Friday, May 8, 2009

We mtoto utalaaniwa, maweeeeeee

Basi bwana, katika safari yangu ya home, pamoja na mambo mengine, nilijulishwa na kukumbushwa sana juu ya uwezekano wangu wa kulaaniwa kama vile kuna watu Fulani ninaolazimika kuwaangukia, kuwakubalia hata wakifanya fyongo eti ili wasinilaani!

Nilikataa kumtembelea na kumjulia khali kiongozi mmoja wa dini, nikakumbushwa kua yeye ndiye mtoa laana na baraka na hivyo anaweza kunifanya zoba na kuniamria kwenda kwa kaka shetani \9kama kweli yupo)

Nikajulishwa juu ya stairi ya maisha yangu kuwa nisipokuwa makini na kufuata ninayoambiwa na wazee, basi nitaalaaniwa na kufia mbali au kuwa zoba!

Duh! Nilienda kumtembelea mchungaji Fulani, nikambishia na kukataa mikwara yake, akanishitaki nikaonywa juu ya laana!

Kila ubishi wangu au mtizamo wangu, ni wa kudai laana tu. Yaani mimi siwezi kuwa na maoni au mitizamo kwani kufanya hivyo nitalaaniwa!

Aisee yaani kila maongezi ni lazima nipigwe mkwara wa laana. Ila niligundua wazee wanatumia msemo huu ili kulinda hatma yao kwani uzee umeingia na hivyo wanahitaji ukaribu na vijana kwa hiyo wanajilinda kwa kukumbusha juu ya uwepo wa laana bila kukumbuka kuwa dua la kuku halimpatagi mwewe siku zote kwani anapaa na kuruka dua hilo

Siamini juu ya uwepo wa laana hata kidogo. Lakini nilijiuliz swali ,je kwani mimi sina laana? Nikimaanisha; mimi siwezi kuwawahi na kuwalaani wale woote wajifanyao wana uwezo wa kunilaani?

Mtu akinipiga mkwara wa kunilaaani, namtangulia na kumwahi kwani na mimi laana ninayo na haina umri na labda yangu nikali kuliko yake!

3 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Kamala wala usiogope hakuna mtu anaweza kumlaani mtu. Na pia nasema tena kama UNAAMINI basi kuna laana. wanasema hivyo ili kutishia tu.Huu ni mtazamo wangu

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Kwa kweli elimu ya UTAMBUZI imekufanya UJITAMBUE!

Chacha Wambura said...

Kamala, shaurilo!!!!!

Anyway, kwa kawaida unachokiamini ndicho huwa. Tatizo linakuja wakati unapo-counter hiyo imani ya mitu igine!!!