Thursday, April 30, 2009

picha za home bwana
nitakuwa nikiweka picha kidogo kidogo kutokea huko bk, hizi mnaziona, jamaa anakunywa Lubisi (pombe kwa njia ya jani la mgomba-Lubabi) na jamaa anashusha baisikeli yenye ndizi kuelekea melini ili zisafiri mpaka mwanza kwa meli. baisikeli haina break kwa hiyo anatumia mgongo. hapa ni eneo la kashura kutokea Rugambwa SS

5 comments:

Mzee wa Changamoto said...

Duh!!! Hii Kaka ni swafi. Endelea kutuunganisha na nyumbani kwa njia ya taswira za namna hii. Huyo wa Lubisi naye kaniacha hoiiii.
Hahahahahahaa

Yasinta Ngonyani said...

Hiyo Lubisi ya kunywa kwa maganda ya migomba mmh kazi kwelikweli. Hizo ndizi hizo basi tu:-(

Mwanasosholojia said...

Kamarade Kamala, fafanua kidogo basi unywaji wa Lubisi, ukimaliza kunywa hiyo Lubisi, unatafuna na cha kunywea (jani la mgomba)?au unalihifadhi na kulitumia tena na tena kama bilauri? au unalitupa na kutafuta jingine?teh! teh!Shukrani kwa taswira!

Koero Mkundi said...

Nangoja picha yako ukinywa Lubisi nicheke kidogoooo.....
Usije ukatudanganya kwamba hukunywa.....

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

yasinta ndizi ni fahari yetu!

mwanasoc, inafuatatana. unaweza kunya ukapumzisha sehemu au ukampatia mwingine naye apige 'pafu'

kama lengo ni kuficha kama umekunywa Lubisi, basi unalitafuna ili usijenukia pombe kwenu au kwa mkeo, vinginevyo uanalitupa kwani yako mengi na mengine huwa yamepitiwa na kono kono!!!!!

koeroooo!! mimi na lubisi au pombe siku hizi hatuendani, kwahiyo sikunywa, japo jani kama hilo laweza kutumika kunywea maji pia!!