Tuesday, August 4, 2009

Hivi kwani nini watu huoga?Kama kuoga ni usafi basi taulo isingechafuka”…… by unknown.


“Nimesikia habari za kusikitisha sana juu yako na zinaweza kuharibu urafiki uliojengeka kati yetu na labda nidhibitishe kutoka kwako wewe mwenyewe, eti ni kweli huwa unaoga uchi bafuni? Badilika ndugu yangu” …… by Anonymous.


Hizi ni nukuu mbili zilizonijaa kichwani kwangu. Ni siku ya jana niliporudi nyumbani mapema si unajua mambo ya foleni? Jana niliwahi ili nipate wasaa wa kupumzika na kutahajudi vya kutosha. Nilipofika home nikajikuta nikielekea bafuni.

Baada ya kuchojoa nguo zoote na kubaki uchi mzee mwenye ndevu akininginia, nikajiuliza hivi kwa nini niko hapa? Kwa nini niko uchi? Yaani nashika maji najirushia harafu nachukua sabuni na kujipaka, ili iweje? Ehe? Basi bwana nikaanza kufanya kile niaminicho ni kujisafisha mwili. Sasa mbona siwezi kutoka uchi mbele yako na mbele yaw engine lakini kwa ujinga najifungia mbele ya wadudu, maji na uchafu lukuki, nabaki uchi wakati wewe nakukimbia?

Kama maji dili mbona inyeshapo mvua huwa nachukua mwavuli au nakimbia kama sio kukingama ili imalizike? Kwani mvua na tendo la kuoga tofauti yake i-wapi? Mbona sielewi hapa, ni kwa nini tunaoga??

Sasa kwa nini tunaendeleza ujinga huu wa kuonga kama hatutakati kwani tunachafua taulo? Au kwa nini hatuvui barabarani kwenye wengi waliona viungo kama vya kwetu au vihitajivyo vya kwetu tukibaki uchi mbele ya milango, maji, wadudu na sabuni?


Itaendelea...........Basi nakumbuka nikiwa mdogo kule bush kwetu kuoga ilikuwa mara moja kwa mwezi au noma. Kufua nguo tulifua zile za shule tu. Nakumbuka baadhi yetu walipatwa na mabaka meusi kwenye ngozi japo hawakutoa harufu, life was always better, kama unabishi mimi sijui.

Kuna nyakati shuleni walianza kukagua usafi, duh palikuwa hapatoshi. Ipo siku walipoanza kukagua usafi, mzee mzima nili tafuna kucha za vidole vyoote kumi ndani ya dakika moja kabla mwalimu hajanifikia kwani nilikuwa sijazikata wala nini. Washikaji walikuwa wanafuga chawa (enda) vichwani. Ipo siku mwalimu alikuagua vinywa kama vimepigwa mswaki. Nilipitishaga fasta pembe ya shati na kuyasukutua nikameza!

Bahati nzuri dingi alikuwa nazo na kwa hiyo nilivaa viatu sikuzote na viatu vyenyewe hata kama hajavifua (kwa laba) au kupitisha kiwi hamna noma kwani hakuna wa kulinganisha naye, umependeza tu ndugu. Mambo hayo ya shule za udogoni kuonga ilikuwa siyo muhimu wala nini zaidi ya adhabu.

4 comments:

Chacha Wambura said...

KL, wakati mungine uwe mwangalifu kwa maswali yako...

Hii ni kwa sababu utatusababishia matatizo wengine...

Mbona hujatwambia ufugaji wako wa ndevu kama chuchunge umeishia wapi? Je ilikuwa ni kukwepa ununuaji wa sabuni ama ubahiri wa kwenda kwa kinyozi? Ama kuna sababu nyingine ya domestic ya ndani?

Mie napenda sana majinzi na kwa story hii umenikuna kwani mie mpaka jinzi ukilisimamisha lisimame kwa uchafu ama yule my wife wako alitumbukize kwenye maji!!;>(

Fadhy Mtanga said...

Kwi kwi kwi kwi kwi kwiii!

E bwana ndio!

Mzee wa Changamoto said...

Tobaaaaaaaaa!!!!!!!!!!!!!!!@#$%^&*(

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

chacha juu ya ndevu na nywere ndiyo majibu yenyewe ila, my wife sasa kelele! mimi nasevu tu pesa ya saluni na hata nisipoziosha powa tu.