Friday, June 26, 2009

Michael Jackson alipata maumivu ya kihisia na kiakili akajikana


Sipendelei saana kuongelea maisha ya ma superstar. Mimi sio mpenzi sana wa mambo yao lakini baada ya kifo cha mike Jackson nimeamua kufuatilia kisa cha kubadili sura yake, rangi na jinsia.

Nimesoma kwenye mtandao mmoja kwamba baba yake Jackson alipendendelea kumuita bignNose a.k.a puaKubwa. Bila shaka Jackson alibeba kichwani mwake kuwa pua lake ni libaya na labda ngozi yake ni mbaya na labda jinsia yake ni mbaya, nk nk. Hapo ndipo lilipotatizo la kutukana watoto wetu na kwa hiyo mike Jackson kujibadili rangi na kila kitu ilianzia kwa babake.

Mwalimu wangu wa maarifa ya utambuzi hayati Munga tehenan aliwahi kutembelewa na mtu mmoja akitaka ushauri kuwa afanya nini kwani alijiona mbaya na mwenye masikio mabaya saana. Munga akamwita mwanae aliyesoma darasa la saba wakati huo. Akamwambia amwangalie jamaa Yule kwa dakika kama mbili, na baadaye akamwambia unamwonaje? Motto akajibu ni mzuuri sana. Akamwuliza tena, na masikio yake Je? Mtoto akayaangalia masikio na kujibu ‘mbona mazuri sana kuliko hata ya kwako baba?’

Jamaa hakuamini, alipoulizwa kwanini alijiona vibaya, akajibu kuwa tangu azaliwe mamaye alikuwa akimtusi kuwa yeye ni mbaya, mjinga na hana akili. Mimasikio yake imekaa kama ya popo na matundu ya pua yake ni mabaaaya sana

Hivyo hivyo namdada mmoja alikuwa akitukanwa usukumani kwao kuwa ni mbaya. Akakutana na shangaziye jijini Dar, shangaziye akamsifia, kuwa ni mzuri, hakuamini na alipojalibu kuingia katika mashindano ya urembo na kupata nafasi ya juu. Yeye alijiona mbaya na kuambiwa kuwa wewe ni jinga na baya ni hatua ya kuizarau sipoweza kuziepuka.

Hata mimi ndugu msomaji, udogoni nilikuwa nikiambiwa kuwa mimi ni jeusi na baya kule shuleni. Jinga nyumbani na nina bichwa kubwa. Duh, kumbe sifai. Nilipoenda kusoma mjini moshi, nikashangaa na kujisikia vibaya kwani wacchaga (na hasa mabinti) walikuwa wakiniangalia kwa mshangao na kwa mud mrefu. Kwa hiyo kila niliposalimiana na mchaga kwa kusikana mikono, niliangalia rangi. Kono langu lilionekana jeusi kama mkaa mbele ya ule wa mchagga!

Duh nikaja kugundua baadaye kwamba kumbe wachaga walinipenda na walishangaa sana kuona rangi ya ngozi yangu. Kumbe hata kama ni mweusi, bado ninangozi nzuuri ya kuvutia nay a ajabu *(si unajua weusi wa kihaya) kumbe wachaga walinifuraia na kunipenda wakati nikijikana na kujiogopa. Ningekuwa Michael Jackson, ningejichubua kumbe najiharibu.

Hata wewe jikague, linganisha maneno uliyoambiwa udogoni na jinsi yanavyokuathiri saana maishani mwako, lakini pia kuwa makini na maneno unayowaambia watu na hasa watoto na wale walioko chini ya mamlaka yetu, yanaweza kuwaathiri maisha yao yoote na kujikuta tunawapoteza. Penda kuwa chanya a.k.a positive katika maneno na matendo uwatendeayo wengine, ni muhimusana. Mike aliharibiwa na baba yake bila baba kujua, kwa kumwita pua kubwa!

2 comments:

chib said...

Mzee, hapo nimekupa shavu. Big up.
Ahsante kwa kuwatia moyo watu waliokwisha poteza mwelekeo kwa muonekano wao. Na hasa wanaong'arisha nyuso zao kwa mkorogo

Mzee wa Changamoto said...

Unasema kweli sana Kaka. TUNAJIPOTEZA TUKIWA KWENYE HARAKATI ZA KUJITAFUTA. Kuambiwa sisi ni wabaya ni jambo la kawaida hasa kwa watoto wa nezi na kabla yetu na kwa hakika wale ambao wanawafanya watu wengine wawaamulie wao ni nani wanakuwa wajinga. Unapojifikiria kuwa uko kama ambavyo mtu anayekuchukia ama ambaye amechukia anasema, basi ujue kuwa una issue.
Nimesikia habari mbalimbali kuhusu kujibadili sura kwa Michael na ntajitahidi ku-dig kuona kama ntapata zaidi.
Blessings