Friday, July 17, 2009

nawapenda sana wanawake na ma Jike pia


ukisema au ukisikia wanasema jamaa anapenda sana wanawake, waelewa kuwa anapenda zaidi labda ''kusini mwa Afrika'' mimi nafagilia kila kiumbe cha kike, wanasema wanawake ni wadhaifu, kumbe sio, bali ni walaini. kwa sababu yao, ndiyo maana ulimwengu unazidi kuwepo. kwa sababu ya uwepo wa viumbe wengine wa kike ndio maana ulimwengu unazidi kuwa na viumbe hivyo. uanaume wangu, unajidhihirisha ndani ya mwanamke. ni kwa kumpataia mbegu, ndipo anazaliwa mtoto wa kuniita baba. ni mwanamke. upendo wa mama sio wa kawaida kwa wanae, atafanya kila awezalo kumlinda mwanae. Mwanamke anatumbo la ajabu, ni tumbo linalotunza na kuzaa viumbe vingine. tunamla mwanamke kwa kunyonya maziwa yake na kwa hiyo mwili wake ndio chakula chetu. mwanamke sauti yake ni nzuri, sauti yake ni njema sio ya kibesi wala nini. NAMPENDA mwanamke. lakini unaweza kuamini kuwa tangu nizaliwe sijawahi kuunja upendo wa mama wala wa Mwanamke yeyote?? nakosa mengi ndugu, sikuwahi kuuonja upendo wa kweli japo natambuaumuhimu wa mwanamke. aaaamina

5 comments:

mumyhery said...

fanya subira iko siku

Bwaya said...

Pole kaka. Uliwahi kusema hili kipindi kwamba hujawahi kuuonja upendo wa mama.

Farijika kwamba hata sasa bado unaweza kuupata upendo huo. Na kama unavyosema mwenyewe, unawapenda wanawake. Kaka wapende. Ni haki yako kuwapenda. Na watajaza pengo ambalo pengine unaliona japo siamini kwamba ni lazima liwepo.

Kuna jamaa aliwahi kusema: historia haina kauli ya mwenendo wa maisha yetu ya sasa. Ni leo na kuendelea ndivyo vyenye kutufaa. Japo psycholoanalysts wanatuaminisha kwamba historia ina nguvu, lakini binafsi siamini kuwa hatuwezi kukabiliana na yaliyopita kwa maamuzi sahihi yayayohusu leo na kuendelea.

Yasinta Ngonyani said...

Kamala pole sana mada yako ya leo umenifanya nilie. Nasema kama da Mumyhery fanya subira iko siku. Na nasema tena pole sana nipo nawe.

Bennet said...

Kwangu mimi nyumba ni mwanamke, kwani nyumba isiyo na mwanamke utaigundua ukiingia tu (si zote) mara nyingi huwa hazina mpangilio mzuri
Kamala muda sahihi ukifika, Mungu atakujaalia mke mzuri wa tabia na sura pia

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

asante wote, sina cha kuongeza, ila huko mbeleni nitajaribu kuongea kwa kina kidogo. nadhani juma lijalo nitasema kwa nini inakuwa hivyo