Tuesday, May 5, 2009

Munga tehenan; kifo chake sasa ni mwaka M1

tarehe tano mwezi wa tano mwaka 2008, ndiyo siku aliyoondokea kwenye mwili (kufariki?) bwana Munga Tehenan mwandishi mahiri na mwanazuoni wa elimu ya utambuzi. aliugua kwa muda wa wiki mbili na kulazwa hindo mandal hosp jiji dar kwa wiki moja tu.

nilikwenda kumjulia hali, nikamkuta anapumua kwa mashine, kwa ugumu wa kuongea, akaniangalia na kusema, 'kamala, karibu, hali yangu inaendelea vizuri, kama nisingeletwa hapa (hosp) jana, sasa hivi mngekuwa mnajiuliza huu mwili muutupe wapi, kama ni Moshi, Morogoro au Dar'

alipojaribu kunielekeza kitu, wakaingia madaktari na kuniamuru niwapishe kidogo, na walipoondoka alikuwa amezuiwa kuongea tena na kucheka kwani vilimaliza nguvu. aliongea kwa ishara tu kila nilipomtembelea. ilikuwa ni siku ya jumapili tarehe nne, nikiwa naishi eneo la posta, nilifika Hindu mandal kumjulia khali, nilizuiwa kuingia kwani muda ulienda sana. jumatatu ya terehe tano, nikiwa naelekea hospitalini hapo, ilingia SMS kwenye kiselula changu kuwa, Munga amefariki asubuhi hii!

nikastuka, lakini nikakumbuka jinsi Munga mwenyewe alivyonifiundisha kutokuogopa wala kutishiwa na kifo kwani nikizuri. nilifika hospitalini mida ya saambili asubuhi na kumkuta mwanafuzi mwenzangu Aisha, akiwa amesimama machozi yanamlengalenga. nilichungulia dirishani, mwili wake ulilazwa na kufungwa kama gunia la viazi, basi nikasaidia kuupeleka mochwari, keshoyake tukauzika mwili ule kwenye makaburi ya kisutu hapa jijini.

kifo cha jamaa huyu alikijua mapema kwani alikuwa akituaga darasani nasi tusijue anamaanisha nini. changamoto ikabakia kwetu kueneza alichotufundisha na sisi kuendelea kuwa imara. mpaka sasa tunaendelea kujifunza utambuzi, kujitambua na kuwaelimisha wengine kwa njia ya ana kwaana na mtandaoni. bado tunachangamoto ya kurudisha gazeti la jitambue sokoni.

namshukuru Munga kwani alinibadilisha haswa, maisha yangu yakawa yamaana na kuondoa vurugu, maumivu na matatizo ya kihaiba (ego). japokuwa hakuwa muumini wa dini yoyote, mwili wake ulizikwa kwa taratibu na 'heshima' zote za dini ya kiisilamu aliyokuwa amezaliwa na kulazimishwa kuifuata kama wengi mfuatavyo dini mlizochaguliwa na kulazimishwa kuzifuata.

aliacha mke, watoto wa 3; Kilonzo, Nuru tatu na mwingine. kituo chetu alichokianzisha kinaendelea vizuri pale kimara-Rombo.
sasa anafurahia maisha nje ya mwili kwani alionekana kuchoshwa sana namaisha ya mwili na kabla ya kufa aliandika makala tatu za kutuaga ikiwemo ile ya tutaogopa kufa mpaka lini, maiti hii ni ya nani nk.

je wewe ukifa utaacha nini cha kubadilisha jamii?

15 comments:

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Riwaya yake ya Rais wa Kesho ni mojawapo ya kazi bora kabisa katika fasihi ya Kiswahili. Ameacha matunda mema - akina Kamala, Kaluse na wengineo na kazi yake inaendelea. Huko aliko bila shaka ana furaha. Kuhusu swali lako ulilouliza hapo mwisho wa makala, mimi sitaki kulijibu kwani naamini kwamba kila mtu aliyezaliwa hapa duniani ana mchango wake katika jamii - haidhuru kama ni wa Ki-adolf Hitler, Ki-mother Thereza au Ki-kamala!

Mwanasosholojia said...

Shukrani Kamarade Kamala kwa makala haya!Umevuta sana hisia zangu! Binafsi namkumbuka sana Munga kama mhariri wangu wa kwanza pale Business Times, gazeti la Dar Leo. Nilipokutana na Munga kwa mara ya kwanza niliuona uwezo wake mkubwa si tu katika nyanja ya habari, bali katika utashi na ushawishi! Munga ndiye alikuwa mtu wa kwanza kunifundisha namna ya kuandika habari yenye mvuto, akifuatiwa na Mobhare Matinyi, Masoud Sanani, Jaquiline Liana na wengine. Baadaye mtu huyu muhimu (Munga)aliondoka Dar Leo na kuanzisha gazeti la Jitambue.Sikumpoteza, niliendelea kusoma makala zake siku zote. Na leo pia nasema, ni mwaka mmoja sasa, namuona Munga kimawazo, ingawa kimwili hayupo nasi. Ataendelea kubaki ndani ya nafsi yangu na kuendelea kunipa hamasa ya utambuzi na uchambuzi.

SIMON KITURURU said...

''je wewe ukifa utaacha nini cha kubadilisha jamii?''

Swali gumu!

Lakini hata kwa upumbavu wangu jamii inaweza jifunza kama uerevu hauonekani.

Je kwa kuishi kuna kitu tunaachia wengine, au tunakula mpaka makombo?

