Monday, July 20, 2009

Swali kwa wenye Blogu

eti ni kwa nini wewe huwa unablogu? hata kama huna blogu, kwa nini unatembelea blogu nyingine na unatarajia nini kutoka katika blogu? kwa nini kuna blogu unazopenda kutembelea na usizozopenda?

ni chamgamoto gani unazipata katika blogu? je unadhani blogu zinaweza vp kutuletea mafanikio na maendeleo endelevu? ni matumizi gani mengine ya blou unadhani ni muhimu? je maisha yako yangekuwaje sasa bila blogu?

unadhani kuna umuhimu wa jamii zetu kuwa na blogu? unasemaje juu ya taarifa na uhuru uliyomo kwenye blogu? kuna umhuhimu wa kufundisha watu wengine na hsa vijana kuwa na blogu na kuwawezesha kutembelea blogu nyinginezo?

natanguliza shukurani.

2 comments:

SIMON KITURURU said...

Kwangu nimestukia blogu zinanipunguzia muda wa kusoma vitabu:-(

Mzee wa Changamoto said...

Blogu kama kitu kingine chochote kinaweza kuwa kizuri ama kibaya kulingana na matumizi. Na-blog kwa kuwa naweza kueleza na kuweka kumbukumbu zangu wazi kuhusu yale ninayoamini na kujifunza. Ni sababu hiyohiyo inayonifanya kutembelea na blogu nyingine.
Kubwa ni kuwa ukiifanya blogu kuwa sehemu kubwa ya maisha kuliko maisha yako, utajikuta inakulaani.
Blogu ni nzuri ndio maana ni mbaya.
Bless