Tuesday, April 28, 2009

mimi ni dini gani?-2

safari yanga ya bukoba iliingila mjadala juu ya dini yangu na labda yako. nimechambua haya maoni ili yatukumbushe tulipofikiana labda yana umuhimu fualani katika mjadala huu....


Kamala asiwe na dini ndiyo maana anauliza ajue.
Wengi tunaamini
binadamu + Dini = Imani juu ya Mungu
Binadamu - Dini = Mungu hajupo
Jamani ukiwa katika dini utajikuta unakosa mabo mengi sana juu ya kumjua mungu,lakini ukitoka nje ya dini utamjua mungu na utakuwa na imani nzuri.
April 16, 2009 10:33 AM

Chacha Wambura said...
Kamala, Tweleze kwanza dini yako kwani hatutojua ya kwako mpaka utwambie. Labda kwa kuwa muwazi zaidi twambie unachokiamini; kama ni yesu, mohamadi ama mti uliyoko kanyigo kagera!!!! Lakini pia itatusaidia saaana kama ukitwambia dini ni nini ili tuweze kujua kama tunaamini katika dini ama ushabiki kama wa yanga na simba tu!!
April 14, 2009 12:51 PM

fredkatawa said...
Wewe ni Mkriislabuyahi,yaani mkristo,islam,budha yahudi,hindu.
April 14, 2009 9:15 PM

1 comment:

Nuru Shabani said...

Nadhani hakuna haja ya kujua wewe ni dini gani mi ninaona kuna haja ya watu kuwa na imani zaidi kuliko kuwa wa dini zaidi.
Manaka hat yesu alisema laiti mngekuwa na imani ndogo kama chembe ya haradani mngeweza kuuambia huu mlima ung'oke na ungeng'oka.
Lets be spiritous lather than be a religious people.