Thursday, May 7, 2009

kinyawawa, ekinyawawa au ebinyawawa


ndege hawa kwa kikwetu huitwa 'kinyawawa' akiwa m1 au binyawawa wakiwa wengi, sijawahi kuwaona kwingine.kule kwetu kuna amani lukuki juuya hawa. eti wakilili kwenye bati (paa) la Nyumba yako usiku, basi kuna mtu atakufa. ukiwasikia we kemea tu. au wakija shambani wako, rusha mawe kufukuza balaa.ukikuta ka

fu shambani mwako au karibu na kwenu ndo maweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee ukimkuta kafa njiani wewe geuza njia urudi kwako. ukimsikia analia usigeuka asije akakutwanga mkosi wa kifo! duh naishia hapa

6 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Mmh! Kamala; Je? wewe unaamini haya?. Unajua umenikumbusha kule kwetu ni bundi akitua kwenye paa la nyumba ni mkosi, akifa karibu na nyumba yako basi ni kwamba atakufa mtu pia. Lakini mimi nadhani ni imani tu. Hii ni IMANI ya mimi.

Bennet said...

huyu ndege sijawahi kumuona ila bundi kama alivyosema Dada yasinta ni sehemu nyingi watu wana imani mbaya naye, kuna sehemu pia paka watu wana mhusisha na hizi imani za kishirikina.
Kama mtakumbuka miaka fulani nyuma kidogo sehemu za Lushoto zilisumbuliwa sana na ugonjwa wa tauni unaosababishwa na viroboto wa panya, wakati huo watu wengi wa Lushoto waliogopa kufuga paka wakihofia kuhusishwa na imani za kishirikina. Siku hizi ukienda minyau imejaa kibao na ugonjwa umebaki stori tu

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

wala sio imani na porojo tu.

soma makala hii ya kisayansi zaidi:

Mauaji ya albino na uchuro wa bundi

Maggid Mjengwa Januari 28, 2009
BUNDI ni aina ya ndege anayehusianishwa sana na masuala ya ushirikina. Tumesimuliwa tangu utotoni, kuwa bundi akilia kwenye paa ya nyumba, basi ni uchuro.

Kama kuna mgonjwa ndani, atakufa. Wengi wetu tumekua tukiamini hivyo. Hakuna ukweli katika hilo. Hicho ndicho ninachokiita siku zote 'abrakadabra'. Nitafafanua kwanini bundi kulia kwenye paa si uchuro bali ni hali ya kawaida.
Kwenye msitu wa jirani na ninakoishi Iringa kuna bundi wawili. Imekwisha kutokea mara kadhaa mmoja wa bundi wale kutua juu ya paa ya nyumba ninayoishi usiku wa manane, au kabla ya hakujapambazuka, na akalia pia, kisha akajirukia zake. Sina sababu za kuwa na shaka na bundi kwa vile naelewa kwa nini amekuja kutua kwenye paa ya nyumba ninayoishi.

Ndio, kisayansi bundi ana tabia ya kutulia mchana na kuhangaika kutafuta chakula chake wakati wa usiku. Kama ilivyo kwa popo, bundi anaona zaidi usiku. Anapenda kukamata panya. Bundi anapenda pia kula viumbe vilokufa na kuoza, huvutwa na harufu ya uoza.

Nyumba zetu nyingi zina panya darini, na bundi akikuta usiku kuna nyumba ina mwanga wa taa, basi hutokea akatua kwenye paa ya nyumba hiyo na kuangaza kuona vivuli vya panya. Binafsi nina mazoea ya kuwa macho, wakati mwingine hadi usiku wa manane. Hutokea pia nikaamka kabla ya kupambazuka. Kuwa kwangu macho ina maana ya kuwapo kwa mwanga wa taa pia. Hilo linafafanua kisayansi kwa nini bundi atue kwenye paa la nyumba ninayoishi na si kwenye paa la nyumba ya jirani.

