Monday, May 4, 2009

Hii ndiyo dini yangu -- hitimisho


Tuhitimisho majadala juu ya kile nilichokiita dini yangu.

Katika post ya kwanza juu ya dini yangu ndg fred katawa alitamka dini kadhaa kuwa ndiyo zangu. Nilishangaa na kujaribu kukubaliana naye. Misahafu karibia yoote huongelea kitu kimoja na kitu hicho pia hukiongea kwa lugha na tamaduni tofauti japo ukifuatilia kiini basi huwa kimoja.

Kinachowachanganya binadamu wa sasa wenye kutaka ugomvi huwa ni lugha tu na mazingira kitu hicho kilivyosemwa.

Dini zote huamini katika utu, umoja, ushirikiano na mshikamano. Zote huamini katika Nuru (mwanga), sauti (neno) na upendo. Huwezi kumtofautisha Mungu na upendo na huwezi kumtofautisha mwanadamu na upendo. Kwa hiyio Mungu na mwanadamu na mwanadamu na mwanadamu huunganishwa na upendo na hivyo upendo ndio msingi wa misahafu yote.

Dini nyingi huamini wasichoelekezwa na waasisi wake na hivyo hufuta maagizo ya wanadamu. Wakatoliki hupenda kujigamba walivyo kuwa kanisa kubwa duniani lenye waumini wengi japo waumini hao na ukubwa wa kwanisa hilo havinamaana sana kwani bado yale maasi yanayopingwa na dini hiyo yanazidi kuongezeka kama waumini waongezekavyo.
Mengine huwakumba mpaka viongozi wa dini zenyewe.

Kwahiyo sio vyema kujivunia ufuasi wako badala yake muhimu ni kufuata maelekezo ya dini yako na kukua kiroho zaidi. Tunaenda mbinguni tukiwa hapahapa kwanzana lengo letu liwe na kuifanya dunia kuwa paradizo na sio vinginevyo.

Basi huwa napenda kusalia katika kila dini. Msikitini huwa siendi ila nasikilizaga tu mihadhara yao kwani mike zake ni pana (vipaza sauti). Nikiwa Dar, mara moja kwa mwezi, huwa naenda KKKT-azania, au DPC kinaondoni kubadilishana mawazo na kuonana na washikaji na kufurahi kidogo juu ya vitisho vya kuingia motoni usipotoa sadaka ya kutosha!

Katikati ya wiki nikiwa na muda basi huwa naingia kwenye kijikanisa kidogo cha mtakatifu Yosefu ili kupata meditation moment. Binfasi naamini katika Nuru, sauti, Upendo. (Love and respect to every God’s creation)

Imani yangu inanifanya kutokuwala wenzangu na hivyo kuwa vegetarian! Siamini hata kidogo bali natenda. Wabadha wanaita ‘ihi passika’ njoo uone na sio uamini tu! Kwa hiyo najua na nikishajua natenda na nikishatenda naona na kuzidi kujua—ndiyo sara yangu.

Siombi kimyakimya na kusubili majibu kesho au kwenda mbinguni baada ya kufa. Natenda na kupata majibu pale pale kama ni mbinguni kufika sio ishu yaani, nikukaa na kutulia na kujiendea nakurudi!

Basi naamini katika kutokuwatendea wale ambaya mimi sipendi kutendewa. Kufanya kazi kwa bidii, kuwasaidia wengine nk. Fred alipatia kwani nasoma misahafu karibia yote niliyonayo na niikutayo maktaba na internet. Sisi tu wamoja bwana.

Kwa kifupi hiyo ndiyio imani yangu, iliyonifanya kuijua mbingu na nchi mpya, wakristo waiitayo Yerusalemu Mpya.

Niulize ni ipi hiyo?

3 comments:

Chacha Wambura said...

Kamala, mbona alama ulizozionesha kuwakilisha dini yako nyingine ni zile za wanaojihusisha na chinjachinja? Umeniogopesha japo nimekuelewa mkuu katika narrative part ya dini yako.

Chacha Wambura said...

Haya, malizia kipande kilichobaki. NI IPI HIYO?

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

chacha.
wanasema baniani mbaya kiatu chake dawa!

hata chinja chinja bado wana maandiko mazuri kuchinja ni nguvu ya akili lakini ukiangalia maandiko yao kwa nguvu ya roho, basi kuna ukwel na uhalisia ambao kama tungeongozwa na roho ndio tuliopaswa kuupa kipaumbele.