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

matondo, ni kweli matunda yake ni mengi. Munga aliweka elimu ya kujitambua katika njia nyepesi sana ya kufundishia, kiasi kwamba wengi wa walionufaika nayo, ni wale mnaopendelea kuwaita watu wa kawaida nikimaanisha wasio soma walanini, wamejitambua maisha ni mazuri na rahisi sana kwao, wanafurahia vya kutosha.

ndio kila mtu anamchango katika jamii, hata akina idd amini ni muhimu sana, yawezekana umaarufu wa nyerere unaongezwa na 'ubaya' wa idd amini, mimi sijui nitaacha nini na ni upi mchango wangu kwani naishi maisha yangu na kufanya majukumu yangu yote vyema, nikifa watakaobaki watajua.

mwanasosh,

Mungu yupo ndani mwetu, nainapendeza akiendelea kuwemo huku tukiyaishi na kuyatanguliza aliyotuachia

kitururu, ni kweli hata unayemuita mpumbavua ana umuhimu wake japo unamuona mpumbavu au tuseme ndio maana unawezakusema kuna mpumbavu kwa sababu anawakilisha mtizamo wako wa kipumbavu kwa kutafuta wapumbavu.

hata vichaa wana umuhimu pia. hata tukila mpaka makombo kuna kitu tunawaachia wengine, watatukumbuka angalau kwa uchoyo, uroho ubinafsi au angalau roho mbaya. wewe unafikkiri wanasiasa wa leo hawatakumbukwa?

nyerere anakumbukwa,amini anakumbukwa, lowasa atakumbukwa hata wewe usiye mwanasiasa

nuru Shabani said...

Binafsi namkumbuka Munga kama mtu aliyenionyesha mwelekeo wa maisha yangu.Nilianza kumfahamu kupitia kipindi chake cha Jitanbue kilichokuwa kikirushwa na TVT sas ni TBC1.Baadaye nikawa msomaji wa vitabu vyake vya utambuzi kabla ya kuingia na kuwa mwanafunzi wake wa madarasa ya utambuzi.
Nitaendelea kumwona Munga kihisia zaidi katika maisha yangu.Kwani elimu aliyotuachia imeendelea kubadilisha maisha ya watu wengi sana.
Swali ulilouliza Kamala ni la msingi sana ila linahitaji watu wenye utambuzi tu.

Anonymous said...

NURU SHABAN..."Swali ulilouliza Kamala ni la msingi sana ila linahitaji watu wenye utambuzi tu"

Msipokuwa makini nanyi watu wa utambuzi mtakuwa kama WALOKOLE - mtaanza kubagua, mkitongozana, kuzini na kuzalishana ninyi kwa ninyi. Kama kweli mnajitambua - fungueni macho muone ndipo mtaweza kuona na kuwafungua macho wengine. Mmeanza KUNIUDDHI!!!!

Koero Mkundi said...

Hata mimi nimejifunza mengi kupitia makala zake......

Wewe usie na jina mbona kama una jazba?
Sidhani kama huyo Munga mwenyewe atafurahia hayo malumbano unayotaka kuyaanzisha....

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

Anonymous, tatizo hajajitamua kama na wewe sasa ni mtambuzi na unadhani kuna watambuzi wengine (labda akina mimi, nuru, kaluse nk) ambao nuru anawaongelea.

iko hivi; unapoanza tu kusoma makala, maandishi na blogu za utambuzi, tayari na wewe ni mwanautambuzi kwa hiyo wanautambuzi anaowaongela nuru na wewe umo!

Nuru Shabani said...

Asante Kamala kwa kunisaidia.Ila naona huyo bwana ana kuwa kama anachokozeka haraka sana.
Elimu ya utambuzi ni elimu ambayo inakufanya uwe na fikra au mawazo chanya muda wote.

Nuru Shabani said...

Asante Kamala kwa kunisaidia.Ila naona huyo bwana ana kuwa kama anachokozeka haraka sana.
Elimu ya utambuzi ni elimu ambayo inakufanya uwe na fikra au mawazo chanya muda wote.

Anonymous said...

NURU SHABANI

"Elimu ya utambuzi ni elimu ambayo inakufanya uwe na fikra au mawazo chanya muda wote"

Si kweli unless kama unaishi heaven. Nuru Shabani bado unayo safari ndefu sana katika haya mambo na hili ni wazi. Mawazo chanya wakati wote, sidhani aisee!!!

UTAMBUZI huu naamini huko mbele utageuka kuwa kama CULT hivi. Ngoja tuone mnakoelekea. Kila kitu UTAMBUZI....

Anonymous said...

hivi magazeti ya jitambue bado yanatoka au kunablog ya jitambue ya munganimemiss makala zake kaka kamala

Anonymous said...

jamani in my life sijawahi kupata mshituko mzito kama huu
ni jana saa saba nilipokuwa nimekaa ofisini nikasema nimemkumbuka sana rafiki yangu mpendwa bwana Mungu ni takribani more than 1 year sijawasiliana nae ,sijamwambia kama nilifunga ndoa kama alivyonitia moyo....na kunishauli mengi tukiwa tumekaaa pamoja

lol naangalia namba yake na kupiga haipatikani nikasema lol labda kachenji namba ila huwa nikiingiwa kwenye mtandao napata info zake

Jamani nimetype Tehenan Mungu alimanusura nizimie baada ya kuona hatunaye tena duniani
Nikasema ni makosa nimerudia na kurudia toka jana leo ndo naamini ni kweli ametutoka

eeeh mungu tulimpenda na kumuhitaji zaidi lakini wewe ndie uliyempenda zaidi jina lako libalikiwe

Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi
Nimepata simanzi moyoni kila mala nashituka nikitafakari

17/09/2009

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

anony, huo ndio uhalisia. pole sana

Anonymous said...

thanks god bless you all katika kazi zenu