Monday, June 8, 2009

furaha nini na iko wapi?

katika ulimwengu huu tunaoishi, mwanadamu amehangahika na anaendelea kuhangahika akaiitafuta furaha, amani na upendo wa kweli. katika hilo, kwa kutumia akili zake, binadamu ameishia kutengeneza matatiizo lukuki yasiyoongeleka.

je wewe unajua furaha ni nini na inapatikana wapi? amani ya kweli na upendo je?

tunafananisha furaha na vitu vya duniani kama vile fedha, utajiri, majumba magari nk, lakini wenyenavyo nao hawana furaha wala amani. wanajifungia jera kwa kulinda mali zao hizo. je furaha ya kweli iko wapi sasa? na mamani je?

hata kwenye nyumba za ibada ni vita. mitaani mamamaa, baa duh. elimu ndo maweee, utawala wakisiasa nk. wengine wamekuwa wachawi, ulevi nao ndo hhuo lakini mwisho wa yote nimateso.

waafrika tunatafuta utajiri japo nchi tajiri watu wanaongoza kwa kujiua kisa? hawaoni maana ya maishi hata kwa kuzunguwa na utajiri. je waafrika tunaishi maisha yenye maana zaidi? furaha inakaa wapi lakini?

Obama anatafuta amani ya dunia huku akiwa na siraha kali na jeshi kubwa, kamwe hawezi kuipata. tumeshindwa kujua kuwa furaha na amani ya kweli vimo ndani mwetu. tunasahau msemo wa bible kuwa amani ya Mungu ipitayo uelewa woote......

vijana wanapiga miziki yamapenzi na kutogozana, wanaishia kuchanganyikiwa na kuuwana kama sio kubadili wachumba na kupata ukimwi

Je Unafurahi kwa kusoma hap?

7 comments:

chib said...

Furaha ni hali ya mtu kuridhika na maisha anayoishi kwa namna yoyote ile. Miezi michache liyopita nilimuona mtu kwenye mahojiano ya TV huko Uingereza akielezea furaha yake jinsi anavyo bakiza pound kadhaa kwa mwezi kwa kwenda kuokota vyakula vilivyotupwa na supermarket baada ya kwisha muda wake. Anachojali yeye ni kusevu pesa!!

Yasinta Ngonyani said...

Kwa mimi, furaha ni kuamka kila asubuhi na kujua kuwa ni mzima wa afya pia kuwa na familia ambayo inanijali na kunipenda mimi kama nilivyo.

Pia Mtu /watu mwenye/wenye furaha huishi maisha marefu

Chacha Wambura said...

Kwa kamala furaha ni kuwa bilionea maanake ni kuwa na mipesa kibaaaaaao!

au siyo kamala?

Chacha Wambura said...

furaha ni relative kwangu. Yawezekana kuwa kile ambacho wengine wanakiona kama kiini cha furaha siyo kipaumbele kwa wengine.

angalizo: pesa siyo yenye kuleta furaha kama wengine wanavodai. the more you have access to money the more insecure, frustrated, unhappy you become.

ukitaka kuona hilo angalia waloweka mahekalu yao huko na huko...nyumba ina uzio wa nyaya za umeme, ndani ya uzio huo kuna mlinzi na mbwa wakubwa toka ujerumani wa3; nyumba nzima ina grils ikiwa ni pamoja na madirisha; mlango wa kuingia chumbani kwake kuna gril na mwisho mchagoni kwa bosi kuna ki-dito (bastola) kidogo cha kisasa. Si ajabu ukakuta mtu huyu ana bodigadi pia.

kama chapaa ingekuwa inawapa furaha basi wabunge wetu wangekuwa watu wenye furaha sana kwani ukiwaangalia bungeni kila mtu na wake tu.

mimi napayuka tu; siyo kama kitururu anayewaza!!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

aisee, Chib, yule jamaa wa fedha anafuraha ya muda tu kwa sababu hana fefdha na akizipata nyingi ndo hivyoo ataaza kufanya kama asemavyo chacha.

yasinta furaha ya kweli kamwe haitoki kwenye watu wengine bali imo ndani mwako. familia ndugu na jamaa hawawezi kukupendi kama wewe kwanza hujajipenda na usipojipenda basi huwezi pata furaha wala kupendwa.

furaha ya kweli imo ndani mwetu. mimi furaha yangu ni kufanya tahajudi *meditation*

VERONICA JOHN said...

Furaha ni hali ya mtu kuridhika na maisha anayoishi kwa namna yoyote ile.

Na furaha ya kweli yatoka kwa Mungu tu. Tusipoteze muda kwa kutafuta wenyewe furaha kwa kumtegemea mtu fulani atanipa furaha ya kweli na utakayoridhika nayo bila kulalamika. Hela, raha ya mapenzi kwa mamna yoyote ile mtu akikupa bado kama wewe hauta mtegemea MUNGU mwenye furaha na raha ya ukweli.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

asante kwa mchango wako veronika, karibu kijiweni