Monday, July 13, 2009

unamtafuta Mungu? acha hizo!

Kumtafuta Mungu ni sawa na kujitafuta na hivyo tutakapoacha kumtafuta tutampata.
Hatuwezi kumjua Mungu na hivyo tunachokijua ni kama punje ya mchanga baharini. Mungu hayuko mbali nasi. Hatuwezi kumtafuta huku au kule, tunaweza kumpata kwa njia ya uamsho pekee, uamsho (awakening) wa roho zetu. Roho pekee ndiyo inayoweza kumwona Mungu. Ndio maana wanasayansi hukataa juu ya uwepo wa Mungu hata kama ukubali juu ya uwepo wa nguvu wasiyoielewa inayomiliki na kutawala kila kitu..
Uamsho wa roho zetu huanza kwa kujitambua. Ukijitambua utamtambua Mungu. Uamsho wa roho ni sawa na sayansi ya roho, sayansi iwezeshayo kumuona Mungu. Kwa uamsho wa roho zetu, tutamhishi na kumfurahia Mungu. Roho ina kazi maarumu ambayo ni kumhisi, kumjua na kufurahia baraka za Mungu.
Vitabu vya dini (misaafu) husisitiza kuwa sisi ni roho na kama ni roho sisi hatuna mwanzo wala mwisho na sisi na Mungu ni sawa na maji. Mungu ni mkubwa kama bahari na sisi ni wadogo kama tone la mvua na hivyo basi tone la nvua lidondokapo baharini huwezi tena kuyatenganisha. Bahari hupokea maji ya kutoka kila upande kama ishara ya umoja wa binadamu wote wenye rangi, kabila na mataifa tofauti. Bahari hupokea maji kutoka bara ulaya, Amerika, Afrika na kwingineko lakini maji yale yaingiapo baharini huwa kitu kimoja. Rangi moja, radha moja na sifa zilezile. Huwezi kuyatenganisha tena kwa kuangalia yalipotoka. Hivyo ndivyo ilivyo kwetu sisi kama roho tukifika mbele ya Mungu huwa kitu kimoja
Vitabu vya dini pia huongelea juu ya nuru na sauti (neno). Mungu yumo ndani mwetu na nilazima tumjue huyo wa ndani kabla ya kumtafuta wa nje yetu kwani tukimhishi ndani mwetu tutapata Muunganisho naye (kwanjia ya roho) na hivyo sisi na yeye kuwa wamoja kama ulivyo ukweli mkuu. (kumbuka sisi ni sehemu ya ukweli mkuu au ukweli mkuu umo ndani mwetu)

5 comments:

chib said...

Itakuwaje maji ya bahari yakiamua kuingia kwenye mito na maziwa, je ladha ya maji ya mito na maziwa itabaki ileile au itabadilika.
Ni wazo tu...

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

chib. kwani maji yana radha gani? hujasikia Uarabuni wanakunywa maji ya bahari?
kipi kizuri kati ya maji na radha ya maji? ni maji yapi yanavutia kati ya yale ya mito baharini nk? je hujwahi kusikia maziwa kama lile la singida maji yake ni kama ya bahari kwa ladha?

je nikweli kuwa maji ya bahari hayaendi mtoni? kwani jua likiwaka iinakuwaje mpaka mvua inyeshe? si yanaenda juu na kurudi kama mvua na kuelekea / kurudi baharini?

na ya kisima je? si yana ladha lukuki?
maji ni maji mkuu AU?

Yasinta Ngonyani said...

Nimenukuu kwani sentensi hii nimeipenda. "Uamsho wa roho zetu huanza kwa kujitambua. Ukijitambua utamtambua Mungu". Ni kweli mungu yupo mahali popote pale ndio maana tunomba/sali mahali popote pale.

chib said...

UMENIKUMBUSHA WALE WALOKOLE AMBAO WAMESHIKA NENO NA WALA SI KULIFAHAMU NENO!

Waarabu wanakunywa maji ya bahari baada ya kuyaondoa chumvi yote kwa kutumia mitambo maalum. Na chumvi ipatikanayo hutumika sehemu nyingine wakati wa baridi kali

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

na bado ni maji tu ndg