Friday, June 19, 2009

maisha ya Bongo, vijana wa bongo maisha yetu duh-3


wazee kama hawa ni mikwara kibao jinsi wanavyojua kila kitu na wanamiliki laana (ubaya) badala ya baraka (uzuri)
hii ni sehemu nyigine ya maisha ya bongo na ya kijana wa bongo. maisha ya Bongo ni ya kutisha, hayaelewiki na hayana maana. kila mtua analalamika, ni vitisho kwa kwenda mbele. mzazi anamlalamikia mtoto, mtoto naye anamlalamikia mzazi, anaishia kuwa mvuta bangi, mlevi na mzinzi.
maisha yanatisha na kijana anatishiwa zaidi. naambiwa uchumi wa dunia umeshuka naye anaogopa utadhani aliwahi kushiriki katika kuupandisha au tuadhani alizaliwa na pesa mkononi badala ya kuuacha ujiendee unavyotaka kwenda. kila mta ana wasiwasi. asiye na gari analitamani na mwenye nalo anataka zuri zaidi

ndani ya daladala ni lawama kwa kwenda mbele! hakuna maongezi mema. mtu analipa nauli na kubakiza hamsini ili tu wabishane na kukorofishana. ni ugomvi na ubishi. Mzazi anamtishia mtoto kuwa akizubaa atamtwanga laana! na kijana anaogopa laana hiyo utadhani waliwekeana mkataba wa kuzaana, kijana badala ya kuogopa inabidi ajiulize;

kwani mimi niliomba kuzaliwa? nilimuomba nani anizae? si kuzaliwa kwangu ni matokeo ya anasa na starehe za watu fulani? je huyu anayenilingishia kunizaa wakati mimi sifurahii haya maisha au najutia kuzaliwa, ananiambia vitu gani? yaani ananilingishia uzazi wake kwangu wakati mimi najuuta kuzaliwa? maswali kama haya ni msingi mwema wa mabadiliko na kuchukua hatua madhubuti na kwenda mbele zaidi.

hata hivyo kijana inabidi atumie busara na kumuelewa mzee kwani mzee hana uhakika wa pensheni na anahofu juu ya maisha ya uzeeni kwa hiyo onyo juu ya laana linatumika kama bima ya kumpatia pensheni kwani kijana atamfanyia mema akitarajia baraka.

vijana wana dini, wakienda kwenye nyumba za ibada wanaambiwa kuwa wao ni wadhambi, hawafai na wataingia motoni, nao wanaamini na kuendelea kwenda badala ya kuachana na vitisho hivyo. wanashindwa kujua kuwa bila wao kupeleka sadaka kanisa haliwezi kuwepo na huyo anayewapiga mkwara hatakuwepo kwani hana chakula.

ni maisha ya bongo, yanashangaza, yanatisha na yanasikitisha, kumbe suruhu ni kuachana na ujinga woote, ukawa wewe na kuishi maisha yako! kijana wa bongo jamani

3 comments:

chib said...

tehe tehe teheee, naona wewe kweli ni mchambuzi wa maisha ya vijana wa Bongo

Mzee wa Changamoto said...

Tunasonga hatua moja kila siku. Nimeelewa na nazidi kuerevuka. Na tusubiri nyingine (kama ipo)
Blessings

munale said...

Ni kweli,hata mimi ni kijana wa bongo na nilishaamua kuwa mimi,sina ushabiki wa ho
vyo wa mambo ya siasa na dini.