Wednesday, July 15, 2009

Kila kitu kinazunguka.!

Waweza kushangaa na kushindwa kuelewa mambo ya dunia na jinsi maumbile yalivyo. Kila kitu kinazunguka na wakati mwingine yawezekana kabisa kwamba hamna viumbe vipya bali vile vile katika muonekano mpya au wa tofauti.

Wanasayansi wanatwambia kuwa ulimwengu / dunia tuishimo ni duara na kwamba inazunguka jua. Mzee mmoja kule kwetu anabishi kwamba dunia imetulia ila jua ndo lenye kiherehere linazunguka dunia. Kwake dunia ni kubwa kukliko jua.

Basi nyota nazo zinazunguka, mwezi nao mala kipande, mala mzima. Wengine wanasema macho yetu ndiyo yaonayo mviringo.

Basi bwana, maji tunayokunywa yanazunguka. Yanatoka mitoni, baharini au kwenye madimbwi kwa kuakisiwa au kuchavushwa na baadaye kunyesha kama mvua. Hata mikojo, vinyesi na mate, yanaakisiwa na kunyesha kama mvua harafu wewe unakunywa. Yawezekana maji unywayo sasa ni mkoja au mimate ya lijamaa usilolipenda!!

Chakula nacho ndo hivyo. Ukijisaidia shambani yanaota mazao mazuri yenye mbolea na matamu kula, yanazunguka. Binadamu naye anazunguka, tuachane na reincarnation, unatoka hapa na pale huku na huku kule na kule. Damu inazunguka mwilini na ikisimama hamna uhai!!

Akili zetu nazo ziko bize, mara hiki, mara kile, mara sijui nini. Mchana mawazo, usiku ndoto, zikisimama wafa. Kila kitu ni mzunguko tu. Basi kama kuna herufi nzuri, ni O au 0 kwani zinaonyesha uhalisi. Ni mzunguko tu ndg.
Nini kingine kizugukacho? Si hata gari lazima lizunguke ili kukufikisha uelekeako?

ZUNGUKA TU

2 comments:

Nuru Shabani said...

Darasa limetulia kaka.

chib said...

Ukifikiria sana hutaweza kula chochote. Cha muhimu ni biodegrability ambapo kitu kikitupwa kuna vijidudu vingine kukipangua katika vijichembechembe vidogo ambavyo ndio huchukuliwa na vitu kama mimea na kutengeneza kirutubisho kingine ambacho huwa na manufaa kwa binadamu.
Habari hii si haba, safi sana