Tuesday, June 16, 2009

maisha ya Bongo, vijana wa bongo maisha yetu duh-1


zinakuja series za maisha yetu ya bongo. leo nianze na vijana kwa vijana.

sikua ya leo nimetembea kwa miguu kutoka eneo la kitunda ukonga na kuelekea kinyerezi. ni mwendo mreefu sana. ilikuwa ni mida ya asubuhi. njiani nakutana na vijana wamekaa vijweni au wanafanya kazi ngumu.


nikakutana na machinga eneo la relini ukitokea kinyerezi amebeba ungo kama mbili hivi na anauza sumu ya panya. nilikuwa natafuta kipande cha mkate na nikishikilia mkononi. kijana huyo aliniangalia na kukiangalia kipande hicho na jinsi ninavyokitafuna, duh nadhani alitamani angekuwa mimi, kwa kweli alitia huruma!

ghafra akageuka na kuelekea nilipokua nikielekea au alikotokea. ikiwa na maana kuwa hakujua anaenda wapi au anaishi kwa nguvu ya macho na labda siku zinyewe hazisogei. ndio taifa tulilojenga na tunaloishi. vijana hawajui chochote, hawajijui na wala hawajitambui, hawajui lolote, hawana nyuma wala mbele. wanaishi kama vile walizaliwa kwa bahati mbaya.


huyo ni kijana wa hapa town, wa kijijini je? ndiye kijana ambaye Kikwete anaenda marekani na kumwombea msaada wa ubia katika kilimo. nikijana masikini anayekula mara moja kwa siku mbili. kwa kweli imeniuma. mimi kama mwanautambuzi, sipaswi kusikitika, kuumia au kuona uchungu kwani siongozwi kihisia, lakini kwa kijana huyo, hisia zimenipitiliza na kunitawala


imeniuma saana. tunaendelea kuangazia maisha ya bongo na hali halisi

3 comments:

chib said...

Tunatakiwa kufikiria nini cha kufanya kuleta manufaa sio kwetu tu, bli na kwa taifa zima la wabongo.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

chib

unachokisema ni sahihi na labda ndio dawa pekee na mimi natekeleza mikakati kadhaa sasa ya kibongo na inayoendana na wabongo

Yasinta Ngonyani said...

Nilipokuwa Songea kuna kipindi niliacha kula kwa jinsi nilivyokuwa nawahurumia wale wauza urembo maana walikuwa wanafanya kazi ile ngumu. Kutembea na jua kali lile toka Songea mjini mpaka Peramiho na kurudi bila kula kitu. Ni kweli inahuzunisha sana