Wednesday, June 10, 2009

nyimbo hii nazo

mzee wa c/moto huweka nyimbo live sasa mimi naweka zisizo rekodiwa japo wazifahamu.

Sikiri mimi masikini uvivu wangu nyumbaani,
ukiwa huunjiana nakufa hapa kwa nini
sadiki sasa ashiiba chakula kingi kwa baba
nirudi tena kwa baba nakufa hapa kwa nini

naombaradhi nimekoosa ntakuwa mtoto mwema sasa
nitakuwa kama sadiki
na nyumbani tena sitooki baba na mamanisameeni


au
asiyependa shule ni mjinga kabisa
twapenda mambo yoote ya shule kabisa
kujua kusooomatwaona furaha

hhhA hhhE hhhI hhhO hhhU
twaimbavyema leo..

ongeza nyinine basi na wewe. hii inaitwa short break

5 comments:

chib said...

Kwa kweli hapo nimecheka!! Ingekuwa vizuri ukarekodi tusikie sauti yako jinsi unavyouimba huo wimbo.

Yasinta Ngonyani said...

Kamal! hata mimi nimecheka mpaka nikakimbia chooni na pia mpaka nimepangusa machozi safi sana. nimeimba sana nyimbo hizi na bado naimba na watoto wangu: ngoja nami nikuimbie huu,
Maua mazuri yapendezax2 Ukiyatazama utachekelea
Hakuna mmoja asiyeyapendax2.

asante Kamala.

Chacha Wambura said...

mh! mbona mimi sina mistari?

lini mkurya akawa na nyimbo? Anyway, nami nimeziiimbaga huko.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

chib, mipango ya kuziimba ipo siku nyingi na nafikiri hivi karibuni utanisikia.

yasinta
inafurahisha, inakumbusha mbaali sana. jinsi ulivyokuwa kajitu sasa ni mtu mzima fulani.

nitendelea kuweka na nyingine

Mzee wa Changamoto said...

Hahahaaaaaa. Kuna ule wimbo wa kuimba wakati mnacheza kombolela.
Kuna zile za za kuimba wakati wa kwenda "kushenya" na kuvuta kokoro.
Dah! Safi sana