Monday, June 22, 2009

Maisha yetu bongo na jamii yetu…

Ni miradi kwa kwenda mbele. NGOs zimefunguliwa za kutosha. Tunafanywa miradi. Ukiangalia hata wewe ni mradi wajanja Fulani. Tumeona jinsia. Kwa kushindwa kujitammbua, mambo ya jinsia yamekuwa miradi mikubwa.

Bongo kuna shirika la TGNP, linapambana na matatizo ya kijinsia, kweli? Si mradi ule? Unadhani wanapenda kupunguza matatizo ya wanawake? Yakiisha watakula wapi? Angalia machapisho yao, mengi yameandikwa kwa kiingereza! Na picha zake zinaonyesha wale wanaopigwa na kunyanyaswa, hazionyeshi wale wanaoishi vyema na siri ya wema huo ili kiwe chanzo cha mabadiliko!

Kwenye mikutano yao wanawajaza hasira wamama! Hivi mtu ambaye hajajitambua anaweza kweli kushinda matatizo ya kijisinsia? Shirika la kupigania wamama wa Tanzania linatoa machapisho kwa kizungu. Lipo mtandaoni, linajulikana kwa wato wa nje (watoa pesa aka donors kuliko walengwa). Machapisho ndo hivyo ya kizungu kwani si donor anajua kizungu?

Wanaonesha matatizo na sababu ya kuendelea kupewa pesa badala ya kumaliza tatizo. Liishe ili? Kila mtu ni mradi. Wajanja wanatumia matatizo yawengine kuwa miradi kuna mashirika kibao ya vijana, wafungwa, wazee, wagonjwa nk.

Yanajulikana zaidi kwa wenye fedha kuliko walengwa. DUH inatisha, wajanja wameshatufanya miradi yao, wanafanikiwa pia. Ni maisha ya Bongo. Kila kitu kina milikiwa na kina wenye nacho.
Tamaa zatuongoza. Kila mtu anatamani mke, wake waume nyumba, magari nk. Bongo ni kulewa na kukimbizana. Sisi ni masikini, hatuna kitu. Tunalia tunajiendea tu

Vijana wanatafuta nafasi za kwenda nje kusoma, na kufanya utumwa, wanaita green pastures! Ni maisha ya bongo, watoto wa mitaani wanaongezeka, wanajilea, wanapigwa tu. Hupigwa na jua, mvua, baridi, joto, mawe, wapiti njia na hata miti. Hawajawahi kupendwa, hawajui kupendwa, wakiwa wakubwa itakuwaje? Ni bora ufe wapate sh 500 kuliko kuishi wakaikosa.

Ni maisha ya bongo, ni utanda wazi, ni diri za miradi! Kila mtu sasa diri. Kuna mradi unaokufanana unaendelea. Vijana wanaamini kutika imani za ajabu kupata utajiri. Dini zipo na vitisho zinavyojua kupeleka watu mbinguni wakati duh? Tungekuwa na dini matatizo yangeongezeka hivi?

Bongo, bOngo, boNgo, bonGo, bongO ni maisha ya BONGO ndani ya ugiligili na ubeuzi

4 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Maisha ya Bongo bongo mmmmhhh!!!

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Kamala, leo umegonga pointi. Rafiki yangu mmoja alikuwa na NGO yake na alitajirika kwa haraka sana. Bongo ni ujanja ati, ndiyo maana karibu kila mtu nimjuaye anaendesha Shangingi - hata wale ambao hawana "kazi za kueleweka" Ni "don't ask don't tell" mtu kapataje hilo shangingi - gari ghali kabisa ambalo hata wazungu huku wanaogopa kulinunua mbali na kwamba kuna mikopo. Ni kazi kweli kweli. Wewe Kamala huna shangingi kweli? Afadhali wewe ambaye unawafanya watu wajitambue ili waondokane na matatizo yao.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

ndio mimi sina shangingi. naisha maisha ya kawaida tu. usafiri wangu mkuu ni tz11 (kutembea kwa miguu) dala dala na tax mara chaache au pikipiki aina ya bajaji

SIMON KITURURU said...

DUH!