Thursday, June 11, 2009

Turudi kwa wakristo na msalaba.

Unajua toka nikiwa mdogo ilipenda sana utafiti. Na ndio maana ninablog kwani inanisaidia kujua mengi na kuwajulisha mengi wengine. Udogoni nilipouliza maswali ya kutaka kujua zaidi hasa juu ya dini nilikwidwa. Kwa mfano kuna siku tulienda kanisani kumwomba mungu atulinde dhidi ya wezi wa usiku, kesho yake kanisa tuliliosalia likavyunjwa na kuibwa viyoo na milango, nilipouliza juu ya huyu mungu asiyelinda kanisa atatulindaje sisi? Nikajibiwa eh? Unasemaje


Nikadhani sikueleweka nikauliza tena, mbona kanisa tusaliamo limeibiwa sasa tutakuwaje na usalama?


We!! Nilisikia kofi nikadhani ni muujiza na lundo la fimbo, kisa? Nimekufuru na nisipotubu nitaenda motoni. Ningekuwa nimepata kipaimara basi ningezuiwa kushiriki mpaka chini ya marudi, we?


Tuyaache hayo. Swali langu la wakristo kuutukuza msala na kuufanyia biashara limepanuka na labda kujibiwa. Gazeti moja linaonyesha ushahidi kuwa hapo kale warumi walinyanyasa watu na kuwatundika kwenye mti imara ulionyooka na sio msalaba. Linasema msalaba ni ishara ya kumtukuza Mungu wa uzazi wa enzi za mababiloni na sio kweli kuwa alitundikwa Yesu bali yesu alitundikwa kwenye mti mmoja ulioonyooka kwani wanasema biblia ya kigiriki inasema tauros likinaanisha mti mmoja na sio msalaba kama tudanganywavyo


Linauliza swali juu ya kuutukuza msalaba kuwa kama nduguyo kapigwa na rungu kichwani na kufa, utapenda kuchukua rungu hiyo kama ukumbusho? Je utaiigiriza na kutoa nyingine kama hizo na kuwsambazia nduguzo wote ili muutuze kama ukumbusho wa hasira na kifo au mtautupilia mbali kupunguza hisia kali?


Ukiangalia siku hizi misalaba ni dili namingine ni ya dhahabu na bei juu. Mingine inauzwa bei kali na inaabudiwa kuliko hata Yesu mwenyewe namafundisho yake, je wewe unafikiri vipi juu ya Mungu wa kibabiloni na alama zake? sijiui

4 comments:

Mzee wa Changamoto said...

Kwani unadhani kazi ya msalaba ni ipi? Unadhani kama ni mmoja ama miwili na yote inatim,iza wajibu kuna haja ya kujua idadi ya miti?
Misalaba imekuwa dili kwa kuwa dini nzima ni dili kwa sasa. Tazama wanavyojitahidi kuonekana kwenye Tv ili kuonesha wana uwezo wa kuwavuta na kuwahudumia wengi ili wahudhurie na kutoa fungu la kumi.
Naamini nguvu ya maombi inavuka umbali mrefu na hakuna haja ya kuwa na watu pembeni mwako ili kutimiliza lengo. Lakini sasa hivi hata wakikosa attention wataandaa kitu cha kuwavuta watu kuwaamini wao kisha wakusanye kitu baada ya hapo. Niliuliza swali hapa japo hakuna aliyenijibu kwa ufasaha. Hebu nawe chungulia ujaribu kabla hatujarejea kwenye MSALABA. http://changamotoyetu.blogspot.com/2008/11/ni-maandamano-yasioenda-ama-maonesho-ya.html

SIMON KITURURU said...

Anzisha dini Kamala naamini ni bomba la dili!Halafu dini yako unaweza ukaifanya iwe sawa sawa na ya Kilokole ila wewe unakazia kwenye sadaka na msalaba kuwa ulikuwa ni mti mmoja. Atakaye kubishia mtishe akiingia mkenge mchangishe sadaka zaidi.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

mzee wa chaimoto, nimeiona hoja yako na kazi ya msalaba. vitu lukuki tumeingizwa mtini.

kitururu, sijaja duiniani kuingiza watu mikenge bwana. duh si unajua kanuni ya nguvu?

SIMON KITURURU said...

:-)