Friday, July 31, 2009

kifo cha mzee Jasson Lutabasibwa kamala.

mambo hayo, baada ya birthday yangu ya tarehe 30 july, basi tarehe 1 aug 1998, mpendwa mzee wangu, omwami Ta Jassson Lutabasibwa Kamala aliaga dunia. nilikuwa mwanafunzi wa kidato cha pili, ikawa jumapili mida ya saa mbili asubuhi, nikaitwa nyumbani kwa mkuu wa Shule, nilipoitwa nilijisikia kama napipgwa butwaa vile nikaenda.
basi nikamkuta mzee F.kabigiza akiwa na piki piki cd fulani hivi. nilipomsalimia, mzee kabigiza hakujibu lolote, mzee kabigiza akaniambia kwa kihaya kuwa nahitajika Nyumbani kwetu. sikuuliza swali ila nilimwona headmaster akiniangalia kwa uzuni kubwa mno. nikawa kama nimechanganyikiwa na kuondoka mbiyo mpaka bwenini na kuchukua nguo mbili tatu.

nikiwa nimebebwa juu ya pikipiki, roho yangu haikuwa na amani na baada ya mwendo fulani nilisikia homa kubwa nikakaa kimya. tulipofika Bukoba mjini, kote nilikopita nikiwa kwenye piki piki niliangaliwa kwa uzuni na wale walionifahamu. twakaribia Nyumbani, mzee kabigiza akapunguza mwendo na kuniambia kuwa mzee amefariki jana yake. bado ilikuwa butwaa pia.

kufika eneo la kashura tulipokuwa tukiishi, nikaona watu wengi na hasa wale wa dini wanaimba nyimbo za kuommboleza, machozi yakanitoka, nikalia na kutamani kukaa chini. shangazi yangu akanishika na kunipeleka ndani, nikakuta mzee yumo ndani ya sanduku, ilikuwa ni kilio na kusaga meno.

tukasafirisha kwenda kijijini na kesho yake tukazika. maisha yakawa kama vile niko porini, kijana mdogo naachwa na dingi kumbuka sikuwahi kulelewa na mama wala simjui. duh niende wapi mimi mkosaji nisiye nazuri. yataisha tu lakini. tukamzika mzee wangu, nikabaki kuangalia kaburi na kulia, mara kadhaa nilikimbilia pale na kuongea na baba asiyeonekana!

baada ya kujitambua siku hizi nikagudua kumbe ni mambo ya kawaida na mzee ilibidi aondoke tu kwani isingekuwa hivyo asingeondoka. sasa nimezoea na nachuklia siiimpo baada ya miaka lukuki japo enzi zile nililia na kusaga meno japo hayakuisha. sasa ni miaka 11 na mimi ni jibaba na maisha ni meeema sana na namshukulu mzee wangu kwa upendo na kunizaa japo sikuliomba hilo.

kifo cha mzee kilinisaidia kumuona mama kwani baada ya kama mwezi mmoja hivi, mama alikuja kunitembelea shuleni, nikaitwa na na kumwona mwanamke aliyenizaa pale shuleni. hata hivyo alikaa kama dakika kumi na kuondoka kwa hiyo sikuweza hata kuikariri sura yake lakini nilifurahi mmno. mwaka wa 2001 nikaja dar es salaa na kumwona rasimi japo kwa siri au kwa kujificha.

duh sikuamini kumwona mwanamke aliyenizaa, nilijisikia kuwa mbinguni vile. nilimwangalia tumboni nilipoanzia maisha na kusema duh! japo sikukaa naye sana kwani ilibidi niwahi home na nilienda pale kisirisiri ili isiwe noma japo duh mama ndo hivyo. life is a process bwana na tumetokea kwingi na tunafanya mengi.


mpendwa msomaji wa blogu hii usione nakuzingua na mambo binafsi bwana kwani ni mambo ambayo nikishea na wewe najisikia vyema kwani wakushea naye ni kama sina vile! sijui niseme alazwe mahala pemo peponi mzee japo kutoka kwenye miili (KUFA) ni kawaida, muhimu na nilazima tu na sasa ni mambo ya kawaida kwa sasa.

6 comments:

Nicky Mwangoka said...

Pole sana kaka Kamala, hiyo ni njia ambayo kila mmoja lazima apitie. Hawa wapendwa waliotutangulia tuwaombee ili nao wawe waombezi wetu wakitutayarishia makazi mema. Nami ni juzi tu Machi 2009 nimempoteza Baba. Jipe Moyo kwani najua kila unapokumbuka hayo moyo unaumia sana.

Mzee wa Changamoto said...

Nafurahi kuwa unaweza kujitambua na kutambua umuhimu wa PUMZIKO la Mzee. Hakuna apendaye kuondokewa na ampendaye, lakini pia hakuna ambaye anapenda mtu ampendaye na ambaye amefanya mengi mema asipumzike. Haijalishi mtu atakuwa katika maisha, hali na uwezo wa namna gani kifikra na kiuchumi, wakati ufikapo atahitaji pumziko. Na kama alifanya yote ayo (ikiwa ni pamoja na kukulea) basi alihitaji pumziko na tuendelee kuamini kuwa amelipata.
Furaha kubwa huko aliko ni kujua kuwa mwanae anaendelea vema na anawaendeleza vema wale wenye uhitaji HASA WA KUJITAMBUA.
Blessings

chib said...

Pole kwa masahibu yaliyokukuta wakati huo.
Lakini uliyashinda na kupiga moyo konde na sasa unaishi vizuri

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

very encouraging message. I really appriciate them. thanx

Yasinta Ngonyani said...

Kamala pole sana najisikia nipo nawe kwa yote uliyopitia. Na nakushukuru kwa kuliweka hili jambo hapa kibarazani kwako kwani kama ulivyosema kushea na sisi wanablog(ndugu zako) umefanya vizuri sana kwani ukishashea na wengine inakuwa nafuu fulani. Simulizi yako imenigusa sana nasema tena Pole sana. Na kumbuka Mzee Lutabasibwa yupo nawe wakati wote. Apumzike peponi mzee wetu Amina. Tupo pamoja.

SIMON KITURURU said...

Tuko pamoja Mkuu!