Thursday, July 9, 2009

Njia ya kuelekea kwa Mungu

Mungu huweza kufikia kwa njia zifuatazo:

Kutoa huduma kwa wengine bila kujigamba na kuheshimu kila kiumbe chake kuazia kwa binadamu, wanyama miti nk.

Kukumbuka na kulinuiza jina lake na upendo wake wakati wote (tahajudi ya nuru / inner-light meditation).

Kusikiliza maneno yake na sauti yake kupitia kwa viumbe vyake (tahajudi ya sauti / inner-sound meditation)

Na kuishi kwa uwepo (kuishi sasa / consiousness)

Haya yote yatatuelekeza kuishi kwa upendo, amani, mafanikio vitakavyo zaa heshima, umoja, kuvumiliana, heshima na kutupelekea kwenye uhalisia wetu (ukweli mkuu) ambao inasemwa kuwa mkiijua kweli itawaweka huru na hakuna uhuru bila kujitambua (self realization) ili kumtambua Mungu (God realization)

Kristo (yesu) anatwambia kuwa kama mnanipenda, basi ziiishi amri zangu

8 comments:

SIMON KITURURU said...

DUH tutafika kweli wajameni?

Kwa mfano kama nikikunukuu ....''Kukumbuka na kulinuiza jina lake na upendo wake wakati wote ''...

...katika hali halisi ya shughuli za kibinadamu si inamaana kuna muda tutachanganya mambo kama si jina la kulinuiza?:-(

Chacha Wambura said...

kusikiliza sauti za bundi?

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

kitururu, ukisahau ni mwanzo wa kukumbuka kuwa ulisahau, ndio maana inabidi ukumbuke.

chacha, ndio, msikilize huyu bundi vyema na kwa utulivu kisha niabie

Nuru Shabani said...

Asante kwa darasa

Mzee wa Changamoto said...

Haya ndio tunayokosa katika maisha ya sasa. "kuishi kwa upendo, amani, mafanikio vitakavyo zaa heshima, umoja, kuvumiliana, heshima na kutupelekea kwenye uhalisia wetu (ukweli mkuu) ambao inasemwa kuwa mkiijua kweli itawaweka huru na hakuna uhuru bila kujitambua (self realization) ili kumtambua Mungu (God realization)" Basi hapa haijalishi ni Mbingu ipi isemwayo ama ifikiriwayo, lakini tukiishi kwa hayo niliyokunukuu ukisema, ni kama tutaanza kuiona Mbungi hapahapa duniani. Itakuwa saafi sana.
Nani atataka kufa maisha yakiwa na hayo yote? Pengine hata kifo kitaogopa kutuchukua.
Asante kwa darasa

chib said...

:-)

Yasinta Ngonyani said...

Kamala Asante kwa darasa. Tutafika tu!

Bennet said...

Lakini mkumbuke kwamba USILITAJE JINA LA BWANA WAKO BURE....