bila kumsahau Kyaruzi.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

tehe, tehe. yasinta turudi kwa simon juu ya uhuru!

mwanasosho, mimi najembe ni mafuta na maji.

salamu zinafika kama kawa hapa.