Saturday, May 16, 2009

vijana wana umhuhimu gani katika mabadiliko ya kiuchumi na kisiasa?

niko bize, shughuli zanibana. nina kazi nyingi sana na kazi kuuubwa ya kuandaa presentation. sasa ukilinganisha kazi za kila siku na nyongeza ya kufanya presentation, akili lazima ifanye kazi kweli kweli huku nikiwa bize na shughuli za kila siku.

basi nipatieni japo yako maoni juu ya nafasi/umhuhimu wa vijan katika mabadiliko ya kijamii-kisiasa na kiuchumi "the role of the youth in socio-political and economic transformation".

nataka iwe pepa itakayobadilisha watu, vijana na sera za mataifa ya africa na kwa hiyo ni kazi kubwa naomba maoni yako. nitaiwasilisha pale IFM kwa njia ya video conference mwezi ujao na wewe nitakualika rasmi tuwe wote. ni mkutano utakaounganisha matifa zaidi ya saba ya kiafrika ikiwemo Tanzania, Uganda, Ghana, Ethiopian, Kenya, Madagascar, Zimbabwe, na afrika ya kusini

naomba maoni yako bwana si unajua tenaaaaaaa

1 comment:

Chacha Wambura said...

Kijana ni nguzo ya Uchumi na demokrasia ya nchi yoyote ile. Hawa ndo nguvu kazi tulo nayo. Ili tuweze kupata maendeleo inabidi vijana wawezeshwe. si kama vile mbavyo iko sasa ambapo vijana wanapata elimu na kisha wanangojea kuajiriwa, la hasha. Hata mfumo wa zimamoto wa Veta nao haufai katika kuwaandaa vijana katika maendeleo ya kiuchumi.

mfumo wetu wa elimu uko duni. haumuandai kijana akishamaliza darasa la saba moja kwa moja aweze kujiajiri. ndiyo sababu utakuta wewe kamala umemaliza hapo chuo unahangaika kutafuta kazi.

Kisiasa bado kijana hajaandaliwa kwa makini kwani kwa sasa anatumiwa na wanasiasa kuwapandisha madarakani. Kwa bahati mbaya viongozi wetu wa kisiasa hawajui watokako wala waendako na ninyi wasomi (technical people)wa sasa ambao mnapaswa ku tusaidia mmeishia kula pesa tu ndo tunakumbana na makesi ya kijinga ya akina richmondo nk.

kwa ufupi, kijana ni machine ya taifa katika uzalishaji mali na hasa vijijini. Mazingira ya sasa yametufanya wengi tuamini kuwa kijana wa kisasa lazima awe mjini ambako kuna kila facility ambazo inatufanya tuwe wezi.

pili vijana wana nguvu ya kuongoza. Kwa sasa hawapewi nafasi na matokeo yake wamebaki kutumiwa na wanasiasa. Wanasiasa wetu wamebaki kung'ang'ania madaraka mpaka wanafia hapo.

Changamoto hizi tutazimalisa kama vijana tutajitambuwa umuhimu wetu katika kujenga na kuleta maendeleo kijamii, kiuchumi na kisiasa na kudai uwajibikaji wa state katika kuwawezesha vijana kufikia lengo hili. Hapo haina maana ya kutoa mabilioni kama mabilioni ya jk kuwapa vijana (ambao hawakuyapata kwani yaliishia kwa vigogo), bali kuwapo kuwa uwanja sawa kisera na sheria zinazofaa katika kuelekea kwenye kufikia lengo hilo kwani waweza kuwa na mabilioni lakini kama sera na sheria ni mbovu wafwa.

naacha kwani kuhubiri siwezi hasa baada ya upadre kunishindaga!!!!!!!!!!!