Monday, June 29, 2009

unapolazimika kuficha kicwa, unaacha nguo......


Mzee wa duh aka Simon Kitururu anadai kuwa kuna vitu huwezi kuviomba ila inabidi ujifanye unaongelea mengine kumbe lengo lako ni kunanilii. Kwa mfano huwezi kumwambia mvua nguo ukaoge ila unamwambia kaoge kama vile hujui kama atavua. Sasa hap ndipo mambo yalipo.

Ukimfumania Nyani au ngedere shambani mwako badala ya kukimbia huwa anachukua vidole na kujificha uso akidhani humwoni kumba unaweza kumtungua utumbo ukumwagika woote nje! Duh

Kuna yule ndege maarufu akikuona anaficha kichwa mchangani na kuacha kiwiliwili nje akidhani kwa kuwa hukuoni basi na wewe humwoni na kwa hiyo utaendele kumbe anaogopa kufa anaona!

Sasa angalia huu ubunifu. Jamaa anaacha miguo yake michafu, anakimbia kuingia nyuma ya pazia kumbe kuna kijibwa chenye kiherehere. Imajini jamaa kaacha kila chake, harafu yuko mbele ya luteni Kanala ambaye kwa vyovyote ana mguu wa kuku! Duh sijui anafikiria nini hapa.

Walianza labda kwa kutaniana na kujikuwa sehemu za kusini kwa miili yao zinachekelea kwa misuguano na migogoro ya kelele zisizosemekana na kusahau kufunga mlango. Hapa wanatamani wasingejuana aka wanajuuuuuuta kujuana.

Je ungekuwa wewe mmoja wa hawa na hasa huyu nyuma ya pazia, ungefanyaji? Au iliwahi kukutokea? Unadhani ungekuwa hili lijamaa la manyota ungepata fundisho gani? Au ungepige mtu tu ili akukome?

Unataka kujua ningekuwa mimi ningefanyaje? Je huyo nyuma ya pazia akijulikana kuwa ni ndugu wa hili lenye manyota, au bosi wake au mwajiriwa wake, house boy je? Nini kiliendelea?

Mimi simo!