Thursday, April 16, 2009

naelekea Bukoba kwanza, byeee

nitapanda basi la Mohammed trans kueleke bukoba mkoani kagera alfajiri ya ijamaa saa chache baada yakutundika taarifa hii hapa kijiweni kwetu.

ukisikia basi hilo limepinduka na kuuwa basi ujue naacha mwili, japo muda bado na hilo halipo, kwa hiyo ni safari ya kurudi kule ninaokuita kwetu japo mwili huu nyumba yake ni udongo na nyumbani kwetu ni kule mbaali kufia kwa mwili lakini karibu sana kwa roho

najiuliza itakuwaje viwanja vya kwetu. mimi nafika nymbani, kuna washikaji wangu wa BK town tuliozoea kunywa na kulewa katika baa za garden, west point, contena, softrok, bunena beach nk.

nikienda kijijini basi tunaingia kwenye vilabu vya pombe na kunywa konyagi, nguuli, kalinya, na lubisi lukusharila na olwikunulila. sasa naenda home nikiwa sionji hata punje ya pombe, sasas je, washikaji watanipokeaje? je utamaduni wetu wa pombe?

ndo nimekuwa wa mjini kwa kupuuzia kinywaji muhimu cha utamaduni wangu? je wanaojiandaa kuikaribisha nitawaambiaje? si ni ishara yaupendo kwao kuniandalia Lubisi?

sili tena nyama wala samaki, nimekuwa vegeterian, je, familia nayo itanipokeaje? nitawaambia ni sababu gani sili nyama wala samaki? dokta kanizuia au nimeutelekeza ukristo na kubadili dini wakati lengo ni niwe mkristo?

maswali lukuki ndugu japo kwenda ni lazima.

nimelazimika kusimamisha mjadala wa dini kwani safari ya mamba na kenge wamo kumbuka mikoani net nd hivyo lakin i tutakuwa pamoja na nikirudi, nitaendeleza na labda kumalizia mada juu ya dini yangu.

all the best. byeee siwezi kumisi blug zenu ni lazima nijikomit. nitakaa kijijini bila net, sijui nitakuta post ngapi na email ngapi kwenye inbox.

mwenda kwao si mtoro.

8 comments:

Subi said...

Msafiri kafiri basi usafiri salama na ufikishe salam huko uendako.
Mimi na wengine tunasubiri habari za safari na huko utakakokuwa.

Yasinta Ngonyani said...

Salafi salama na ukifika tujulishe umefika salama. na ni kweli tunasubiri habari za Bukoba.

SIMON KITURURU said...

Duh!

We mwanawane nahisi unajifagilia watu wakupe mabinti zao:-)

Ukifa katika Mohamedi BASi, nisalimie Yesu!

Na safari ijayo ya Bukoba twende wote.Mie sijafika huko .

Na unahisi kuna wahaya watakao tolereti chotara wa Kipare na Kijita?

Nuru Shabani said...

safari njema kaka

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Usisahau senene utakaporudi...

Chacha Wambura said...

Mie sitakutakia safari njema kwani sijui waenda kufanya nini. Kama ni msiba waenda kuhani si unapingana na maandiko ya waache wafu wazike wafu wao? Na huyo alokufa si amekwenda kusalimia yesu kwa mujibu wa kitururu?

Kama unakwenda kwenye harusi waenda kufanya nini kwani ulivovitaja hapo ndo vipo na weye ndo hutumii? halafu unaenda kushiriki wizi mtupu ambapo watu wanatafuna zaidi ya milioni 5 kwa usiku mmoja halafu baada ya kuvunja kamati bw & Bi arusi wanaulizana wataishije (arusi moja siku hizi inatumia mpaka milioni 60). Huoni kama utakuwa unashiriki katika ujambazi bila kutumia silaha kama mwanautambuzi mmoja alivoweza kusema wakati fulani? Basi halahala funga virago urudi ili tukuone kijiweni!

Bwaya said...

Safari njema mkubwa. Twasubiri khabari za huko katika kina chake...