Tuesday, April 14, 2009

mimi ni dini gani?

najiuliza dini yangu ni ipi na nimetundika hapa kwani siku zote nimekuwa nikiandika juu ya dini na kuonekana kutofautiana na baadhi ya mienendo yake. lakini bado nina wasiwasi kama kweli mimi nina dini na bado najiuliza mimi ni dini gani? wewe unadhani mimi ni dini gani?

kumbuka kuna tofauti kubwa kati ya dini, imani na kukua kiroho. natafuta sana kukua kiroho bila kujali sana dini. je wewe uko dini gani na unadhani mimi ni dini gani? dini iipi niliyoichagua na labda kwa nini watu wengi wana dini japo wanashindwa kuziishi bado wanazig'ang'ania na kuonekana kuzimiliki hadi kizihodhi?

je, wewe waweza kufia dini gani au kuhangaika kusambaza dini ipi ikizingatiwa unataka wengine wanufaike na habari nzuri na maisha mema kama ya kwako?

mimi ni dini gani na wewe ni dini gani unaifuata na kwa nini? je umewahi kujuliza maswali juu ya dini yako au unaogopa kukufuru zaidi ya kupenda kukua kiroho?

7 comments:

Chacha Wambura said...

Kamala, Tweleze kwanza dini yako kwani hatutojua ya kwako mpaka utwambie. Labda kwa kuwa muwazi zaidi twambie unachokiamini; kama ni yesu, mohamadi ama mti uliyoko kanyigo kagera!!!! Lakini pia itatusaidia saaana kama ukitwambia dini ni nini ili tuweze kujua kama tunaamini katika dini ama ushabiki kama wa yanga na simba tu!!

fredkatawa said...

Wewe ni Mkriislabuyahi,yaani mkristo,islam,budha yahudi,hindu.

Mzee wa Changamoto said...

Amani kwenu. Sina tafsiri ya dini maana niliwahi kuandika kwenye maoni ya blog ya Strictly Gospel kuhusu dini nikajikuta naelezwa tofauti na nilivyodhania (http://strictlygospel.wordpress.com/2009/04/07/mkristo/#comments) na sasa nadhani niko shule nikifunzwa kuhusu DINI na MADHEHEBU. Labda nikishafunzika nitarejea na kujibu kwa ufasaha kuhusu mimi kwanza, kisha nijaribu kuhusu wewe.
Baraka kwenu

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

chacha, wakristo wanasema matendo ni muhimu kuliko maneno na hivyo kwa muda mrefu tumekuwa wote hapa unaweza kubuni.
fredkatawa, ni kama umejaribu kuifahamu dini yangu japo kwa mbaaali kidogo.

mzee wa C/moto, nimesoma pale strictly gospel, kwa bahati mbaya comments zangu pale huwa hazitundikwi kwa kuwa labda naonekana kutofautiana nao ki mtizamo au kiimani au labda kwa sababu majina yangu hayatambulikani kwa Mungu wamwaminio.

ila nikisoma maoni yao na kama ilivyo, biblia inawachanganya kidogo na kujikuta wanaongelea vitu kinyume kidogo. kwa mfano wao wanaamini kuwa wale waliompokea walifanywa kuwa wana. na wanaseama walio mpokea ni wale jamaa (labda kama wewe) wanaopiga makelele kwa kujionesha na kujifanya wanakuubiri ili na wewe uwe kama wao yaani ufuate wakifuatacho bila hiari wala kujua na bila kutenda na kuona matokeo, wanaamini kinadharia zaidi.

pamoja na ukristo wao mzuri, wakristo wamepuuzia maandiko muhimu yaliyo maagizo na sasa wanafuta yale ya wanadamu. kwa mfanoandiko la mwanzo 1:29 hawalifanyii kazi kama wasivyolifanyia kazi la warumi 14:21 au 1korintho 6: 34 or 31.

inabidi kuwa makini juu ya kukua kiakirinakuweza kubishana juuya dini zetu na kukua kiroho.

nasema katawa amejaribu kunipata kwa sababu ametaja dini lukikui zinazofanana kimalengo kuliko lugha na njia zitumikazo

Yasinta Ngonyani said...

Kamala kama wewe usipojua ni dini gani? Je sisi tutajuaje wewe ni dini gani? Au niseme hiyo dini uliyo nayo basi ni ndo dini yako

Nuru Shabani said...

Vile vile inawezekana Kamala asiwe na dini ndiyo maana anauliza ajue.
Wengi tunaamini
binadamu + Dini = Imani juu ya Mungu
Binadamu - Dini = Mungu hajupo
Jamani ukiwa katika dini utajikuta unakosa mabo mengi sana juu ya kumjua mungu,lakini ukitoka nje ya dini utamjua mungu na utakuwa na imani nzuri.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

yasintaaaaaaa. funny. sijui kama ninayo harafu unasema niliyonayo?

nuru kajaribu kuongea itu kizuri kwamba, usipojifunga na imani moja tu na kutaka kujua wenzio wanasemaje, unamjua na kumumuelewa huyo aitwaye mungu na labda kumfuata vizuri zaidi.