Monday, April 20, 2009

net inazingua ngoja niende bush labda

Heee, kama alivyosema bwaya, yaani internet cafee za hapa ni noma
Mtu unaweza kusoma makala nzima kwenye gazeti na kuimaliza kabla page haiafunguka. Kwa mfano hiyo post hapo chini, niliweka stori nzima ya safari yangu sasa nashangaa kiliingi kichwa cha habari tu. Nilikuwa nimetundika stori na picha juu ya safari.

Yaani neti iko slow harafu bei juu. Ukiwa na hasira unaweza kulima screen makofi harafu na kumfuata cafee operata na kumpatia matusi yoote unayoyajua. Yaani? We acha tuu.

Basi wandugu, nilikuja kupost hii mara moja kabla ya kuelekea kijijini ketu. Kwa ukimya wangu nimekula ugali na chai kwani majamaa walipika zile mboga. Ngoja nikaone bush kukoje na labda kesho ntawapeni habari kwa kina kizuri japo sijui kama net ya hapa itaruhusu.

Inaonekana bwaya ana uzoefu na net zetu hizi huku. Yaaaa.

Vinginevyo huku ni kihya kwa kwenda mbele vitu kama maweeeeeeeeeeeeeeee ndo lugha ya kawaida sana hapa

Vinginevyo nafurahia maisha, hali ya hewa ni bariidiiiii mazingira ni yakijaniii ukiwa na mke au mume basi njoo hanimuni uku maana du! Joto ni muhimu kupeana hapa

Ngoja nikimbilie bush bwana, habari zaja msiwe na hofu

3 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Kamala hayo ndo maisha ya kijijini. Hii ndio sababu nilipokuwa Songea sikuwa nablog mara kwa mara ni kazi kweli kweli. Nakutajia furaha, Furahia maisha ya kijijini:-)

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Usisahau picha. Miaka mingi sana sijapita mitaa hiyo!

Koero Mkundi said...

We Kamala......
Usisahau kuniletea senene, na Matoke...