Saturday, August 8, 2009

busara za shaaban Robert

mwandishi wa enzi hizo shaaban Robert katika kitabu chake kiitwacho ......UTUBORA MKULIMA.... nilimsoma na kunukuu maneno fulani na kuamua kuweka hapa ili uonje kwani kkupata kitabu hicho enzi hizi ni ndoto kiasi........

Mwaminifu kama mchana, msiri kama usiku

Ulimwengu umewateua watu wachache kama watu bora

Yawezekana mimi ni mjinga, bali fikra yangu ndivyo innavyoniongoza

Ukiwa na fedha utajuta, ukiwa huna utajuta pia, cha nini kitu hiki?

Mauti yaliweza kuwatoa wapenzi machoni pake, kamwe hayakuweza kuwatoa moyoni mwake

Siifu jambo ilipendalo kwa sifa upendayo lakini matokeo yake huwa mamoja siku zote.

Kwa kuwa nimebaki peke yangu sasa, naweza kutenda nipendavyo bila lazima ya kufikiri habari za mtu mwingine

Kila mtu anahangahika shughulika kupata kilichokuwa mbali (tajiri, masikini, wagonjwa, wazima nk) mbali kabisa kama zilivyokuwa nyota za mbinguni

Moyo wa mtu ni msitu mkubwa

Mfalme huchukua raia kuwa malkia wake na malkia huchagua raia akawa mume wake, matajiri huoa masikini na masikini huolewa na matajiri.

Kukatariwa hutia hasira, uchungu, uzni na hata msiba moyoni lakini kufikiria hatua ya kujiua ni upuuzi.

Hapana mwanaume mbaya kwa wanawake wote wala hakuna mwanamke mzuri kwa wanaume wote, mkimkosa huyu utampata yule.

Ufunguo mdogo hufungua kufuli kubwa na mlango mkubwa komeo lake dogo. Kadhalika ubongo wakia chanche katika kicho cha mwanadamu ni kurasa zilizohifadhi fikra zisizo na mwisho

Adam alishindwa kufanya kazi yake borra na akafukuzwa Eden

Sioni akili kusema kuwa neno Fulani haliwezekani eti kwa sababu watangullizi wake walishindwa kulitenda.

Hakuna roho kongwe

Moyo wake ni kama mtoto asiyejua bugdha

Asili yetu ina nguvu kubwa katika mioyo yetu.

Asipojaribu kutendo neno/wazo, utakufa bila kutenda kitu chochote katika dunia.

Miguu ya mtu, humwongoza katika neno lililo katika moyo wake

Humwaziaye harusi, hukuwazia matanga.

Mapenzi ya mwisho ndiyo yaliyo bora

Ndoa ni jambo kubwa sana kwa wanawake, ndio maana hawataki kuingia kabla ya kufkiri sana.

Pang’okapo jina pana pengo, lakini haidhuru.

Pengo la jino moja, halizuii kinywa kutafuna.

Siri ni kitu kimoja katika vitu vinavyotisha.

Kutafuta furaha maishani ni kama kumtafuta paka mweusi katika chumba chenye giza.

Kuwa na furaha katika mwanzo wa maisha ni jambo jema, katikati ni bora na mwisho ni bora kabisa.

Cha mbayo wako hulishwa na mwema wako

Mali huzidisha furaha ya mwanamke katika maisha

Tunaishi katika dunia ya ajabu, hatumiliki vitu vyote, wala hatukosi vyote.

‘nchi ya usahalifu – usingizi’

Mwivu hatoshwi na nafasi, hata katika jangwa hataka kupishwa njia

Upotevu wa mtoto, hufufua tabu ya malezi kwa baba na hurudisha uchungu wa uzazi kwa mama

4 comments:

Mbele said...

Huyu ndio Shaaban Robert. Maandishi yake huwa yamejaa falsafa na maadili. Siku za karibuni nimekuwa nayasoma tena haya maandishi, na ninaamini kuwa yanapaswa kusomwa na kila mtu katika jamii yetu, kuanzia majumbani hadi shuleni. Watoto wetu wangelelewa katika maandishi hayo, naamni yangesaidia kujenga upya maadili, kwa jinsi Shaaban Robert alivyo na uwezo kugusa hisia. Inatisha kuwa leo hii, maandishi yanayotamba zaidi katika jamii yetu ni udaku.

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Yap. Huyo ndiye Pablo Neruda wetu - mwandishi bora kabisa katika fasihi ya Kiswahili na mwanafalsafa aliyekomaa. Yeye hakuwa na PhD na kitaaluma alikuwa karani tu katika serikali ya kikoloni lakini alikuwa na kipaji cha pekee. Kitabu chake cha Wasifu wa Binti Saad mimi huwa natembea nacho katika mkoba wangu kwani lugha iliyotumiwa mle na jinsi anavyoyaeleza maisha ya Siti ni kwa namna ya pekee mno. Pengine hiyo ndiyo kazi ya kiwasifu bora kabisa iliyowahi kuandikwa.

Niliwahi kulalamika kuhusu kutothaminiwa kwa mashujaa wetu nikitumia mfano wa Shaaban Robert. Sijui vijana wa sasa kama wanamjua. Nilichokuwa nauliza ni kwamba kama Waingereza wanamuenzi Shakespeare wao, mbona nasi tusimuenzi Shaaban Robert wetu? Tazama malalamiko yangu hapa http://matondo.blogspot.com/2009/04/tutatukuza-vya-wengine-na-kudharau-vya.html

Asante kwa maandishi haya.

ENTERPRISE ASSET MANAGEMENT(T) said...

kwakweli maandishi ya huyu bwana ni kama msemavyo na nitaendelea kuweka nukuu zake hapa. interesting kukwa mpaka sasa ni nyie ma prof, (wazee kidogo), mliojitokeza kucoment. inamaaana mkiondoka na maandishi ya shaaban yanaondoka nayi.

juhudu zahitajika

chib said...

Ni mtu aliyekuwa na kipaji cha aina yake katika fani ya uandishi