Thursday, June 4, 2009

sara na maombi, je wewe unaombaga?


Sijui cha kupost nini maana nimebanwa na shughuli za kidunia vya kutosha sana. Japo tunasubilia majibu ya yasinta juu ya incarnation. Tuna kiporo cha meditation lakini duh, mambo magumu.\

Labda tuongelee juu ya sala. Eti sala au maombi ninini? Kwa nini watu huomba? Tofauti kati ya prayer / praying ndo ipi? Je unaamini juu ya nguvu ya maombi kwamba yaweza kuamisha milima? Kama ndio, wewe uliwahi kuombea nini kisicho cha kawaida na kikawa? Je ni kwanini sala au maombi ya wengi huwa hayafiki au hayajibiwi? Lakini ni kweli kuwa hayajibiwi?

Kwani wewe huwa unasali au kuomba? Je inabidi tusalie na kuombea wapi na wakati gani kwa kuelekea wapi? Kwanini kuna wanaoomba vijisanamu kama wakatoliki vile?

Jibu kadri ya majibu uliyonayo

6 comments:

Ivo Serentha and Friends said...

Greetings from Italy,good luck

Marlow

SIMON KITURURU said...

Maswala ya lugha haya!:-(

Hukawii kusikia watu wako mezani wanaombea chakula, sina uhakika kabla chakula hakijaota mashambani ndio wanashukuru?

Lugha ina mchezo mbaya usipoangalia!

Chacha Wambura said...

naombaga wakati wa kutaka kukon'goli msosi na of koz jumapili nakandamiza masala kwa kwenda mbele!!!

Yasinta Ngonyani said...

Kuomba hakuna sehemu wala wakati yaani lini niombe. Kuomba ni sehemu yoyote na wakati wowote.

fred katawa said...

Sara mimi maana yake na faida zake sizijui.Nimerithi kusali na kuombea chakula kutoka kwa katekista wangu.Wakati ukila chakula bila kukiombea niliambiwa kuwa jina langu litaandikwa kwenye kitabu cha wanaosubiriwa kuchomwa moto na Mungu mwenye huruma na Upendo anayemiliki Jehanamu.Mpaka leo hii ninasali na kuombea chakula kwa kuogopa kuchomwa moto.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

duh, ivo thanx. kitururu hata mie sijui.

katawa umeniacha hoi kwa moto huo wa kukuchoma wewe, duh!