Sunday, August 16, 2009

Ajira zetu na mikopo ya kudhalilishana.

Umeajiriwa na unafanyishwa kazi? Ni ajira bongo na kuna nafasi nyiingi saana za kuajiriwa. Mwandishi wa kitabu cha rich dad poor dad, mmarekani Robert kiyosaki kuna kitu anakiita rati race a.k.a Mbio za panya. Anasema maisha yetu ni ya kuzunguka na kuhangahika tu. Master wa Santmat meditation, sant Baljit Singh, yeye anasema kuwa binadamu wa leo hatuishi, bali tuna kimbizana tu na kujaribu kupata tusichoweza kukipata tuakiamini kitatupa furaha kumbe hata tukikipata hakituridhishi na tunaendelea kukimbiza kingine.\

Kwamba hata tulichonacho tunaking’ang’ania hatuko tayari kukiachia huki tukikimbiza kilichoko mbali tukiamini kitatupa furaha na ridhiko. Hayo ndiyo maisha yetu binadamu wa leo katika ulimwengu huu. Hatuishi sasa bali tunaishi jana na kesho. Tumeiacha sasa ijiendee ipendavyo wakati ndiyo halali yetu.

Mtoto akizaliwa anaambiwa asome ili apate maisha mazuri utadhani wasio soma wana maisha mabaya wakati ulimwengu ulibadirishwa na wasiosoma zaidi ya wasomi, na anachaguliwa cha kusomea na wazazi wake badala ya yeye mwenyewe kuchagua apendalo na siku zote huambiwa maishani magumu wakati hata wanaomwambia hivyo bado wa naishi sasa kama ni magumu mbona nyi mnanishi?

Kila siku kabla ya kuendeleza shuguli zangu na haraka baada ya meditations zangu, huwa naomgea na jamaa yangu kwa jina joram. Tunaongea mengi juu ya maisha kwa kuangalia hali halisi. Huwa tunaketi karibu na parking moja ya magari ya jamaa wafanyao kazi ofisini. Basi siku hiyo tukawa tumeyaangalia magari, jinsi yanavyoegeshwa na kubaki vile, kwa kweli yanapendeza.

Unajua nini? Wafanyakazi wana magari mazuri kwa kweli. Lakini je, sote tunahitaji magari? Hapana! Waajiri wa sekta binafsi wanatupumbaza na kutufanya kuwa tegemezi daima kwao. Wengi wa waajiri hao hutoa mikopa (wakati mwingine) ya lazima kwa wafanyakazi wao ya magari. Inafika hatua ukibadili kazi, basi mwajiri mpya anakununua wewe na mkopo wako ukamfanyie kazi.

Eti mtu anakukopesha gari tena la kifahali na unalilipia hela kidogo huku ukijiona umeula! Sehemu ya mshahara inaelekea kulipa gharama za gari lako. Kusema kweli unaanza kulihudumia gari kwa kulinunulia mafuta, kulilinda na kulikarabati na hivyo sehemu ya mshahara hiyo kwenye gari. Kumbe jamaa kakukopesha gari ili uwahi kazini au akikutuma basi ufanye shuta.

Baada ya miaka mitatu au mine gari lako hilooo limechoka na kupitwa na wakati na hivyo linakugharimu kulitengeneza au kuliuza kwa hasara na ni wakati huo umemalizia au hujamalizia kulilipia, si ni mkopo tu ule? Kwa hiyo unalipia kisichokuwepo au unalipia unachokilipa tena!

Mwisho wa siku sio wewe wala gari, umeliwa. Hata wakati mwingine huna ela ya mafuta ya kuendesha gari lenyewe. Sijui utachukua mkopo. Pesa ambayo ungeitumia wasomesha wadogo, watoto, ndugu nk, zimeshia kweenye gari ili wakuone kuwa na wewe una gari! Maisha ya show, ni noma.

Rafiki yangu Joram ambaya ni mfanyakazi mwenye cheo serikalini, yeye hataki mkopo wa gari wala kununua gari kwa pesa zake hata kama anauwezo huo kwani anaamini magari yoote ni yake. Dala dala, Tex hata mgari binafsi yampayo lift yanamtosha sana kuliko kununua la kwake binafsi.

Labda ndio maisha yetu hayo ya mbio za panya, ‘rat race’ wakati tunaenda kanisani kumshukuru ‘mungu kichaa wetu’ kwa kutupatia magari mazuri, interesting ehe? Tunahitaji nini haswa sisi? Kipi kitangulie? Gari, mke,nyumba, computer, wanyama au?

2 comments:

Mzee wa Changamoto said...

Naamini tunahitaji kuwa sisi., Bahati mbaya nimejifunza hii THE HARD WAY lakini naamini itatusaidia. Tatizo ni kuwa kuna upumbavu mwingine unaoendelea amba unawafanya wanaotaka kuwa wao kuonekana wasioijua kweli yao. Hivyo ukweli unaonekana ujinga kwa kuwa ujinga unatumia ujinga kuupinga ukweli.
Mpaka pale tutakapoacha kujikimbia, tutakuwa wenye shida tuu.
Can't run away from yourself

Chacha Wambura said...

mada zako wakati mwingine huwa zimepindapinda kama upinde wa kihaya! sasa umenishawishi hata nikauze kale kamkweche kangu ili nitembee peku kama mtawa wa zamani wa ki-fransiskani ama ki-benediktini kule kwa akina Ngonyani!!!!

KL, ulosema yana mantiki na laiti yangekuja kabla ya mwaka 2005 ingekuwa kheri sana kwani yangetufaa sana. Hata hifo tuko pamoja mkuu.