Monday, May 18, 2009

wakazi wa Dar wanaisha kwenye magari na vituoni!

watanzania mnaoishi Dar mnajua kuwa muda mwingi mnakuwa barabarani na magarini? - hamna!!!!

nikiongea na jaamaa yangu aishiye mbezi bich na kufanya kazi posta, aliniambia
kuwa kila siku huamka saa kumi asubuhi na kupanda basi saa kumi namoja na nusu asubuhi. hufika posta saa mbili kasoro. basi jamaa huyo hutoka kazini na kupanda gari saa kumi na moja na kufika saambili na nusu au tatu nyumbani!! ukipiga hesabu jumla, jamaa huyu anakaa kwenye dala dala zaidi ya masaa sita kila siku!!

duh, unashangaa! ama wewe ni mwanafunzi ndo maweeeeeee. saa kumi namoja upo kituoni daladala zinakuepuka kama mafua ya nguruwe. unakaa masaa lukuki na ukipanda ndo foleni kurudi hivyo hivyo! DUH

basi bwana, stori sio nyingi, kwa foleni za dar, watanzaniawaishio dar tunaishi kwenye dala dala na wengine kulala kwenye magari binafsi, kuna haja ya kujenga, kupanda na kununu nyumba nzuri wakati wanaishi ma-hausi gelo tu?

ndio maana washikaji wanaotamani kuhamia dar huwa nawashangaa na nashidwa kuwashauri, japo mimi naonekana bonge la chiiiizi kupanga kuhama dar! mh, niishi kwenye dala dala tena kwa kushika bomba au kwenye gari binafsi? duh.

7 comments:

Digna said...

Aah kaka ili ni kweli kabisa, sasa hiyo habari ipo pia watu tunaokaa tabata segerea, yani nahisi sisi tunakaa masaa nane kabisa, hapo kama ni chuo umemaliza shahada. Ukisema ununue gari nayo ni tabu lakini bora gari utapita njia za panya kuliko daladala ni moja kwa moja mpaka unapofika,ufumbuzi wa hili tatizo sijui utaisha lini jamani?

Chacha Wambura said...

Mtajiju huko. Fanyeni halahala mje Musoma. Jioni utachelewa kwenye kuvua samaki siyo katika jam.

Mshazoea kulamba chumvi je mtaweza kutoka huko tanzania mje huku danganyika?

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

chacha nanikadanganyika, wewe unayeishi nyumbani bila stress au sisi tunaoishi kwenye magari, vituoni na kwenye daladala?

sijui yupi anaishi danganyika!

chib said...

Huo ndio ukweli wa Dar. Ni jiji ninalolipenda, lakini tangu nimelihama, nimegundua unafuu wa kuweza kupanga mihadi na kuweza kuwahi sehemu ninayokwenda, sio Dar, unaondoka nyumbani masaa 2 kabla ya appointment yako. Jumla masaa manne kusafiri kwenda kupata jibu na ndio au hapana!! Ahsante Mzee wa kijiweni kwa uchambuzi. Natumaini wewe sio dalali!!

SIMON KITURURU said...

Nilizoe kustukia watu wanavyoamka mapema Dar mpaka nilipoenda Mwanza na kustukia mji mtupu asubuhi mpaka raha.

Bado nawalaumu wasiotustua kuhusu usafiri wa ungo. Wote tungeujua mambo yangekuwa shwari kabisa Dar-es- Salaam. Sinasikia usafiri wa fisi ni hadimu Dar?:-)

EDWIN NDAKI said...

naungana na Kitururu tungetumiwa technolojia giza..hakika ingekuwa mkombozi kuanzia mafuta,hali ya hewa na muda..

so imefika wakati tuongee vema na vigagula kama kweli taaluma bado wanayo watusaidie tuwe tunawahi kwenye matukio badala ya kuishi kwenye usafiri.

tutafika tu kamala

Mija Shija Sayi said...

Kitururu hujatulia...!!!!!