Wednesday, April 29, 2009

milipuko ya mabomu na ugomvi wa binadamu!

kama unajiamini matendo yako ni mema, kwa nini uwe na hofu ya kushika siraha kama vile kiboko, rungu, bomu,risasi nk?

ukiwa na kijiti namimi ninakijiti, basi tutachokonoana macho ili tuanze kupigana. kama unakijiti peke yako, basi utajiumiza mwenyewe na kuanza kulia lia.

ndilo lililotokea mbagala leo hii. mimi nilidhani ni radi kwani kulikuwepo na mawingu ya mvua.

jiulize ni kwanini mwl Nyerere alitumia pesa nyingi kumpinga Amini asichukue kale kaeneno ka Kyaka? kwani mpaka wa Tz na Ug uliwekwa na Nyerere, au amini? si wakoloni waroho? ina maana nyerere aliheshimu mipaka ya kikoloni na hivyo kutotaka kuona mswahili akitengua mipaka hiyo? kwani amini au uganda wangechukua eneo hilo, Nyerere au Tz tungepoteza nini?

sasa nchi inayoamini katika amani, leo siraha zimeuwa raia wema wasio jua hata kuwasonya wanajeshi, kwa nini? hivi ni uelewa gani wa mtu wa leo kukaa na kubuni siraha hatari za kuua? anataka kumuua nani?

sasa zimekosa wa kumuua, zimeuwa wenzetu wema tu kuliko hata waliozitengeneza. badala ya kununua madawa na mahitaji muhimu, tunanunua siraha za kivita eti kulinda mipaka iliyowekwa na wakoloni, ili iweje? kwani mtu akitanua mpaka tutakosa nini?

yaani vitu vingine bwana,binadamu wa leo na mawzo ya kumiliki nchi wakati nchi inammiliki yeye. very interesting ehe?

4 comments:

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Mimi naamini kwamba hata hizi silaha za Kinyuklia ambazo Marekani, Urusi na wengine wamejirundikia siku moja zitaripuka tu - ama kwa bahati mbaya au kwa makusudi. Sasa wana wasiwasi kwamba nyingi zimezeeka na hawana mahali pa kuziweka. Mbaya zaidi silaha hizi hazina uwezekano wa kutumiwa kwani ni za hatari mno na zinaweza kuiangamiza dunia nzima. Sasa swali linakuja: walizitengeneza za nini? Binadamu....

Chacha Wambura said...

Masangu, umesahau kuwa sisi ndo walengwa wa hizo silaha!! Kama hawatazitumia wao watawanunua 'viongozi' wetu ili tupigane wenyewe kwa wenyewe na wao wapate soko la silaha zao na waje kwa urahizi katika majina mengi sana.

Au hujasikia kigamboni nzima mpaka kimbiji wanahamishwa ili wamarekani wajenge kijiji chao a.k.a Africom? Na bado...kufa hatitokufa ila cha moto sisi tasikilisiaga!!!!!!!!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

chacha unamaanisha hawa jamaa ndo hivyo wameanza kwakurusha ambomu ili wakazi wa kigamboni wahame kwa hiari?

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

chacha unamaanisha hawa jamaa ndo hivyo wameanza kwakurusha ambomu ili wakazi wa kigamboni wahame kwa hiari?