Monday, May 25, 2009

Tahajudi na wengine huita taamuli basi sisi tuiite meditation.

mdada kama huyu waweza dhanimkosawa kumbe labda ashapasua hanga yuko kama mbingu ya nane hivi kwa mjuao spiritual planes
Kwa washauri au counselors watu kibao hulalamika juu ya ukosefu wa amani, upendo na utulivu. Swali la kwanza unaloweza kuwauliza hao walalamikiao wengine kuwa wanawanyima amani ni je, wewe uko katika amani na wewe mwenyewe? Au una amani binafsi?

Swali hili lina maana kuwa amani ya kweli imo ndani mwako na hakuna awezaye kukupa wala kukunyanganya amani hiyo japo wengi hatuna na tunaitafuta kwa wenzetu na kamwe hatutaipata Utulivu wa akili kwa kiingereza wanasema ni peace of mind ndio utuletea amani ya roho na nyinginezo.

Kwa njia ya tahajudi na meditation utapata amani. Inasemekana nusu ya wakazi wa Dar ni nusu-vichaa kwa sababu ya kutokutulia wala kupata muda wa kulala vya kutosha. Wengi hushinda barbarani, kwenye daladala na ukiwa nyumbani kamwe huna utulivu. Usiposikia kelele za majirani basi utasikia mtoto akilia au gari likipiga honi au kelele za mwizi angalau jirani yako kafungulia redio hiyoooooo.

Ukifuatailia kwa miaka kadhaa wewe mkazi wa Bongo hujawahi kuwa Kimya bali unashinda kwenye kelele na hivyo huwezi kuisikia asili ikikuliwaza. (nature au Mungu)

Ni lazima tuwe na utaratibu wa kukaa mahali patulivu na kujiambia maneno yenye furaha naya kututia amani. Kwa mfano waweza kuandaa neno au kikundi cha maneno wengine huita mantra na kukirudia rudia. Kwa mfano; Amani, upendo mafanikio. Kaa mahali penye ukimya peke yako pasipo kuongea na mtu, fumba macho au angalia upande mmoja tu kama vile pembe, picha, kiti, nk.

Kaa zaidi ya muda wa nusu saa na ukiweza masaa ukirudia maneno hayo bila kusikiliza kelele za nje au kufikiria kitu kingine. Baada ya muda ukimaliza utajisikia amani, furaha na upendo wa kutosha. Ni vyema kufanya hivi kabla ya kulala na baada ya kuamuka kabla ya kuondoka kitandani.

Kaa jiambie unataka siku yako ienende vipi au kaa kumbuka yoote uliyoyafanya siku nzima kabla ya kulala na kujisifia kuwa umeweza kuyafanya yale uliyoyafanya kisha lala. Utapata amani ya kutosha nakwambia. Ni vyema kufanya meditation kwa masaa zaidi ya mawili lakini kwa kuanza, anza na nusu saa tu.

ONYO!!! Usiinuke haraka baada ya meditation. Kaa kidogo kama dakika tano kwani kuinuka ghafra sio vyema sana.

Kama wewe ni mtu wa dini basi waweza kuunda maneno au mantra inayoendana na dini yako lakini chunga kujiambia yale usiyoyapenda au mabaya. Kwa mfano usijiambie au kumwambia Mungu wako ulivyokuwa mtenda dhambi,no! kwani utazitenda kweli. Jiambie meneno kama, Yesu nakupenda, au nataka nimwone Yesu au Yesu kimbilio
langu au Mungu ni mkubwa.

Kwa waisilamu tumia kama ile ya ALLAH AKBAR nk.

Rudia rudi maneno haya kwa Muda mrefu na kwa utulivu. Huu sio muujiza kwani utaoona matokeo yake kila umalizapo kuyasema, utaondoa kelele kichwani mwako na kuwa na amani. Kichwa chako kina kelele ndio maana hata ukiwa peke yako utulii. Utasoma gazeti, utafugulia redio, utaenda kijiweni kuongea na washikaji au utamkaribisha mgeni lakini ukiwa na utulivu yote sawa.
Meditation ijaribu sio imani wala kusubili kufurahi baada ya kifo, ni uhalisia

Ifuatayo tutaona juu ya kuvuta vitu vizuri kwa njia ya meditation.
.

2 comments:

chib said...

Kazi ipoooo, tutafuatilia

Anonymous said...

Ich wollte dieses Thema nicht entwickeln. viagra preisg?nstig viagra ohne rezept [url=http//t7-isis.org]viagra f?r die frau bestellen[/url]