Friday, April 24, 2009

niko wilaya ya karagweni ndani ya mkoa wa kagera, niko kwenye mji wa kayanga yaani makao makuuya wilaya ya karagwe. ni mbali kidogo na mji wa Bukoba na tupo hapa kwa ajili ya matembezi fulani.


pamoja na kwamba kuna harusi, lakini nimekuja hapa kwa sababu nyingine pia. safari yangu imegongana na harusi, msiba na kuzaliwa mtoto mpya. sasa nipo hapa kwa Muda huu naangalia mienendo ya jamii. mtu kama mimi asiyetumia kilevi, anayeepuka soda na asiyekula nyama wala kupenda vitu fulani. anayeamini katika usema ule wa ' japo kuwa mtu hawezi kuishi bila mkate, lakini hataishi kwa mkate tu......'


hata hivyo, nimejifunza mengi. mvua zinanyesha kinoma na watu wa hapa wanajitahidi sana kutunza mazingira kwa kupanda miti nk. nitarudi bk town baada ya usiku mmoja tu.

4 comments:

Mzee wa Changamoto said...

Kayanga!! Nimekumbuka mbaali sana. Nashukuru kwa taarifa za maendeleo yako na pia mihangaiko yote. Salamu kwa Da A.K na wote. Unasikiliza Karagwe Fm? Hahahahahahaa. Kayanga kumekucha kwelikweli
Enjoy

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

yap. huku life m na zuri kinoma. sasa narudi hivyo,.

Anonymous said...

NIMEFURAHI SANA KUTEMBELEA BLOG YAKO ACHILIA MBALI MAWAZO YAKO MAZURI KWANYE BLOG YAKO MIMI NI MTU WA KARAGWE TENA KAYANGA BAADA YA KUONA HAKO KA BANGO KA KARAGWE NIMEFARIJIKA KWANI NINA MIAKA MITANO SIJAENDA KARAGWE ILA KI UKWELI MAISHA YA HUKO NI MAZURI SANA HALI YA HEWA NZURI WE ACHA. ASANTE KAKA

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

anony karibu sana bwana. nilikwenda ukweni najiandaa kunanilii huko isijekuwa kwenye familia yako!! asante