Tuesday, May 26, 2009

Nyegerage waitu! Amana vijana senta, byalimana

Ijumaa iliyopita nilikuta na blogger Markus Mpangala wa Lundu Nyasa. Kwanza ndg Mpangala hakunifahamu mpaka nilipomwambia kuwa mimi ndiye Kamala Lutatinabigamobyabantukyomakyamukalanyondoetelaamabale. Aliyemzoea kwenye blog na asiwe na wasi wasi. Hakunifahamu kwa sababu ya busitani izungukayo mdomo hadi kichwani nyie mnaita ndevu.

Utaratibu wa kunyoa nimeutelekeza kwa Muda. Kila nikienda saluni mashine zinawasha na muda unabana lakini pia nimeachana na mashindano ya kunyoa leo kesho zinaota. Kwa hiyo Markus aliona kama naelekeana na picha kwenye blog lakini akakaa kimya. Nilipomwambia kuwa ndiye Mimi mwenyewe, basi alishutuka, alifurahi na kunikumbatia. Tuliongea kwa Muda mfupi na akahaidi kukwambia na wewe kuwa tumeonana.

Mpangala aliniuliza, lilli neno Nyegerage linamaana gani? Nikajua ameshawaza sauzi Africa ya nguoni!. Basi nikafikiri na wewe una hofu na neno hili si unajua linafanana na yale ya kuamsha waliolala? Basi leo mambo yanabwagwa hadharani.

Neno Nyegerage linatokana na neno la Kihaya a.k.a kikwetu, Nyegera, Lenye maana ya karibu na nyegerage ni karibuni sana, huwa wanasema nyegerage mugile akanyeto wakimaanisha njoo kwa kwa madaha mmeshafika, karibuni. Hiyo ndiyo maana yenyewe.

Basi bwana, ukiwa maeneo ya Ilala to Buguruni, kuna kituo kinaitwa AMANA. Duh! Ili neno amana kule kwetu ukilitamka wanakushangaa kwani halitamkwigi hadharani. Kwetu ukisema amana ni kuongelea pale njiani ulipopitia kuingilia duniani a.k.a kuzaliwa. Basi usimwambie mhaya ashuke amana, atakuchapa makofi na kukushitaki, atakuuliza; wangambila nshuke amana? Olifakubi iwe kyana!

Basi bwana neno amana halitamkwi bukoba (buhaya) kwani ni tusi a.k.a siri wakati Rwanda wana neno Imana, neno hila hufanana lile la kihaya la kituo cha basi Amana japo kwao ndo jina la Mungu. Wanyaranda huita majina ya Byalimana wakimaanisha yote kwa Mungu lakini jina hili likitamkwa, wahaya huinama na kucheka kinoma eti kwao linamaanisha vimekula ile njia ielekeayo duniani kutoka mimbani! Duh basi kama wewe unaitwa byalimana, ukitambulishwa kule Bukoba, utaona majamaa yanakukaribisha kwa furaha na vicheko, usidhana yanakufurahia, yanakucheka ile mbaaaya kwa chakula hicho.

Hiyo ndiyo maana ya neno Nyegerage, karibuni sana. Kikwenu inamaana gani?

3 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Kamala asante kwa hili somo. mimi sina la kusema kwani sina lugha

Bennet said...

Kwa hiyo Ndugu yangu ukiumwa na kulazwa hospitali ya AMANA utawaambiaje ndugu zako?

Kweli hii lugha gongana, sie kwetu Tanga mtumba maana yake MJOMBA

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

yaani, we acha tu. swali zuri kuwa umelezwa wapi? duh! naomba isitokee kabla sijaaibika