Tuesday, July 7, 2009

njoo darasani tujitambue wewe!

SEMINA ZA ELIMU YA UTAMBUZI

Familia ya Jitambue (FAJI) ni Umoja wa Wananchi wa Tanzania wanaojishughulisha na maarifa ya utambuzi. FAJI ni Taasisi iliyosajiliwa Mwaka 2007 yenye namba ya Usajili 15579 chini ya Msajili wa Jumuiya, Wizara ya Mambo ya Ndani.

Utambuzi ni maarifa yanayolenga kumuwezesha mtu kubaini kuhusu yeye na yanayomzunguka ili aweze kukua, Kimwili, Kiakili, Kihisia na Kiroho. Kwa kuyapata maarifa hayo yanamuwezesha kuachana na mazoea yanayomuumiza na kuumiza wengine; kukabiliana na vikwazo, vurugu na changamoto mbalimbali za kimaisha; kufikiri vizuri, kujiamini, kuwa mbunifu, kufikia malengo yake na hivyo kujiletea mabadiliko katika maisha yake na maendeleo ya jamii kwa ujumla. Pia humfanya mtu awe na ufahamu yakinifu wa ubinadamu wake na hivyo kuweza kuishi maisha yenye Furaha, Amani, Utulivu na Upendo wa kweli. Kujifunza maarifa hayo huhitaji kuwa na sifa yoyote maalumu kama cheti cha shule, umri, jinsia, dini, imani nk. Kitu kikubwa ni uwezo wako wa kuyatekeleza unayojifunza kwa vitendo.

Kwa sasa FAJI inajishughulisha kusambaza maarifa hayo kupitia vyombo mbalimbali vya habari pamoja na Madarasa yaliyopo kwenye Kituo cha FAJI Kimara Rombo Dar es Salaam.

Maarifa haya pia yanatolewa kwa njia ya Semina kwenye Shule, Vyuo, Taasisi na Mashirika mbalimbali.

Baadhi ya mada zinazofundishwa ni:-

Namna ya kupata utajiri pamoja na mafanikio katika biashara, kiuchumi, kazini na shuleni; namna ya kujenga mahusiano mema kazini na upendo wa kweli katika ndoa, suluhu ya tendo la ndoa; namna ya kujiamini; kuondoa msongo wa mawazo, chuki, kijicho na hasira za ziada; kinga ya uchawi; namna ya kupata chochote utakacho maishani; kuondoa tabia sugu kama ulevi, uvutaji sigara n.k., kuondoa hofu na aibu, kupata afya nzuri kimwili kwa njia ya tiba mbadala, kufikiri vizuri, n.k.

Tunafundisha mada nyingi zaidi ya zilizotajwa hapo juu.

Kwa maelezo zaidi tafadhali wasiliana nasi kupitia:
Sanduku la barua namba 22040 Dar es Salaam. Simu namba 0652 626996, 0715 627003 au 0784771301 na 0713 250701, Email – faji.jopo@gmail.com au fika katika kituo cha FAJI kilichopo barabara ya Morogoro Kimara Rombo na utaliaona Jengo la Taasisi ya FAJI kulia kwako ukiwa unatokea Ubungo.


wakazi wa Mwanza darasalitakuwepo kabla mwaka huu haujamalizika, jiandikishe kwangu kupitia 0754 771 601

3 comments:

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Ningekuwa karibu ningependa kuhudhuria - darasa linalofundishwa na kamala lutatinisibwa Lutabasibwa. Siku mkianza kutoa mafunzo haya katika mtandao nijulishe na nitajiandikisha mara moja. Elimu haina mwisho ati! Kwingineko wewe na Kaluse endeleeni kutuelimisha kupitia blogu zenu. Bado unaandika makala za utambuzi katika gazeti la Kwanza Jamii? Sijaziona ukizitunduka hapa kwa muda mrefu.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

prof. mtandaoni tuko kwenye maandalizi. tunaangalia uwezekano wa kuwa na website yetu na ikibidi tutarekodi kwa sauti na kwa picha.

kwanza jamii naona kama wanawaandishi wengi labda lakini wakinikaribisha tena sitosita kuendeleza ngoma hiyo.

chib said...

Usisahau kuianika wazi hiyo website siku mtakapoizindua.
Wazo lenu ni zuri sana, na mnastahili kuungwa mikono na sio mkono