Monday, June 1, 2009

Tuangalie juu ya re-incarnation

Kuna kitu kiitwacho incarnation au re-incarnation. Hili ni neno la kiingereza ambalo nikiri kuwa sijui kabisa Kiswahili chake. Lakini linamaanisha kuzaliwa tena hasa baada ya kufa na kuishi tena na tena. Kwa wale wanaoamini katika ‘evolution’ huamini na kukubali juu ya uwezekano wa binadamu kuzaliwa tena na tena.

Maumbile (Mungu?) yaliumba mara moja. Ni siku ya uumbaji pekee ndipo kila kitu kilipoumbwa. Hakuna kazi nyingine ya kuumba iliyofanyika baadaye kama unaamini katika uumbaji kwani hata vitabu vitakatifu vinatwambia hilo.

Basi bwana, mimi nimekuwa nikiamini juu ya hilo na ninaamini kuwa niliwahi kuishi sehemu fulani kabla ya kuzaliwa tena leo nikiwa mhaya wa bukoba. Nimekuwa nikihoji watu wengi juu ya hili, wengi ukiri kuwa walipokuwa wadogo waliwahi kufikiria juu ya watu kuzaliwa pahala na kuzaliwa tena. Yanakumbukwa udogoni labda kutokana na kuwa na kumbukumbu ya tulipotoka.

Semina ya utambuzi pale FAJI, mwanafunzi mmoja alifundishwa meditation na hypnosis, kesho yake alitwambia kuwa alifanya hivyo akarudi nyuma na kuwaona wazazi wake wakifanya ile ngono iliyomleta yeye duniani! Hii inadhihirisha kuwa sisi ni zaidi ya miili na hatuna mahala pamoja.

Ilitokea nchini India, mtoto wa miaka kama 15 akafariki kwa ajali ya baiskieli na baadaye akazaliwa mtoto katika familia ya jirani, ajabu mtoto huyo alianza kuongelea juu ya ajali hiyo na alivyokufa! Mtoto huyo alianza kudai hata nguo zake za zamani kwani walizivaa wale waliokuwa wadogo zake kabla hajafa. Alisema jina lake alilotumia nk, nk.

Sasa katika TV show moja ya Oprah mmalekani, alionyesha dakatri mmoja nchini humo akiwa-hypnotize watu na kuwafanyia regression mmoja aliongea kichina, alipoletwa mkalimani, akasema huyu jamaa anajiona akiwa china sijui na watu gani hivi. Mwingine ni mwanamama naye ni mmarekani, alianza kuonge lugha ya majamaa wa Nepal, akaletwa makalimani.

Mama yule alijiona akiwa nchini Nepal kijiji fulani akiuza gengeni kwenye soko moja. Ili kujua kama ni kweli, wakasafiri kwenda Nepal. Wakauwauliza wenyeji wa mji ule juu ya uwezekano wa kuwepo soko na kila kitu. Wakapelekwa kwa mbabu mmoja. Mbabu yule alikubali kuwa enzi zili lilikuwepo soko na mambo kadhaa aliyoyasema yule mama.

Na Mzungu mwingine alienda nchini Mali, alipofika eneo fualani akahisi kama anapafahamu vile kama ndo kwao vile NK. Je wewe unaamini katika re-incarnation? Kumbuka sisi ni zaidi ya mwili na hivyo ni kweli kuwa tulikuwepo, tupo na tutakuwepo. Sio swala la imani bali la kisayansi. Kama unataka kujua uliishi vipi na wapi kabla ya kuishi kwenye mwili wako wa sasa, nendo kwa ma-hypnotist au tuwasiliane na kupeana tekiniki za hypnosisi. Sio imani bali ni ukweli na ni uhalisia.

Hiyo ndiyo proof kwamba binadamu wote ni kitu kimoja na sisi sote ni wa moja. Hata mitume kama Kristo ukisoma utagundua kuwa aliwahi kuishi kama watu fulani na baada ya kufa, nguvu yake ikaingia kwa petro na baadaye kwa Paul au Sauli. Mpaka sasa yupo ila hatumwoni kwa sababu tunamtafuta kwa macho, kiburi na ujuaji, ukitulia utamwona.

Je wewe utakufa au unataka kufa au kuishi milele?

4 comments:

fred katawa said...

Kamala kamala hayo sasa mambo ya giza,ushindwe na ulegee kwa jina la y..u

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

wa nini sio kwa jina lao na ni la Y..U?

Chacha Wambura said...

hapo patamu sasa! utaanza kuitwa mganga wa kienyeji sasa nahivo ushayatundika madevu kama osama, mh!

Yasinta Ngonyani said...

Kamala ntajaribu na ntakuambia nimeona nini. Na hapana mi sitaki kuishi milele