Thursday, May 21, 2009

kwa nini wakristo hujiita wana wa ISRAEL?

leo nimepata jibu la swali gumu na refu la siku nyingi juu ya wakristo kujiita wana wa israel na kulifananisha taifa la Israel na Mungu. sasa sijui kwa nini taifa hilo liliitwa Israel lakini kumbe jina Israel linatokana na maneno mawili, yaani ISR na EL. ISR likimaanisha Rightiousness na EL = Omnipotent yaani those who rightiously work un the law of God. msiniulize kiswahili chake japo naelewa maana na kwa wanaotaka rejea zaidi, soma kitabu cha; Prayer, its nature and techniques cha Sant Kirpal singh wa santmat meditation.

kwa maana hiyo kumbe na wewe unaweza kuwa mu-Israel na usichangaye kutembea katika sheria ya Mungu na hofu juu ya Mungu kwani kumbuka Mungu ni upendo na sio vitisho vya kuogopwa. basi ndiyo maana wakristo huongela mbingu mpya na nchi mpya (yerusalemu mpya) sio mashariki ya kati plz. mbingu mpya ni pale utakapo mgundua Mungu wa ndani yako esp. kwa njia ya tahajudi (meditation) na kupata 'connection' na kuishi ukiwa connected na ile mbingu mpya (ndani mwako) ikitoka nje yako basi hiyo ndiyo nchi mpya (yerusalemu mpya) mwisho wa dunia ni pale tutakapo pata na kuishi katika uwepo wa Mungu (devine connectio) ambapo mwili wa akili (mind) utashindwa na kutawaliwa na mwili wa roho.

hapo hakutakuwepo na jambo baya wala zuri. kila jambo litakuwa ni jema kama biblia inavyosema kuwa alipomaliza kuumba, Mungu alsema yoooote ni mema japo mwanadamu akataka kujua mabaya kwa kula mti wa uelewa, akayajua mabaya mpaka leo yanampeleka puta.
zambi tano za kifo ndo zinatawala; tamaa, hasira/visasi, ujuaji/ubinafsi, attachment, uchoyo na matatizo ya kiaiba (ego) mwisho wa dunia undugu, utaifa, ubaguzi wa rangi, mataba nk vitaisha kwani binadamu ataona ukweli kuwa woote tu wamoja tukiunganishwa na Mungu na Mungu ni mmoja na sote ni ndugu.

ndipo tutakapothamini viumbe na kuwa kitu kimoja, tutaishi kwa kumtukuza Mungu, tutaimba, tutasifu, tutawapenda wenzetu.
ujinga wa kutengeneza siraha utaisha tutaingia kwenye ukweli halisi nayo hiyo kweli itatuweka huru. waubiri wenye kuombea watu wapate wake/waume, utajiri, vyeo nk watapukutika na tutakuwa na lengo la kumtukuza Mungu. upendo utaongezeka, amani ndo basi nk. hiyo ndiyo Yerusalemu mpya, mwili wako utakapotumika kama hekalu la Mungu badala ya kuwa karakana la kutoa mawazo, maneno na matendo mabaya.

yerusalemu mpya sio ile wanayopigwa wapalestina ili ijengwa, bali ni ile utakapofika mbingu mpya moyoni mwako na mbingu hiyo ikijidhiirisha kwa nje, basi hiyo ndiyo nchi mpya, itakuwa raha mustarehe, raha kuliko zile uziitazo raha. sihubiri wandugu, najaribu tu kuelezea maaana ya jina Israel na kuwa taifa teule la MUNGU aka NGUVU KUU aka SUPREME BEING aka UNMOVABLE MOVER aka THE ONE nk nk nk.

je unatamani kwenda yerusalemu wewe?

2 comments:

Bwaya said...

Kaka umenipa cha kutafakari!

Japo nahisi wakristo hujiita hivyo kwa maana iliyofichika, lakini hiyo haiondoi mashaka ya ujimilikishaji wa nchi na utamaduni wa watu.

Ngoja nitanye utafiti zaidi kwa hili.

Mzee wa Changamoto said...

Mara nyingi mtu hutoa maoni mengi akiwa na mengi ya kueleza. Lakini si mimi kwa leo, maana nimepata mengi ya kutafakari.
Asante