Sunday, June 21, 2009

maisha ya Bongo.... --4

tunaendelea na kuyaangalia maisha ya Bongo, maisha ya watu wenye hasira, wengi hupelekwa kama msukule vile. kuna wanawake wenye mimba, watoto, vijana na watu wazima. wanapelekwa msukule na dini, NGOs, Serkali, vyama vya siasa nk.

sasa tuangalia juu ya kinachoitwa vita ya kijinsia. eti mwanamke ananyanyaswa na kuna watu wanapigania kinachoitwa haki sawa, eti kumtetea mwanamke asinyanyaswem wanataka mwanamke awe kama mwanamume, naye afanye kazi kama afanyazo mwanamume.

unaweza kujiuliza bila jibu kuwa; haki za mwanamke ni kuwa kama mwanamume au zimeshikiliwa na huyo mwanamume? sasa mambo yamebadilika, mwanamke anafanya kazi kufukuzia ela ili aheshimiwe na mwanaume hivyo hivyo, watoto wanajilea kupitia house girl kwa kusaidiana na TV, ndo hilo taifa la hovyo linajengwa
vita ya kijinsia inapamba moto, mitandao kama TGNP inaangahika kutetea haki za wanawake, inawashauri waachane na mijianaume ya hovyo, mama anatii, unakuwa mwanzo wa watoto wasio na baba wala wazazi,. baada ya kutoka kwenye ndoa, mwanamke anagundua sio suruhu ya matatizo, anatamani kurudi, Mume alishaoa tena, ni matatizo juu ya matatizo kumbe yawezekana tatizo sio mwanaume.
tunaishi tu, tumeoana bila elimu yoyote juu ya ndoa wala tendo la ngono. mambo ni hovyo, haielewiki hatuelewani. maisha ya bongo yamejaa simanzi na majuto ya hapa na pale. tunajiendea hovyo. fumanizi ni nyingi. watu wanajaribu kuonja radha tofuti, kumbe si suruhu pia. ni ndoa Bongo ni maisha ya vijana wa bongo; yamepoteza maana, yamepoteza uhalisia, ni hovyo, ni vurugu kwa kwenda mbele!

3 comments:

EDWIN NDAKI said...

nimekusoma kamanda Kamala..

safari bado inaendelea tutafika tu

mumyhery said...

Ahsante Mkuu nimekupata

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

karibuni, safari bado inaendelea kama usemavyo ndaki