Thursday, July 30, 2009

Ni ‘birthday’ yangu jamani.

hakuna mtoto mbaya bwana, udogoni nilikuwa booomba we angalia mwenyewe

Sio miaka yoote huwa naikumbuka siku hi kwani wakati mwingine hupita bila kustuka na wakati mwingine sionagi umuhimu wake sana lakini leo nimeikumbuka.

Ni tarehe 30 July miaka 28 iliyopita ndipo kifaa nilipokatiza njia na kujitumbukiza ndani ya ulimwengu huu na kuwa binadamu mpya. Japo naamini kuwa niliwahikuishi sehemu, sijawweza kukumbuka ni wapi kabla ya kuuvua mwili (kufa) na kuuvaa mwili huu mpya tena nikiwa mhaya wa bugandika Bukoba mkoani kagera.

Tarehe 12/12/1982, nilibatizwa rasmi bila ridhaa yangu na kuwa mkrsto mfuasi wa uluteri ambao mpaka leo sijaweza kuuelewa wala malengo yake na hivyo nakaitwa James, Lutatinisibwa japo hivi sasa jina la james silitaki na silitambui tena na linikome kabisaa kwani sijui maana yaki ninini mimi na kwahiyo naitwa Kamala Lutatinisibwanikiwa kidato cha pili, toto hilooo!


Mwishoni mwa miaka ya 1980 nikaanza vidudu a.k.a chekechea za dini. Nakumbuka nilivyochapwa saaana ili niingie darasani kwani siku nyingine niliishia tu njiani na kurudi home. Nilipokuwa darasa la tatu, nikasomeshwa kipaimara na kuanza kula mkate kanisani wao wanaita kushiriki meza takatifu ambayo mpaka sasa nahoji utakatifu wake kama sio utakafujo na sikuwahi kupenda kula mikate hiyo (one size fits all)

Kuna wakati nilipenda mambo ya dini na kutaka kusomea uchungaji lakini ilikuwa ni kihere here baadaye nikabadirisha njia kwani utakatifu woote unaosemwa mimi naufanya bili kivuli cha dini wala unafiki wa kujificha mkuu. Kweli kwangu ni daima na unafiki ni mwiko! Kama ningekuwa na kauli mbiu.

Basi bwana, nilisoma vitu lukuki mpaka sasa kitaaluma ni mambo ya Compyuta nayo ni kwa kiherehere siifagilii wala nini ndio maana napenda kuandika na kuishi kama mwandishi zaidi ya chochote kile kwani compyuta nilimhiga dingi tu.

Maisha yangu ya udogoni yalikuwa ni meema sana ili sikuwahi kufurahia upendo wa mama kwani inasemekana baba na mama walitengana mwaka mmoja tu baada ya mimi kuzaliwa (kumbuka ni mtoto wa mwisho) na hivyo nikalelewa na bibi yangu (ma yuliyana) na shangazi zangu kadhaa na binamuz.

Maisha yalikuwa mazuri japo mara nyingi ilikuwa ni kukwidwa na kuambiwa maneno fulani ambayo ni duh! I still miss something mother wise, am not yet mothered.

Mpaka sasa naishi maisha kama ya mwanampotevu kwani sina uhusiano wa karibu au wa maana na yeyeyote aaminikaye kuwa ni ndugu au mzazi kwani imebidi iwe hivyo na sio chagua langu na inabidi nikubali matokeo.

Kama kuna ndugu yeyote anayesoma hapa (najua mpo) basi nawasalimu, sijambo na mambo poa na maisha ni mema huku nilipo.

Hata hivyo namshukuru kila mmoja aliyesababisha maisha yangu kuwa kama yalivyo kwani nayafurahia zaidi labda kuliko vinginevyovyote yangekuwavyo. Nawashukuru walezi wangu, majirani hata wambea wale walionishitakia siku zote.

Mabaya hukumbukwa na hivyo nakumbuka saana matusi na masimango yoote niliyorushiwa kwani wakati mwingine nikiyakumbukia hujisikia kulia kidoogo hata kama nimejitambua likini duh! Naghairishaga tu ili yaishe na naomba nisikushirikishe kwani ntakuwa nimekutunaka pia.

Shukrani maalamu zimwendee binamu yangu Jennifer Lukambuzi, upendo wake kwangu kama mtoto hausaahauliki na unajenga historia muhimu katika maisha yangu, siwezi kuusahau kwakweli japo unaonekana kupwya na kupotelea mbali ukubwani! Pia Jovian na Elivida Binomutonzi tuliolelewa wote hawa ni muhimu kwangu kwani ndio binadamu wa kwanza kuwafahamu na kuhishi nao katika enzi za utoto. Love you so much!

