Thursday, May 28, 2009

mbibi akisubilia mambomnamuona alivyompole, kuna jamaa kavaa 'vyeupe' anataka kumkabidhi kachakula fulani ka baada ya kipaimara. sasa nami naingia msituni ili nikue kiroho usiponiona hapa siku mbili tatu ujue sijakususa niko msituni, hija, polini natafuta kukua zaidi na zaidi au sio?

nakumbuka enzi hizo wanakuja kwetu kumlisha bibi kamkate hako, duh nilidhani kanatokea mbinguni

6 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Kamala mi nilidhani ni mkate wa kweli. Lakini baba akaniambia ni mwili wa Yesu na ili mvinyo ni damu ya Yesu. Hapo aliniacha hoi. Kama kawa nikamwuuliza kwa nini tunakula mwili wa Yesu na kunywa damu? Je? sisi wote ni wachawi? Mpaka leo sijapata jibu:-(

chib said...

Kamala, bora upotelee huko msituni, ukirudi tusikie mapambio. Sasa kijiwe chako utaendelea kukiita kijiwe au utakiita hekalu au sInagogi la Bwana!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

yasinta maswali yako ukiyaleta hapa utakuwa umekufuru si unajua tena ukitaka kujua unamkosea Mungu japo humuulizi Mungu unamuuliza faza?

chib umeniacha njia panda, ngoja tuone upako utakaotoka huko.
yawezekana likazaliwa jina jipya!

bado niko kijiweni nilichomoka kuja kuchukua mvinyo tu ilionekana waombaji hawalii lalbda ulevi umepungua!!!

mumyhery said...

ukirudi tuletee zawadi ya mramba

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

duhu, haya ndo nimechomoka hivyo na kurudi mjini, maombi yalikuwa mema, safi na salama

Chacha Wambura said...

hukutwambia umeona nini huko porini...isije ikawa umekuwa freemason...ukatenguliwa uaskofu wako!!!