Inakuwaje basi mgonjwa anapofariki dunia usiku ambapo bundi ametua kwenye paa na kulia? Hapa hakuna cha uchuro. Ni hali ile ile niliyoilezea hapo juu. Kinachoongezeka hapa ni harufu ya mgonjwa. Ni kawaida ya jadi yetu kwa wanandugu kupangiana zamu ya kukesha na mgonjwa aliye kitandani mahututi. Anayekesha huacha taa ikiwaka.

Hutokea, kwa sababu za masharti ya dawa za kupaka au hali nyingine, mgonjwa akaachwa akilala bila kuoga. Mgonjwa hutoa harufu. Mazingira hayo, kama ni ya kijijini au mahali palipo na msitu wenye bundi, humvutia bundi kutua kwenye paa ya nyumba alimo mgonjwa.

Bundi huyo atakaa juu ya paa akisikilizia panya na hata kuvutwa na harufu. Atachoka kusubiri, atalia na kujirukia zake akiacha nyuma kilio kikubwa. Kila aliyesikia sauti ya bundi huyo atashtuka na hata kuanzisha kilio. Kisaikolojia mgonjwa naye atakata tamaa ya kuishi, yawezekana kabisa, kabla ya kupambazuka, mgonjwa atakata roho.

Ni hapo ataanza kutafutwa mchawi, maana bundi haji bure kwenye paa ya mgonjwa, kuna aliyemleta! Masikini, wenye macho mekundu kama yangu wataanza kuingiwa na shaka. Na shaka yao ndiyo itakayorahisisha kazi ya kunyoshewa vidole, kwamba ni wachawi. Na hapo ndipo lilipo shina la matatizo yenye kuzua mauaji kwa wasio na hatia. Inahusu imani potofu.

Hivi sasa jamii yetu ina tatizo kubwa la mauaji ya ndugu zetu albino kutokana na imani potofu. Hali hii inatutaka, kama taifa, tumeze vipande vya barafu, tutulie. Tutafakari kwa makini kabla kufanya maamuzi. Tusiamue halafu tuanze kutafakari maamuzi yetu.

Maamuzi mengine ya haraka yanaweza kuleta kukiukwa kwa utawala wa sheria na haki za kibinadamu. Yatatuongezea machungu zaidi kuliko kuponyesha majeraha tuliyo nayo.

Itakumbukwa, mwaka 1977 waziri Ali Hassan Mwinyi alilazimika kujiuzulu wadhifa wake wa Waziri wa Mambo ya Ndani kutokana na kukiukwa kwa utawala wa sheria na haki za kibinadamu. Matukio yaliyomlazimisha Mwinyi ajiuzulu yalitokea Kanda ya Ziwa na yalihusiana na imani za kishirikina pia. Baadaye Mwinyi akafanywa kuwa Balozi wetu Misri.

Ni lazima tufikiri kwa bidii. Tujiulize, ni nini kitatokea baada ya wimbi la mauji ya albino? Maana huko nyuma wenye vipara walisakwa na kuuawa. Tukawa na wachuna ngozi pia. Naam. Tulifatute shina la tatizo, tushughulike nalo. Tukipuuzia hili la kufikiri kwa bidii kuna hatari ya kuiingiza nchi kwenye matatizo makubwa. Wengine watatushangaa.

Naam. Tuache kutafuta majibu mepesi kwa maswali magumu. Imekuwa kama hulka yetu. Moja ya jibu jepesi kwa matatizo yetu ni ' kurogwa'.

Mtu amefanya ngono zembe, amekufa kwa ukimwi na sisi tunaacha kufikiri na badala yake tunatamka; amerogwa. Biashara zako hazikuendei vema kwa vile unatafuna mpaka mtaji, lakini bado unasingizia ' kurogwa'. Ndio mwanzo wa kwenda kwa waganga na kupewa masharti ya kutafuta vipande vya miili ya wanadamu wenzako.