My sister Julieth, bro japhet nafwagilia kuwa na ndugu kama nyie. Jackson ndo maweeeee,

Kila aliyefanya maisha yangu kuwa hivi, nampenda na kumfagilia na nashukuru kila mmoja aliyefanya kila juhudi kwa moyo ili kunitakia mema hata kama mimi sikulijua hilo, basi nampenda sana na kumfagilia bila kutaja jina.\

Hata aliyelazimika kunisaidia ili jamiii imwone mwema naye namshukuru pia. Its my birthday, thanks to my beloved Vaileth for reminding me of this special day for she woke up yesternight and screemed; Happy birthday, happy birthday my love! Thanks and I appreciate to be with u.

Santamat spiritual master and fellow initiates, what a grace to realize my higher self? We shall never die but merge back to be one with HIM, thanks to sant Baljit Singh and all past masters!hapa nshajua kuruka juuuuuuu na kucheza, 2002, moshi

10 comments:

shadrack said...

happy bithday brother!

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Sikukuu njema ya kuzaliwa mkuu. Unasherehekeaje? Nauliza kwa sababu sidhani kama kuna mambo ya keki na vikorokocho vingine tulivyoviiga kutoka kwa utamaduni wa Kizungu. Nina hamu ya kujua besdei ya Kihaya/Kiutambuzi inavyosherehekewa!
Kwa sisi Wasukuma enzi zile wala hatukujua siku zetu za kuzaliwa - achilia mbali mambo ya besdei.

SIMON KITURURU said...

Hongera Mkuu kwa kufikisha siku nyingine! Labda kesho tusherehekee kama tutaifikisha tena!

:-)
Ukiamua kusherehekea kwa tendo la ndoa kumbuka stahili hiyo huzalisha watoto au ukicheza vibaya kuukwaa mdudu!

Ukisherehekea kwa keki kwa soda, kumbuka vinaozesha meno na ukizidisha tu obesity.

Ukisherehekea kwa pombe kumbuka pombe si chai:-)

Happy Birthday Kamala au tu EX-James!

Fadhy Mtanga said...

Happy birthday brother.

Nimesoma maelezo yako, nimefeel kitu.

Yasinta Ngonyani said...

Hongera kwa kuongeza miaka au kuongezeka uzee. Ni kweli si wengi tunakumbuka hii siku. Hongera sana Kamala.

Mzee wa Changamoto said...

Niseme nini?
Umesema unalotakiwa kusema na si kusemewa na sasa ni wakati wa kurejea ile "post" ya HUYU NI NANI.
Nadhani wakati mwingine ukiuliza utapata jibu la zaidi ya awali.
Pole kwa kuwa ulivyokuwa na hongera kuwa ulivyo. Shukrani kwa shukrani ulizozitoa kwani zaonesha shukrani kwa washukuriwao.
Naona umekwenda kule ambako Bob Marley alikusema kuwa "we refuse to be what you wanted us to be. We are what we are and that's the way it is going to be"
Baraka kwako kuwa uwavyo na kuwa na huyo aliye alivyo kwani yaonesha pamoja mko mlivyo.
Hongera kwa siku ya kuzaliwa. Yaani HAPPY BIRTHDATE
By the way nimependa ile "yesternight" That's cool. Lol

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

sharack. nibyema kuwa nawe hapa. thanx once again kwamba ndugu kama wewe tunakuatana kwa njia ya blog pia.

matondo, nimesheherekea kwa kuwa na wewe hapa bloguni na ndio sherehe yenyewe. Wahaya tulijiua sana siku za kuzaliwa kwani tulirejea majira kwamba huyualizaliwa iliponyesha mvua kubwa, au samaki walipopatikana kwa wingi!

kitururu nashukuru kwa maoni na yoote niliyazingatia kabla hujanionya na sikuyatenda ila kuzalisha watoto siogopi kwani na mimi nilizaliwa pia.
mzee wa changamoto changamooto zako no comment na ziendelee kuchangamotisha tu.

Egidio Ndabagoye said...

Heri ya siku ya kuzaliwa.Kuna umuhimu wa kuikumbuka sku ya kuzaliwa?

Naona wafuasi wa Yeshua wanakumbuka ile tarehe 25 kama siku ya kuzaliwa kwake pamoja sijaonaa andiko lolote Yeshua alipoikumbuka siku yake.

Kaka Kamala nimependa lile pozi ulipokuwa sekondari,shule gani hiyo Kahororo,Nyakato.Ihungo au seminari gaani?

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

egidio, ile ni shule mpya ya vijiji falani, inaitwa tweyambe ishozi gera development society (TIDESO)

Anonymous said...

kwenu bugandika sehemu ki maana hata mimi ndo kwetu,umenikumbusha mbali sana,mimi natoka bwoki.