Monday, July 6, 2009

wajasiliamali wa bongo wanaigana!

nimetembelea maonyesgo ya Sabasaba, kwanza unajua saba saba nini ana ilianzaje? kumbe TANU aka CCM. basi wajasiliamali wa Bongo wanauza bidhaa zoote zinazofanana. nguo, vyakula na vinywaji vyoote vinafanana au ni vile vile nadhani wanaiga.

ubunifu ni mdogo sana. yaani mtu anashindwa hata kuogeza vikolombweizo na kuwa na tofauti na mwenzie, kila bidhaa ni zile zile. kwa maneno mengine ukitembelea banda moja la wajasiliamali wa bongo huhitaji wenda kwingine kwani unakuwa umeona kila kitu ambacho labda ungekiona kwingine! duh

mimi ni mpenzi wa nguo za kiafrika, hakuna jipya! nguo zote zinafanana. nilipowatembelea wakenye, kidogo nikaona utafouti na mvuto. sikupiga picha labda ningekushirikisha kwa picha ukaona. ni lini wajasiliamali watakuwa wabunifu na kushindana vyema? mimi sijui na labda sitaki kujua saana.

ndo hayo

6 comments:

Bennet said...

Hii hali ya kufanana kila banda ilinifanya nikaingia mabanda manne (4) tu ambayo ni PTA, VETA, MALIASILI na POLISI humu ndio kidogo niliona vitu viko tofauti na nikajifunza mambo mapya, ule mvuto wa 77 wa zamani naona sasa hivi haupo tena imebaki mazoea tu

Yasinta Ngonyani said...

Kamala hapa umesema hata mimi hili nilikuwa naliwaza sana na pia linaniuzi sana sio kwetu Afrika tu hata hapa nilipo ukiingia kila duka ni nguo za aina moja tu kwa hiyo watu wote mnakuwa kama wanafunzi yaani mmevaa sale.

Anonymous said...

Pengine wateja wa wajasiriamali hao ndo wanaochangia kwa kiasi fulani kufanana kwa bidhaa sokoni.Nafanya biashara na ninapoleta bidhaa mpya sokoni ambayo inakuwa tofauti na bidhaa za wafanyabiashara wengine huwa inanisumbua kupata soko.

Kwa hiyo wateja wananilazimisha kutengeneza bidhaa zilizopo sokoni.Pengine tatizo sio wajasiriamali kuwa wabunifu bali ni wanunuzi wa bidhaa ndo wanaoigana.Mnunuzi akiona mwenzake kavaa nguo nyekundu na imempendeza naye atahitaji kama hiyo.Namaliza kwa kusisitiza kuwa tatizo lipo kwa wanunuzi waliozoea kuuza machungwa na kunua FANTA.

Mzee wa Changamoto said...

Ntarejea. Wacha niwaze vema
Asante kwa hili

SIMON KITURURU said...

DUH!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

yasinta na sale! ndio hata ukiwa uchi unafanana na wengine!

anony umenena na ulichokisema kinahitaji utafiti makini. asante kwa kututoa ukungu wa kuuza machungwa ili ununue fanta!!!!!!