Hata Ulaya waliwahi kuwa katika hali kama yetu. Ni katika karne ya 14. Nao, kama sisi, wakati huo walikuwa wameacha kufikiri. Waliamini katika 'uchawi'. Waliamini pia kuwa baadhi ya wanawake wazee walikuwa ni wachawi hasa wale wenye pua ndefu. Waliamini kuna ' wachawi' walioweza kusafiri angani kwa kukaa kwenye ncha ya ufagio.

Ilipofika karne ya 18 Wazungu wakaanza kufikiri. Wakaanza kuendelea kiuchumi. Waliachana na imani za kijinga ambazo sisi bado tunazo hadi hii leo. Ndiyo, ni sisi ambao katika karne hii ya 21, bado tunaamini mtu anaweza kutoka Mtwara hadi Morogoro kwa kusafiri na ungo! Na vyombo vya habari ' vinashabikia' ujinga huu.

Tumefika mahali inaandikwa magazetini kuwa mtoto ameanguka kutoka kwenye ungo akiwa safarini kutoka Mtwara! Kwamba mtoto huyo ameangukia kanisani. Hapo ndipo ilipo chachandu ya simulizi kama hiyo kuweza kuwavuta wanajamii; kuna nguvu za giza na imani za dini. Na hapa kuna giza kubwa lililowafunika wanajamii. Katika hilo kuna makanisa na wachungaji wasiojulikana wamejijengea majina kwa simulizi kama hizo.

Mambo haya yanabaki kuwa ni simulizi tu zinazotungwa na baadhi ya 'wajanja ' na kuwaacha baadhi ya wanajamii kwenye giza nene. Ni ujinga tu kuamini kuwa mtoto wa miaka 12 anaweza kusafiri na ungo kutoka Mtwara na kuja kuangukia kando ya kanisa, Tabata! Na kwamba kuna mtoto mchawi anayelamba kichwa cha mtu aliyekufa. Hakuna anayechukua muda wake kuwauliza watalaam wa saikolojia ya watoto juu ya jambo hilo.

Watanzania tuamke. Kuna masuala ya kimsingi tunapaswa kuyafikiri na kuyafanyia kazi ili tusibaki kwenye karne ya 14. Leo wanajamii wanalishwa simulizi za mtoto mchawi wa miaka 12 na kusahaulishwa mambo muhimu ya kijamii.

Wakati tunaambiwa ameonekana mtoto mchawi wa miaka 12 akilamba kichwa cha binadamu jamii inasahau kuwa kuna mamia ya 'wachawi' katika jamii yao wanaowatafuna Watanzania kwa kuwaibia fedha zao.

Ndiyo, tuna watoto na watu wazima wanaokufa hospitalini kwa kukosa dawa kwa vile miongoni mwetu tuna 'wachawi' walioamua 'kuwaroga na kuwatafuna' Watanzania kwa kuwaibia fedha zao ambazo zingetosha kununulia madawa na kuwapa elimu ya kuwatoa gizani. Tuanze sasa kufikiri.

Yasinta Ngonyani said...

Ndio maana nilikuambia haya mambo yote yanatokana na imani ya watu na sehmu watokayo. Binafsi siamini lolote. Asante kwa maelezo yako Kamala

Mzee wa Changamoto said...

Ahaaaaaaaaaaaaa! Basi Da Yasinta unaamini kutoamini. Ni wengi walio hivyo. Imani ni ngumu kwa kuwa huonekana kufanya kazi kwa wote. WAMINIO NA WASIOAMINI. Mwenye kuamini aahusisha kila kimtokeacho na imani yake, na asiyeamini ataweka kando fikra za uhusiano kati ya kiaminicho na kisichoaminiwa. Kwangu naamini kuwa imani ni pamoj na kutoamini pia na vyote ni vyema kama vitachukuliwa vema.
Salaam toka hapa Shambani

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

imani nyingine bwana! sijui tuite nini!